Hakuna umuhimu wa ndoa karne hii kwa sababu hizi

Hakuna umuhimu wa ndoa karne hii kwa sababu hizi

Na kwanini umfuge binadamu mwenzako!!!?
Kama viungo vyangu mwenyewe tu vinatofautiana sembuse nikaishi na mtu ninayetofautiana naye tabia na mtazamo kisa kutafuta heshima!!!
Kwaio unawashaurije wanawake wenzio sasa?
 
Kwaio unawashaurije wanawake wenzio sasa?
1623682072716.png
 
HAKUNA UMUHIMU WA NDOA KARNE HII KWA SABABU...

Na, Robert Ng'apos Heriel

Hakuna umuhimu wa ndoa katika Karne hii Kwa sababu;

1. THAMANI YA MWANAMKE IMESHUKA NA INAKARIBIA KUTOWEKA
Unapozungumzia Ndoa unamzungumzia Mwanamke, kadiri mwanamke anavyokuwa na thamani ndivyo thamani ya ndoa nayo inakuwa na thamani. Mwanamke yupo Kama Mratibu Mkuu wa Ndoa. Kushuka Kwa hadhi ya wanawake Duniani kunatokana na wao KUJIRAHISISHA. Kadiri mwanamke anavyopewa Uhuru ndivyo thamani yake inazidi kuporomoka, ni hakika itatoweka kabisa. Lengo la sheria za kubinya Uhuru wa mwanamke tangu zamani ni kulinda thamani yake. Uhuru uliopitiliza wa wanawake utazidi kushusha utu wa mwanamke.

2. KUPOROMOKA KWA BIASHARA YA UMALAYA
Kuporomoka kwa biashara ya umalaya kutokana na wanawake wengi kugawa uchi kiholela Umalaya na ndoa ni mambo yanayoenda sambamba. Ndoa ikiwa na thamani basi na umalaya utakuwa na thamani. Katika tafiti zangu za kiuchunguzi, Bei ya kununua Malaya miaka ya 2011 ilikuwa juu ukilinganisha na Mwaka 2020. Malaya alikuwa akinunulia miaka hiyo 10,000 -20,000 Kwa Bao moja Maeneo ya kawaida Kama Sinza Mori, Ambiance n.k. lakini kutokana na wanawake wengi kujirahisi na kugawa penzi kiholela hali inayopelekea umuhimu wa ndoa kutokuonekana, hii imefanya biashara ya Umalaya kuanguka, Kwa sasa unaweza pata Malaya Kwa bei ya 2000 -8000. Mke wa ndoa Kwa sasa Hana ubavu wa kumbabaisha mume wake kwani akimnyima tendo, basi huko barabarani na mitandaoni wanawake Buku wanamsubiri Wampe penzi.

Hata hivyo umalaya siku hizi unafanywa hata na Wake za watu Hali inayowakatisha tamaa WAOAJI. Umalaya unapofanywa na wanawake wengi unafanya soko kudondoka na bei kushuka chini. Kama wanawake wangekuwa na AKILI basi Jambo la Kwanza kabisa kulipigania lilikuwa ni THAMANI zao, kupitia kudhibiti ongezeko la Umalaya. Hii ingeongeza thamani mara elfu kuliko kupiganka vitu visivyo na maana yoyote katika utu wao. Udhibiti wa Msamiati KUDANGA ungedhibitiwa, na hao wapigania HAKI SAWA. Maneno ya namna hii sio tuu hayafurahishi bali pia yanawadhalilisha wanawake pasipo ya wao kujua wenyewe.

Ongezeko la Umalaya limefanya tendo la ndoa kupoteza uthamani, kupata tendo la ndoa kwa sasa sio HABARI kama ilivyokuwa zamani ambapo ilikuwa mshike mkamate kukubaliwa na mwanamke.

3. KUZAA SIKU HIZI SIO MPAKA NDOA
Siku hizi hakuna tofauti kubwa baina ya Mtu na Mnyama. Moja ya mambo yaliyomtofautisha binadamu na mnyama ni pamoja na ndoa, ili uweze kupata watoto basi ilikubidi Ufunge Ndoa, yaani Uoe au Uolewe. Bila kuoa au kuolewa ilikuwa ngumu kupata mtoto.

Thamani ya ndoa pia ilijengwa kwenye kupata watoto, Binadamu wengi asilimia 99% huwa na ndoto siku moja wawe na watoto na kwa zamani mahali pekee pakupata watoto ni ndani ya ndoa. Hii iliipa thamani taasisi ya ndoa.

