Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

Sijakuelewa Lini Shetani alifukuzwa na Yesu?
Sijaelewa Ulichoandika kabisa hebu Jitahidi kama Utaweza unielewwshe zaidi..

Siwezi kusema ni tarehe ipi shetani aliyofukuzwa mbinguni. Lkn naweza kuwa na uhakika kwamba alifukuzwa baada ya Yesu kuzaliwa, kuishi duniani, kufa, kufufuka na kwenda mbinguni. Maana Mtume Yohana alivyokuwa anafunuliwa maono hayo alikuwa kwenye kisiwa cha Patmos. Muda mrefu baada ya Yesu kurudi mbinguni.
 
Ndugu Mimi huko siwezi kurudi maana hoja zangu umezijibu juu juu tu ,

Kwanza ndio unazidi kuzalisha maswali mengi zaidi ,

Kupanua Hoja na Kukanusha

Nitapanga hoja na kuzikanusha moja baada ya nyingine, kisha nitatengeneza maswali ya kumchallange kutokana na mada hii.

Hoja 1: Uzima wa milele unapatikana kwa kumtambua Mungu mmoja na Yesu kama mjumbe wake (Yohana 17:3).

Yohana 17:3 haisemi kuwa Yesu ni mjumbe tu wa Mungu kama inavyodaiwa. Yesu alitumia neno "kujua" kwa maana ya uhusiano wa karibu na wa kiroho kati ya mwanadamu na Mungu kupitia kwake. Hii ni tofauti kabisa na maana inayotolewa katika Uislamu. Zaidi ya hayo, Yohana 14:6 Yesu alisema, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Hii inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu kama njia pekee ya uzima wa milele.

Hoja 2: Mungu hana mtoto, na watu wote ni watoto wa Mungu.

Yesu alijitaja kama Mwana wa Mungu kwa maana ya kipekee (Yohana 10:30), akithibitisha uhusiano wake wa kiungu na Baba. Lugha ya Biblia kuhusu "Mwana wa Mungu" haimaanishi uzazi wa kibinadamu, bali inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu katika utatu mtakatifu. Wakati Yohana 20:17 inataja "Baba yangu na Baba yenu," Yesu hakumaanisha usawa baina yake na wanadamu, bali alitofautisha uhusiano wake wa kiungu.

Hoja 3: Uislamu ulianza na manabii wote wa zamani.

Quran inadai kuwa manabii wote walikuwa Waislamu, lakini historia ya Biblia inaonyesha kwamba Wayahudi waliabudu kwa mujibu wa Agano la Kale, si kwa kufuata Qur’an. Hakuna ushahidi wa kihistoria au wa maandiko unaoonyesha kuwa Ibrahim, Isaka, au Yakobo walikuwa Waislamu kwa maana inayotolewa na Uislamu. Uislamu kama dini ya Muhammad ulianza karne ya 7 BK, wakati Uyahudi na Ukristo vimekuwepo karne nyingi kabla yake.

Hoja 4: Yesu alisali kwa kusujudu na kufuata Taurati.

Yesu hakufundisha sheria za Taurati pekee bali alikamilisha maana yake (Mathayo 5:17). Kusujudu kwake katika Mathayo 26:39 ni ishara ya unyenyekevu, si ibada ya Kiislamu. Yesu alifundisha kwamba uhusiano na Mungu unapatikana kupitia imani kwake, si kufuata sheria ya Taurati tu (Yohana 6:29).

Hoja 5: Injili zimepotoshwa na hazina uthibitisho.

Kuna ushahidi wa kihistoria kwamba Injili ziliandikwa na watu waliokuwa karibu na Yesu au walioshuhudia matukio yake. Ingawa ziliandikwa kati ya miaka 30-70 baada ya Yesu, maandishi hayo yaliendelezwa kwa mdomo kabla ya kuandikwa. Ushahidi wa maandiko ya kale, kama vile manuskripti za Dead Sea Scrolls, unaonyesha uthabiti wa maandiko ya Biblia. Tuhuma dhidi ya Injili hazina uthibitisho wa kitaalamu bali ni maoni yasiyo na msingi.

Nina maswali kwako

1. Yohana 17:3 inasema kumjua Yesu ni sehemu ya uzima wa milele, je, hili linafanana na imani ya Kiislamu ambayo inamwona Yesu kama nabii wa kawaida?

2. Ikiwa manabii wote walikuwa Waislamu, kwa nini hakuna ushahidi wa kihistoria wa maandiko yao yanayosema hivyo kabla ya Qur’an?

3. Je, unakubaliana kuwa Ibrahim, Isaka, na Yakobo walikuwa Wayahudi kwa mujibu wa Biblia, si Waislamu?

4. Mathayo 26:39 inaonyesha Yesu akisali kwa Baba yake. Kwa nini unadhani Yesu alifundisha Mungu kama Baba wa pekee wa wanafunzi wake?

