Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden

Watu hawaelewi kwa vile hawana experience ya kusafiri au kukaa hizi nchi zilizoendelea. Kwani nini cha ajabu kwa viongozi kupanda bus, trams au trains/subways? Ebu waafrika muwe wastaarabu, au kwa sababu mmezoea corruptions. Maisha ni ku-simplify. Ya nini kufanya maisha yawe complex? Paskali, asante kwa andiko lako.
 
Atasoma post yako huko aliko atakuelewa
 
You nailed it !! Mujica wa Uruguay alikuwa anatembelea Volkswagen Beetle na bado haikuondoa hadhi yake ya URais wa Nchi !!
 
Lakini pascal ukubali tulihudhuria kama makoloni yao tulihudhuria like everybody else
 
Mkuu sio kwamba watu ni wajinga hawafahamu mambo yote hayo unayoyasema wewe hapana.

Bali wanawakumbusha watawala wetu kuwa wao ni watu wa kawaida tu kama sisi.

Ili wakati mwingine wakumbuke kutupa na sisi hadhi tunayostahili.

Ni hayo tu.
 
Wewe nawe umesoma ulichoandika?
Tunakemea matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi… hili neno logistic ndio unaona umeeleza vizuri… hebu ondoeni huu upulusi wenu
Eti waafrika wanakuza mambo… ok tunakuza kwahiyo next….
Unajua walipa kodi wa uingereza wameidhinisha kiasi gani cha paundi zitumike kwa ajili ya huo msiba?. Unaujua umuhimu wa Queen Elizabeth na ukubwa aliokuwa nao maishani mwa waingereza?.
 
Wapo nje ya nchi mkuu, kumbuka Clinton alipandishwa ndani ya coaster hapa Dar tena akiwa rais wa USA.

Hakuna mmarekani alichukulia nongwa suala hilo, hakuna aliyelifanya kama vile ni big deal.
 
Naunga mkono Hoja, wanaoshadadia hili hawana uelewa au hawautaki huo uelewa wanaona kama dharau while it is not! KILA rais angeenda na msafara wake Huko kungekalika? Ule ni Msiba sio ziara ya Rais!
Mnachanganya mambo sana, kwenye msiba wa Jana hakukuwa na maraisi wengi kulinganisha na mikutano ya UN. Ila issue Ni utaratibu tu ambao wenyewe uingereza wameweka na sioni shida ya hilo. Ila pia wangeweza kuwapa magari napo kusingekua na shida yoyote.

Mikutano ya UN inakusanya maraisi wengi duniani na wote hupewa magari, hivyo Ni jambo la utaratibu tu
 
Pascal umetetea kwa nguvu zako zote, umeenda mbali zaidi kwa kutoa mifano uliiyoishuhudia na kuiishi.
Pamoja na maelezo yote hayo ya kuwa kawaida bado hujatuambia ni kwa nini hawa marais wetu watendewe kama miungu watu wawapo hapa nchini?
Kwanini walindwe na mabunduki? Kwa nini wasipande mwendokasi kwenda kuzika Mabwepande au Mpitimbi?
Miaka ya 80/90 Mzee Ruksa akiwa Sweden ugenini, waswede hawakumruhusu mpambe wake kukaribia meza kuu kwa kuwa hakukuwa na ulazima huo maana kiongozi alikuwa mahali salama, kwa nini hapa kwetu kiongozi aonekane kuwa wapili kutoka kwa Mungu wakati sisi ndio tuliompa mamlaka? 🤔
 
KUMBE UMEONA TENA RAIS SAMIA ANAENEA KWENYE SEAT YA BUS VIZURI TU. Kuanzia sasa mabus yaanze kutumika kubeba viongozi na kupunguza msafara toka magari60+ mpaka makari 5
 
KUMBE UMEONA TENA RAIS SAMIA ANAENEA KWENYE SEAT YA BUS VIZURI TU. Kuanzia sasa mabus yaanze kutumika kubeba viongozi na kupunguza msafara toka magari60+ mpaka makari 5
Tena mama yetu hana nongwa ndo kwanza anacheka tu na kujaribu kujiziba uso. I love our president 😁😁😁
 
Bila picha ya huko Sweden hii ni chai tu
 
Wakili Msomi kwa nini katika ziara zao sa ndani mi-vieite 50 Huwa inasindikizana?
 
Sijui kwanini wana CCM mmejipambanua kuwa watu wa kuitetea serikali na kuwananga wananchi, mnajua malengo ya chama from the first place??

Watu hawashangai hayo mnayodhani wanashangaa, infact wanawakejeli kama ninyi mnavyowakejeli na kuwaita wajinga na washamba.

Mnahamisha mjadala wa msingi kwamba kumbe inawezekana kubana matumizi na kupunguza kadhia tunayosababishiwa na viongozi wetu kwa kupunguza misafara?

Acheni kuhamisha magoli.
 
Uncle mayalla unajua watu wanakuheshimu? Acha nyuzi za kishamba sasa, Hawa jamaa hata uwatetee vp watakuchinja tuu, wajifunze kubana matumizi wakija huku Africa Kama Wana akili lakini.

Pili sio ushamba kutoa mtazamo wa picha ya Marais wakiwa kwenye basi[emoji23], Bali ushamba ni kumuona atoaye maoni kakosea utadhani wote mna akili moja.

In short ni kwamba wameyumba sana
 
Kumbe hii habari ni ya kitambo sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…