Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden

Hakuna ubaya wowote wala ajabu yoyote Marais kupanda pamoja! Tulipanda basi moja na Rais Mkapa nchini Sweden

Ni kweli kabisa, lakini huu ushamba wetu unatokana ni viongozi wetu kujikuza sana. Hao wanaoendesha baiskeli kwenda kazini ni hao wazungu. Hao hata wakipanda basi hatuta shangaa. Kutoka kwenye msafara wa magari 100 mpaka kupanda basi! Lazima washamba tutakuwa wengi.
 
Mkuu Pascal Mayalla ijapokuwa linaweza kuwa jambo la kawaida lakini 'reaction' iliyoonyeshwa na wengi tusiiite ni ushamba bali ni kujitambua.. Ni vyema mjadala ukaendelea sehemu mbalimbali kwani hata nchi nyingine za Africa kama Kenya ,SA n.k. mjadala huu bado unapamba moto.
Pia watu wengi waliona jinsi viongozi wetu walivyokuwa 'uncomfortable' wakati wakiwa katika hizo 'commuter'..
Huu utakuwa mwanzo wa kupenda vya kwetu na kukazana kujitegemea kiuchumi na kuungana kama Afrika ..
Ijapokuwa UK ilikuwa inafuata itifaki yao ya mazishi ya Kifalme na Viongozi wetu walijulishwa kutoka mwanzo kuwa hawataweza kwenda kwenye mazishi na magari yao.. kwa hiyo walikuwa na uchaguzi wa kwenda au kutuma wawakilishi 🙁
 
Hata msiba wa Nyeyere...Marais waliokuja hapa walipandishwa basi moja....ushamba kweli ni tatizo Kwa watoto hawa ambao ndo wameanza tumia smartphone siku hizi
 
Screenshot_20220920-234812.png

Marais wa Afrika wakikwea daladala kuhudhuria mazishi ya Malkia Eliza.
Tunashukuru mama yetu Samia alipata siti. Ya dirishani! Kwa kutumia uzoefu wake na mafundisho ya kukwea basi enzi hizo akiwa shule jkt na chuo.
Akiwashangaza marais wenzake hasa wanaume kama Ruto Ramadhosa na rais wa Malaysia
 
Sawa tunakubali kaka. Siye tumeona yawezekana viongozi wetu wanaweza bana matumizi kwenye shughuli kama hizo. Iwe mikutano ya chama. Kumpokea rais kutoka nje. Na hafla nyingine zozote kubwa. Yawezekana wakakwea hiace. Coaster na hata daladala. Kumbuka nchi yetu maskini wa kutupa. Kuna ubaya gani viongozi wetu wenye weledi wakaamuwa kufanya hivyo kama ulaya?

Ya nini kumpa shida zaidi mlalahoi wakati yawezekana?
Viongozi wetu wakiwa nchini wanaogopa wananchi wao wanapita kwa kukimbia barabarani kama wanakimbizwa .
 
Viongozi wetu wakiwa nchini wanaogopa wananchi wao wanapita kwa kukimbia barabarani kama wanakimbizwa .
Sababu?
Je wanaiba maliasili na rasilimali sana?
Wanawanyima haki zao za msingi?
Wanaishi kama miungu mitu?
Wanawatumia kama watumwa?
Ebu nipe jibu mkuu...
 
Wanabodi

Hii issue ya Rais Samia kupandishwa basi moja na viongozi wengine wa Africa kwenye mazishi ya Malkia, imegubikwa maneno mengi, ujuaji mwingi, na kujua kwingi, lakini ukweli wennyewe halisi, tatiza ni ushamba tuu mwing zaidi ya uhalisia!. Watu wakimuona Rais lazima apande benzi na kutembea na msafara, basi wanadhani rais akipanda basi anakuwa sio rais au amedharauliwa!. Nini basi, watu tumewaona marais wanatembea kwa miguu na wengine wanatumia baiskeli kwenda kazini!

Natoa wito kwa sisi Wabongo tupunguze ushamba jameni!, hakuna kitu cha ajabu yoyote kwa viongozi kupanda usafiri wa pamoja wa basi as long as issue za kiusalama zimezingatiwa.

Mwaka 1998, Katika ziara yake nchini Sweden, rais Benjamin Mkapa na ujumbe wake na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Sweden, na sisi waandishi wa habari, wote tulipanda basi moja kutoka Stockholm kwenda Uppsala. Hivyo ni jambo la kawaida sana, when in Rome, do as the Romans does! Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Mwaka 1995 tulisafiri ndege moja na Waziri Mkuu Fredric Sumaye, kwenda South aboard Alliance Air. Ndege ikafika few minutes ahead of schedule, hivyo kushuka abiria wote mnaingia kwenye zile basi trums za airport, hivyo tukashuka na Sumaye na mkewe na walinzi wote kwenye basi na halina siti!, hivyo tunapanda basi moja na Waziri Mkuu wa nchi yako halafu anashika mchuma!