5. Umewezaje kuhitimisha kuwa Injili zimepotoshwa wakati ushahidi wa kihistoria wa maandiko ya kale unaonyesha uthabiti wake?

6. Yesu alisema alikuja kukamilisha Taurati (Mathayo 5:17). Kwa nini unadai alikuwa mfuasi wa Taurati bila mabadiliko?

7. Ikiwa Yesu alisujudu kwa Mungu, je, hili linathibitisha kuwa alikuwa Muislamu au ni ishara ya unyenyekevu wake kama mwana wa Mungu?

8. Kwa nini Qur’an inadai Yesu hajisulubiwa, wakati ushahidi wa kihistoria wa Kirumi unathibitisha kifo chake msalabani?

9. Je, unakubaliana kwamba imani ya Kikristo kuhusu Yesu inategemea maandiko ya kale yaliyoandikwa karne nyingi kabla ya Uislamu?

10. Ikiwa Injili ziliandikwa na watu waliomshuhudia Yesu, kwa nini unakubali Qur’an iliyoandikwa karne kadhaa baadaye bila mashahidi wa moja kwa moja?
Hakuna kazi ngumu Kwa mgalatia kama kuutetea ukristo Kwa kutumia maandiko

1)
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Hili andiko limekamilika na lipo Kwa lugha nyepesi sana wewe sio kama haulielewi ila wewe hauliamini Kwa sababu ukiliamini hili andiko utakuwa Muislam kama Yesu

Jambo la Yesu kuwa ni nabii aliyetumwa na Mungu hilo halina mjadala

Utabiri wa Yesu hili andiko limekopiwa kutoka Kwa mtume Mika Mungu anasema atamtuma Yesu kuwachunga waisrael
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

Hapa Yesu anathibisha kuwa utabiri wa Mika upo sahihi
Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Na ndipo Yesu akapigia msumali kuwa Ili uende peponi lazima ukubali Yesu ametumwa na Mungu mmoja tu

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Quran nayo ilipokuja ikapigilia msumali kuwa Yesu ni mtume wa Mungu

Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati

Kwahiyo hayo mnayofundishana huko kanisani hizo zinaitwa DOGMA Yani kubadilisha ukweli na kuwa uongo

Ila ukweli utabaki kama ulivyo Yesu ni binadamu wa kawaida na ni mtume wa Mungu kama walivyo mitume wengine

2) Manabii wote walikuwa waislam na ushahidi ndani ya Bibilia upo
Nguzo za uislam
1) kuamini Mungu ni mmoja na Mtume wenu ametumwa na huyo Mungu mmoja
2) kufanya ibada ya kusali Kwa kusujudi
3) Kutoa zaka
4) kuifunga saumu
5) kuenda Hija

Hayo yote yapo ndani ya Bibilia nakuonyedha mawili kusali Kwa kusujudi na Hija
Hija ni eneo ambalo Mungu analichagua mnatakiwa mkisali muangalie huko na pia muende huko

Kumbukumbu la Torati 12:5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko
Kumbukumbu la Torati 12:6
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;

Nabii Musa anasali
Kutoka 34:8
Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu.
Kutoka 34:9
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.

Hapa Ezra ni Imamu anawasalisha wenziwe
Nehemia 8:4
Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu.
Nehemia 8:5
Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama;
Nehemia 8:6
Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.

3) Kusema kuwa Ibrahim, Isaka na Yakobo walikuwa Wayahudi huo ni umbumbu wako wa kiwango Cha Rami

Yahudi ni Jina la mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda kabla huyo mtoto hajazaliwa kulikuwa hakuna jina linaloitwa Uyahudi
Hapo ju Kuna comment mgalatia mwenzako pia anasema Ibrahim na Isaka na Yakobo hawakuwa na dini ya kiyahudi hi ni jinsi gani inaonyesha hamuna mlijualo mpo mpo tu

Ibrahim Isaka na Yakobo walikuwa waislam

4) Kwa mujibu wa bibilia sala aliyofundisha Yesu ni hii

Mungu sio baba yake peke yake ila ni baba yenu nyote

Kila kitu unatakiwa umuombe Mungu na Wala sio Yesu

Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mathayo 6:10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Mathayo 6:11
Mathayo 6:12
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6:13
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.

5) Injili Ina majanga makubwa sana ila ndio hivyo hao wandishi wamspewa majina ya wanafunzi wa Yesu Ili wakudanganyeni vizuri

A) Idadi ya Chapter inatofautiana katika Injili zote nne Mathayo 28, Mariko 16, Luka 24, Yohana 21 kama wote walikuwa wanaandika anayoyasema Yesu Kwa Nini watofautiane tena Kwa kiwango kikubwa

B) Wandishi wa hizo Injili sio wanafunzi wa Yesu

Luka aliandika Kwa uliza uliza na kutunga

Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Aliye andika Injili ya Yohana Hadi Leo hii hajulikani ni nani
Na kuanzia Yohana 1:1 Hadi Yohana 1:36 ni Maneno ya mwandishi ambaye hajulikani

