Hakuna ulazima Tanzania kuwa na Waziri Mkuu

Hakuna ulazima Tanzania kuwa na Waziri Mkuu

Cheo cha waziri mkuu kina tija
Ila hapa kwetu tumekiweka kama class monitor wa darasa la 6
Ilipaswa Waziri Mkuu asiteuliwa Bali agombee na achaguliwe na wananchi katika uchaguzi mkuu tena Kwa tume ya huru ya uchaguzi yenye maadili.
 
Nyerere aliiga ktk ufaransa, ni mfumo unaotumika ufaransa kuwa na raisi na waziri mkuu, sema hapo kwenye makamu wa raisi kuna ahusiano na mambo ya muungano, ufaransa hawana makamu wa raisi wana raisi na waziri mkuu.
kwa maoni yangu tatizo la tanzagiza ni aina ya watu wanaofika juu na mwishowe kutawala, hatufwati meritocracy, hivyo hakuna chujio la kuchuja watu incompetent kufika juu, hapo ndipo tatizo lilipo, lkn kama ukiwa na watu competent juu na mfumo huu bado tunaweza kutoboa.

angalia mifano tu wizara za elimu na afya, wizara ya afya inaongozwa na mtu ambaye hana medical background anawezaje hata kuelewa matakwa ya tiba na mambo mengine yote yahusiyo afya? haya waziri wa elimu na yeye cv yake iliwekwa hapa jf, huyo ndiyo mtu anayepaswa kutambua mapungufu ya elimu na kuyarekebisha wakati yeye mwenyewe hiyo elimu hana, how is it even possible? ...
Nyerere kuna mambo alituachia ya ajabu ajabu sana, mojawapo ni hili la kuwa na vyeo vingi vya kisiasa visivyo na tija yoyote.
 
Nyerere kuna mambo alituachia ya ajabu ajabu sana, mojawapo ni hili la kuwa na vyeo vingi vya kisiasa visivyo na tija yoyote.

lkn bado tunaweza kubadilisha kama tunaona havina faida, sidhani kama ni sahihi leo hii kumlaumu mtu aliyejiuzulu uraisi mwaka 1985.

nafikiri tatizo la hivi vyeo ni pale siku mnanopata mtu ambaye hana uwezo nacho ndiyo mnaanza kuhoji uhalali wa hicho cheo.

maadamu hatufwati meritocracy, tutaona kila cheo hakina maana kwa maana aliyekishika hana sifa na wala hana uwezo …
 
Katika wakati hii nchi iliwahi kupatwa, basi ni awamu hii! Yaani kuanzia juu mpaka chini, ni vituko tu! Sijui Mungu ana makusudi gani na sisi waja wake.
 
Kwa kuondoa ''nonsense'' kama anazofanya Mwingulu sasa hivi.

Mwigulu yupo kikatiba, katiba inaruhusu afanye hayo usiyoyapenda wewe...na unatikiwa kumtii kama Kiongozi wako wa nchi. Tii mamlaka bila shuruti
 
Mwigulu yupo kikatiba, katiba inaruhusu afanye hayo usiyoyapenda wewe...na unatikiwa kumtii kama Kiongozi wako wa nchi. Tii mamlaka bila shuruti
Nyumbu at its best. Haya ni mawazo ya kitanzania kwa asilimia zote.
 
Ashikilie wapi ambapo hasa ameshika, so far kama waziri mkuu hafanyi majukumu yake, he's spreading propaganda badala ya kuwa kiranja mkuu wa serikali.
Tulieni sindano iwaingie
 