Lakini zama hizi, kupata watoto sio sababu tena ya kuingia ndani ya ndoa. Mtu anaweza akawa na watoto bila hata ya ndoa. Tena anaweza akawa na watoto na wanawake hata kumi, au wanaume wengi pasipokuoa au kuolewa nao.

Zamani ukimpa mwanamke mimba hesabu umeshamuoa, lakini sio siku hizi.

Kama serikali na taasisi za dini zingekuwa zinataka ziondoe tatizo la watoto wasiolelewa na wazazi wawili lingeboresha sheria za ndoa na uzazi. Haya mambo ya Single mother yasingekuwepo.
Ingekuwa sheria kuwa ni marufuku kuwa na mtoto pasipokuwa ndani ya ndoa ingawaje ingeleta athari kubwa kijamii lakini ingesaidia sana hapo baadaye.

Vijana wa sasa wengi wao huwapachika mimba wasichana kisha huwatelekeza na kuishi kibachela, wanajua wanawatoto tayari sasa ndoa ya nini ikiwa mahitaji yote ya ndoa wanayapata hata wakiwa hawajaoa.

Kwanza kuishi ndani ya ndoa katika zama hizi inachukuliwa kama mateso makubwa kuliko unafuu.

4. SHERIA YA PASU KWA PASU
Karne hii vijana wengi hawataki kusikia habari za ndoa kutokana na aidha uelewa mdogo kuhusu sheria za pasu kwa pasu, au kuzijua sheria hizo kupitiliza. Niliwahi kumsikia rafiki yangu ambaye kimsingi amefanikiwa kwa umri wake, ana nyumba mbili, gari moja pamoja na vimiradi midogo midogo akiwa na umri mdogo tuu wa miaka 33. Rafiki yangu huyu nilimuuliza kwa nini asioe kwani umri wa kuoa anao, na anauwezo wa kumudu mahitaji ya kifamilia alichonijibu kilinishangaza. Alinijibu hivi; Nina watoto wawili kwa nini nioe, unataka nioe alafu nigawane mali na mwanamke siku tutakapoachana?"

Nilimuuliza kwa nini anafikiri kuachana zaidi kuliko kuishi mpaka kifo, akaniambia nisijifanye sioni wanawake wa zama hizi.

Vijana wengi wanafikiri habari ya Pasu kwa Pasu, sheria hii inawaumiza kila wakiifikiria linapokuja suala la kuoa, hata hivyo hawaoni sababu ya kuoa ikiwa tayari wameshapata kila kitu kilichopo ndani ya ndoa.

Vitu vilivyopo ndani ya ndoa ambavyo kwa karne hii vinapatikana hata mitaani
i. Tendo la ndoa
ii. Watoto
iii. Kazi za nyumbani kama Kufua, kupika, vyombo, usafi n.k
iv. Ushauri na kusaidizana

Vitu ambavyo vipo nje ya ndoa lakini ndani ya ndoa havipo

i. Uhuru
Ndani ya ndoa hakuna uhuru kwani wewe ni mali ya mtu, nje ya ndoa wewe sio mali ya mtu unafanya utakavyo, urudi usirudi nyumbani yote sawa, ulale usilale na mwanamke yote sawa.

ii. Hakuna sheria inayokulazimisha kumhudumia yeyote yule kwani sio mke wako lakini ndani ya ndoa zipo sheria zinazokulazimisha kumhudumia mke wako

iii. Tahadhari
Nje ya ndoa kuna tahadhari kwa sababu unawachukulia wanawake wote utakaodate nao ni Malaya, hivyo utaogopa Maradhi, pia utakuwa makini na pesa unazotoa.

Ndani ya ndoa hakunaga tahadhari kubwa kwa maana unaamini huyo ni mkeo, na ni rahisi kupata UKIMWI ndani ya ndoa kuliko nje ya ndoa.

Ni ngumu kwa mtu ambaye hajaoa na hana mpango kujiua kisa mapenzi ila ni rahisi kwa mtu aliyeoa au mwenye matarajio ya kuoa kujiua kisa mapenzi

Wanawake ni lazima walazimishe ndoa kwa sababu thamani na utu wao unalindwa zaidi akiwa ndani ya ndoa kuliko akiwa nje.
Sasa Ongezeko la wanawake wasiotaka ndoa kutokana na sababu mbalimbali zinazidi kuondoa utu wa mwanamke.

Hata hivyo wapo wanawake ambao bado wanazijua thamani zao, ingawaje thamani zao zipo mashakani kutokana na kundi kubwa la wanawake kuamua kujipa uhuru unaowavua nguo wanawake wote duniani.

