Hakuna Taifa lililoendelea kwa ziara za Rais Nje ya Nchi

Atamleta Mange kimambi
Ova
 
Mbona Jiwe hakusafiri?
Ninyi watu mnajifanya mnajua sana kuendesha serikali. Raisi wa nchi hapangiwi cha kufanya na watu wasio na kazi wanaoshida mitandaoni. Raisi anaweza kupanga safari zake duniani kote pale anapoona inafaa na ina munufaa kwa wanaichi wake. Tuache tabia hizi za kujifanya wajuaji wa mambo, mlisema Hayati hasafiri, ameharibu uhusiano wa Kimataifa, mama anasafiri kiasi na anajaribu tutoa taarifa za safari zake, na bado mnamuandama. Muwe na adabu
 
Wewe ndiyo uwe na adabu haswaaa
 
We nae na huyo Mbowe wako utafikiri ndio mtanzania pekee aliyebambikiwa kesi Tanzania.
 
Magufuri katika miaka mitano na robo alisafiri alisafiri mara sita alileta mapinduzi gani chanya Tanzania?
 
Mawazo yaliyokufa kama ya mwendazake.
 
Umetoa maelezo mazuri sana hata nilitamani kulia. Asante sana kwa mada na maelezo uliyo yatoa. Nakubaliana na wewe 100% kuwa hakuna Taifa lililo endelea kwa ziara ya Rais za nje ya nchi.

Sidhani kama kuna Rais ambaye hivi karibuni amepiga safari za nje nyingi kama Rais wetu mstaafu Kikwete. Yeye atakuwa anevunha Recorde. Nafikiri tumejionea wenyewe jinsi nchi ilivyo poromoka kiuchumi na maisha huko nyuma.

Rais wetu wa sasa hajajifunza na wala kulitambua hilo. Ni Rais ambaye ana fikra na mawazo ambayo yamepitwa na wakati. Yeye badala ya kuchukua maamuzi mazito ya kuwajenga watanzania kuwa katika level ya kujitegemea wenyewe kifikra, kiutendaji na kitekinolojia ili wawe na uwezo wa kutatua matatizo yao wenyewe, yeye anatafuta urahisi na mtelääemko wa kuindeleza nchi kwa kutumia pesa za wahisani na wawekezaji.

Kwa maneno mengine ni kwamba Rais wetu hataki au tuseme, hana uwezo wa kujipinda kuchukua maamuzi magumu ya kuleta Reforms ambazo zitakuwa chachu ya kuwahamasisha vijana kuwa na uwezo wa kuwaza na kuwa wabunifu kutoa majawabu ya maendeleo yao kwa ku create vitu ambavyo vitawasidia wao wenyewe kwemye maisha yao.

Nimmpe wazo moja la kuijenga nchi. Afanye kama alivyosema; "Yeye awaangalie watendaji wa serikali yake kwa matendo yao na akiona hawa perform ipasavyo, asisite kuchukua maamuzi ya kuwatoa madarakani mara moja na bila huruma yoyote ile kwa kalamu yake. Ikibidi wachukuliwe hatua kali za kisheria kama China." Vinginevyo hii nchi na hili Taifa litakuwa kama DRC na tukifikia hiyo level basi tena haita tawalika.

Wewe ukitaka kujua huyu Rais alivyo na jinsi alivyo kuwa hafuatilii mambo, sikiliza mwenyewe debates za wabunge Bungeni.

Kwa mfano jana, wabunge ambao ni vijana; Mbunge Tweve wa Iringa na Mbunge Judith Kapinga walivyo uliza maswali yao kwa waziri Mkuu Kasim Majaliwa na naibu wa waziri wa TEMISEMI Mh. Ummi Ndeliyananga. Majibu ya waziri Mkuu yalikuwa ni porojo tu ya maneno na hayakuwa majibu yenye substance ambayo sisi tunaweza kuyaamini na kuyategemea, vile vile naibu waziri Mh. Ndeliyananga naye ametoa majibu ambayo ni irrelevant na maswali yaliyo ulizwa.

Hii hali ya kutoa majibu ya ubabaishaji kwa kusoma texts ambazo zimeandikwa na watu wengine, inasikitisha sana kuishuhudia. Hii ni ishara kubwa ya kuelewa na kutambua kuwa Tanzania kwa hivi sasa tuna kiongozi wa aina gani serikalini. Maana kama nchi ina kiongozi ambaye yuko serious na maendeleo ya wananchi wake, hawa mawaziri wasinge pata nafasi ya kutoa maelezo ambayo ni irrelevant kwenye maswali muhimu ya kitaifa. Ni dharau tu iliyo wajaa. Wanafikiri sisi hatuna uwezo wa kuchambua nini kiini na malengo ya maswali yanayo ulizwa.

Mbunge Stela Manyanya wa Nyasa, Mbamba Bay naye aliuliza swali la msingi sana kuhusu barabara ya lami ya km moja kwenye mji mkwonge wa Mbamba Bay, Naibu waziri wa TEMISEMI, Mbunge Silinde, naye amekuja na jibu ambalo unsatisfactory. Yaani serikali inashindwa kujenga barabara za jumla ya km 10 tu ikamaliza tatizo lote la barabara za lami na pavements kwenye huo mji mkwonge, badala yake wana debate kujenga km moja tu ya barabara ya lami. It is disgusting!

