Hakuna ubishi, S2kizzy ni producer bora kuzidi mkongwe Master Jay

Hakuna ubishi, S2kizzy ni producer bora kuzidi mkongwe Master Jay

Eti Grammy nominated, what a fuckin joke 😅

Kushirikishwa kweny moja ya nyimbo ya album ambayo imekuwa Grammy nominated haikufanyi na wewe uwe Grammy nominated artist, wewe unapata tuu certificate kwamba ulishiriki kweny hio album, Grammy nominated artist ni Maluma na album yake, hao wakina Rayvanny na S2kizzy wanadanganya watu.

Mfano Wizkid asingeshinda Grammy kweny nyimbo ya "Brown skin girl" aliyofanya collaboration na Beyonce, hapo sasa yeye ndo angestahili kujiita Grammy nominated artist kwa sababu nyimbo ndo imekuwa nominated na sio album kama kweny case ya Maluma, sasa wizkid na beyonce walivoshinda, wizkid akapewa ile tuzo ya Grammy iliyondikwa jina lake kabisa na dedication kwake, sasa kwann nimesema hv, rayvanny na s2kizzy wanadanganya watu kwa sababu wao hata album ya maluma ingeshinda Grammy wao wangepata nahic certificate tuu ya kwamba walishiriki kweny hio album.

A Record/Song nomination is very different from an album nomination.
The artists that are featured on the album do not receive a Grammy but are guest featured on a Grammy award winning album which is a high accomplishment in its own.
Master jay aliwai fanya jipya gani zaidi ya kutengeneza beat? Niambie nini special alichofanya jay kumshinda zombie?
 
Music production ya sasa kila mtu anawezafanya ila kwa zamani ilikuwa lazima ujue kutumia vyombo so producers wa zamani tuwape heshima yao maana waliproduce kwa uwezo wao na product zilikuwa na ubunifu na ubora mkubwa sana kuliko hizi copy & paste za leo. Siku hizi kuna dum loops ambazo hata kipofu anatumia na anaunda mdundo mzuri tu! Njoo inbox nikupe loops ukaunde beatz then uone kama utarudi hapa kumsifia huyo s2kizzy
Master jay anaweza kutumia chombo gani?
 
Hawa ni founders wa ladha halisi za bongo fleva..... Tofauti na kukopy wanaigeria na amapiano stukizzy ana kipi cha kukumbukwa bongo fleva?
Founder wa muziki wa bongofleva ni Mika mwamba. Master hajawai introduce sound yoyote kwenye hii nchi amekopi nje kila kitu
 
Mziki wa sasa hata kina chino kidd na jaiva nao wanaimba....kipindi kile hawa wasanii wa sasa wengi wasingeweza kiingia MJ au Bongo record kurekodi nyimbo
 
Kila zama na kitabu chake...huwezi kusema mwanajeshi wa leo wa jeshi la marekani ni bora zaidi ya mwanajeshi wa dola ya Roma ambae alikuwa akipambana kwa kutumia panga na visu.

Teknolojia imefanya mambo leo hii kuwa mepesi zaidi ,mwanajeshi anarusha mabomu kwenda Middle East akiwa yupo kwenye kambi ya kijeshi huko California.
 
S2kizzy ni mtaalam wa kusample sio Creativity. Bahati mbaya wateja wake wengi ndo wanamfanya awe mtu wa kusample tu. Kamwe huwezi kumfananisha na master jay aisee yule hakuwa mtu wa kusample.

Wachache sana wataelewa kwanini S2kizzy hastaili hata kubeba tuzo ya grammy.
 
Wabongo wengi wana tatizo la kufikiri kwa muktadha wa "all or nothing at all".

Yani, wengi hatuna nuance ya kuona kwamba hapa kuna zama tofauti, na wale wakongwe walikuwa na changamoto tofauti sana za teknolojia, za biashara etc. Na wao ndio waliochanja njia mpaka kufanya hawa wa baadaye wapate urahisi.

Na hivyo, kuwalinganisha hawa wa sasa na wale ni kulinganisha vitu viwili tofauti kabisa.

Unalinganishaje watu walioanza kufanya experiment kwa vifaa duni, na wengine waliokuja baadaye na kuona experiment ya awali ilivyoenda na kufanikiwa kwa kuona matokeo ya hiyo experiment ya awali na kutumia vifaa bora zaidi?
Master Jay kwani alikuwa RTD production? Ametumia mpaka hizi software mpya akachemka akaikimbia game.
Technically S2kizzy ni mkali kuliko Master... Huwezi sema Messi ni bora kuliko Maradona sababu Messi kacheza wakati wa VAR ishu ni uwezo na impact
 
Nachojua s2kizzy ni beatmaker na master jay Ni music producer kwaiy apo umefananisha vitu viwil tofaut
 
S2kizzy ni mtaalam wa kusample sio Creativity. Bahati mbaya wateja wake wengi ndo wanamfanya awe mtu wa kusample tu. Kamwe huwezi kumfananisha na master jay aisee yule hakuwa mtu wa kusample.