We may never know for certain who wrote the Gospel of John, any more than we can know who wrote the books of Matthew, Mark and Luke. We do know that John is a gospel apart, however. Early Matthew, Mark and Luke are so alike in their telling that they are called the Synoptic Gospels, meaning “seen together”—the parallels are clear when they are looked at side by side. Matthew and Luke follow the version of events in Mark, which is thought by scholars to be the earliest and most historically accurate Gospel. John, however, does not include the same incidents or chronology found in the other three Gospels, and the fact that it is so different has spurred a debate over whether John’s Gospel is historical or not, something that has been noted in Gospel of John commentary for hundreds—even thousands—of years.
Source website ya Cambridge university
C) Injili ya Barnabas ndio Injili pekee ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu lakini imetolewa katika Bibilia Ili nyinyi wakristo msiisome it's means ipo tofauti kabisa na mafundisho ya ukristo
6) Yesu na Taurati
Mbona maandiko yapo wazi kuhusu Yesu na Taurati
Mathayo 5:17
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Mathayo 5:18
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Mathayo 5:19
Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

7) Kusujudi
Lengo la kusujudi ni kumnyenyekea Mungu muumba wa Kila kitu na sio ombi ni amri
Mathayo 4:9
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

8) Quran inasema hajusurubiwa na Wala hajafa msalabani
Nao wanasema hayo hawana uhakika ila wanadhania dhania tu
Tuangalie ndani ya Bibilia je waliosema Yesu amesurubiwa wanao uhakika?

Mariko anasema saa tatu Yesu yupo msalabani anasurubiwa

Marko 15:25
Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Marko 15:26
Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.

Yohana anapinga Mariko anasema hapa Saa sita Yesu alikuwa yupo mahakamani Kwa Pilato

Yohana 19:13
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Yohana 19:14
Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Yohana 19:15
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.

Labda wewe ujibu swali ni Yesu gani saa tatu yupo msalabani? Na Yesu gani saa sita yupo Mahakamani?

9) Ni kweli maandiko yalioanzisha dini ya ukristo yalikuwepo kabla ya uislam ila sio mandiko ya Mungu ni maandiko ya uongo yakiwepo maandiko ya Paulo maana Paulo sio mtume wa Mungu ni tapeli tu wa kidini wakolitho, wagalatia, Warumi,Tito sijui Efeso hivi ndio vitabu vya wakristo na ndio vilivyoleta ukristo

10) Injili hazijaandikwa na watu walio mshuhudia Yesu acha uongo Injili tukuamini wewe au tuamini maandiko?

Injili ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu ni Moja tu ya Barnaba na hao walianzisha ukristo wameificha Ili musiione

Kuhusu Quran kitabu chenyewe kinasema hakina shaka
Quran 2:2
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,
 
Bila biblia na ukristo, hakuna quran wala uislam. Quran na uislam vimejengwa kwenye torati ambayo ilianzia kwenye ukristo. Hadithi zake kuu kama vile uumbaji wa Adam na Hawa, ukuu wa Ibrahim kama baba wa wote, sharia, tabia na mengine vina asili kwenye torati. Najiuliza. Kama ukristo ungedukua quran, ingekuwaje?
Unamaanisha hakuna ukristo bila uyahudi pia au sio? ... Yesu, Musa, Daudi, Isaac n.k wote walikuwa wayahudi sasa vp wewe unaona kuwa wewe ndo una hati miliki nao?

Kwenye biblia yenu mna mpaka torati humo, inawahusu vp torati wakristo?

Usiendeshwe na chuki, tumia fuvu hilo kufikiria sio kusikitika tu.
 
Siwezi kusema ni tarehe ipi shetani aliyofukuzwa mbinguni. Lkn naweza kuwa na uhakika kwamba alifukuzwa baada ya Yesu kuzaliwa, kuishi duniani, kufa, kufufuka na kwenda mbinguni. Maana Mtume Yohana alivyokuwa anafunuliwa maono hayo alikuwa kwenye kisiwa cha Patmos. Muda mrefu baada ya Yesu kurudi mbinguni.
I just went to see hizo verses na sidhani kama huyo aliyemtokea alikuwa na nia njema nae, yani
  • Kinywani anatoa upanga wenye makali pande mbili, kwa ajili ya nani?
  • Sauti yake ni kama maporomoko ya maji, anamtisha nani?
  • Ana miguu ya shaba, ili iweje?
Tunaona Yohana anabashiriwa kuhusu kanisa wakati Yesu mpaka anaondoka hajawahi kutaja neno kanisa achilia mbali kujenga imani yake juu ya hiyo kitu

Yani just kwa kutokewa na kiumbe wa ajabu ndo nyie mnafuata, uthibitisho wa hayo mumeyatoa wapi?