Niliona jinsi gani Naibu waziri alivyokuwa anapata shida ya ku figur out thamani ya distance ya km 0.5. Inaelekea hata hiyo Mbamba Bay yenyewe haijui na wala hana hata ile chembe chembe ya idea jinsi huo mji ulivyo na ulivyo kaa.

Yeye anazungumzia Kilosa, Kilosa ni makao makuu ya wilaya lakini mji wenyewe wa Mbamba Bay uko kilometa chache tu kutoka kilosa na ambako ndiyo huko hiyo bandari mpya ya Mbamba Bay inategemewa kujengwa, hatuji lini. Ü

Tatizo ambalo huyu Rais analo, naona anamsikiliza sana Rais Kikwete. Nina uhakika mkubwa kuwa Rais Kikwete ndiyo mentor wake mkubwa. Hawa watu bado wanafikra za kishamba sana za kumdekeza mzungu au mtu mwenye pesa. Wanafikra za kizamani za kudhani mwenye pesa ndiye ataleta maendeleo na ajira kwenye nchi yetu. Kama mambo yangekuwa Rais ki hivyo, nadhani nchi hizo za kizungu, wanazo ziita zimenedelea, wananchi wao wasingekuwa watumwa wa mabepari ambao wamewafuga wenyewe.

Hawa Marais waache tu waendelee kubweteka kwa sababu rasilimali bado zipo. Lakini wajue wanalitengeneza bomu ambalo likilipuka, hapatakuwa na mswalie mtume tena, rasilimali zikikaribia kumalizika. Machafuko yatatapakaa kila sehemu. Hapo ndiyo nadhani watajua wamejifunza nini walichokikosea huko nyuma. Lakini cha kusikitisha ni kwamba wao wenyewe hawatakuwepo, ni vizazi vyo ndivyo vitakavyo hangaika na kuteseka na makosa hayo wanayo yafanya sasa ya kushindwa kuchukua maamuzi mazito.

Amerika na Europe watu wengi wanafanya kazi za kitumwa. Nina uhakika mkubwa siku sio nyingi kama hali itaendelea kuwa hivi, mtapata kusikia mizinga itakayo tokea. Miaka 30 haipiti. Chaos kubwa itatokea Amerika na Europe, kama hakuta kuwa na mabadiliko ya mfumo wa maisha! Watu wana haha ile kishenzi wako karibu kupasuka.

Haya mambo mnayo yasikia na kuyaona wazungu wakiwakataa wageni na kuwaacha wapoteze maisha yao kwenye Mediterranian Sea na kwenye mipaka yao, huo ni mwazo wa dalili za uozo wa System ya maisha waliyo nayo. Sasa hivi ni wageni hasa sisi watu weusi na waislam, lakini watakapo zidi kuona kuwa hata sisi Aliens sio sababu ya matatzo yao, hapo ndipo itajulikana makosa ni ya nani. Itawatafuna wenyewe!

Kazi za msingi nyingi Europe na Amerika hazipo na maisha ya bila kazi hayana matokeo chanya kwa individuals. Msuguano hapo is inevitable!

Hawajajifunza bado!
 
Utakua mgeni nchi hii. Hakuna rais aliyeajiri kwa kipindi kifupi cha miezi 6 tuu zaidi ya watanzania elfu 7 wamepata ajira rasmi serikalini hapo sijazungumzia sector binafsi. Hii haijawahi kutokea tangu tupate uhuru. Suala la kuajiri foreigners hili ni la kisera tuu hata huko marekani na UK wapo watanzania kibao wanafanya kazi. Watanzania tuache uvivu wa kufikiri mama anaupiga mwingi sana.
 

Umesema vyema mkuu
 
Umemelaza kila kitu hapo chini,wewe una dhahabu anayetaka atakuja tu,ukimufuata atakupa mashariti anayotaka yeye.
Rais wetu sijui kadanganywa na Nani tu! Maana aliona kila kitu JPM alivyofanya.
Au wanafikiri alikuwa mwehu.
JPM alikuwa mwehu. Kwa wehu wake ndo maana alitangaza Corona ingeisha kwa sala na dua yaani sala ya msambaa iwe na nguvu kuliko mkatoroki wa Roma?? Yule alikuwa mwehu haswaaaa
 
Maneno meengi pumba tupu,Kikwete anamwongozaje mama??? Ungesema Kassim Majaliwa,Job Ndugai,Mwigulu Nchemba,Paramagamba Kabudi na Alli Hassan Mwinyi hapo ungeeleweka.Chuki binafsi tu zinawasumbua ninyi na ukoo wote wa mwendazake.
 
Maneno meengi pumba tupu,Kikwete anamwongozaje mama??? Ungesema Kassim Majaliwa,Job Ndugai,Mwigulu Nchemba,Paramagamba Kabudi na Alli Hassan Mwinyi hapo ungeeleweka.Chuki binafsi tu zinawasumbua ninyi na ukoo wote wa mwendazake.
Nasikitikia kukuambia kuwa hujaelewa nini kinazungumziwa. Ungejua kijerumani, nafikiri ungenielewa kitu gani namaanisha. Mtafute mtu anaye jua kijerumani ili akutafsirie nini kinazungumzwa kwenye hii clip.


Nasikitika kukuambia kuwa, wewe uko kwenye shimo ambalo huwezi sikia na wala kuelewa nini kinatokea kwenye ulimwengu wa leo. Mawazo na ufahamu wa mitandao ya udaku wa kibongo ndiyo unakufanya ushindwe kuwa na mawazo mapana ya ulimwengu wa leo. Wewe huna tofauti na mtu ambaye ni mfu wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…