Wanawake wasafi na waaminifu wapo, namaanisha wasiopenda kutembea na wanaume hovyo kama wanyama, lakini wanajikuta katika wakati mgumu pale anapotaka kumnyima Mwenza wake mpaka ndoa ilhali anajua kabisa akimnyima basi wapo wenzake kama mia wanamsubiria huyo mchumba wake, hivyo wanaamua kutoa uroda na kujikuta wakiwa kundi moja la wale wasiosafi na wasiowaaminifu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
Sasa hivi vitu vyote vipo available hata ukiwa nje ya ndoa na tunakoelekea ndio itakua hatari zaidi, nafikiri maombi yanahitajika hapa..
 
Namuwazia sana binti yangu Miaka 16 ijayo Hali itakuaje
hahahaha!! muombee sana mkuu, kuna vitoto vya certificate na diploma vimepanga kwenye nyumba ninayoishi hapa. Huwa najisemeaga kimoyomoyo kama wazazi wangefahamu wanachofanya watoto wao huko waliko hakika wangepata mstuko wa moyo. Yaani mazazi anajua mtoto anasoma kumbe yeye huku ameshaolewa tayari tena bila hata mali...
 
Wiki iliyopita nilikuwa nmeboreka nkaenda kukaa na wazee wa mtaan ni wazee kwl kwa umri wangu nawaita babu. Kuna Mzee m1 alieleza jambo 1 nkawaza kama kuna kaukwl kwanz alisema yy alioa bint mdg sana wakati yy tayar ashakuw mkubwa alisema alioa mwaka1995 wakati uyo bint akiwa na miaka13 yy hakutaj umri wake akasema kwa umri alonao mke wake anajua kabisa kuwa anachepuka na akadai mara nyng anaporud nyumbani kwake uwa anaimb kwa saut ili kama kuna mwanaume ndani kwake aondoke alisema anajua kama co kuhis kuwa mkew anaweza kuwa anacheat ila kumuacha HAWEZI kwa sababu alisema ipo siku magonjwa yatamnyemelea na HAKUNA ndugu ataeweza kuja kumsaidia eidha kumlisha,kumsafisha au kumuhudumia coz binadam tuna kinyaa sana akatoa mfano mgonjwa akiwa na hal mbaya kalazw kwa muda mref hospital ndugu wengi uwa wanakwepa kwenda asbh kumsafisha mgnjw wao, hvy akatushaur ss vjana kuoa kuna umuhim wake kwa baadae ila mwisho alisema muda mkew akimnunia bac anaingia chaka la tandika kula NYAPU au kuna maeneo vipo vibinti vdogo tu vinapenda NDONGA kama pipi uwa anadeal navy.

Kazi ni kwako
 
hahahaha!! muombee sana mkuu, kuna vitoto vya certificate na diploma vimepanga kwenye nyumba ninayoishi hapa. Huwa najisemeaga kimoyomoyo kama wazazi wangefahamu wanachofanya watoto wao huko waliko hakika wangepata mstuko wa moyo. Yaani mazazi anajua mtoto anasoma kumbe yeye huku ameshaolewa tayari tena bila hata mali...
So sad[emoji26]
 
Hv mkuu unapojiita Taikoni una maana gani!!!?
ni kijeba flani au mbobezi katika jambo flani!!?
 
mbona kama umenihamasisha nisioe maana naona kama tupo wengi vile hivyo nisiwe na hofu
 
Utoa ufafanuzi makini sana katika swala la ndoa kwenye jamii yetu kwa sasa, japo uchambuzi wako umeegemea upande mmoja ila ndio upande wenye nguvu kwa sasa kutokana na namna tunavyoishi.

Watu wanaishi katika jamii zao kwenye mazingira ya aina tatu, Kimila Kidini na Kiserikali.

Ukiutazama msingi wa ndoa Kimila utaona bado ndoa za kimila zinampa thamani mwanamke katika ndoa yake lakini sheria hizohizo za kimila bado zinatambuwa mahawara na watoto wa nje.
Madhaifu katika sheria za kimila Kwa wanaoishi kimila yanapunguza commitment ya ndoa. Maana unaweza kuoa kimila na bado ukawa huru kulala na yeyote.

Wanaoishi Kiserikali hawa ndio wengi maana hata wanamila na wanadini naowamo japo si wote.
Kundi hili ndilo kundi alilolilenga mtoa mada.

Kwa wanaoishi Kidini na wameshika dini hapa ndoa bado inathamani kubwa, na thamani ya mwanamke bado ipo juu.
Tatizo hizi sheria za Kidini wanawake wenyewe hawapendezwi nazo maana wanaona zinawanyima uhuru katika baadhi ya mambo.