Pia, inanishangaza sana nyie kuegemeza imani yenu kwa madai ya watu bila ya ushahidi wala evidence yoyote, huyu alitokewa na huyo aliyemtokea na alikuwa peke yake, kakuambieni (kama sio story ya kutengenezwa na warumi) na nyie mumeamini mazima. Paulo pia alikuleteeni hadithi kama hizi na ndo mkajenga dini yenu kupitia hadithi zake.
 
Hilo tatizo lingine, unajua kama Uyahudi ni Ukafiri ? Vipi Yesu awe Myahudi ? Unajua maana ya tamko Uyahudi au dini ya Uyahudi ?

Unajua Uyahudi kama dini imeanza lini ?
Yesu Kristo alizaliwa katika familia ya Kiyahudi na kulelewa katika mila na desturi za Wayahudi. Uyahudi, kama kitambulisho cha kijamii, kikabila, na kidini, kilikuwa sehemu ya maisha ya watu wa Israeli wa wakati huo. Yesu alizaliwa huko Bethlehemu (eneo la Wayahudi) na wazazi wake walikuwa Waisraeli wa ukoo wa Daudi.

Katika maisha yake, Yesu alifuata baadhi ya sheria za Kiyahudi, kama vile kuhudhuria masinagogi, kusherehekea sikukuu za Kiyahudi kama Pasaka (Passover), na kusoma Torati.

Uyahudi (Judaism) ni mchanganyiko wa dini, tamaduni, na historia ya Wayahudi. Kwa kifupi:

Uyahudi ni mfumo wa imani unaojikita kwenye Torati (vitabu vitano vya kwanza vya Biblia) na maandiko ya Kiyahudi (Tanakh).

Kiutamaduni, Uyahudi unajumuisha mila, desturi, na historia ya watu walio wa ukoo wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo.

Uyahudi haukuanza kama dini rasmi mara moja, bali ulijengwa hatua kwa hatua kupitia matukio ya kihistoria:

Msingi wa Uyahudi: Unahusishwa na Agano la Mungu na Abrahamu, takriban miaka 2000-1800 KK. Hii ni kama asili ya kiimani ya Uyahudi.

Torati ya Musa: Inachukuliwa kama hatua rasmi ya Uyahudi wa kidini, takriban 1200 KK, baada ya Musa kupokea Amri Kumi na sheria nyingine kutoka kwa Mungu katika Mlima Sinai.

Uyahudi wa kisasa: Ulianza kuonekana baada ya Uhamisho wa Babeli (karne ya 6 KK) ambapo Wayahudi waliimarisha taasisi kama masinagogi na maandiko ya kidini yaliandikwa kwa umakini zaidi.

Kwa hivyo, Uyahudi kama dini ya kimapokeo ulianza kuchukua sura yake rasmi karibu na karne ya 6 KK.
 
Uislamu hujui, hili la kwanza. Uislamu umegawanyika sehemu kuu mbili :
1. Uislamu wa ujumla, ambao ndio manabii na mitume wote dini yao ni Moja.

2. Uislamu alio kuja nao Mtume Muhammad, huu ni tofauti kwa sababu ya Sheria tu ila Imani ni Moja kwa mitume wote na manabii wote.

Hivi unaujua Uyahudi lakini au unaandika tu. Yaani kwa akili yako tu ya kawaida, Mtume wa Allah awe Myahudi yaani kafiri aliye potea ? Hivi marejeo yenu ya haya mnayo yaandika huwa ni wapi ?

Yesu alisema kuwa njia ya wokovu ni kupitia kwake tu (Yohana 14:6). Manabii wa Agano la Kale walifundisha Torati kama sheria ya imani (Kutoka 19:5), tofauti na Uislamu wa ujumla.

Qur'an: Mitume walikuja na ujumbe maalum kwa kila taifa (Qur'an 16:36), kinyume na wazo la "Uislamu wa ujumla."

Alichofundisha Yesu na manabii wengine ni tofauti kabisa na Muhammad

Biblia: Yesu alifundisha juu ya neema, sio sheria nyingi (Waefeso 2:8-9).

Qur'an: Sheria za dini zilikuwa tofauti kwa kila mtume (Qur'an 5:48), hivyo Uislamu wa Mtume Muhammad hauwezi kuwa sawa na dini za manabii wengine.

Kwahiyo Yesu mnayemuita Mtume wa Allah kuwa ni "kafiri aliye potea" maana ni myahudi ,ushahidi huu hapa👇👇

Biblia: Yesu alikuwa Myahudi (Warumi 15:12).

Qur'an: Manabii wengi walikuwa wa Wana wa Israeli (Qur'an 2:87)

Maandiko ya Biblia na Qur'an yanaonyesha kuwa mafundisho na sheria za mitume zilikuwa tofauti, na hoja ya "Uislamu wa ujumla" inapinga ukweli wa maandiko haya.

Na maswali haya👇👇

1. Kama manabii walikuwa na "Imani Moja," kwa nini sheria zao zilikuwa tofauti?

2. Ikiwa Yesu alikuwa Myahudi na Qur'an inamkubali kama Mtume, kwa nini Uyahudi uonekane kama "ukafiri"?

3. Qur'an inasema mitume walitumwa kwa taifa lao maalum (Qur'an 16:36). Hii haipingani vipi na wazo la Uislamu wa ujumla?
 
