Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

We jamaa unaandika sana unajua Kwa Nini? Ni Kwa sababu unatetea uongo kwahiyo ni lazima uweke polojo nyingi kuliko facts Ili uwadanganye wagalatia wenzanko

Nimeona katika hilo garazeti lako unasema nabii yule ni Yesu ila mafarisayo hawajui mandiko unachekesha sana soma vizuri bibilia Ili ujue mafarisayo ni akina nani
Yani wewe ujue mandiko ya manabii kuliko mafarisayo? Unachekesha

Twende kwenye point za muhimu unasema Parani haiko Saudi Arabia
Ngoja nikufundishe

Kwanza kabisa Ishmael ndio mtoto aliyeishi jangwa la Parani Baada ya kuondoka Jerusalem

Mwanzo 21:20
Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Mwanzo 21:21
Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

Ishmael ndio aliayoanzisha kizazi katika Jangwa la Parani na kuza watoto 12 ambao ndio wasaudi Arabia wa Leo
Na si Dhani kama Kuna mtu anapinga kuwa warabu wa Saudi Arabia sio kizazi Cha Ishmael labda wewe mbumbu

Zamani kabisa lilikuwa linaitwa Jangwa la Parani Baada ya watoto wa Ishmael kuzaana na kuwa wengi likaitwa Jangwa la Arabu

So Jangwa la Parani ndio Jangwa la Arabu

Angalia ramani hapo chini

Tumesha ona hapo katika ramani Parani ipo Saudi Arabia na hapo ndipo vilipo vizazi vya nabii Ishmael

Je Mungu anasemaje kupitia manabii wa kale kuhusu kuhusu eneo la Parani

Kumbukumbu la Torati 33:2
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.

Sinai nabii Musa, Seiri nabii Yesu na Parani ni nabii Muhammad
Na hilo neno Sheria moto moto linawakilisha kitabu Cha Quran

Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.

Hilo andiko linamuhu nabii Muhammad peke yake

Labda utoe ushahidi Parani alitoka mtume gani zaidi ya mtume Muhammad?
 

Attachments

  • Screenshot_20241215-150645.jpg
    453.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241215-150919.jpg
    459.9 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241215-154538.jpg
    420 KB · Views: 3
Unaokoteza sana ,unaungaunga sana ,nipo hapa Leo utaelewa vizuri sana ,

Twende taratibu tu

Unasema Mafarisayo walijua maandiko vizuri kuliko Yesu. Biblia inatoa ushahidi kwamba Mafarisayo walikuwa na mapungufu makubwa katika kuelewa maandiko:

Yesu aliwakaripia Mafarisayo mara nyingi kwa unafiki na kutokuelewa kweli za maandiko.
Yesu alisema:

“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa maana mnajenga makaburi ya manabii, na kuwapamba waliotakaswa, na kusema, Kama tungalikuwa siku za baba zetu, hatungalikuwa washirika wao katika damu ya manabii.” (Mathayo 23:29-30)

Pia alisema:

“Mwapotea, kwa kuwa hamjui maandiko wala uweza wa Mungu.” (Mathayo 22:29)


Yesu alithibitisha kwamba Mafarisayo walikuwa na elimu ya maandiko lakini waliikosa tafsiri sahihi. Ujuzi wao ulikuwa wa juu juu, si wa kiroho.

Unasema Parani iko Saudi Arabia, na unatetea kwamba ni sehemu ya Nabii Muhammad. Hata hivyo, Biblia haionyeshi kuwa Parani iko Saudi Arabia. Tafsiri ya eneo la Parani inahitajika kueleweka katika muktadha wa maandiko:

Biblia inaonyesha kwamba Parani iko karibu na Sinai, sio mbali sana kutoka Misri.
Ishmaeli alikaa katika jangwa la Parani, lakini maandiko hayaonyeshi kwamba Parani ilikuwa Saudi Arabia. Soma maandiko haya:

“Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke kutoka Misri.” (Mwanzo 21:21)


Historia pia inaonyesha kwamba Parani iko katika eneo linalojulikana leo kama Negev, karibu na Sinai, siyo katikati ya Saudi Arabia.