Kaka Allen Kilewella nikupongeze kwa kuanzisha hoja hii chokonozi, nawapongeza wakuu Kijakazi , macho_mdiliko na wengine wenye michango chanya
Nadhani shida siyo nafasi ya waziri mkuu bali tatizo linaanzia kwenye bunge, yani 'Majority' hivyo kumfanya ndugu waziri mkuu kuwa kama kipaza sauti ama garasha kwa lugha za mtaani.
Hapa nchini CCM wamefanikiwa sana kumiliki bunge, je ikitokea chama pinzani kikapata viti vingi zaidi bungeni tutakuwa na waziri mkuu wa namna gani? Au bado hatakuwa na tija?
Nadhani katiba inasema waziri mkuu atatoka kwenye chama chenye wabunge wengi, kama sivyo nielimisheni wananzengo
 
Kaka Allen Kilewella nikupongeze kwa kuanzisha hoja hii chokonozi, nawapongeza wakuu Kijakazi , macho_mdiliko na wengine wenye michango chanya
Nadhani shida siyo nafasi ya waziri mkuu bali tatizo linaanzia kwenye bunge, yani 'Majority' hivyo kumfanya ndugu waziri mkuu kuwa kama kipaza sauti ama garasha kwa lugha za mtaani.
Hapa nchini CCM wamefanikiwa sana kumiliki bunge, je ikitokea chama pinzani kikapata viti vingi zaidi bungeni tutakuwa na waziri mkuu wa namna gani? Au bado hatakuwa na tija?
Nadhani katiba inasema waziri mkuu atatoka kwenye chama chenye wabunge wengi, kama sivyo nielimisheni wananzengo
Hoja yako ni sahihi kabisa. Lakini haiondoi swali la msingi, ni kwa nini tuna nafasi ya Waziri Mkuu?

Asipokuwepo kutatokea upungufu gani kwenye utendaji wa Serikali ya Tanzania?
 
Waziri Mkuu anasimama jukwaani anachamba anashika kiuno
 
Hoja yako ni sahihi kabisa. Lakini haiondoi swali la msingi, ni kwa nini tuna nafasi ya Waziri Mkuu?

Asipokuwepo kutatokea upungufu gani kwenye utendaji wa Serikali ya Tanzania?
SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU,
BARAZA LA MAWAZIRI NA SERIKALI
Waziri Mkuu
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo
kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika
madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au, kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi.
(3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba
hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi -
(a)siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake; au
b)siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au
(c)siku atakapojiuzulu; au
(d)siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu; au
(e)atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
52.-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli
za Serikali Bungeni.
(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.
53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

53A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 51 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo
itatolewa hoja kupendekeza hivyo na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kutaka kupitisha kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitatolewa Bungeni
endapo----
(a)haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 52 ya Katiba, wala hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; au
(b)haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa;
(c)haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa kuipitisha.
(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitapitishwa na Bunge isipokuwa tu kama----
(a)taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku angalau kumi na nne kabla ya siku inapokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;
(b)Spika atajiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa.
(4) Hoja iliyotimiza masharti ya ibara hii itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo kwa
mujibu wa Kanuni za Bunge.
(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.
(6) Endapo hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu itaungwa mkono na Wabunge wengi, Spika atawasilisha azimio hilo kwa Rais, na mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha azimio la hoja ya kura ya kutokuwa na imani kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu atatakiwa ajiuzulu, na Rais atamteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu.
........................................................................

Kwakuwa nafasi yake ipo kikatiba, na ndiyo sheria mama, basi tuzikite hoja zetu katika vifungu hivyo hapo juu. Mapema kabisa utagundua 'ujanjaujanja' ulitumika kuiandika katiba yetu.
Kwanini awajibike kwa Rais?
Kama atatoka kwenye chama tofauti na Rais, itakuwaje?

KATIBA KATIBA KATIBA,

alamsik.
 
Inatosha tuwe tu na Rais, Makamu wa Rais, Spika na Jaji Mkuu.

Kimuundo Tanzania haina ulazima wa kuwa na waziri Mkuu.
Anafuga mustachi uyo , sijui anataka muiga Rais Cuba enzi zile , ipo siku ,tutamlazimisha kunyoa ilo limistachi
 
Back
Top Bottom