Hakuna tajiri aliyekuwa tajiri kwa kuomba kwa Mungu apewe utajiri

Hakuna tajiri aliyekuwa tajiri kwa kuomba kwa Mungu apewe utajiri

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Siri ya kufanikiwa kiuchumi ni kuenenda katika HAKI!

Kwenye Biblia hakuna tajiri yeyote aliyemuambia Mungu "naomba unipe utajiri" na akapata, never na sijaona andiko hilo kwa mwenye nalo alilete.

Wajanja walishaachaga kuomba utajiri. Kumbuka, Ufalme wa Mungu hutekwa na WENYE NGUVU NA MAARIFA. Yatafute sana maarifa.

Mkristo na hata Muislam hutakiwi kuomba utajiri wala mafanikio ya mwili. Ombea adui zako, fanya kazi kwa maarifa na uyatafute popote yatakapopatikana. Narudia, popote yatakapopatikana.

Mungu anajua wewe unahitaji nini! Anakujua kuliko unavyojijua. Anajua haja ya moyoni mwako.

Tembea humo humo ili baraka zake ndizo zikupe utajiri. Naam, baraka za kuishika haki na kuifuata.

Kamwe usiombe Mungu akupe sijui mavazi mazuri[emoji38], magari, hela n.k[emoji10]

Wewe fanya aliyoyaagiza tu utaona mambo yatakavyojipa. Huna haja ya kumpigia kelele kumuomba hela!

Tafuta sana neno la kweli lililofichwa karne na karne, na baadhi ya hawa Wachungaji na uanze kuliishi, narudia, NENO LA KWELI.

Chukua hiyo!
 
Kuna watu Toka hawajazaliwa wameumbwa kuwa masikini maana Mungu amesema nakujua toka kuzaliwa kwako mpaka kufa kwako.

Je utafanyaje kupindua Meza?

Roga Baba😅😅😅
😅😅😅😅aroge
 
Kuna watu Toka hawajazaliwa wameumbwa kuwa masikini maana Mungu amesema nakujua toka kuzaliwa kwako mpaka kufa kwako.

Je utafanyaje kupindua Meza?

Roga Baba[emoji28][emoji28][emoji28]

Ogopa matapeli na maandiko ya uongo. Kaa nayo mbali. Hayo ni ya kukatisha watu tamaa kwa agenda maalumu.
 
hata wewe hatujathibitisha kama upo
Sawa, hoja hapa ni Mungu, si mimi.

Hata kama mimi sipo, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Hata kama mimi nipo, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Habari ya mimi kuwapo au kutokuwapo ni moot, haina mashiko.

Logical non sequitur. Unachanganya madawa.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Back
Top Bottom