Wazolee
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 3,183
- 3,660
We jamaa unaandika sana unajua Kwa Nini? Ni Kwa sababu unatetea uongo kwahiyo ni lazima uweke polojo nyingi kuliko facts Ili uwadanganye wagalatia wenzankoNakuja na Ushahidi mwingine zaidi wa kimaandiko kuwa NABII YULE sio tapeli Muhammad,Ni Yesu .,hii hoja hata waislamu wenzako kina Mazinge wameshaiacha kwenye mijadala ,maana walishaelewa
NABII YULE NI NANI?
Hoja yako kubwa umejenga kupitia unabii wa nabii Musa (Hazrat Musa) katika Kumb-torati 18 na Yohana 1, 14 na 16 katika kumbashiri Muhammad, nami nitaanzia hapo hapo tuone ukweli wa mambo.
TUANZE NA YOHANA SURA YA KWANZA.
Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? Yohana 1:19-25
Hapo umejenga hoja kuwa kuna watu watatu ambao Wayahudi wanamuulizia Yohana kama ni mmoja wao, na hao ni Kristo, Eliya na Nabii yule. Yohana Mbatizaji akakataa na kuwajibu vinginevyo. Najua hauna vita na hoja ya Kristo ni nani ama Eliya, vita inakuja katika mtu anayeitwa nabii yule ambaye kwa asili ameongelewa katika Kumb 18 ambayo pia nitakuja kuibanisha kwa kina. Kifupi Kristo na Nabii yule ni mtu mmoja yule yule, shida tu ilikuwa katika mtazamo wa Kifarisayo, maana hata huyo Eliya kiroho ni Yohana Mbatizaji, ingawa Wayahudi waliamini Eliya atarudi kibinafsi, kumbe atakuja mtu mwenye roho ya Eliya. Katika Luka 1:17 Malaika akimtabiri Yohana Mbatizaji alisema:
Naye atatangulia mbele zake katika ROHO YA ELIYA, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa.
Hivyo basi tumepata picha halisi juu ya Eliya, kwahiyo tusidumu kukataa jambo kupitia kutokujua kwa viongozi wa dini ya Kiyahudi maana hata Yesu walimkataa kuwa si Kristo aliye tabiriwa na manabii kwa kuona hatimizi vigezo vyao (criteria). Kwahiyo juu ya nabii yule maandiko yapo wazi kuwa ni Yesu. Watu wa zama za Yesu kulingana na unabii wa Musa katika Kumb 18 walijua dhahiri sharti nabii yule awe kama Musa atendaye miujiza na mwenye ujumbe wa pekee, na walikuwa sahihi…maana nabii yule ni nabii mfano wa Musa na sharti atokee miongoni mwao na si nje yao. Katika maandiko yafuatayo tunasoma:
“Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni YULE NABII, YESU, WA NAZARETI YA GALILAYA. Mathayo 21:10,11
Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni NABII YULE AJAYE ULIMWENGUNI. Yohana 6:14
Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, HAKIKA HUYU NDIYE NABII YULE. Yohana 7:40
Biblia inatuambia ujumbe wa mashaidi watatu ndio kweli, lakini kwa upande wa Muhamad alijiita na kujitangaza kuwa nabii jambo ambalo linatia shaka, maana nabii ajibainishi kwa kujiita, bali kazi zake ndizo zitamfunua kuwa yeye ni nani hasa. Hivyo basi tunapata hakika kuwa nabii yule ni Yesu mwenyewe, ingawa Waislam mnadai kuwa sisi Wakristo tunamwita Yesu kuwa Mungu ama Mwana wa Mungu, iweje tena tumwite nabii?. Swali zuri sana hilo, kuhusu Yesu maandiko yanamsema hivi:
“…..bali Kristo ni yote, na katika yote. Wakolosai 3:11
Hivyo Yesu ana vyeo vingi sana mfano: Kristo, Mwana wa Adamu, Mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, Mwana – Kondoo, Simba wa Yuda, Mwana wa Mungu, mkuu wa wafalme wa dunia, mshauri wa ajabu, Shina la Yese, na mengine mengi. Hivyo anatimiza kazi zote hizo kulingana na wito wa jina husika. Nabii yule ni ofisi ambayo inahusika na nabii kama Musa, ingawa kulikuwa na wingi wa manabii lakini kulikuwa na nabii mkuu ambaye ni Musa na yule ajaye aliye kama Musa ambaye atafunga historia ya Maandiko matakatifu na kazi ya Mungu kwa ujumla.