Hakuna kazi ngumu Kwa mgalatia kama kuutetea ukristo Kwa kutumia maandiko

1)
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Hili andiko limekamilika na lipo Kwa lugha nyepesi sana wewe sio kama haulielewi ila wewe hauliamini Kwa sababu ukiliamini hili andiko utakuwa Muislam kama Yesu

Jambo la Yesu kuwa ni nabii aliyetumwa na Mungu hilo halina mjadala

Utabiri wa Yesu hili andiko limekopiwa kutoka Kwa mtume Mika Mungu anasema atamtuma Yesu kuwachunga waisrael
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

Hapa Yesu anathibisha kuwa utabiri wa Mika upo sahihi
Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Na ndipo Yesu akapigia msumali kuwa Ili uende peponi lazima ukubali Yesu ametumwa na Mungu mmoja tu

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Quran nayo ilipokuja ikapigilia msumali kuwa Yesu ni mtume wa Mungu

Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati

Kwahiyo hayo mnayofundishana huko kanisani hizo zinaitwa DOGMA Yani kubadilisha ukweli na kuwa uongo

Ila ukweli utabaki kama ulivyo Yesu ni binadamu wa kawaida na ni mtume wa Mungu kama walivyo mitume wengine

2) Manabii wote walikuwa waislam na ushahidi ndani ya Bibilia upo
Nguzo za uislam
1) kuamini Mungu ni mmoja na Mtume wenu ametumwa na huyo Mungu mmoja
2) kufanya ibada ya kusali Kwa kusujudi
3) Kutoa zaka
4) kuifunga saumu
5) kuenda Hija

Hayo yote yapo ndani ya Bibilia nakuonyedha mawili kusali Kwa kusujudi na Hija
Hija ni eneo ambalo Mungu analichagua mnatakiwa mkisali muangalie huko na pia muende huko

Kumbukumbu la Torati 12:5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko
Kumbukumbu la Torati 12:6
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;

Nabii Musa anasali
Kutoka 34:8
Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu.
Kutoka 34:9
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.

Hapa Ezra ni Imamu anawasalisha wenziwe
Nehemia 8:4
Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu.
Nehemia 8:5
Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama;
Nehemia 8:6
Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.

3) Kusema kuwa Ibrahim, Isaka na Yakobo walikuwa Wayahudi huo ni umbumbu wako wa kiwango Cha Rami

Yahudi ni Jina la mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda kabla huyo mtoto hajazaliwa kulikuwa hakuna jina linaloitwa Uyahudi
Hapo ju Kuna comment mgalatia mwenzako pia anasema Ibrahim na Isaka na Yakobo hawakuwa na dini ya kiyahudi hi ni jinsi gani inaonyesha hamuna mlijualo mpo mpo tu

Ibrahim Isaka na Yakobo walikuwa waislam

4) Kwa mujibu wa bibilia sala aliyofundisha Yesu ni hii

Mungu sio baba yake peke yake ila ni baba yenu nyote

Kila kitu unatakiwa umuombe Mungu na Wala sio Yesu

Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mathayo 6:10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Mathayo 6:11
Mathayo 6:12
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6:13
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.

5) Injili Ina majanga makubwa sana ila ndio hivyo hao wandishi wamspewa majina ya wanafunzi wa Yesu Ili wakudanganyeni vizuri

A) Idadi ya Chapter inatofautiana katika Injili zote nne Mathayo 28, Mariko 16, Luka 24, Yohana 21 kama wote walikuwa wanaandika anayoyasema Yesu Kwa Nini watofautiane tena Kwa kiwango kikubwa

B) Wandishi wa hizo Injili sio wanafunzi wa Yesu

Luka aliandika Kwa uliza uliza na kutunga

Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Aliye andika Injili ya Yohana Hadi Leo hii hajulikani ni nani
Na kuanzia Yohana 1:1 Hadi Yohana 1:36 ni Maneno ya mwandishi ambaye hajulikani

We may never know for certain who wrote the Gospel of John, any more than we can know who wrote the books of Matthew, Mark and Luke. We do know that John is a gospel apart, however. Early Matthew, Mark and Luke are so alike in their telling that they are called the Synoptic Gospels, meaning “seen together”—the parallels are clear when they are looked at side by side. Matthew and Luke follow the version of events in Mark, which is thought by scholars to be the earliest and most historically accurate Gospel. John, however, does not include the same incidents or chronology found in the other three Gospels, and the fact that it is so different has spurred a debate over whether John’s Gospel is historical or not, something that has been noted in Gospel of John commentary for hundreds—even thousands—of years.
Source website ya Cambridge university
C) Injili ya Barnabas ndio Injili pekee ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu lakini imetolewa katika Bibilia Ili nyinyi wakristo msiisome it's means ipo tofauti kabisa na mafundisho ya ukristo
6) Yesu na Taurati
Mbona maandiko yapo wazi kuhusu Yesu na Taurati
Mathayo 5:17
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Mathayo 5:18
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Mathayo 5:19
Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

7) Kusujudi
Lengo la kusujudi ni kumnyenyekea Mungu muumba wa Kila kitu na sio ombi ni amri
Mathayo 4:9
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

8) Quran inasema hajusurubiwa na Wala hajafa msalabani
Nao wanasema hayo hawana uhakika ila wanadhania dhania tu
Tuangalie ndani ya Bibilia je waliosema Yesu amesurubiwa wanao uhakika?

