Naunga mkono jitihada za kuifungua nchi, ila sikubaliani na approach inayotumika katika kufanya hivyo.
Ni kweli tunahitaji wawekezaji , ni kweli tunahitaji ajira lakini namna tunavyowatafuta na kushirikiana nao sioni hiyo faida inayosemekena itapatikana.
Tunaweka mazingira mazuri ya uwekezaji ndio , at the expense ya kurisk rasilimali zetu lakini tunachokipata hakilingani na risk yenyewe.
Hizo Multinational Corporations ni wazoefu wa kufanya investments katika developed countries, wanajua namna ya kufanya ili kupata faida.
Wanajua udhaifu wa watendaji na viongozi wa developed countries, na pia wana wataalam lukuki wa namna ya kukwepa kodi , hivyo naamini kabisa kuwa hatutaambulia chochote. Historia ni shahidi na tumeona namna Accacia ilivyotufanya over the years.
Moja ya mambo ambayo wawekezaji hao wanayataka ni upatikanaji kwa urahisi kwa Work Permit.
Sasa kama tunataka watanzania wafaidike na hizo ajira sioni namna gani watafaidika nazo kama wageni nao watafurika kupigania hizo nafasi.
Hao wawekezaji ndio hulalamika kuwa watanzania hawaajiriki kwakua ni wezi, hivyo wanapenda kutoa wafanyakazi nje ya nchi sasa kama watanzania ni wezi, kwanini wageni wanapewa nafasi ya kuwekeza katika nchi ya wezi.
Kwakweli sijawahi kuona nchi ikipata maendeleo kwa njia ya uwekezaji wa Taifa jingine.
Kwa Mfano Rais wa Taifa kubwa kabisa lenye uchumi mkubwa marekani , Bwn Trump katika kipindi cha miaka mi nne alisafiri mara 19 tu katika nchi 24 duniani, sasa Rais wetu kwa miezi sita tu anazo safari zaidi ya 6 unaweza ona miaka yake 10 itakua na safari si chini ya mia na zaidi.
Tunapenda nchi yetu iendelee na ifunguke lakini tujadiliane na kuangalia ni namna gani tunaweza kufanya hivyo na tukanufaika, ila binafsi sioni kama kusafiri sana nje ya nchi ndio suluhu, na pia sioni sana kama Direct Foreign Investment ni suluhu tosha.
Nawasilisha.
Umetoa maelezo mazuri sana hata nilitamani kulia. Asante sana kwa mada na maelezo uliyo yatoa. Nakubaliana na wewe 100% kuwa hakuna Taifa lililo endelea kwa ziara ya Rais za nje ya nchi.
Sidhani kama kuna Rais ambaye hivi karibuni amepiga safari za nje nyingi kama Rais wetu mstaafu Kikwete. Yeye atakuwa anevunha Recorde. Nafikiri tumejionea wenyewe jinsi nchi ilivyo poromoka kiuchumi na maisha huko nyuma.
Rais wetu wa sasa hajajifunza na wala kulitambua hilo. Ni Rais ambaye ana fikra na mawazo ambayo yamepitwa na wakati. Yeye badala ya kuchukua maamuzi mazito ya kuwajenga watanzania kuwa katika level ya kujitegemea wenyewe kifikra, kiutendaji na kitekinolojia ili wawe na uwezo wa kutatua matatizo yao wenyewe, yeye anatafuta urahisi na mtelääemko wa kuindeleza nchi kwa kutumia pesa za wahisani na wawekezaji.
Kwa maneno mengine ni kwamba Rais wetu hataki au tuseme, hana uwezo wa kujipinda kuchukua maamuzi magumu ya kuleta Reforms ambazo zitakuwa chachu ya kuwahamasisha vijana kuwa na uwezo wa kuwaza na kuwa wabunifu kutoa majawabu ya maendeleo yao kwa ku create vitu ambavyo vitawasidia wao wenyewe kwemye maisha yao.
Nimmpe wazo moja la kuijenga nchi. Afanye kama alivyosema; "Yeye awaangalie watendaji wa serikali yake kwa matendo yao na akiona hawa perform ipasavyo, asisite kuchukua maamuzi ya kuwatoa madarakani mara moja na bila huruma yoyote ile kwa kalamu yake. Ikibidi wachukuliwe hatua kali za kisheria kama China." Vinginevyo hii nchi na hili Taifa litakuwa kama DRC na tukifikia hiyo level basi tena haita tawalika.
Wewe ukitaka kujua huyu Rais alivyo na jinsi alivyo kuwa hafuatilii mambo, sikiliza mwenyewe debates za wabunge Bungeni.