Ile trum inaondoka ndipo motorcade ya kumpokea inaingia hapo uwanjani, huku balozi Ami Mpungwe behind the stearing wheel akiendesha mwenyewe, anashuka na kupungia mkono trum lisimame, ndipo Waziri Mkuu wetu na msafara wake wakaachia mchuma na kupokelewa!

Kiukweli sisi wabongo kwa kushadadia mambo madogo madogo yasiyo na maana yoyote!, nilidhani watu wangenote organization ya msiba, watu wanavyolia kizungu! Hakuna watu kughalaghala na kukanyagana, hakuna Red Cross walio busy kubeba watu waliozimia.

Misiba TV zetu huku misiba ya viongozi ni nyimbo za maombolezo, TV za wenzetu msiba wa kiongozi ni documentaries za her legacy!. Full time ni interviews kumhusu Malkia, sikuona kiongozi yoyote akihojiwa hata Waziri Mkuu wao!, huku ni mihotuba na mihotuba ya viongozi kuchoshana tuu bure!

Msafara wa mwili just 5 cars piki piki tatu mbele, mbili nyuma, ingekuwa ni huku!. Kunapotokea misiba kama hii, ya wenzetu walio staarabika, we should use them as a learning experience, sisi tunashikia bango rais wetu kupanda basi as if Mama Samia ni katope, angeyeyuka!

Mbona viongozi kupanda mabasi ya pamoja ni kawaida, hili jambo linafanyika kila siku kwenye mikutano ya nchi za Jumuiya ya Madola and in fact its a good thing viongozi wana ji mix na ku mingle!

Hata siku ya Uhuru pale uwanja wa taifa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, wanakuja pale Karimjee wanakuwa dropped off, kisha wanapanda usafiri wa pamoja, wanapelekwa uwanja wa Taifa na mabasi maalum, baada ya shughuli mabasi yanawarudisha Karimjee ndipo kila mmoja anapeperusha tena bendera yake kwenye magari yao!

Kipi cha ajabu jameni?, ushamba ukizidi nao ni issue. Natoa wito kwa Venus Nyota, fanya utaratibu wa kusafiri na few private media ili wakati wewe unatuma press release za hard news, hao private media watume color stories, Watanzania wapatiwe exposure na wajue mambo mengine ya mambo ya kimataifa.

Paskali

Rejea Ukiwa Rais katika nchi za Kiafrika unapewa utukufu uliopitiliza
Mi nafikiri wengi hawajaelewa kinachofanya wabongo,Waafrika kushangazwa na kufurahi viongozi wao walivyolazimishwa kuwa "humble ndani ya kimbinyiko"
Ipo hv,kama watu wale wale,wapo ulaya wamepandishwa basi,ishu ya usalama haikuwepo,inakuwaje huku bongo,Afrika,waziri,naibu waziri,mkurugenzi hawawezi kupanda gari moja hata kama wnatoka ofc moja kwenda eneo moja kufanya uzinduzi!?kila mtu anataka avimbe kwenye vieite yake!!!sasa ukija huku juu,PM,makamu,na Raisi misafsra yao huwa na magari zaidi ya 50!!hata kama wanaenda kuzindua choo!!
Sasa kitendo Cha wazungu kuwalazimisha hawa wajuba kukwea basi moja,bila kujali kuvimba kwao,kimetuthibitishia,kumbe ni wakawaida tu,hawana maajabu,ile misafara ya V8 100,huwa ni mbwembwe tu!!hakuna Cha usalama Wala nini,
Kama ni Swala la usalama hata huko ulaya sio salama kivyo,911 imetokea US,UK watu walilipuwa train!
Cha msingi,tulizani,Viongozi wetu wakitumia magari machache kwenye misafara,watapata "mafuta"sasa wazungu wametuonyesha sio kweli,unaweza kuwalundika kwenye mabasi,na mambo yakawa poa,kumbe swaga za nyumbani ni mbwembwe tu.
Mnaosema kupanda mabasi ni kawaida,mbona bongo hawapandi mabasi?,badala ya kuwaita wananchi washamba,waulizeni hao vongozi wa Afrika
 
Wanabodi

Hii issue ya Rais Samia kupandishwa basi moja na viongozi wengine wa Afrika kwenye mazishi ya Malkia, imegubikwa maneno mengi, ujuaji mwingi, na kujua kwingi, lakini ukweli wennyewe halisi, tatiza ni ushamba tuu mwingi zaidi ya uhalisia!. Watu wakimuona Rais lazima apande benzi na kutembea na msafara, basi wanadhani Rais akipanda basi anakuwa sio Rais au amedharauliwa!. Nini basi, watu tumewaona marais wanatembea kwa miguu na wengine wanatumia baiskeli kwenda kazini!