Mariko anasema saa tatu Yesu yupo msalabani anasurubiwa

Marko 15:25
Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Marko 15:26
Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.

Yohana anapinga Mariko anasema hapa Saa sita Yesu alikuwa yupo mahakamani Kwa Pilato

Yohana 19:13
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Yohana 19:14
Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Yohana 19:15
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.

Labda wewe ujibu swali ni Yesu gani saa tatu yupo msalabani? Na Yesu gani saa sita yupo Mahakamani?

9) Ni kweli maandiko yalioanzisha dini ya ukristo yalikuwepo kabla ya uislam ila sio mandiko ya Mungu ni maandiko ya uongo yakiwepo maandiko ya Paulo maana Paulo sio mtume wa Mungu ni tapeli tu wa kidini wakolitho, wagalatia, Warumi,Tito sijui Efeso hivi ndio vitabu vya wakristo na ndio vilivyoleta ukristo

10) Injili hazijaandikwa na watu walio mshuhudia Yesu acha uongo Injili tukuamini wewe au tuamini maandiko?

Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,

Injili ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu ni Moja tu ya Barnaba na hao walianzisha ukristo wameificha Ili musiione

Kuhusu Quran kitabu chenyewe kinasema hakina shaka
Quran 2:2
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,
Umeleta hoja nyepesi sana, kwanza unabagua maandiko, unadokoa yale unayoona yanaku favor,huo ni upuuzi

Nitajibu hoja zako kwa maandiko

1) Yesu kama Mtume wa Mungu

Ni kweli kuwa Yesu alitambulika kama mtume wa Mungu, lakini hii haimaanishi kuwa alikataa kuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Biblia inaonyesha wazi kuwa Yesu alijua nafasi yake kama Mwana wa Mungu. Katika Mathayo 16:15-17, Yesu alikubaliana na ukweli kuwa yeye ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Hata hivyo, Yesu alikubali kuwa alitumwa na Mungu, lakini hii haimnyimi kuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Hivyo, haifai kusema kuwa Yesu ni mtume tu na si Mungu, kwa kuwa yeye ni sehemu ya Utatu Mtakatifu, ambapo Yesu, Baba, na Roho Mtakatifu ni mmoja.

2) Manabii wote walikuwa Waislamu

Hii ni hoja ya kupotosha. Ingawa manabii wote walikuwa wakiishi kwa imani katika Mungu mmoja, hakuna ushahidi wa maandiko ambao unathibitisha kuwa manabii walikuwa waislamu kama vile Uislamu unavyofundishwa leo. Biblia inaonyesha kuwa manabii walikuwa wakimwabudu Mungu wa Israeli, na siyo tu Mungu mmoja wa Uislamu. Kwa mfano, Musa na nabii Daudi walikuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu wa Israeli, na walifuata sheria zilizotolewa kwao. Hivyo, kusema kuwa manabii wote walikuwa Waislamu ni kupotosha maana ya dini ya Uislamu na dini ya Israeli.

3) Ibrahim, Isaka na Yakobo hawakuwa Wayahudi

Hii ni kweli katika maana ya kisheria, kwa sababu "Wayahudi" wanahusiana na kizazi cha Yuda, mtoto wa Yakobo. Hata hivyo, Ibrahim, Isaka, na Yakobo walikuwa na imani katika Mungu mmoja, na ndilo lilikuwa lengo kuu la dini ya Israeli, ambayo baadaye ilijulikana kama dini ya Wayahudi. Biblia inasema wazi kuwa Ibrahim aliitwa rafiki wa Mungu (Isaya 41:8), na Yakobo alikubali ahadi ya Mungu kwa kizazi chake. Hivyo, wao walikuwa sehemu ya historia ya Wayahudi, ingawa hawakuwa Wayahudi kama vile tunavyowafahamu leo.

4) Sala aliyofundisha Yesu

Katika Mathayo 6:9-13, Yesu alifundisha sala ya kumwomba Mungu mmoja, na hili ni somo muhimu. Lakini kusema kuwa Yesu alikataa kumwabudu au kumsujudia Mungu mwenyewe ni kupotosha ukweli wa imani ya Kikristo. Yesu mwenyewe alijua kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, na alijua kuwa ni sehemu ya utatu mtakatifu, ambapo Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni mmoja. Hivyo, kumwomba Mungu ni muhimu, lakini kumtambua Yesu kama Mwana wa Mungu na sehemu ya Utatu ni muhimu katika imani ya Kikristo.