Ramani za kihistoria zinaonyesha Parani iko upande wa magharibi wa Saudi Arabia, karibu na Misri na Israel, sio ndani kabisa ya jangwa la Arabia.

Nabii Muhammad katika Kumbukumbu la Torati 33:2 na Habakuki 3:3

Hoja zako kwamba maandiko haya yanamhusu Muhammad hayana msingi thabiti kwa sababu:

Kumbukumbu la Torati 33:2

“Bwana alitoka Sinai, akawaondokea kutoka Seiri; aliangaza katika kilima cha Parani...”
Hapa Bwana anatajwa, si Muhammad. Tafsiri ya Kiebrania inaonyesha kuwa maandiko haya yanazungumzia ufunuo wa Mungu kwa Musa, Yesu, na watu wake. Hakuna mahali yanamtaja Muhammad.


Habakuki 3:3

“Mungu alikuja kutoka Temani, yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani...”
Habakuki anaeleza ufunuo wa Mungu kutoka Sinai na Parani kama ishara ya nguvu zake kwa Israeli. Hakuna muktadha unaounga mkono kuwa andiko hili linamhusu Muhammad.

Unasema sheria moto-moto ni Quran, lakini Biblia haionyeshi hivyo. Sheria hii inahusiana na agano la Musa kwenye Mlima Sinai, ambapo Mungu alitoa Amri Kumi (Kutoka 19:18-19). Quran haikuwahi kutajwa katika Biblia.
 
Zamani kabisa lilikuwa linaitwa Jangwa la Parani Baada ya watoto wa Ishmael kuzaana na kuwa wengi likaitwa Jangwa la Arabu

So Jangwa la Parani ndio Jangwa la Arabu

Angalia ramani hapo chini
Kaa utulie upate elimu,maana Uislamu umejengwa kwa Propaganda na uongo ,

Ili kuthibitisha kwamba Parani siyo Saudi Arabia, nitachambua hoja hii kwa kutumia Biblia, historia ya kihistoria ya maeneo, na hata maelezo kutoka vyanzo vya Kiislamu.

Parani katika Maandiko ya Biblia

Biblia inatoa ushahidi wa kijiografia unaoonyesha kwamba Parani haiko Saudi Arabia:

(a) Parani ni Sehemu Karibu na Sinai

Mwanzo 21:21

“Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke kutoka Misri.”
Ishmaeli alihamia Parani baada ya kuondoka na mama yake kutoka Kanaan, lakini maandiko yanaonyesha kuwa mama yake, Hagar, alimtwaa mke kutoka Misri. Hii inamaanisha Parani ilikuwa karibu na Misri, si mbali kama Saudi Arabia.

(b) Mahali pa Kutembea kwa Wana wa Israeli

Hesabu 10:12

“Nao wana wa Israeli wakaondoka wakatoka mahali pa mlima wa Bwana, wakaenda safari zao hata jangwa la Parani...”
Parani inatajwa kama moja ya maeneo ambayo wana wa Israeli walipitia baada ya kuondoka Sinai. Historia ya safari ya Wana wa Israeli inaonyesha kuwa walitembea katika maeneo ya karibu na Sinai (eneo la Negev), si mbali kama Saudi Arabia.

(c) Kutoka kwa Biblia, Parani ni Karibu na Edomu

Kumbukumbu la Torati 1:1

“Haya ndiyo maneno aliyowaambia Musa Israeli wote ng'ambo ya Yordani, bara ya Araba, kulikabili Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu.”
Hii inaonyesha Parani iko karibu na maeneo ya Tofeli, Hazerothi, na Labani, ambayo ni magharibi ya Kaanani na Sinai, si katika kina cha jangwa la Saudi Arabia.