Kwa mfano jana, wabunge ambao ni vijana; Mbunge Tweve wa Iringa na Mbunge Judith Kapinga walivyo uliza maswali yao kwa waziri Mkuu Kasim Majaliwa na naibu wa waziri wa TEMISEMI Mh. Ummi Ndeliyananga. Majibu ya waziri Mkuu yalikuwa ni porojo tu ya maneno na hayakuwa majibu yenye substance ambayo sisi tunaweza kuyaamini na kuyategemea, vile vile naibu waziri Mh. Ndeliyananga naye ametoa majibu ambayo ni irrelevant na maswali yaliyo ulizwa.
Hii hali ya kutoa majibu ya ubabaishaji kwa kusoma texts ambazo zimeandikwa na watu wengine, inasikitisha sana kuishuhudia. Hii ni ishara kubwa ya kuelewa na kutambua kuwa Tanzania kwa hivi sasa tuna kiongozi wa aina gani serikalini. Maana kama nchi ina kiongozi ambaye yuko serious na maendeleo ya wananchi wake, hawa mawaziri wasinge pata nafasi ya kutoa maelezo ambayo ni irrelevant kwenye maswali muhimu ya kitaifa. Ni dharau tu iliyo wajaa. Wanafikiri sisi hatuna uwezo wa kuchambua nini kiini na malengo ya maswali yanayo ulizwa.
Mbunge Stela Manyanya wa Nyasa, Mbamba Bay naye aliuliza swali la msingi sana kuhusu barabara ya lami ya km moja kwenye mji mkwonge wa Mbamba Bay, Naibu waziri wa TEMISEMI, Mbunge Silinde, naye amekuja na jibu ambalo unsatisfactory. Yaani serikali inashindwa kujenga barabara za jumla ya km 10 tu ikamaliza tatizo lote la barabara za lami na pavements kwenye huo mji mkwonge, badala yake wana debate kujenga km moja tu ya barabara ya lami. It is disgusting!
Niliona jinsi gani Naibu waziri alivyokuwa anapata shida ya ku figur out thamani ya distance ya km 0.5. Inaelekea hata hiyo Mbamba Bay yenyewe haijui na wala hana hata ile chembe chembe ya idea jinsi huo mji ulivyo na ulivyo kaa.
Yeye anazungumzia Kilosa, Kilosa ni makao makuu ya wilaya lakini mji wenyewe wa Mbamba Bay uko kilometa chache tu kutoka kilosa na ambako ndiyo huko hiyo bandari mpya ya Mbamba Bay inategemewa kujengwa, hatuji lini. Ü
Tatizo ambalo huyu Rais analo, naona anamsikiliza sana Rais Kikwete. Nina uhakika mkubwa kuwa Rais Kikwete ndiyo mentor wake mkubwa. Hawa watu bado wanafikra za kishamba sana za kumdekeza mzungu au mtu mwenye pesa. Wanafikra za kizamani za kudhani mwenye pesa ndiye ataleta maendeleo na ajira kwenye nchi yetu. Kama mambo yangekuwa Rais ki hivyo, nadhani nchi hizo za kizungu, wanazo ziita zimenedelea, wananchi wao wasingekuwa watumwa wa mabepari ambao wamewafuga wenyewe.
Hawa Marais waache tu waendelee kubweteka kwa sababu rasilimali bado zipo. Lakini wajue wanalitengeneza bomu ambalo likilipuka, hapatakuwa na mswalie mtume tena, rasilimali zikikaribia kumalizika. Machafuko yatatapakaa kila sehemu. Hapo ndiyo nadhani watajua wamejifunza nini walichokikosea huko nyuma. Lakini cha kusikitisha ni kwamba wao wenyewe hawatakuwepo, ni vizazi vyo ndivyo vitakavyo hangaika na kuteseka na makosa hayo wanayo yafanya sasa ya kushindwa kuchukua maamuzi mazito.
Amerika na Europe watu wengi wanafanya kazi za kitumwa. Nina uhakika mkubwa siku sio nyingi kama hali itaendelea kuwa hivi, mtapata kusikia mizinga itakayo tokea. Miaka 30 haipiti. Chaos kubwa itatokea Amerika na Europe, kama hakuta kuwa na mabadiliko ya mfumo wa maisha! Watu wana haha ile kishenzi wako karibu kupasuka.
Haya mambo mnayo yasikia na kuyaona wazungu wakiwakataa wageni na kuwaacha wapoteze maisha yao kwenye Mediterranian Sea na kwenye mipaka yao, huo ni mwazo wa dalili za uozo wa System ya maisha waliyo nayo. Sasa hivi ni wageni hasa sisi watu weusi na waislam, lakini watakapo zidi kuona kuwa hata sisi Aliens sio sababu ya matatzo yao, hapo ndipo itajulikana makosa ni ya nani. Itawatafuna wenyewe!
Kazi za msingi nyingi Europe na Amerika hazipo na maisha ya bila kazi hayana matokeo chanya kwa individuals. Msuguano hapo is inevitable!
Hawajajifunza bado!