Uhuru huo ambao wao wanadai wameukosa ndio unaowafanya wawe na thamani, na kadiri wanavyopambana utaka uhuru ndivyo wanavyoshusha thamani yao.
 
Utoa ufafanuzi makini sana katika swala la ndoa kwenye jamii yetu kwa sasa, japo uchambuzi wako umeegemea upande mmoja ila ndio upande wenye nguvu kwa sasa kutokana na namna tunavyoishi.

Watu wanaishi katika jamii zao kwenye mazingira ya aina tatu, Kimila Kidini na Kiserikali.

Ukiutazama msingi wa ndoa Kimila utaona bado ndoa za kimila zinampa thamani mwanamke katika ndoa yake lakini sheria hizohizo za kimila bado zinatambuwa mahawara na watoto wa nje.
Madhaifu katika sheria za kimila Kwa wanaoishi kimila yanapunguza commitment ya ndoa. Maana unaweza kuoa kimila na bado ukawa huru kulala na yeyote.

Wanaoishi Kiserikali hawa ndio wengi maana hata wanamila na wanadini naowamo japo si wote.
Kundi hili ndilo kundi alilolilenga mtoa mada.

Kwa wanaoishi Kidini na wameshika dini hapa ndoa bado inathamani kubwa, na thamani ya mwanamke bado ipo juu.
Tatizo hizi sheria za Kidini wanawake wenyewe hawapendezwi nazo maana wanaona zinawanyima uhuru katika baadhi ya mambo.

Uhuru huo ambao wao wanadai wameukosa ndio unaowafanya wawe na thamani, na kadiri wanavyopambana utaka uhuru ndivyo wanavyoshusha thamani yao.

Mkuu kongole kwako, umefafanua vyema kabisa
 
Kuna muda ukikaa unawawazia kaka na ndugu wa kiume kwa jinsi mambo yanavyokwenda uhakika wa kupata mke aliye bora ni kwa 20% tu (hasa mijini). Na hiki ndo chanzo cha hofu kwa wanaume kuhusu NDOA.
1623686879615.png
 
Leo kuna mrembo kaniambia "Mimi sitaki kuolewa nataka tu mtoto" yote hiyo imekuja baada ya kuona picha nilio ipamba kwenye screen ya laptop yangu ....na kumpa sifa kedekede baby boy wangu kuwa ni ka handsome ...kazuri sijui nini nini huko .....nimecheka tu na kumtakia kila la heri kwenye hiyo safari yake
 
Hivi comments humu JamiiForums huwa zinaweza kufutwa? Maana nashangaa comment yangu siioni humu nikiingia wakati notification pale juu imeonesha mtoa post kaniquote kabisa.

Sasa naandika tena
WEWE (MTOA MADA) NI PUNDA... TENA SI WEWE TU BALI NA WOTE WANAOKUSAPOTI

ifuteni na hiyo sasa maana inaonesha ni jinsi gani mlivyodhamiria kuporomosha jamii. Yaani mtu ananyong'onyeza kabisa harakati za jamii katika kudumisha utamaduni halafu mnachukulia poa duh! Kweli kua uyaone- siyo maghorofa.

Ndoa ina faida sana tofauti na KakaMkubwa anavyotuaminisha hapa. Kwa ufupi nitataja faida chache tu

1. Kuunga (udugu/Undugu)
Ndoa inasababisha watu kuwa ndugu moja hivyo kuongeza wigo wa ushirikiano. Angalia familia zenye upweke kijana akija na mchumba members wanavyofurahia utasikia "nafuu baba ulete mtu ili na mimi nipate wa kupiga nae stori". Usipooa kama ukoo/familia yenu ina member wanne mtabaki hivyo hivyo wanne tu lakini ukioa mnakuwa ndugu kubwa ambapo faida yake sisi walala hoi ndo tunaijua (hasa kwenye matukio makubwa) ila wewe kwakuwa 'umejitosheleza' utasema "wingi si hoja"

2. Kustiriana
Mashimo makubwa vibamia wenye makovu wasio na nywele nk wote hao isingekuwa ndoa wangetangazika balaa ila ndoa zinawasitiri. Pia wenye kipato wanawasitiri wasio kipato, wenye kukubalika kuwasitiri wasiokubalika nk. Hamu za kingono bila ndoa watu wangedhalilika lakini angalia watu wanasitirika kingono kupitia ndoa na ukitaka kuamini wewe kama hujaoa ngoja apite mdada anatingisha matako halafu hamu ikaja na simu haina chaji wala hela huna. Vilevile wenye upweke kusitiriwa na wenye furaha (rejea hoja namba 1). Bila ndoa watu wangedanga sana ila mahitaji ya kifedha mtu anakuwa anayapata kwa mwenza wake mambo fresh. Kwa kifupi vyovyote utakavyoiweka hiyo faida ila hoja inabaki kwamba ndoa inastiri watu.