Ushahidi wa Kihistoria

(a) Jangwa la Parani Lilijulikana Kama Eneo la Sinai

Ramani za kale zinaonyesha Parani iko katika eneo la Negev na karibu na Mlima Sinai. Historia ya majangwa inahusisha Parani na maeneo ya Sinai kutokana na ukaribu wake na Kanaan.

(b) Saudi Arabia Iliitwa Arabu, Siyo Parani

Katika historia ya kale, Saudi Arabia ilijulikana kama "Arabu" au "Jangwa la Arabia." Hakuna rekodi ya kihistoria inayohusisha Saudi Arabia na jina "Parani."

(c) Ushahidi wa Wana wa Ishmaeli

Ingawa Waismaeli walienea katika jangwa, kizazi chao kilihusiana na maeneo ya karibu na Kanaan, siyo sehemu za mbali za Saudi Arabia. Hii inathibitishwa na ndoa za Ishmaeli zilizoanzia Misri (Mwanzo 21:21).


Ushahidi Kutoka Kwa Vyanzo vya Kiislamu

(a) Tafsiri za Kiislamu Kuhusu Parani

Watafsiri wa Kiislamu kama Ibn Kathir na wengine mara nyingi walitaja Parani kwa jina lake la Kibiblia. Hata hivyo, tafsiri zao hazikuonyesha kuwa Parani iko katikati ya Saudi Arabia, bali walichukua tafsiri ya kihistoria inayosema iko Sinai.


(b) Maelezo ya Hajir na Ishmael

Quran inataja safari ya Hajir na Ishmael (Quran 14:37), lakini haina jina la Parani. Vyanzo vya hadithi za Kiislamu kama Hadithi za Ibn Ishaq vilielezea Makkah na maeneo ya Saudi Arabia, lakini hazikuonyesha moja kwa moja kuwa Makkah ni Parani.


Kusema Parani ni Saudi Arabia,ni ukosefu wa Elimu au ni dhana ya Uislamu kama kawaida yenu kujishobokesha kwa Uyahudi,kwanini nasema hivo?

(a) Umbali wa Safari ya Hajir na Ishmael

Biblia inataja Hajiri akienda na mtoto wake Ishmael kutoka Kanaan hadi Parani na kisha kurudi Misri kutafuta mke (Mwanzo 21:21). Safari ya kwenda na kurudi ingekuwa karibu na maeneo ya Negev au Sinai, si mbali kama Saudi Arabia.


(b) Mahali Walipotembea Wana wa Israeli

Wana wa Israeli walitembea kutoka Sinai kwenda Parani. Hii inamaanisha Parani ilikuwa sehemu ya maeneo yaliyopitiwa kati ya Kanaan na Sinai. Haikuwezekana kwao kufika Saudi Arabia wakati wa safari yao.
 
Zamani kabisa lilikuwa linaitwa Jangwa la Parani Baada ya watoto wa Ishmael kuzaana na kuwa wengi likaitwa Jangwa la Arabu

1. Biblia: Maandiko yanaonyesha Parani iko karibu na Sinai, si Saudi Arabia.

2. Historia: Rekodi za kihistoria zinaonyesha Parani ni sehemu ya Negev au karibu na Mlima Sinai, si katika jangwa la Arabia.


3. Vyanzo vya Kiislamu: Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kutoka vyanzo vya Kiislamu vinavyohusisha Parani na Saudi Arabia.


Kwa mujibu wa ushahidi wa Biblia, historia, na hata vyanzo vya Kiislamu, Parani iko Sinai au Negev, si Saudi Arabia.
 