Wachache sana wataelewa kwanini S2kizzy hastaili hata kubeba tuzo ya grammy.
Nani kakwambia kusampo sio creativity? Kanye West asilimia 98 ya production zake ni sampling na wanamuita music genius.

Hakuna producer bongo hajawai fanya sampling tena Jay alikuwa anakopi na kupest hamkuwa na exposure ya muziki ndio maana
 
Mziki wa sasa hata kina chino kidd na jaiva nao wanaimba....kipindi kile hawa wasanii wa sasa wengi wasingeweza kiingia MJ au Bongo record kurekodi nyimbo
Kipindi cha kina ndukulusukucho na john walker anawawekea beat wanafanya comedy yani unaskiza unasema hii mbona kama demo 😂😂😂
 
View attachment 2891931

S2kizzy aka Zombie ni producer mkali kuliko Master Jay.
Zombie ambaye ni Grammy nominated mara kadhaa na kafanya nyimbo ambazo ana international hits kuzidi Master Jay ambaye alikuwa akimiliki studio ya MJ production ambayo alitumia wataalam wa kutengeneza muziki kama Maron linje, Profesa Ludigo, Maundi na wengine kadhaa uku akiweka sign yake kwenye nyimbo aonekane kazitengeneza yeye.

Naandika haya ili kumpa maua yake S2kizzyy ili jamii ijue ukubwa alionao kuzidi mkongwe Master Jay ambaye tunamheshimu licha ya kuwa mzee mwenye mihemko sana anaependa kutrend ambae ana historia mbaya ya kutumia wasanii wa kike kama Shaa akiwarubuni kwa studio time.

Zombie apewe heshima yake sio kila aliyetangulia anamzidi wa sasa lazima tuelezane ukweli.
Kwa kizazi chenu ambacho kila mwezi unapaswa kutoa nyimbo ila usisahaulike

Enzi ya master jay kwa mwaka msanii anatoa nyimbo mbili au tatu tu
 
Kwa kizazi chenu ambacho kila mwezi unapaswa kutoa nyimbo ila usisahaulike

Enzi ya master jay kwa mwaka msanii anatoa nyimbo mbili au tatu tu
So point yako ni nini?

Production zake zilikuwa very poor.

Au nitajie nyimbo tano alizotengeneza unazoamini ni classic production alafu mimi nitakupa tatu tu za zombie
 
Mziki wa sasa hata kina chino kidd na jaiva nao wanaimba....kipindi kile hawa wasanii wa sasa wengi wasingeweza kiingia MJ au Bongo record kurekodi nyimbo
Huyo Jaiva kwa siku ya Leo nasikia watu wanamtajataja sana, ngoja niende YouTube nikamsikilize, duh! Kweli nipo busy. Mziki wa siku hizi bwana
 
Master Jay kwani alikuwa RTD production? Ametumia mpaka hizi software mpya akachemka akaikimbia game.
Technically S2kizzy ni mkali kuliko Master... Huwezi sema Messi ni bora kuliko Maradona sababu Messi kacheza wakati wa VAR ishu ni uwezo na impact
You are comparing apples to oranges without any equivocating metric.
 
Skills na impact
Skills inapimwa kwa kutumia Tools za analogs na sio AI tools Mkuu..
Mwwnye skills ni yule aliyeweza kutumia Tools kipindi technology haikuwepo..

Mwanajeshi Bora ni yule atakayetumia Vifaa Dhaifu na kushinda vita..
Ila sio Yule atakayetumia Vifaa na Nyenzo zenye Nguvu na bado akatoka Draw.kwenye Battlefield
 
Kwa kizazi chenu ambacho kila mwezi unapaswa kutoa nyimbo ila usisahaulike

Enzi ya master jay kwa mwaka msanii anatoa nyimbo mbili au tatu tu
Angalau mziki ulikuwa una maana na mafunzo,vina vilipangiliwa vizuri,mizani ilizingatiwa ila sasa hivi unaweza ukapiga tu miluzi...inaingizwa kwenye beat na mziki tayari umekamilika
 
Skills inapimwa kwa kutumia Tools za analogs na sio AI tools Mkuu..
Mwwnye skills ni yule aliyeweza kutumia Tools kipindi technology haikuwepo..

Mwanajeshi Bora ni yule atakayetumia Vifaa Dhaifu na kushinda vita..
Ila sio Yule atakayetumia Vifaa na Nyenzo zenye Nguvu na bado akatoka Draw.kwenye Battlefield
Huwa nawaambia watu kuwa zamani kulikuwa na mashujaa fikiria unakamata panga unaenda kupambana uso kwa uso na adui katika uwanja wa vita. Halafu unasoma historia unaelezwa kuwa kamanda kapambana zaidi ya miaka 30 katika uwanja wa vita akiwa na upanga tu. Waliopita wanastahili pongezi kubwa sana.
 
Producer bora wa Amapiano? Nyimbo zenye codes mbili tu! Hebu nyie kizazi kipya kuweni na mipaka, jilinganisheni kizazi chenu. Ndio yule shoga lil nas eti anajifananisha na Nas escobar.

Kina Master jay, Majani, Ludigo wale ndio wanawake linganishwa wao kwa wao. Huwezi fanya crossgeneration challenging.
 
Back
Top Bottom