5) Utofauti katika Injili

Ni kweli kuwa kuna tofauti kati ya Injili za Mathayo, Marko, Luka, na Yohana, lakini hili haliwezi kuthibitisha kuwa Injili hizi ni za uongo. Utofauti huu unadhihirisha utofauti wa mtindo wa uandishi na mtazamo wa kila mwandishi, lakini zote zinathibitisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na alikuja duniani kwa ajili ya wokovu wa watu. Utofauti huu pia unahakikisha kuwa Injili za Kikristo zinatokana na mashahidi wa moja kwa moja na kwamba hazikupotoshwa.

6) Yesu na Taurati

Yesu alikubali na kutimiza Taurati, kama ilivyoelezwa katika Mathayo 5:17-19. Hii haiondoi ukweli kwamba yeye ni Kristo na Mwana wa Mungu. Yesu alikubali sheria na alikamilisha maana yake kwa kuwafundisha watu kumwambia Mungu kwa roho na ukweli, na siyo tu kwa kufuata sheria za kimwili. Alitimiza Taurati kwa kutoa agizo jipya la upendo na kumwabudu Mungu kwa moyo wote.

7) Kusujudi kwa Mungu

Ni kweli kuwa kusujudu ni kumwonyesha Mungu heshima, na hili linaonekana katika Mathayo 4:10. Lakini tunapaswa kuelewa kuwa kusujudu kwa Yesu ni kumtambua kuwa yeye ni Mwana wa Mungu na sehemu ya Utatu Mtakatifu. Yesu hakuzuia watu kumwabudu, na alikubali kwamba yeye ni Mungu mwenyewe. Katika Yohana 14:9, Yesu alisema kuwa aliyeona yeye ameona Baba, na hii inaonyesha umoja wao katika utatu.

8) Yesu na Kifo msalabani

Maandiko ya Biblia yanaendelea kudhibitisha kuwa Yesu alisulubiwa, na hili linathibitishwa katika Mathayo 27, Marko 15, Luka 23, na Yohana 19. Hata hivyo, watu wengine wanaweza kuwa na maswali kuhusu jinsi matukio hayo yalivyokuwa, lakini ukweli wa kifo cha Yesu msalabani ni sehemu muhimu ya wokovu wa Wakristo. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za dunia, na alifufuka kwa ushindi juu ya mauti.

9) Maandiko ya Paulo na Ukristo

Maandiko ya Paulo ni muhimu katika ufafanuzi wa imani ya Kikristo. Paulo alikuwa mtume wa Yesu na alifundisha juu ya wokovu kupitia imani katika Yesu Kristo. Vitabu vya Paulo, kama Warumi, Wagalatia, na Wafilipi, vinafundisha kuhusu wokovu na maisha ya Kikristo. Hivyo, kusema kwamba Paulo ni tapeli wa kidini ni kupotosha ukweli wa mafundisho yake.

10) Injili Hazijaandikwa na Wanafunzi wa Yesu

Injili za Mathayo, Marko, Luka, na Yohana zinajulikana kuwa ziliandikwa na waandishi waliokuwa na uhusiano wa karibu na matukio yaliyotokea wakati wa Yesu. Ingawa baadhi ya waandishi walikusanya habari kutoka kwa mashahidi wengine, maandiko haya yanahusiana na uhalisia wa maisha ya Yesu na mafundisho yake. Hivyo, kusema kuwa Injili hazijaandikwa na mashahidi wa Yesu ni kupotosha ukweli wa maandiko ya Biblia.
 
Biblia ndo kitabu gani hamna sehemu quran inasema bibli bali inataja taurat, zaburi na injil not bible
 
I just went to see hizo verses na sidhani kama huyo aliyemtokea alikuwa na nia njema nae, yani
  • Kinywani anatoa upanga wenye makali pande mbili, kwa ajili ya nani?
  • Sauti yake ni kama maporomoko ya maji, anamtisha nani?
  • Ana miguu ya shaba, ili iweje?
Tunaona Yohana anabashiriwa kuhusu kanisa wakati Yesu mpaka anaondoka hajawahi kutaja neno kanisa achilia mbali kujenga imani yake juu ya hiyo kitu

Yani just kwa kutokewa na kiumbe wa ajabu ndo nyie mnafuata, uthibitisho wa hayo mumeyatoa wapi?

Pia, inanishangaza sana nyie kuegemeza imani yenu kwa madai ya watu bila ya ushahidi wala evidence yoyote, huyu alitokewa na huyo aliyemtokea na alikuwa peke yake, kakuambieni (kama sio story ya kutengenezwa na warumi) na nyie mumeamini mazima. Paulo pia alikuleteeni hadithi kama hizi na ndo mkajenga dini yenu kupitia hadithi zake.

