Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden

Ni kweli kabisa, lakini huu ushamba wetu unatokana ni viongozi wetu kujikuza sana. Hao wanaoendesha baiskeli kwenda kazini ni hao wazungu. Hao hata wakipanda basi hatuta shangaa. Kutoka kwenye msafara wa magari 100 mpaka kupanda basi! Lazima washamba tutakuwa wengi.
 
Mkuu Pascal Mayalla ijapokuwa linaweza kuwa jambo la kawaida lakini 'reaction' iliyoonyeshwa na wengi tusiiite ni ushamba bali ni kujitambua.. Ni vyema mjadala ukaendelea sehemu mbalimbali kwani hata nchi nyingine za Africa kama Kenya ,SA n.k. mjadala huu bado unapamba moto.
Pia watu wengi waliona jinsi viongozi wetu walivyokuwa 'uncomfortable' wakati wakiwa katika hizo 'commuter'..
Huu utakuwa mwanzo wa kupenda vya kwetu na kukazana kujitegemea kiuchumi na kuungana kama Afrika ..
Ijapokuwa UK ilikuwa inafuata itifaki yao ya mazishi ya Kifalme na Viongozi wetu walijulishwa kutoka mwanzo kuwa hawataweza kwenda kwenye mazishi na magari yao.. kwa hiyo walikuwa na uchaguzi wa kwenda au kutuma wawakilishi 🙁
 
Hata msiba wa Nyeyere...Marais waliokuja hapa walipandishwa basi moja....ushamba kweli ni tatizo Kwa watoto hawa ambao ndo wameanza tumia smartphone siku hizi
 

Marais wa Afrika wakikwea daladala kuhudhuria mazishi ya Malkia Eliza.
Tunashukuru mama yetu Samia alipata siti. Ya dirishani! Kwa kutumia uzoefu wake na mafundisho ya kukwea basi enzi hizo akiwa shule jkt na chuo.
Akiwashangaza marais wenzake hasa wanaume kama Ruto Ramadhosa na rais wa Malaysia
 
Viongozi wetu wakiwa nchini wanaogopa wananchi wao wanapita kwa kukimbia barabarani kama wanakimbizwa .
 
Viongozi wetu wakiwa nchini wanaogopa wananchi wao wanapita kwa kukimbia barabarani kama wanakimbizwa .
Sababu?
Je wanaiba maliasili na rasilimali sana?
Wanawanyima haki zao za msingi?
Wanaishi kama miungu mitu?
Wanawatumia kama watumwa?
Ebu nipe jibu mkuu...
 
Mi nafikiri wengi hawajaelewa kinachofanya wabongo,Waafrika kushangazwa na kufurahi viongozi wao walivyolazimishwa kuwa "humble ndani ya kimbinyiko"
Ipo hv,kama watu wale wale,wapo ulaya wamepandishwa basi,ishu ya usalama haikuwepo,inakuwaje huku bongo,Afrika,waziri,naibu waziri,mkurugenzi hawawezi kupanda gari moja hata kama wnatoka ofc moja kwenda eneo moja kufanya uzinduzi!?kila mtu anataka avimbe kwenye vieite yake!!!sasa ukija huku juu,PM,makamu,na Raisi misafsra yao huwa na magari zaidi ya 50!!hata kama wanaenda kuzindua choo!!
Sasa kitendo Cha wazungu kuwalazimisha hawa wajuba kukwea basi moja,bila kujali kuvimba kwao,kimetuthibitishia,kumbe ni wakawaida tu,hawana maajabu,ile misafara ya V8 100,huwa ni mbwembwe tu!!hakuna Cha usalama Wala nini,
Kama ni Swala la usalama hata huko ulaya sio salama kivyo,911 imetokea US,UK watu walilipuwa train!
Cha msingi,tulizani,Viongozi wetu wakitumia magari machache kwenye misafara,watapata "mafuta"sasa wazungu wametuonyesha sio kweli,unaweza kuwalundika kwenye mabasi,na mambo yakawa poa,kumbe swaga za nyumbani ni mbwembwe tu.
Mnaosema kupanda mabasi ni kawaida,mbona bongo hawapandi mabasi?,badala ya kuwaita wananchi washamba,waulizeni hao vongozi wa Afrika
 

Kwa taarifa yako wala sio ushamba bali kilichofanyika ni kuwabeza viongozi wetu kwani wakiwa huku kwetu Afrika kwenye lindi la umasikini, hujifanya miungu watu. Utawaona na misafara mirefu yenye magari mengi na ulinzi kama wameingia madarakani kwa kupindua nchi! Kama inawezekana kupakia mabus, ule msururu wa ma VX huwa ni wa nini? Sio mara moja au mbili huwa tunasema misururu ya viongozi wetu ni ufujaji wa kodi za wananchi, je wamewahi kusikia? Kilichofanyika huko UK ni somo kuwafikia kwa vitendo hao majizi ya kura.
 
Naomba kuuliza ,hivi Biden alishea basi na mama?
Kama hujui kwanini Rais wa Marekani na Ufaransa walitumia usafiri tofauti basi hujui siasa na mienendo ya usalama kimataifa.
Rais wa USA akienda nchi yoyote anasafiri na msafara wake na magari yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…