Hadi Sasa sijajua unabishana na nani

Bibilia inasema Ishmael aliishi katika Jangwa la Parani wewe unabisha
Lazima ubishe maana hiyo ndio sifa ya makafiri kupinga maandiko ya Mungu

ISHMAEL ALIISHI PARANI
Mwanzo 21:20
Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Mwanzo 21:21
Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

ISHMAEL AMEZAA WATOTO AKIWA HAPO PARANI
Mwanzo 25:13
Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,
Mwanzo 25:14
na Mishma, na Duma, na Masa,
Mwanzo 25:15
na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.
Mwanzo 25:16
Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Nakuwekea ramani ya kale kukuonyesha watoto wa Ishmael wakiwa katika Jangwa la Parani

Pia nakuwekea ramani ya Sasa ya Saudi Arabia kukuonyesha kuwa hilo Jangwa la Parani lipo katika nchi ya Saudi Arabia
Na Kuna baadhi ya miji Hadi Leo ipo Saudi Arabia ukiwepo mji wa Tyma

Habakuki 3:3
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.

Huo ni utabiri wa Mtume Muhammad
Tema ni jina la mtoto nabii Ishmael na Kwa Sasa ni jina la mji na huo mji Hadi Leo hii upo Saudi Arabia

Parani ipo Saudi Arabia hilo Jangwa la Parani linaanzia mpakani kati ya Saudi Arabia na Jordan kuteremka huku chini kama unakuja katika miji ya Maka na Madina

Kwa kuwa kazi ya kafiri ni kupinga maandiko ya Mungu wewe endelea tu kupinga

Haya mandiko umezaliwa umeyakuta na utakufa utayaacha

By the way Mimi napenda sana ubishi wako maana ndio unawafanya wagalatia wenzanko waelewe ukweli zaidi kuhusu mtume Muhammad
 

Attachments

  • Screenshot_20241215-213828.jpg
    519.4 KB · Views: 4
  • Screenshot_20241215-221922.jpg
    303.5 KB · Views: 3
  • Screenshot_20241215-215915.jpg
    433.5 KB · Views: 2
Uzuri Mimi Sifanyi mipasho ,Mimi nakuchapa tu na maandiko na historia ambayo ipo wazi, wala siungiungi kama wewe ili umpachike tapeli Muhammad

Majibu ya Kupinga na Hoja za Maandiko:

Biblia Inayojulikana ni ya Ukristo na Haizungumzi Kumpa Mtume Muhammad Sifa Maalum
Mwanzo 21:20-21 inathibitisha kuwa Ishmael aliishi jangwa la Parani, lakini Biblia haijatoa mwelekeo wowote unaohusiana na unabii wa Mtume Muhammad au dini ya Uislamu. Katika maandiko haya, Ishmael alibarikiwa kama mmoja wa watoto wa Abrahamu, lakini haimaanishi alizaliwa kwa misingi ya kufanikisha dini nyingine.
Habakuki 3:3 haitaji Mtume Muhammad kwa jina. Hapa, inaelezea utukufu wa Mungu wa Israeli akitoka Temani na Parani, inavyotafsiriwa katika muktadha wa Kiyahudi na Kikristo, ina maana ya kuonyesha uweza wa Mungu, sio unabii wa Muhammad.

Maana ya Parani na Ramani
Jangwa la Parani linatajwa kijiografia na kihistoria katika Biblia likiwa karibu na Sinai, na hakuna ushahidi wa maandiko wa moja kwa moja unaounganisha eneo hili na miji ya kisasa ya Saudi Arabia au kuwepo kwa miji ya Kiislamu wakati huo.
Ramani za sasa haziwezi kutumika kuonyesha maana za maandiko ya kale isipokuwa kwa kuzingatia tafiti za kihistoria na tafsiri zilizo wazi. Tafsiri ya Uislamu ya kuunganisha Parani na Saudi Arabia ni ya mtazamo wa Kiislamu lakini haithibitishwi ndani ya Biblia.