Natoa wito kwa sisi Wabongo tupunguze ushamba jameni!, hakuna kitu cha ajabu yoyote kwa viongozi kupanda usafiri wa pamoja wa basi as long as issue za kiusalama zimezingatiwa.

Mwaka 1998, Katika ziara yake nchini Sweden, rais Benjamin Mkapa na ujumbe wake na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Sweden, na sisi waandishi wa habari, wote tulipanda basi moja kutoka Stockholm kwenda Uppsala. Hivyo ni jambo la kawaida sana, when in Rome, do as the Romans does! Misafara ya viongozi inachosha, inatesa na kurudisha nyuma maendeleo, IGP Sirro peleka Traffic Sweden kujifunza misafara ya wenzetu, Time is Money!

Mwaka 1995 tulisafiri ndege moja na Waziri Mkuu Fredric Sumaye, kwenda South aboard Alliance Air. Ndege ikafika few minutes ahead of schedule, hivyo kushuka abiria wote mnaingia kwenye zile basi trums za airport, hivyo tukashuka na Sumaye na mkewe na walinzi wote kwenye basi na halina siti!, hivyo tunapanda basi moja na Waziri Mkuu wa nchi yako halafu anashika mchuma!

Ile trum inaondoka ndipo motorcade ya kumpokea inaingia hapo uwanjani, huku balozi Ami Mpungwe behind the stearing wheel akiendesha mwenyewe, anashuka na kupungia mkono trum lisimame, ndipo Waziri Mkuu wetu na msafara wake wakaachia mchuma na kupokelewa!

Kiukweli sisi wabongo kwa kushadadia mambo madogo madogo yasiyo na maana yoyote!, nilidhani watu wangenote organization ya msiba, watu wanavyolia kizungu! Hakuna watu kughalaghala na kukanyagana, hakuna Red Cross walio busy kubeba watu waliozimia.

Misiba TV zetu huku misiba ya viongozi ni nyimbo za maombolezo, TV za wenzetu msiba wa kiongozi ni documentaries za her legacy!. Full time ni interviews kumhusu Malkia, sikuona kiongozi yoyote akihojiwa hata Waziri Mkuu wao!, huku ni mihotuba na mihotuba ya viongozi kuchoshana tuu bure!

Msafara wa mwili just 5 cars piki piki tatu mbele, mbili nyuma, ingekuwa ni huku!. Kunapotokea misiba kama hii, ya wenzetu walio staarabika, we should use them as a learning experience, sisi tunashikia bango Rais wetu kupanda basi as if Mama Samia ni katope, angeyeyuka!

Mbona viongozi kupanda mabasi ya pamoja ni kawaida, hili jambo linafanyika kila siku kwenye mikutano ya nchi za Jumuiya ya Madola and in fact its a good thing viongozi wana ji mix na ku mingle!

Hata siku ya Uhuru pale uwanja wa taifa, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, wanakuja pale Karimjee wanakuwa dropped off, kisha wanapanda usafiri wa pamoja, wanapelekwa uwanja wa Taifa na mabasi maalum, baada ya shughuli mabasi yanawarudisha Karimjee ndipo kila mmoja anapeperusha tena bendera yake kwenye magari yao!

Kipi cha ajabu jameni?, ushamba ukizidi nao ni issue. Natoa wito kwa Venus Nyota, fanya utaratibu wa kusafiri na few private media ili wakati wewe unatuma press release za hard news, hao private media watume color stories, Watanzania wapatiwe exposure na wajue mambo mengine ya mambo ya kimataifa.

Paska
Rejea Ukiwa Rais katika nchi za Kiafrika unapewa utukufu uliopitiliza

Kwa taarifa yako wala sio ushamba bali kilichofanyika ni kuwabeza viongozi wetu kwani wakiwa huku kwetu Afrika kwenye lindi la umasikini, hujifanya miungu watu. Utawaona na misafara mirefu yenye magari mengi na ulinzi kama wameingia madarakani kwa kupindua nchi! Kama inawezekana kupakia mabus, ule msururu wa ma VX huwa ni wa nini? Sio mara moja au mbili huwa tunasema misururu ya viongozi wetu ni ufujaji wa kodi za wananchi, je wamewahi kusikia? Kilichofanyika huko UK ni somo kuwafikia kwa vitendo hao majizi ya kura.
 
Naomba kuuliza ,hivi Biden alishea basi na mama?
Kama hujui kwanini Rais wa Marekani na Ufaransa walitumia usafiri tofauti basi hujui siasa na mienendo ya usalama kimataifa.
Rais wa USA akienda nchi yoyote anasafiri na msafara wake na magari yake.
 
Back
Top Bottom