Mwisho kwa mujibu wa hoja katika Yohana 1 ni kwamba Kristo, Eliya na nabii yule "wanabatiza? kama Muhamad ndiye nabii yule je alibatiza? na Waislamu leo wanabatizwa? hili ni swali nimeweka. Hivyo mwalimu wa Kislamu atakayekuja ajibu swali hili katika uchambuzi wake.
HOJA JUU YA KUMBUKUMBU LA TORATI 18
Imeandikwa, "Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake." Kumb 18:18-19
Ndugu yangu kama ni kweli maneno ya kumb 18:18 uongea habari za Muhammad, kwanini katika zama za Yesu walisema kuwa Yesu ndiye aliyekuwa akitajwa katika mstari huo? Katika Yohana 1:45 tunasoma:
"" Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.
Pia watu walioishi na Kristo walipoiona miujiza aliyotenda Yesu walisema hivi "" Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.(Yohana 6:14).
Na Bwana Yesu aliwambia hivi Marabi waliokuwa wanatwist maandiko kwa matamanio yao,
""Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu, (Yohana 5:46).
Hata mitume wa Yesu walifundisha unabii wa Kumb 18 ulimlenga Kristo, kama Kristo mwenyewe alivyosema rejea Matendo 3:22-24, 7:37.
Kwahiyo Nabii yule na Kristo ni Bwana Yesu kwa mujibu wa maandiko. Mafarisayo (marabi) walikuwa hawana ujuzi sahihi wa unabii huo ila wachache pamoja na wale waliokuwa wanamcha Mungu kwa moyo safi kama mzee Zacharia, Simioni, Nicodemo, Yusufu wa Arimasaya, Nathanael nk, ukijenga mantiki ya unabii huo juu ya matashi yao unapotea bayana.
• Bwana Yesu aliwambia marabi hivi...
Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia, (Yohana 5:39).
Kwahiyo maandiko yanamshuhudia Kristo ila marabi walipindisha ndimi zao juu yake kwa matamanio yao. Tena Bwana Yesu aliwakemea hivi kwa kupindisha kwao,
"Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.(Marko 7:8-12)
Sasa twende kwenye suala la kulinganisha Musa na Muhamad na Bwana Yesu. Umetoa dondoo za maandiko zilizo sawai lakini maantiki ya ulinganifu si sawia.
1. Kwa mfano wakati wa Musa, Waisrael walikuwa wanatawaliwa na Wamisri na mfalme wa Misri aliwaua watoto wote kiume wa Kiebrania, kwa kuhofia madaraka yake (Kut 1:22). Je hii ilitokea wakati wa Muhamad? La haikutokea. Na wakati wa Bwana Yesu Waisrael walikuwa wanatawaliwa na Warumi, na mfalme Herode aliwaua watoto wa kiume kuhofia madaraka yake (Mathayo 2:16,17).
2. Musa aliishi katika jumba la mfalme wa Misri kwa kuhepa kifo, na Bwana Yesu alikimbizwa Misri kuhepa kifo, Musa alitoka Misri ili kutimiza huduma (Waebrania 11:27), na Bwana Yesu alitoka Misri kutimiza huduma yake. Kutoka Misri nalimwita mwanangu (Mathayo 2:15). Muhamad hajawai ishi Misri.
3. Musa aliwakomboa Waisrael toka katika utumwa wa Farao, na Bwana Yesu anakomboa watu wake toka katika utumwa wa dhambi ""Mathayo 1:21 ‘Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. Muhamad si mwokozi wala hawezi kuokoa (Quran 46:9)
4. Musa aliongea na Mungu bayana hata akapewa jina "mwongeaji na Mungu" Quran 19:51,52, 4:164, na biblia inasema hivi "" Naye BWANA akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake (Kut 33:11) na Waisrael walisikia sauti ya Mungu kama ngurumo katika zama za Musa. Lakini Muhamad hakuongea na Mungu bali alipata wahyi kupitia malaika Jibril na hajawai mwona Mungu. Lakini Bwana Yesu aliongea na Mungu na alimwona Mungu, na katika zama zake watu walisikia sauti ya Mungu kama ngurumo, Biblia inasema hivi:
"Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena. Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo...(Yohana 12:28,29).
