Hebu tutafakari kidogo..Inadaiwa Uislamu ulikuwepo toka enzi za kale Ibrahimu,yesu na manabii wengine wote wanadaiwa kuwa walikuwa waislamu.
Maswali ya kujiuliza:
1.Inakuwaje vitabu vilivyotangulia..torati,injili na zaburi havijataja neno uislamu kama ilivyo katika quran?
2.Kama yesu alikuwa muislamu mbona mafundisho yanaonesha mara kadhaa wakati anaomba alikuwa anataja baba yangu?? kitu kinachopingana na uislqmu kuwa Mungu hana mwana.Pia katika kuomba mara nyingi Yesu alikuwa anaangalia mbinguni,wakati waislamu wakiswali wanakuwa wanaelekea kibra?
Mimi naamini Quran imecopy biblia kwa sababu zifuatazo;
Biblia inasema Yesu ni neno -Quran nayo inasema ni neno
Biblia inasema Yesu ni roho wa Mungu-Quran nayo inasema vivyo hivyo
Biblia inasema yesu alizaliwa na Bikira na alianza kuongea toka akiwa mdogo -Quran nayo inasema hivyo hivyo
Biblia inasema Yesu alikufa ,akafufuka na akapaa mbinguni..Hapa ndio waislamu walipoitengeneza imani yao..ila kitabu chao kinawasuta bado
Kwenye quran Yesu mwenyewe anatamka kwamba amani iwe juu yake siku aliyozaliwa,siku atakayokufa na siku atakayonyanyuliwa Je tujiulize swali dogo tu je Yesu hajafa bado kwa Mujibu wa quran?
Kama jibu ni kuwa hajafa kwa nini aanze kunyanyuliwa kabla ya kufa..kwa nini step moja irukwe?
Allah mwenyewe anasema Issa nitakufisha na nitakunyanyua kwangu.
Kwa mujibu wa quran Yesu ameshanyanyuliwa na yupo kwa Allah kama biblia inavyoamini yupo kuume kwa Mungu baba.Sasa swali linakuja ,kwa nini aanze kumnyanyua kabla ya kumfisha.Wanazuoni wengi wamekuja na hoja dhaifu kwamba aliposema nitakufisha hakumaanisha kwamba atakufa,bali atawababaisha wauaji waone kama aliyemuua ni yeye kumbe mtu mwingine kavishwa sura ya Yesu(Seriously)? Kwa nini Allah afanye mazingaombwe hayo na wakati yesu mwenyewe alijitabiria kufa kabla ya kunyanyuliwa(Something fishy).
Unasema Muhammad amekopi ndani ya vitabu vya kale Yani ufahamu wako ndio umeishia hapo
Tofauti ya wakristo na Wayahudi ni hii
Wayahudi wanajua kabisa kuwa ni kweli Muhammad ni Mtume wa Mungu ila ni jeuri Yao tu na walikuwa wanajua kuwa Kuna mtume wa mwisho atakuja ila walitamani atoke kwao ikawa kinyume chake
Lakini nyinyi wakristo mmevurugwa vurugwa na hao Wazungu walianzisha ukristo kiasi kwamba mpo mpo tu
Wayahudi walikuwa wanajua ujio wa Mtume Muhammad
Yohana 1:19
Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
Yohana 1:20
Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo.
Yohana 1:21
Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.
Baada ya Yohana kuanza mahubiri wayahudi wakamfuata kumuliza
Wewe ni kristo,?
Yohana akasema hapana
Wewe u Eliya?
Yohana akasema hapana
Wewe u nabii yule?
Yohana akasema hapana
Eliya anajulikana, kristo anajulika huyo nabii yule ni nani? Ambaye wayahudi walikuwa wanajua ujio wake? Jibu ni mtume Muhammad
Na Wayahudi walijua ujio wa Mtume Muhammad Kwa sababu ametabiliwa na manabii wao
Kumbukumbu la Torati 33:2
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Katika mlima Sinai alipewa utume Nabii Musa
Mlima Seiri upo Jerusalem hivyo unahusu utume wa Yesu
Mlima Parani upo Saudi Arabia huyo ni mtume Muhammad
Sasa nyinyi wagalatia endeleeni tu kupingana na maandiko ambayo mmezaliwa mmeyakuta na mtakufa mtayaacha
Jahanamu inawasubiri maana Mungu alishasema anasemehe makosa yote lakini kosa la kuchukua kiumbe alicho kiumba yeye ukakifanya ndio Mungu wako na kukiabudu hilo kosa hasamei