Ndugu Mimi huko siwezi kurudi maana hoja zangu umezijibu juu juu tu ,
Kwanza ndio unazidi kuzalisha maswali mengi zaidi ,
Kupanua Hoja na Kukanusha
Nitapanga hoja na kuzikanusha moja baada ya nyingine, kisha nitatengeneza maswali ya kumchallange kutokana na mada hii.
Hoja 1: Uzima wa milele unapatikana kwa kumtambua Mungu mmoja na Yesu kama mjumbe wake (Yohana 17:3).
Yohana 17:3 haisemi kuwa Yesu ni mjumbe tu wa Mungu kama inavyodaiwa. Yesu alitumia neno "kujua" kwa maana ya uhusiano wa karibu na wa kiroho kati ya mwanadamu na Mungu kupitia kwake. Hii ni tofauti kabisa na maana inayotolewa katika Uislamu. Zaidi ya hayo, Yohana 14:6 Yesu alisema, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Hii inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu kama njia pekee ya uzima wa milele.
Hoja 2: Mungu hana mtoto, na watu wote ni watoto wa Mungu.
Yesu alijitaja kama Mwana wa Mungu kwa maana ya kipekee (Yohana 10:30), akithibitisha uhusiano wake wa kiungu na Baba. Lugha ya Biblia kuhusu "Mwana wa Mungu" haimaanishi uzazi wa kibinadamu, bali inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu katika utatu mtakatifu. Wakati Yohana 20:17 inataja "Baba yangu na Baba yenu," Yesu hakumaanisha usawa baina yake na wanadamu, bali alitofautisha uhusiano wake wa kiungu.
Hoja 3: Uislamu ulianza na manabii wote wa zamani.
Quran inadai kuwa manabii wote walikuwa Waislamu, lakini historia ya Biblia inaonyesha kwamba Wayahudi waliabudu kwa mujibu wa Agano la Kale, si kwa kufuata Qur’an. Hakuna ushahidi wa kihistoria au wa maandiko unaoonyesha kuwa Ibrahim, Isaka, au Yakobo walikuwa Waislamu kwa maana inayotolewa na Uislamu. Uislamu kama dini ya Muhammad ulianza karne ya 7 BK, wakati Uyahudi na Ukristo vimekuwepo karne nyingi kabla yake.
Hoja 4: Yesu alisali kwa kusujudu na kufuata Taurati.
Yesu hakufundisha sheria za Taurati pekee bali alikamilisha maana yake (Mathayo 5:17). Kusujudu kwake katika Mathayo 26:39 ni ishara ya unyenyekevu, si ibada ya Kiislamu. Yesu alifundisha kwamba uhusiano na Mungu unapatikana kupitia imani kwake, si kufuata sheria ya Taurati tu (Yohana 6:29).
Hoja 5: Injili zimepotoshwa na hazina uthibitisho.
Kuna ushahidi wa kihistoria kwamba Injili ziliandikwa na watu waliokuwa karibu na Yesu au walioshuhudia matukio yake. Ingawa ziliandikwa kati ya miaka 30-70 baada ya Yesu, maandishi hayo yaliendelezwa kwa mdomo kabla ya kuandikwa. Ushahidi wa maandiko ya kale, kama vile manuskripti za Dead Sea Scrolls, unaonyesha uthabiti wa maandiko ya Biblia. Tuhuma dhidi ya Injili hazina uthibitisho wa kitaalamu bali ni maoni yasiyo na msingi.
Nina maswali kwako
1. Yohana 17:3 inasema kumjua Yesu ni sehemu ya uzima wa milele, je, hili linafanana na imani ya Kiislamu ambayo inamwona Yesu kama nabii wa kawaida?
2. Ikiwa manabii wote walikuwa Waislamu, kwa nini hakuna ushahidi wa kihistoria wa maandiko yao yanayosema hivyo kabla ya Qur’an?
3. Je, unakubaliana kuwa Ibrahim, Isaka, na Yakobo walikuwa Wayahudi kwa mujibu wa Biblia, si Waislamu?
4. Mathayo 26:39 inaonyesha Yesu akisali kwa Baba yake. Kwa nini unadhani Yesu alifundisha Mungu kama Baba wa pekee wa wanafunzi wake?
5. Umewezaje kuhitimisha kuwa Injili zimepotoshwa wakati ushahidi wa kihistoria wa maandiko ya kale unaonyesha uthabiti wake?