Na Bwana Yesu alimwona Mungu: “Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. (Yohana 6:46).
5. Musa alifanya ishara kubwa na maajabu. "Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso; katika ishara zote na maajabu yote, ambayo BWANA alimtuma kuyatenda katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote; na katika ule mkono wa nguvu wote, tena katika ule utisho mkuu wote, alioutenda Musa machoni pa Israeli wote. Kumb 34:10-12.
Lakini Muhammad hakufanya mujiza wowote mpaka katika zama zake watu walimuliza hivi:
"....Mbona hakupewa kama aliyo pewa Musa?...Quran 28:48.
Kwa hoja hiyo iweje Muhamad awe nabii mfano wa Musa? Tafakari.
Sehemu nyingine imeandikwa. “Na walisema mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa mola wake? Sema miujiza iko kwake mwenyezi mungu tu akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi nami hakika ni muonyaji mbainishaji (dhahiri tu). Quran 29:50
Lakini kwa Bwana Yesu miujiza kwake ilikuwa kama pumzi tu mpaka watu wakastajabu: “Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Marko 6:2
MIUJIZA YA MUSA NA YESU KATIKA USHABIANO MPAKA WATU WAKATAMBUA YESU NDIYE NABII YULE..
1. Musa alitenda mujiza katika bahari "" Kut 14:21 Musa; akanyosha mkono wake juu ya bahari; BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki, usiku kucha, akaifanya bahari kuwa nchi kavu, maji yakagawanyika. Bwana Yesu pia alifanya mujiza juu ya bahari "" Marko 4:39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. Watu wakastajabu kwa kusema hivi "" ...Ni nani huyu, basi hata upepo na bahari humtii? aya ya 41.
2. Musa aliwalisha Waisrael mikate na nyama ya kware kimujiza (Kutoka 16:13-15) na Bwana Yesu aliwalisha Waisrael mkate na samaki kimujiza mpaka wakastajabu (Yoh 6:10-13)"" na katika aya ya 14 wakasema ""Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Muhamad hajawai fanya hivo milele
3. Musa na Bwana Yesu wote waling'aa sura zao mbele za wafuasi wao ila kwa Muhammad haijawai tokea kamwe.
....hapo (Musa) aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling’aa kwa sababu amesema naye. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling’aa; nao wakaogopa kumkaribia (Kut 34:29,30). "Yesu"akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. (Mathayo 17:2)
NDUGU WA MUSA
Waislamu: Mnadai kwamba Ndugu za Musa atakaye tokea nabii yule katika Kumb 18:15-18 ni waarabu?
Jibu ni Waisraeli, maana Musa ni nabii aliyetokea katika kabila la Lawi lililoteuliwa na Mungu kushika majukumu ya kiroho, kwahiyo ndugu za Walawi ni makabila 11 ya wana Waisrael. Biblia inasema "Makuhani Walawi, kabila yote ya Lawi, wasiwe na fungu wala urithi pamoja na Israeli; watakula sadaka za BWANA zifanywazo kwa moto, na urithi wake. Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; BWANA ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.( Kumb 18:1,2)
Ukija aya ya 15 na 18 katika Kumb 18 tunapata picha kuwa ndugu wa Walawi aliyekuwa anaongelewa hapo katika unabii, ni kabila lingine miongoni mwa Israeli. Andiko linasema hivi.
‘Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. (Kut 2:11).
Sasa Muhammad (mwarabu) lini amekuwa ndugu za Musa Mlawi?. Msemo" ndugu zao" katika biblia unamanisha wana wa Israel na si vinginevyo, Biblia inasema hivi,
"Lakini Benyamini hawakukubali kuisikia sauti ya NDUGU ZAO WANA WA ISRAELI. (Waamuzi 20:13).