Katika Biblia, hakuna sehemu inayomtaja Mtume Muhammad moja kwa moja, na tafsiri ya "utakatifu kutoka Parani" kama kumhusu yeye ni ya kidhanifu bila msaada wa maandiko. Habakuki 3:3 inaelezea ukuu wa Mungu wa Israeli kwa muktadha wa Waisraeli.

Ingawa maandiko yanasema Ishmael alikaa Parani na kuwa na watoto, hayaonyeshi uhusiano wa moja kwa moja na unabii wowote wa baadaye wa Muhammad. Hii ni hadithi ya kizazi cha Ishmael ndani ya Biblia, lakini maandiko ya Kiislamu yana tafsiri yenu ya kubumbabumba

Acha kuikurupukia Biblia , Biblia na Quran ni maandiko mawili tofauti yenye mitazamo tofauti kuhusu historia, unabii, na maana ya Ishmael. Wakati Quran inampa Ishmael nafasi kubwa ya kiunabii, Biblia inamwona kama baba wa mataifa makubwa, lakini si mhusika mkuu katika mpango wa ukombozi wa Mungu.,Ishamael hana historia yoyote katika Uyahudi na Ukristo, Mungu amejitaja sana Yeye ni Mungu wa Ibrahimu, isaka na Yakobo

ujibu haya maswali

Ikiwa Habakuki 3:3 ni utabiri wa Mtume Muhammad, mbona hakutajwa kwa jina waziwazi kama ilivyo kwa manabii wengine kwenye Biblia?

Je, kuna maandiko ya wazi kabisa katika Quran yanayothibitisha kuwa Parani ni Saudi Arabia?naomba uje ujibu hili swali

Ikiwa Jangwa la Parani linaunganishwa na miji ya Saudi Arabia, mbona historia ya Biblia haielezi kuhusu maisha ya Waislamu kabla ya Muhammad?
 
UISLAMU NI DINI ILIYOJENGWA KWA UONGO, PROPAGANDA NA KUUNGAUNGA HUKU NA KULE NDIO MAANA NI RAHISI KUGUNDUA KUWA UISLAMU NI DINI YA UONGO

Wanazuoni wa kiislamu wanakiri Paran sio Saudia Arabia, wewe upo hapa unakazania ili utetee dini kama kawaida yenu kutumia Taqia

Kitabu: "Atlas of the Quran" cha Dr. Shauqi Abu Khalil: Kinatoa ramani zinazohusiana na maeneo yaliyotajwa katika Qur'an na historia ya Kiislamu. Kitabu hiki kinadokeza kuwa Paran inaweza kuwa eneo karibu na Sinai au Petra, badala ya Makka moja kwa moja.

Kitabu: "Arabs and Israel For Beginners" cha Ron David: Kinachunguza asili ya majina ya maeneo kama Paran kutoka kwenye kumbukumbu za Kiyahudi, Kikristo, na Kiislamu. Paran inaonekana kuhusiana zaidi na maeneo ya kaskazini mwa Hijaz.


Maoni ya Wanazuoni wa Kiislamu

Wanazuoni wa Kiislamu kama Dr. Muhammad Hamidullah na Sheikh Imran Hosein wamependekeza kuwa Paran inaweza kuwa karibu na maeneo ya kaskazini mwa Hijaz kutokana na uhusiano wa kihistoria kati ya Hajir, Ismail, na maeneo ya Misri na Palestina. Hii inaungwa mkono na:

Ukaribu wa Mlima Sinai na Paran kama ilivyotajwa katika Biblia.

Hadithi za Ismail zilizoenea kati ya Waarabu wa Petra kabla ya Uislamu.


Kwa kifupi, rejea za vitabu vya Kiislamu na historia zinaonyesha kuwa Paran kuwa eneo nje ya Saudi Arabia, likiwa na uhusiano wa kihistoria na Palestina, Sinai, au Petra.