6. Yesu alisema alikuja kukamilisha Taurati (Mathayo 5:17). Kwa nini unadai alikuwa mfuasi wa Taurati bila mabadiliko?
7. Ikiwa Yesu alisujudu kwa Mungu, je, hili linathibitisha kuwa alikuwa Muislamu au ni ishara ya unyenyekevu wake kama mwana wa Mungu?
8. Kwa nini Qur’an inadai Yesu hajisulubiwa, wakati ushahidi wa kihistoria wa Kirumi unathibitisha kifo chake msalabani?
9. Je, unakubaliana kwamba imani ya Kikristo kuhusu Yesu inategemea maandiko ya kale yaliyoandikwa karne nyingi kabla ya Uislamu?
10. Ikiwa Injili ziliandikwa na watu waliomshuhudia Yesu, kwa nini unakubali Qur’an iliyoandikwa karne kadhaa baadaye bila mashahidi wa moja kwa moja?
Hakuna kazi ngumu Kwa mgalatia kama kuutetea ukristo Kwa kutumia maandiko
1)
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Hili andiko limekamilika na lipo Kwa lugha nyepesi sana wewe sio kama haulielewi ila wewe hauliamini Kwa sababu ukiliamini hili andiko utakuwa Muislam kama Yesu
Jambo la Yesu kuwa ni nabii aliyetumwa na Mungu hilo halina mjadala
Utabiri wa Yesu hili andiko limekopiwa kutoka Kwa mtume Mika Mungu anasema atamtuma Yesu kuwachunga waisrael
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Hapa Yesu anathibisha kuwa utabiri wa Mika upo sahihi
Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Na ndipo Yesu akapigia msumali kuwa Ili uende peponi lazima ukubali Yesu ametumwa na Mungu mmoja tu
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Quran nayo ilipokuja ikapigilia msumali kuwa Yesu ni mtume wa Mungu
Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati
Kwahiyo hayo mnayofundishana huko kanisani hizo zinaitwa DOGMA Yani kubadilisha ukweli na kuwa uongo
Ila ukweli utabaki kama ulivyo Yesu ni binadamu wa kawaida na ni mtume wa Mungu kama walivyo mitume wengine
2) Manabii wote walikuwa waislam na ushahidi ndani ya Bibilia upo
Nguzo za uislam
1) kuamini Mungu ni mmoja na Mtume wenu ametumwa na huyo Mungu mmoja
2) kufanya ibada ya kusali Kwa kusujudi
3) Kutoa zaka
4) kuifunga saumu
5) kuenda Hija
Hayo yote yapo ndani ya Bibilia nakuonyedha mawili kusali Kwa kusujudi na Hija
Hija ni eneo ambalo Mungu analichagua mnatakiwa mkisali muangalie huko na pia muende huko
Kumbukumbu la Torati 12:5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko
Kumbukumbu la Torati 12:6
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;
Nabii Musa anasali
Kutoka 34:8
Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu.
Kutoka 34:9
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
Hapa Ezra ni Imamu anawasalisha wenziwe
Nehemia 8:4
Naye Ezra, kuhani, akasimama juu ya mimbari ya mti, waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo; na karibu naye wakasimama Matithia, na Shema, na Anaya, na Uria, na Hilkia, na Maaseya, mkono wake wa kuume; na mkono wake wa kushoto, Pedaya, na Misbaeli, na Malkiya, na Hashumu, na Hashbadani, na Zekaria, na Meshulamu.
Nehemia 8:5
Ezra akakifunua kitabu machoni pa watu wote; (maana alikuwa juu ya watu wote); na hapo alipokifungua, watu wote walisimama;
Nehemia 8:6
Ezra akamhimidi BWANA, Mungu Mkuu. Nao watu wote wakaitika, Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao; kisha wakainama vichwa vyao, wakamsujudu BWANA kifudifudi.
3) Kusema kuwa Ibrahim, Isaka na Yakobo walikuwa Wayahudi huo ni umbumbu wako wa kiwango Cha Rami
Yahudi ni Jina la mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda kabla huyo mtoto hajazaliwa kulikuwa hakuna jina linaloitwa Uyahudi
Hapo ju Kuna comment mgalatia mwenzako pia anasema Ibrahim na Isaka na Yakobo hawakuwa na dini ya kiyahudi hi ni jinsi gani inaonyesha hamuna mlijualo mpo mpo tu
Ibrahim Isaka na Yakobo walikuwa waislam
4) Kwa mujibu wa bibilia sala aliyofundisha Yesu ni hii
Mungu sio baba yake peke yake ila ni baba yenu nyote
Kila kitu unatakiwa umuombe Mungu na Wala sio Yesu
Mathayo 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
Mathayo 6:10
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
Mathayo 6:11
Mathayo 6:12
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 6:13
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.