Na ukirejea Kumb 17:15, Mungu anapiga marufuku kumweka mgeni asiye ndugu wa wana waisrael kuwa Mfalme wao. Kwahiyo Ishmail si ndugu wa Israel (Yakobo) bali Isaac, Wana wa Israel wanamwita Ishmael Babu na si ndugu (brethren), na ni babu wa kando, ingekuwa na mantiki kama Muhamad angetokea kwa Esau aliye kaka yake Yakobo (Israel) na hata hivo ukoo wa Esau(Edom) hukuwai kutoa nabii. Biblia inasema, ‘Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu (brother) yako….(Kumb 23:7). Hakuna sehemu waarabu wameitwa ndugu (brother) wa Waisraeli.
UADUI KATI YA WAISRAELI NA WAARABU
Na waarabu walikuwa maadui na wana wa Israel "Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na WAARABU, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno; wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo. ( Nehemia 4:7,8.). Na walipigana vita sana na Waisrael zama hizo kama zilivyo zama hizi na Mungu aliwasaidia Waisrael dhidi yao (2 Nyakati 22:1, 26:7). Hata katika Quran sijaona aya inayobainisha kuwa waarabu ni ndugu (brothers) za Waisrael zaidi ya kuwapiga marufu waarabu (waislam) wasiwe na urafiki na Wayahudi nduug za Musa. Quran 5:82
1117. Umar amehadithia kuwa alimsikia Mtume akisema: ‘Nitawatoa Mayahudi na Manasara katika Rasi ya Arabuni hata nisibakishe isipokuwa Muislamu pekee.’ Muslim. Rejea pia Bulugh Al Maramu uk. 496
197 Abu Huraira amesimulia Mtume amesema Allah awalaani Mayahudi na Wakristo……Bulugh al Maram uk. 110
Hitimisho: Ndugu ya Musa Mlawi aliyepokea unabii na agano ni Bwana Yesu aliyetokea katika kabila la Yuda (Luka 3:33 na Waebrania 7:14). Musa Mlawi alikuwa mjumbe wa agano la kale "" Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote. (Kut 24:8). Na Bwana Yesu Myuda ndugu ya Musa Mlawi ni mjumbe wa agano jipya ""..(Yesu) akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.(Luka 22:20)
Nimeona katika hilo garazeti lako unasema nabii yule ni Yesu ila mafarisayo hawajui mandiko unachekesha sana soma vizuri bibilia Ili ujue mafarisayo ni akina nani
Yani wewe ujue mandiko ya manabii kuliko mafarisayo? Unachekesha
Twende kwenye point za muhimu unasema Parani haiko Saudi Arabia
Ngoja nikufundishe
Kwanza kabisa Ishmael ndio mtoto aliyeishi jangwa la Parani Baada ya kuondoka Jerusalem
Mwanzo 21:20
Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Mwanzo 21:21
Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Ishmael ndio aliayoanzisha kizazi katika Jangwa la Parani na kuza watoto 12 ambao ndio wasaudi Arabia wa Leo
Na si Dhani kama Kuna mtu anapinga kuwa warabu wa Saudi Arabia sio kizazi Cha Ishmael labda wewe mbumbu
Zamani kabisa lilikuwa linaitwa Jangwa la Parani Baada ya watoto wa Ishmael kuzaana na kuwa wengi likaitwa Jangwa la Arabu
So Jangwa la Parani ndio Jangwa la Arabu
Angalia ramani hapo chini
Tumesha ona hapo katika ramani Parani ipo Saudi Arabia na hapo ndipo vilipo vizazi vya nabii Ishmael
Je Mungu anasemaje kupitia manabii wa kale kuhusu kuhusu eneo la Parani
Kumbukumbu la Torati 33:2
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Sinai nabii Musa, Seiri nabii Yesu na Parani ni nabii Muhammad
Na hilo neno Sheria moto moto linawakilisha kitabu Cha Quran
Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
Hilo andiko linamuhu nabii Muhammad peke yake
Labda utoe ushahidi Parani alitoka mtume gani zaidi ya mtume Muhammad?