Na uhakika huwezi kutumia Quran maana ni nyeupe pee, unakimbilia kwenye biblia usiyoiamini unaungaunga maneno
 
Wewe ni mwehu wa ufahamu, hayo ni maneno ya paulo, ndio maana
Maneno mengi uelewa ki dogo
 
Sasa eka ahadi hapa Niki leta maandiko yenye ushahidi kutoka Ktk bibilia utafanya nini?, ikiwa YESU ndiye mungu muumbaji basi MARIA asingemkimbiza ili asiuliwe na mfalme, yaani MUNGU anakimbia asi uliwe 😂😂😂😂😂😂😂, lofa wa elimu wewe, Niwekee ahadi hapa
 
Mkuu soma huu uzi vizuri utagundua kuwa nyinyi wa kristo mnategemea maneno ya Paulo ili ku halalisha UUNGU wa YESU, lakini never never ever huyo YESU hakuwahi kujiita yeye ni MUNGU,

kama kuna andiko ktk bibilia yenu ambayo YESU himself kajiita yeye kwa maneno yake mwenyewe ni Mungu basi weka hapa, hiyo sio dini ya ukweli
 
Quraan ni maneno ya Allah ushahidi upo, lakini kiini cha bibilia ni maneno ya Paulo na ndio mnayo yatumia ku mfanya YESU ni Mungu, yaani YESU yupo hai hakusema kuwa yeye ni MUNGU Eti kafa ndio ka pachikwa UUNGU,

Kama YESU angekuwa ni Mungu basi mama yake MARIA asinge mkimbiza ili mfalme asi muue, yaani MUNGU ana ogopa kufa, tena ana muogopa mwanadamu, ukristo umejaa uongo uongo mwingi
 

Wewe ramani uliyoiweka inaonyesha Nyika ya Parani maana yake ni misitu ya parani na Mimi ramani niliyokuwekea inaonyesha Wildness of Parani maana yake ni Jangwa la Parani

Ukitoka Israel kuelekea Saudi Arabia utaanza kuukuta huo msitu wa Parani ukiisha msitu wa Parani utakutana na milima ya parani ukimaliza milima ya parani ndio unakutana na Jangwa la Parani na ndio Saudi Arabia ya Sasa
Mbona ramani zipo wazi na nimekuwekea

Nakuwekea tena majina ya watoto wa Ishmael yakiwa yametapakaa katika hilo Jangwa la Parani pamoja na ramani zinazothibitisha kuwa Jangwa la Parani ndio lipo Saudi Arabia ya Sasa

Mwanzo 25:13
Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu,
Mwanzo 25:14
na Mishma, na Duma, na Masa,
Mwanzo 25:15
na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema.
Mwanzo 25:16

Sasa wewe jibu hili swali maana unapingana na mandiko pamoja na ramani

Jangwa la Parani sehemu ambayo aliishi Ishmael na kizazi chake Kwa Sasa ndio nchi gani?
 

Attachments

  • Screenshot_20241215-150645.jpg
    453.3 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241215-221922.jpg
    303.5 KB · Views: 2
  • Screenshot_20241215-215915.jpg
    433.5 KB · Views: 2
Biblia imeeleza vzr sana na Ina ramani ya kipindi hicho, acha kubumbabumba ,

Kwa mujibu wa Biblia, Jangwa la Parani lilikuwa karibu na Mlima Sinai na linaweza kuwekwa katika ukanda wa Sinai wa sasa (kati ya Misri, Palestina, na Jordan). Quran, kwa upande mwingine, haitaji moja kwa moja Parani, lakini inahusisha Ismail na bonde la Makkah.

Historia inaonyesha kuwa jina "Parani" halijawahi kutumiwa kumaanisha Saudi Arabia nzima, bali linahusishwa na eneo dogo karibu na Peninsula ya Sinai. Tafsiri yoyote inayohusisha Jangwa la Parani na Saudi Arabia nzima inahitaji ushahidi wa ziada wa kihistoria au kijiografi

Leta ushahidi wa Quran
 
Unajua wewe kuniita lofa wa Elimu haithibitishi kuwa Mimi ni lofa.

