DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Ukisoma Waebrania uliyoiandika Utagundua Kitu..Ndiyo, majini ni viumbe ambao asili yao ni ya kimalaika, kwani waliumbwa kama malaika, viumbe wa kiroho wenye nguvu na mamlaka kubwa. Hata hivyo, baada ya kuasi Mungu, sifa zao zilibadilika na kuwa viumbe waovu, lakini hawakupoteza kabisa sifa za msingi za kuwa viumbe wa kiroho. Kwa hivyo, majini wanashiriki baadhi ya sifa za kimalaika, ingawa sasa wanaitwa mapepo au malaika wa giza.
Malaika waliumbwa kwa Moto , Shetani pia ambaye asili yake ni malaika aliumbwa kwa moto
Waebrania 1
7.Lakini kuhusu malaika, alisema:
“Amewafanya malaika wake kuwa upepo,na wahudumu wake ndimi za moto.”
Sema umeenda kasi sana ungeenda Pole pole Ungeelewa Tz mbongo ..
Na hapa Ndo nilitaka Mtu apagusie Kabisa..
Kuna Viumbe wawili wametajwa hapa.. Kwenye Waebrania (Biblia)..
Ngoja Tusome Biblia Sasa tuache longo longo..
Ukisoma Kwenye Lugha Asili ya Ilivyoandikwa Koine Greek Husomeka Hivi..Hii ni Waebrania 1:7
"Καὶ πρὸς μὲν τοὺς ἀγγέλους λέγει· Ὁ ποιῶν τοὺς ἀγγέλους αὐτοῦ πνεύματα καὶ τοὺς λειτουργοὺς αὐτοῦ πυρὸς φλόγα."
Au hutamkwa Hivi..
"Kai pros men tous angelous legei: Ho poiōn tous angelous autou pneumata kai tous leitourgous autou pyros phloga."
Na nikupitishe kwa Tafsiri kidogo.ya Kiswahili..
"Na kwa habari za malaika asema, Yeye Aumbaye malaika kwa Kutumia Upepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto."
Hapo Utaona Kuna Viumbe wawili Mungu ana wataja kuwaumbwa Kiumbe wa Kwanza ἀγγέλους "Angelos" au kwa Lugha yetu ya kiswahili Malaika na Kiumbe wa Pili ambaye ametafsiriwa kama mtumishi ni λειτουργοὺς "leitourgous" ambapo Biblia imemtafasiri kama Mtumishi..
Kwahyo Kati ya Viumbe hawa Wawili malaika na Watumishi wakristo wamebase sana Kuwasoma Hawa malaika ila hakuna mahali wamewahi kuchukua Mda kuwasoma Watumishi...
kwa asili yao Malaika ni wameumbwa kwa Nuru na Upepo hakuna anayepinga kati ya Hizo dini tatu zote Waislamu, Wayahudi na Wakristo..
Malaika hakuumbwa kwa Moto..
sasa Tuangalie Nani aliumbwa Kwa Moto ndo tutamjua Kuwa Huyo ndo mtumishi (Tena Miale ya Moto)
Sasa naona Zaidi Umegusia Quran Kuelezea Ama Kuthibitisha Usemacho na Mimi Naomba Nipitie Quran Hiyo hiyo..
Soma Surah Ar-Rahman aya ya 14 na 1
خَلَقَ ٱلْإِنسَٰنَ مِن صَلْصَٰلٍۢ كَٱلْفَخَّارِ
وَخَلَقَ ٱلْجَآنَّ مِن مَّارِجٍۢ مِّن نَّارٍۢ
Inatakwa Hivi!
"Khalaqa alinsana min salsalin kaalfakhkhari
Wakhalaqa aljanna min marijin min narin"
Kiswahili..
"Amemuumba Mtu kutoka katoka Udongo wa Kufinyanga
Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.."
Sasa Conlusion Yangu Isiyo rasmi kwa Kuwa Kwenye Waebrania Malaika ameumbwa kwa Upepo na Hao "Watumishi kwa Miale ya Moto ambayo ni sawa na Kusema Ulimi wa Moto..
watumishi Hao ni Majini..
Kwahyo Majini waliumbw tofauti kabisa na Malaika na yoyote anayesema Majini ni malaika walioasi aje na Uthibitisho..
Na Umeeleza Vyema sana Hapa Chini
kwa mujibu wa Qur'an na mafundisho ya Uislamu, shetani (Ibilisi) aliumbwa kwa moto. Katika Qur'an, sura ya 15 (Al-Hijr), aya ya 27, inasema:
"Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo wa joto."
Ibilisi alikuwa miongoni mwa majini, na majini waliumbwa kwa moto. Tofauti hii ya asili kati ya Ibilisi na binadamu (ambao waliumbwa kwa udongo) ndiyo moja ya sababu iliyomfanya Ibilisi kumkataa Adamu alipoamrishwa kumsujudia, kama ilivyoelezwa katika Qur'an, sura ya 7 (Al-A'raf), aya ya 12.