Hakuna timu yeyote Barani Africa inayotamani kukutana na hii Simba ya Steve Barker

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
4,994
Reaction score
9,625
Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.

Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.

Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
 
Steve Barker ametengeneza timu ya simba ambayo ina moto wanaoanza na wanaomaliza wote wakali. Timu ipo kiushindani kila mchezaji anapambania namba. Kitu ambacho wanasimba tulikikosa kwa muda mrefu sana. Pia timu imekuwa ni yenye kasi inaposhambulia na inapozuia.

Pongezi ziende kwanza kwa Muumba kisha zifike kwa tajiri Mo na viongozi wote wa Simba ikiwemo na kamati ya Usajili pamoja na benchi zima la ufundi linaloongozwa na Sir Steve Barker na wachezaji kwa ujumla.
 
Suala la muda tu, hawa home ni home na away ni home sio kipimo sahihi.
 
Lipo wazi, SIMBA Ana Timu Na Kocha Mzuri, Cha Msingi Dirisha Dogo Atafutwe Namba 9 Kariba la Fiston Mayele ili Asaidiane na Doumbia.... Oyaah SIMBA Mtatisha Sanaa...!!!
 
Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.

Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.

Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
AMINA
 
Unajisifu Una timu na hujamtoa pyramid,RS berkane,au mamelodi pumbafu kabisa,ubora WA timu haupimwi kwenye hizi hatua uchwara ambazo hata top scorer hawahesabiikwenye hizi hatua
 
Ni kweli Simba ina kocha mzuri na timu nzuri sana lakini ni kwenye ligi ya ndani na hatua hizi za mwanzoni za CL. Lakini itakapofika makundi kuna vitu/ madhaifu ya msingi sana ya kufanyiwa kazi haraka sana hasa wakati wa dirisha dogo.
1. Golikipa - Huyu akumbushwe mambo mawili ya msingi. Apunguze kukaa off position rejea goli la Sele Bwenzi. Akiendelea kufanya hivyo ajue kabisa anajiweka katika hatari ya kukutana na balaa kwenye makundi ya CL. Pia ana footwork mbovu sana halafu anapenda kukaa na mpira mpaka adui afike ndio atoe pasi. Hii ni hatari sana kwani inapoelekea Simba inaenda kukutana na wakubwa wenziwe. Na zaidi akumbushwe aache kupoteza muda kijinga. Huwa anadaka mpira akiwa hajaguswa na mtu halafu anajiangusha kufeki kuwa kaumia. Na wakati mwingine unakuta anafanya hivyo wakati Simba ndio anaongoza kwa margin kubwa mpaka unabaki unashangaa. Matokeo yake huwa anaishia kupata kadi zisizo na msingi.
2. Kiungo mkabaji namba 6. Anahitajika kiungo wa shoka kusaidiana na Kagoma hasa kwenye zile mechi za ugenini za kushika bomba. Anahitajika kiungo atakayefanya kazi mbili kwa wakati mmoja kupora mipira na wakati huo huo aipandishe timu haraka ili iweze kushambulia kwa kushtukiza (counter attack). Kagoma uwezo wake ni mmoja tu kuzuia basi lakini hana uwezo wa kuipandisha timu kwa haraka.
3. Mshambuliaji namba 9. Kama kweli viongozi na mfadhili wa Simba wanamaanisha kuwa wanataka kuleta kombe la Afrika basi wasajili mshambuliaji namba tisa mwenye uwezo binafsi wa kubadilisha matokeo kama alivyo Mayele. Hii ya kusema kuwa unataka kuleta kombe la Afrika halafu mshambuliaji kinara ni Doumbia hii ni propoganda na kujidanganya wenyewe. Mfano mzuri mechi ya leo mwanzoni jamaa walicheza kwa nguvu sana kukawa na migongano kiasi Mpanzu alipotea kabisa. Kama jamaa wangeendela na uchuzaji ule ule basi leo false no. 9 isingefanya kazi kabisa. Ilihitajika awepo namba tisa wa kugonga na wale mabeki wa kati wa De agosto
4. Rushne ni beki mzuri sana hilo halina ubishi hata kidogo. Lakini mapungufu yake makubwa ni kupenda kukaa sana na mpira mguuni kwake wakati mwingine bila hata sababu za msingi wakati wenzake wameshafungua na wanauomba huo mpira.

Kwa sasa Simba wana kocha wa viwango sana na wahakikishe wanamlinda kweli kweli ikiwezekana kwa miaka mitatu ijayo lazima atawaletea kombe kubwa tu. Kikubwa kwa kuanzia dirisha dogo wamsaidie azibe hayo madhaifu matatu hapo juu. Mengine wamwachie afanye kazi kwa uhuru kutengeneza mifumo yake uwanjani.

Ni mtizamo tu.
 
Naunga mkono hoja.
 
Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.

Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.

Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
Kwa timu zipi mlizocheza nazo? Tunasubiri muanze kulia kuwa Mangungu hafai.
 
Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.

Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.

Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
Memelod ameiona isiwe tabu.
Amekimbia
 
Back
Top Bottom