Hakuna ulazima Tanzania kuwa na Waziri Mkuu

Hakuna ulazima Tanzania kuwa na Waziri Mkuu

MUACHENI AFANYE KAZI KWANZA KUONGOZA SIO JAMBO JEPESI BILA AMANI KUHUBIRI UNADHANI UFANISI UTAONEKANAJE
 
Huyu waziri mkuu wa sasa anajiona kama MWENEZI WA CCM
Ukimsikiliza anavyoongea halafu ukasikia wakazi wa Dar wanavyolalamika shida ya maji unapata hasira sana.

Huyu ni waziri mkuu wa aina yake tangu kuzaliwa kwa Tanganyika na Tanzania. Ni PM anayefikiri watanzania wote ni wajinga na yeye pekee ndio mwenye akili, hii ni aina fulani ya tatizo la kisaikolojia.
​
 
Ukimsikiliza anavyoongea halafu ukasikia wakazi wa Dar wanavyolalamika shida ya maji unapata hasira sana.

Huyu ni waziri mkuu wa aina yake tangu kuzaliwa kwa Tanganyika na Tanzania. Ni PM anayefikiri watanzania wote ni wajinga na yeye pekee ndio mwenye akili, hii ni aina fulani ya tatizo la kisaikolojia.
​
Mkuu hawa focus yao sio raia.

Maana wameshajua kwamba bila hata raia kupiga kura wao watashinda tu.
Kwa hiyo hawana shida na matatizo ya kiraia.
 
Wivu tu na kukosa pesa ya Xmas zimekusukuma kuandika mada hii.
Yaani akili zako zote zimezungukaa wee zimeishia kuwaza "Pesa ya Krismasi"... Si ajabu CCM imejaza watu wenye akili na mawazo kama yako.
 
Mtani wangu mwigulu Nchemba

hawa vibaraka wa mabeberu wangeanza tu kukusifia, nakuambia tungepga kelele hadi utenguliwe..
lakini wanaonekana kulia lia, UPO SAHIHI, shikilia hapo hapo...

"hatuwezi kuongozwa na vibaka wa mabeberu"
 
Sahihi kabisa, its either nafasi ya uwaziri mkuu au umakamu wa raisi, moja kati ya hii inatakiwa kuwekwa pembeni, haina manufaa kwa taifa.
 
Inatosha tuwe tu na Rais, Makamu wa Rais, Spika na Jaji Mkuu.

Kimuundo Tanzania haina ulazima wa kuwa na waziri Mkuu.


Upo sahihi sana. Mfumo wetu wa utawala upo shaghala bagala, wala hauendani na mifumo ya kiutawala ya Dunia.

Katika hali ya kawaida, mifumo ya kiutawala Duniani kote huwa ya aina mbili:.
1. Unakuwa na ceremonial president, halafu unakuwa na Prime Minister ambaye ni kiongozi mkuu wa Serikali, na ndiye mtendaji mkuu. Kwenye mfumo huo huwi na Makamu wa Rais.

2. Unakuwa na Rais mtendaji ambaye ni msimamizi mkuu wa Serikali, anakuwa na msaidizi wake wa karibu ambaye anakuwa makamu wa Rais. Kwenye mfumo huu, huwi na Waziri Mkuu.

Sasa kioja cha hapa kwetu, tuna Rais mtendaji, tuna Makamu wa Rais asiye na majukumu muhimu, halafu tena tuna Waziri Mkuu. Kwa kuwa tuna Rais Mtendaji na msimamizi wa Serikali, Waziri Mkuu anakuwa hana kazi, ndiyo maana anazunguka tu nchi nzima, akipiga propaganda za kisiasa, amemnyang'anya kazi katibu mwenezi wa chama.
 
Back
Top Bottom