Hivi comments humu JamiiForums huwa zinaweza kufutwa? Maana nashangaa comment yangu siioni humu nikiingia wakati notification pale juu imeonesha mtoa post kaniquote kabisa.
Sasa naandika tena
WEWE (MTOA MADA) NI PUNDA... TENA SI WEWE TU BALI NA WOTE WANAOKUSAPOTI
ifuteni na hiyo sasa maana inaonesha ni jinsi gani mlivyodhamiria kuporomosha jamii. Yaani mtu ananyong'onyeza kabisa harakati za jamii katika kudumisha utamaduni halafu mnachukulia poa duh! Kweli kua uyaone- siyo maghorofa.
Ndoa ina faida sana tofauti na KakaMkubwa anavyotuaminisha hapa. Kwa ufupi nitataja faida chache tu
1. Kuunga (udugu/Undugu)
Ndoa inasababisha watu kuwa ndugu moja hivyo kuongeza wigo wa ushirikiano. Angalia familia zenye upweke kijana akija na mchumba members wanavyofurahia utasikia "nafuu baba ulete mtu ili na mimi nipate wa kupiga nae stori". Usipooa kama ukoo/familia yenu ina member wanne mtabaki hivyo hivyo wanne tu lakini ukioa mnakuwa ndugu kubwa ambapo faida yake sisi walala hoi ndo tunaijua (hasa kwenye matukio makubwa) ila wewe kwakuwa 'umejitosheleza' utasema "wingi si hoja"
2. Kustiriana
Mashimo makubwa vibamia wenye makovu wasio na nywele nk wote hao isingekuwa ndoa wangetangazika balaa ila ndoa zinawasitiri. Pia wenye kipato wanawasitiri wasio kipato, wenye kukubalika kuwasitiri wasiokubalika nk. Hamu za kingono bila ndoa watu wangedhalilika lakini angalia watu wanasitirika kingono kupitia ndoa na ukitaka kuamini wewe kama hujaoa ngoja apite mdada anatingisha matako halafu hamu ikaja na simu haina chaji wala hela huna. Vilevile wenye upweke kusitiriwa na wenye furaha (rejea hoja namba 1). Bila ndoa watu wangedanga sana ila mahitaji ya kifedha mtu anakuwa anayapata kwa mwenza wake mambo fresh. Kwa kifupi vyovyote utakavyoiweka hiyo faida ila hoja inabaki kwamba ndoa inastiri watu.
3. Kupunguza zinaa
(Wanaita ngono holela) ambapo wasioolewa wanajikuta wanakuwa malaya wahuni na majina mengine pale wanapokosa au wanapohitaji kupata faida za ndoa kwa njia tofauti na ndoa
4.Utulivu
Wewe uliyesema unapata kila wakipatacho waliooa ni mwongo. Leo unalala na mwajuma keshokutwa veronica wiki ijayo suzi asipokuja unajikuta unachukua mpaka yule malaya au hata chizi wa hapo mtaani kwenu ilimradi tu ukidhi haja zako. Mara bahati amesema angekuja halafu hajaja umengoja mpaka basi na simu hapatikani. Siku nyingine unachoka na kazi ukirudi unahitaji mawazo ya kukuimarisha lakini hayupo wa kufanya hivyo. Mara saa zingine hujamalizia "cha pili" simu ya demu imeita anahitajika haraka sana hapo bado hatujaongelea ishu ya purukushani na madume wenzako katika scramble na huyo jike sasa yote hayo utulivu uko wapi
5. Kupata familia (mke na watoto)
Hoja yake mwandishi na wengineo wanasema eti watoto unazaa tu nje. Sasa fuatilia wote wanaozaa nje historia yao na wanawake wazazi wenzao au watoto hao uone kizungumkuti wanachokutana nacho. Mtoto hajulikani baba yake halisi ni nani na tena wanawake wengine anaamua kukufungia vioo kabisa hataki uwazoee 'watoto wake'. Watoto wengi wengi wenye utata juu ya baba zao na mama zao unakuta walizaliwa kwa mtindo huo mnaoushabikia
6. Kuongeza kipato (uchumi)
Hii wengi watapinga lakini kwa mwenye kutafakari vema anaelewa tu hata zile primitive society msingi mkuu wao ni watu. Jamii zote za kale matajiri walikuwa ni zile koo kubwa (zenye watu wengi). Sasa sijui bila kuoa hao watu watakuwaje ukoo mkubwa maana huwezi kwenda kukusanya watoto uliozaa nje kiholela eti uje uwajaze home wakati mama yao nae anataka aijaze familia ya kwao.
7. Kuwa tofauti na viumbe wengine
Binadamu ameumbwa na utashi wa kuishi tofauti na viumbe wengine kama ndege na wanyama na amepewa uwezo wa kuvitawala vitu vyote duniani sasa ikitokea yeye tena hataki kuishi kwa mifumo anataka aishi kama wanyama ni bora kumbe wanyama watutawale sisi sasa
8. Kuleta hadhi na heshima
Ukioa au kuolewa unakuwa na hadhi fulani na utapata heshima. Pia mwenyewe utakuwa mwadilifu na utakuwa mwenye kuheshimu. Angalia baadhi ya mambo utakuta asiyeoa hahitajiki kabisa wala hathaminiki kisa tu haaminiki au angalia baadhi ya hoja za mabachela zinapuuzwa kabisa kisa hajaoa
9. Mwisho niseme tu ndoa ni kiburudisho kwa wanandoa (hasa sisi wanaume) ambao starehe yetu kuu ya pili ukiacha kulala ni ngono, ndoa ni kitulizo, ndoa inaleta uchamungu, ndoa ni nusura pia na ndomaana vijana wanasema ufanye upate nusra uepuke mtihani wa zinaa. Nawashauri hata nyinyi mnaoshabikia hapa kama hamjaoa mfanye muoe (sijui muolewe) na kamwe msigeuze changamoto mlizoziona/sikia/kutana nazo katika ndoa mkazifanya ndo fursa za kukandia ndoa laa! Bali ni muda mwafaka wa kucheki wapi pa kurekebisha ndoa isiwe taabu na maisha ya ndoa yaendelee. Na wengine nyinyi msikatishwe tamaa na maneno ya Instagram au Facebook au JamiiForums au...
Kinyume chake aliyoyaandika hapo mleta uzi yote ni hasara za kukosekana ndoa au hasara za watu kutokufuata misingi ya ndoa
NDOA INA UMUHIMU SANA HASA KWA KARNE HII TULIYONAYO
OENI NA OLEWENI