5) Injili Ina majanga makubwa sana ila ndio hivyo hao wandishi wamspewa majina ya wanafunzi wa Yesu Ili wakudanganyeni vizuri
A) Idadi ya Chapter inatofautiana katika Injili zote nne Mathayo 28, Mariko 16, Luka 24, Yohana 21 kama wote walikuwa wanaandika anayoyasema Yesu Kwa Nini watofautiane tena Kwa kiwango kikubwa
B) Wandishi wa hizo Injili sio wanafunzi wa Yesu
Luka aliandika Kwa uliza uliza na kutunga
Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,
Aliye andika Injili ya Yohana Hadi Leo hii hajulikani ni nani
Na kuanzia Yohana 1:1 Hadi Yohana 1:36 ni Maneno ya mwandishi ambaye hajulikani
We may never know for certain who wrote the Gospel of John, any more than we can know who wrote the books of Matthew, Mark and Luke. We do know that John is a gospel apart, however. Early Matthew, Mark and Luke are so alike in their telling that they are called the Synoptic Gospels, meaning “seen together”—the parallels are clear when they are looked at side by side. Matthew and Luke follow the version of events in Mark, which is thought by scholars to be the earliest and most historically accurate Gospel. John, however, does not include the same incidents or chronology found in the other three Gospels, and the fact that it is so different has spurred a debate over whether John’s Gospel is historical or not, something that has been noted in Gospel of John commentary for hundreds—even thousands—of years.
Source website ya Cambridge university
C) Injili ya Barnabas ndio Injili pekee ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu lakini imetolewa katika Bibilia Ili nyinyi wakristo msiisome it's means ipo tofauti kabisa na mafundisho ya ukristo
6) Yesu na Taurati
Mbona maandiko yapo wazi kuhusu Yesu na Taurati
Mathayo 5:17
Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Mathayo 5:18
Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
Mathayo 5:19
Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
7) Kusujudi
Lengo la kusujudi ni kumnyenyekea Mungu muumba wa Kila kitu na sio ombi ni amri
Mathayo 4:9
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
Mathayo 4:10
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
8) Quran inasema hajusurubiwa na Wala hajafa msalabani
Nao wanasema hayo hawana uhakika ila wanadhania dhania tu
Tuangalie ndani ya Bibilia je waliosema Yesu amesurubiwa wanao uhakika?
Mariko anasema saa tatu Yesu yupo msalabani anasurubiwa
Marko 15:25
Basi ilikuwa saa tatu, nao wakamsulibisha.
Marko 15:26
Palikuwa na anwani ya mashitaka yake iliyoandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDI.
Yohana anapinga Mariko anasema hapa Saa sita Yesu alikuwa yupo mahakamani Kwa Pilato
Yohana 19:13
Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha.
Yohana 19:14
Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu!
Yohana 19:15
Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.
Labda wewe ujibu swali ni Yesu gani saa tatu yupo msalabani? Na Yesu gani saa sita yupo Mahakamani?
9) Ni kweli maandiko yalioanzisha dini ya ukristo yalikuwepo kabla ya uislam ila sio mandiko ya Mungu ni maandiko ya uongo yakiwepo maandiko ya Paulo maana Paulo sio mtume wa Mungu ni tapeli tu wa kidini wakolitho, wagalatia, Warumi,Tito sijui Efeso hivi ndio vitabu vya wakristo na ndio vilivyoleta ukristo
10) Injili hazijaandikwa na watu walio mshuhudia Yesu acha uongo Injili tukuamini wewe au tuamini maandiko?
Luka 1:1
Kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari za mambo yale yaliyotimizwa katikati yetu,
Luka 1:2
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Luka 1:3
nimeona vema mimi nami, kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo, kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu,
Injili ilivyoandikwa na mwanafunzi wa Yesu ni Moja tu ya Barnaba na hao walianzisha ukristo wameificha Ili musiione
Kuhusu Quran kitabu chenyewe kinasema hakina shaka
Quran 2:2
Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,