Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
AMINANimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.
Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.
Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
Naunga mkono hoja.Ni kweli Simba ina kocha mzuri na timu nzuri sana lakini ni kwenye ligi ya ndani na hatua hizi za mwanzoni za CL. Lakini itakapofika makundi kuna vitu/ madhaifu ya msingi sana ya kufanyiwa kazi haraka sana hasa wakati wa dirisha dogo.
1. Golikipa - Huyu akumbushwe mambo mawili ya msingi. Apunguze kukaa off position rejea goli la Sele Bwenzi. Akiendelea kufanya hivyo ajue kabisa anajiweka katika hatari ya kukutana na balaa kwenye makundi ya CL. Pia ana footwork mbovu sana halafu anapenda kukaa na mpira mpaka adui afike ndio atoe pasi. Hii ni hatari sana kwani inapoelekea Simba inaenda kukutana na wakubwa wenziwe. Na zaidi akumbushwe aache kupoteza muda kijinga. Huwa anadaka mpira akiwa hajaguswa na mtu halafu anajiangusha kufeki kuwa kaumia. Na wakati mwingine unakuta anafanya hivyo wakati Simba ndio anaongoza kwa margin kubwa mpaka unabaki unashangaa. Matokeo yake huwa anaishia kupata kadi zisizo na msingi.
2. Kiungo mkabaji namba 6. Anahitajika kiungo wa shoka kusaidiana na Kagoma hasa kwenye zile mechi za ugenini za kushika bomba. Anahitajika kiungo atakayefanya kazi mbili kwa wakati mmoja kupora mipira na wakati huo huo aipandishe timu haraka ili iweze kushambulia kwa kushtukiza (counter attack). Kagoma uwezo wake ni mmoja tu kuzuia basi lakini hana uwezo wa kuipandisha timu kwa haraka.
3. Mshambuliaji namba 9. Kama kweli viongozi na mfadhili wa Simba wanamaanisha kuwa wanataka kuleta kombe la Afrika basi wasajili mshambuliaji namba tisa mwenye uwezo binafsi wa kubadilisha matokeo kama alivyo Mayele. Hii ya kusema kuwa unataka kuleta kombe la Afrika halafu mshambuliaji kinara ni Doumbia hii ni propoganda na kujidanganya wenyewe. Mfano mzuri mechi ya leo mwanzoni jamaa walicheza kwa nguvu sana kukawa na migongano kiasi Mpanzu alipotea kabisa. Kama jamaa wangeendela na uchuzaji ule ule basi leo false no. 9 isingefanya kazi kabisa. Ilihitajika awepo namba tisa wa kugonga na wale mabeki wa kati wa De agosto
4. Rushne ni beki mzuri sana hilo halina ubishi hata kidogo. Lakini mapungufu yake makubwa ni kupenda kukaa sana na mpira mguuni kwake wakati mwingine bila hata sababu za msingi wakati wenzake wameshafungua na wanauomba huo mpira.
Kwa sasa Simba wana kocha wa viwango sana na wahakikishe wanamlinda kweli kweli ikiwezekana kwa miaka mitatu ijayo lazima atawaletea kombe kubwa tu. Kikubwa kwa kuanzia dirisha dogo wamsaidie azibe hayo madhaifu matatu hapo juu. Mengine wamwachie afanye kazi kwa uhuru kutengeneza mifumo yake uwanjani.
Ni mtizamo tu.
labda bingwa wa kukata viunoMwisho wa msimu
YANGA BINGWA
Kwa timu zipi mlizocheza nazo? Tunasubiri muanze kulia kuwa Mangungu hafai.Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.
Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.
Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia
Memelod ameiona isiwe tabu.Nimeutazama huu moto wa timu ya Simba sc ulionao sasa, nikiri wazi kuwa hakuna timu barani afrika inayotamani kukutana na hii Simba sc.
Mpaka sasa tumeshafuzu makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Na ndoto na Shauku yetu kuutwaa huu ubingwa na kuweka historia kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kuutwaa huu Ubingwa.
Nguvu tunayo, Ari tunayo na timu tunayo pia