3. Kupunguza zinaa
(Wanaita ngono holela) ambapo wasioolewa wanajikuta wanakuwa malaya wahuni na majina mengine pale wanapokosa au wanapohitaji kupata faida za ndoa kwa njia tofauti na ndoa

4.Utulivu
Wewe uliyesema unapata kila wakipatacho waliooa ni mwongo. Leo unalala na mwajuma keshokutwa veronica wiki ijayo suzi asipokuja unajikuta unachukua mpaka yule malaya au hata chizi wa hapo mtaani kwenu ilimradi tu ukidhi haja zako. Mara bahati amesema angekuja halafu hajaja umengoja mpaka basi na simu hapatikani. Siku nyingine unachoka na kazi ukirudi unahitaji mawazo ya kukuimarisha lakini hayupo wa kufanya hivyo. Mara saa zingine hujamalizia "cha pili" simu ya demu imeita anahitajika haraka sana hapo bado hatujaongelea ishu ya purukushani na madume wenzako katika scramble na huyo jike sasa yote hayo utulivu uko wapi

5. Kupata familia (mke na watoto)
Hoja yake mwandishi na wengineo wanasema eti watoto unazaa tu nje. Sasa fuatilia wote wanaozaa nje historia yao na wanawake wazazi wenzao au watoto hao uone kizungumkuti wanachokutana nacho. Mtoto hajulikani baba yake halisi ni nani na tena wanawake wengine anaamua kukufungia vioo kabisa hataki uwazoee 'watoto wake'. Watoto wengi wengi wenye utata juu ya baba zao na mama zao unakuta walizaliwa kwa mtindo huo mnaoushabikia

6. Kuongeza kipato (uchumi)
Hii wengi watapinga lakini kwa mwenye kutafakari vema anaelewa tu hata zile primitive society msingi mkuu wao ni watu. Jamii zote za kale matajiri walikuwa ni zile koo kubwa (zenye watu wengi). Sasa sijui bila kuoa hao watu watakuwaje ukoo mkubwa maana huwezi kwenda kukusanya watoto uliozaa nje kiholela eti uje uwajaze home wakati mama yao nae anataka aijaze familia ya kwao.

7. Kuwa tofauti na viumbe wengine
Binadamu ameumbwa na utashi wa kuishi tofauti na viumbe wengine kama ndege na wanyama na amepewa uwezo wa kuvitawala vitu vyote duniani sasa ikitokea yeye tena hataki kuishi kwa mifumo anataka aishi kama wanyama ni bora kumbe wanyama watutawale sisi sasa

8. Kuleta hadhi na heshima
Ukioa au kuolewa unakuwa na hadhi fulani na utapata heshima. Pia mwenyewe utakuwa mwadilifu na utakuwa mwenye kuheshimu. Angalia baadhi ya mambo utakuta asiyeoa hahitajiki kabisa wala hathaminiki kisa tu haaminiki au angalia baadhi ya hoja za mabachela zinapuuzwa kabisa kisa hajaoa

9. Mwisho niseme tu ndoa ni kiburudisho kwa wanandoa (hasa sisi wanaume) ambao starehe yetu kuu ya pili ukiacha kulala ni ngono, ndoa ni kitulizo, ndoa inaleta uchamungu, ndoa ni nusura pia na ndomaana vijana wanasema ufanye upate nusra uepuke mtihani wa zinaa. Nawashauri hata nyinyi mnaoshabikia hapa kama hamjaoa mfanye muoe (sijui muolewe) na kamwe msigeuze changamoto mlizoziona/sikia/kutana nazo katika ndoa mkazifanya ndo fursa za kukandia ndoa laa! Bali ni muda mwafaka wa kucheki wapi pa kurekebisha ndoa isiwe taabu na maisha ya ndoa yaendelee. Na wengine nyinyi msikatishwe tamaa na maneno ya Instagram au Facebook au JamiiForums au...

Kinyume chake aliyoyaandika hapo mleta uzi yote ni hasara za kukosekana ndoa au hasara za watu kutokufuata misingi ya ndoa

NDOA INA UMUHIMU SANA HASA KWA KARNE HII TULIYONAYO

OENI NA OLEWENI
 
Back
Top Bottom