Na Siko hapa kukuonesha kuwa Mimi ni mjuvi sana wa mambo flani.

Na sina kitu chochote Cha kuwekeana ahadi na wewe sababu hainidhuru Kwa vyovyote.

Cha kufanya hapa unapaswa KUJUA hatufahamiani, na hivyo kiwango Cha uzoefu wa maisha(life experience) achana na mambo ya Elimu ya darasani kwanza, tunatofautiana.

Je, wewe hapo umewahi kuzungumza na viumbe visivyo na mwili na ukaongea navyo kubadilishàna mawazo?

Nafkri kuna jamaa kaweka Uzi huko kumhusu Bikira Maria, ndio amekuchajisha umekuja Kwa kuniita lofa.

Sasa mwamuzi mzuri na WA haki juu ya haya tuaminiyo ni KIFO, Kwa hivyo tunapoondoka hapa kila Mmoja kwa wakati wake tunapata mara moja majibu ya misimamo ya Imani zetu.

Unahisi ni kwanini dini Moja kazi yake ni kupingana na Ukristo klla kukicha, na kuna watu wanaabudu ng'ombe, sijui paka, Yani sisi tunakula nyama ya ng'ombe wao wanaabudu ng'ombe na husikii hiyo dini ikipingana na watu wa aina hiyo...

Kaa chini ufikirie sawa sawa, Mungu kaamua kuuvaa mwili wa kibinadamu na aishi kibinadamu Kwa kutimiza lengo lake Sasa unauliza...

Hivi umesoma BIBLIA kuona maisha ya YESU KRISTO yalikuwaje na hata kuondoka kwake hapa duniani?

Sio Kila mtu mitandaoni ana Nia ya kuelimisha mwingine kazi yake ni kupoteza watu.
 
Qur'an si mkusanyiko wa vitabu sasa utasemaje kuna vitabu vya biblia? Biblia ina hadi barua za watu humo ndani. Qur'an haina vitabu vyengine ni kitabu chenye kujitegemea.

Halafu mimi sizungumzii maana ya ukristo au wakristo wanavyoamini kuhusu ukristo, hata mimi naweza kuanzisha dini yangu mwaka huu 2024 nikaiita Tanganyika. Sasa maana ya hilo jina Tanganyika au historia kuhusu hilo jina haifanyi kuwa dini yangu hiyo ilikuwepo kabla ya mwaka 2024.
 
Jibu swali
Taurati inasema Ishmael na kizazi chake waliishi Jangwa la Parani

Ushahidi wa ramamani za Bibilia hapo chini unadhihirisha kuwa kuwa Ishmael na kizazi chake waliishi Saudi Arabia ya Sasa wewe unapinga

Sio unajizungusha na kuleta porojo ambazo hazina maana
Jibu swali hilo Jangwa la Parani ambako kunapatikana vizazi vya Ishmael Kwa Sasa ni nchi gani?
 

Attachments

  • Screenshot_20241215-222726.jpg
    429.8 KB · Views: 5
  • Screenshot_20241215-215915.jpg
    433.5 KB · Views: 5
  • Screenshot_20241215-150429.jpg
    509.3 KB · Views: 4
Kwani Juzuu ni kitu gani?
 
Biblia ilivyo kuna mambo watu wanapingana na wote wanatumia biblia hiyo kutoa ushahidi.
 
Wakati wakristo wakiishi Kwa agano jipya, Uislamu umerudi kuishi kwa agano la kale.

Mambo kama kutokula nyama ya nguruwe, mambo kama adhabu za kupigwa mawe, Sheria za vyakula, hayo ni mambo yapo katika agano la kale.

Tofauti ya BIBLIA na Quran Kwa wakati wote ni mtazamo kumhusu YESU, majini n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…