Kwa hiyo unaona ni kama hekaya tu
 
Bible imenakili ndo maana unakula walaka wa mtu na imeandikwa na watu wasiojulikana luka, mara john
 
Hebu tutafakari kidogo..Inadaiwa Uislamu ulikuwepo toka enzi za kale Ibrahimu,yesu na manabii wengine wote wanadaiwa kuwa walikuwa waislamu.
Maswali ya kujiuliza:
1.Inakuwaje vitabu vilivyotangulia..torati,injili na zaburi havijataja neno uislamu kama ilivyo katika quran?
2.Kama yesu alikuwa muislamu mbona mafundisho yanaonesha mara kadhaa wakati anaomba alikuwa anataja baba yangu?? kitu kinachopingana na uislqmu kuwa Mungu hana mwana.Pia katika kuomba mara nyingi Yesu alikuwa anaangalia mbinguni,wakati waislamu wakiswali wanakuwa wanaelekea kibra?

Mimi naamini Quran imecopy biblia kwa sababu zifuatazo;
Biblia inasema Yesu ni neno -Quran nayo inasema ni neno
Biblia inasema Yesu ni roho wa Mungu-Quran nayo inasema vivyo hivyo
Biblia inasema yesu alizaliwa na Bikira na alianza kuongea toka akiwa mdogo -Quran nayo inasema hivyo hivyo
Biblia inasema Yesu alikufa ,akafufuka na akapaa mbinguni..Hapa ndio waislamu walipoitengeneza imani yao..ila kitabu chao kinawasuta bado
Kwenye quran Yesu mwenyewe anatamka kwamba amani iwe juu yake siku aliyozaliwa,siku atakayokufa na siku atakayonyanyuliwa Je tujiulize swali dogo tu je Yesu hajafa bado kwa Mujibu wa quran?
Kama jibu ni kuwa hajafa kwa nini aanze kunyanyuliwa kabla ya kufa..kwa nini step moja irukwe?
Allah mwenyewe anasema Issa nitakufisha na nitakunyanyua kwangu.
Kwa mujibu wa quran Yesu ameshanyanyuliwa na yupo kwa Allah kama biblia inavyoamini yupo kuume kwa Mungu baba.Sasa swali linakuja ,kwa nini aanze kumnyanyua kabla ya kumfisha.Wanazuoni wengi wamekuja na hoja dhaifu kwamba aliposema nitakufisha hakumaanisha kwamba atakufa,bali atawababaisha wauaji waone kama aliyemuua ni yeye kumbe mtu mwingine kavishwa sura ya Yesu(Seriously)? Kwa nini Allah afanye mazingaombwe hayo na wakati yesu mwenyewe alijitabiria kufa kabla ya kunyanyuliwa(Something fishy).
 
Ndiyo, majini ni viumbe ambao asili yao ni ya kimalaika, kwani waliumbwa kama malaika, viumbe wa kiroho wenye nguvu na mamlaka kubwa. Hata hivyo, baada ya kuasi Mungu, sifa zao zilibadilika na kuwa viumbe waovu, lakini hawakupoteza kabisa sifa za msingi za kuwa viumbe wa kiroho. Kwa hivyo, majini wanashiriki baadhi ya sifa za kimalaika, ingawa sasa wanaitwa mapepo au malaika wa giza.

Malaika waliumbwa kwa Moto , Shetani pia ambaye asili yake ni malaika aliumbwa kwa moto

Waebrania 1

7.Lakini kuhusu malaika, alisema:
“Amewafanya malaika wake kuwa upepo,na wahudumu wake ndimi za moto.”

kwa mujibu wa Qur'an na mafundisho ya Uislamu, shetani (Ibilisi) aliumbwa kwa moto. Katika Qur'an, sura ya 15 (Al-Hijr), aya ya 27, inasema:

"Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo wa joto."

Ibilisi alikuwa miongoni mwa majini, na majini waliumbwa kwa moto. Tofauti hii ya asili kati ya Ibilisi na binadamu (ambao waliumbwa kwa udongo) ndiyo moja ya sababu iliyomfanya Ibilisi kumkataa Adamu alipoamrishwa kumsujudia, kama ilivyoelezwa katika Qur'an, sura ya 7 (Al-A'raf), aya ya 12.
Ila mkuu mafundisho ya uislamu yanamueleza jini kuwa ni kiumbe tofauti na malaika na binaadamu, na hata kuumbwa kwao hao viumbe wameumbwa kwa vyanzo tofauti.
 
Bila biblia na ukristo, hakuna quran wala uislam. Quran na uislam vimejengwa kwenye torati ambayo ilianzia kwenye ukristo. Hadithi zake kuu kama vile uumbaji wa Adam na Hawa, ukuu wa Ibrahim kama baba wa wote, sharia, tabia na mengine vina asili kwenye torati. Najiuliza. Kama ukristo ungedukua quran, ingekuwaje?
Huu ni ugomvi muheshimiwa Nasrallah!
 
Back
Top Bottom