Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Hakuna utajiri wa kishetani, Kama kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina, Kwanini watu maskini wasiutumie kuondokana na umaskini wao?

Waafrika wengi hasa watanzania wamekuwa wakiamini kwa muda mrefu kwamba kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina. Cha kushangaza hali zao za kiuchumi ziko vilevile miaka nenda rudi.

Kama kweli kwa hakika unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote uwe tajiri mkubwa nchini Tanzania, Afrika na duniani?

Kwa nini ujihangaishe kufanya kazi na kuchoka ilhali unajua kuna utajiri wa kishetani?

Kamtumie huyo shetani akutajirishe kama ni rahisi hivyo!!

Katoe kafara za kutosha ikiwezekana hata ukoo wako wote tuone kama biashara yako itakuwa kubwa au utaweza hata kufikia utajiri wa Bakhressa.

Kama kweli kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini usiutumie kwa nguvu zako zote, Uwazidi matajiri wakubwa Afrika kama Aliko Dangote, Bakhressa, Mo Dewji na matajiri wengine wakubwa duniani kama Elon musk, Jeff Bezos?

Kama kweli unajua na kuamini kuna utajiri wa kishetani, kichawi au kishirikina. Kwa nini hujautumia huo uchawi, ushirikina, uganga angalau ufike hata level za utajiri wa Mo Dewji?

Kama unaamini kuna Shetani akitolewa kafara anatoa mali au atakupa mali za kukutajirisha, Katoe kafara wazazi wako au wanao wote tuone kama hata utafika level za utajiri wa Dangote.

Au kama unaamini kuna utajiri wa ndagu, uganga, ulozi n.k
Mwambie huyo mtoa ndagu au mganga, Akupe utajiri angalau umfikie au umzidi Bakhressa kama ana huo uwezo.

Au mwambie huyo mganga akuwezeshe umiliki private jet ✈️, Kiwanda kikubwa cha uzalishaji, Magari makali ya kifahari kama Rolls-Royce Boat tail, Mercedes Maybach, Buggati, Lamborghini, Cadillac escalade au akishindwa sana angalau akupe Range rover sport kwa uganga wake tu.

Waafrika wengi hasa watanzania wana amini kuna utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina lakini bado maisha yao ni ya kimaskini, kikapuku, kifukara pangu pakavu tia mchuzi.

Kama unaamini au unajua kuna Shetani anatoa utajiri, Kamtumie kwa nguvu zako zote akutajirishe na uwe tajiri kweli, Angalau ufike level za utajiri wa kina Dangote.

Kisha ndio uanze kusema kwamba kuna utajiri wa kishetani.

Habari za utajiri wa kishetani, kichawi na kishirikina, Husikika tu kwa waafrika maskini choka mbaya, wajinga, wavivu, makapuku, makabwela na mafukara ambao wanashinda vijiweni na vilabuni waki danganyana na kupeana matumaini uchwara ya utajiri wa kufikirika.

Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani kinacho toa utajiri. Utajiri na pesa hutoka kwa binadamu. Hakuna kiumbe kiitwacho Shetani chenye pesa.

Pesa ni za binadamu, Si za Mungu wala Shetani.

Hakuna Mungu, Shetani, Jini, Pepo au nguvu yeyote ile ya kimiujiza inayotoa Utajiri.

Pesa, Mali na utajiri hupatikana kwa nguvu za kibinadamu na wanadamu.

Ni wajanja wachache tu huwalaghai na kuwadanganya watu wengine kwamba kuna shetani anatoa utajiri ili kuwahadaa na kuwapumbaza watu wajinga wasiotaka kuhustle wenyewe wakitegemea mafanikio ya kuletewa.

Ndio maana unakuta wanawekewa masharti makali ya kupata pesa hizo ambao wao hudhani ndio masharti ya kishetani ya huyo shetani, Kumbe ni masharti ya binadamu wajanja tu.

The supernatural power is You, Yourself.

Hakuna Mungu wala Shetani anayetoa utajiri, pesa au mali.

I'm out.
Rubbish. Shule mnafungua lini 😂
 
Mpaka sasa hakuna aliyethibitisha utajiri wa kichawi kwamba upo zaidi ya makasiriko tu kama mlikua mnategemea kupata utajiri wa uchawi sijui hirizi za kujilinda na ujinga mwingine imekula kwenu .
Wanasema upo hawataji ni nani anao ni vijihadithi tu kupeana moyo na sababu za umasikini wao 😀
 
Njoo ujionee namna tunavyo miliki nyoka wanao tapika pesa Kila ijumaa mchana kiasi Cha 200M inaingia Kila ijumaa Cha muhimu kuzingatia mashart
Hii kitu haipo duniani mpaka akhera kama ipo thibitisha
 
Hivi zile ng’ombe zinazotolewa na waarabu mwaka hadi mwaka zinachinjwa wanagawiwa watu anataka kusema wana roho nzuri wanatoa bure tu??? Huyi hajui mambo ya spiritual ni kumuacha
Thibitisha kwamba hizo ng'ombe zina uchawi na sio nzuri.
 
Hivi zile ng’ombe zinazotolewa na waarabu mwaka hadi mwaka zinachinjwa wanagawiwa watu anataka kusema wana roho nzuri wanatoa bure tu??? Huyi hajui mambo ya spiritual ni kumuacha
Utasema hata nyama tunazokula siku za sikukuu nazo ni kwa ajili ya uchawi
 
Kama huo uchawi wako una nguvu kweli, Nilogee huko huko.

Ukifanikiwa uje na uthibitisho hapa.
Ka huamini jiulize zamani ulivokua mdogo ulikua unaenda kanisani au msikitini...

Na je sasa hivi unaenda hizo sehemu kama hauamini mambo ya msikitini au kanisani basi wewe mchawi na ndio maana huogopi kulogwa maana unajua unajiweza..

Kiufupi we faza unatisha sana
 
Kwahiyo kupitia hiyo tiba ya mama na hayo masharti ndio ukahitimisha kuwa kuna utajiri wa nguvu za giza
Huo Ni mfano tu.
Mama anadai wakati wanahama alipoteza daftari la maelekezo ya dawa tiba za asili hivyo alikuwa amekariri hiyo tu.
Sasa chukulia hiyo ambayo kwa udogo wake lkn pesa zilikuwa zinamkuta amekaa tu nyumbani. Je Kama angekuwa nazo zote unafikiri ingekuwaje? Alafu ujue Mimi mwenyewe najua namna yakutibu coz alivyokuwa anatibu mama hata Mimi nikiamua naweza Tena naweza ifanya kimjini nikapata pesa nyingi sana. Lkn siwezi mimi nimeshaokoka now.
 
Ka huamini jiulize zamani ulivokua mdogo ulikua unaenda kanisani au msikitini...

Na je sasa hivi unaenda hizo sehemu kama hauamini mambo ya msikitini au kanisani basi wewe mchawi na ndio maana huogopi kulogwa maana unajua unajiweza..

Kiufupi we faza unatisha sana
Uchawi wa kiafrika ungekuwa na nguvu kweli wange waloga wazungu kipindi kile cha utumwa na ukoloni.

Uchawi wa kiafrika ndio uleule wa kina Kinjeketile Ngwale kwenye vita vya majimaji alivyo wadanganya wenzake wakisema "maji! maji! maji!" Risasi zitabadilika kuwa maji kweli. Matokeo yake walifyatuliwa kama njiwa wakafa.

Sasa ndio habari zilezile za uchawi huohuo usio na nguvu yeyote,Bado waafrika maskini wanabaki wakiuamini. Kumbe hauna lolote.

If magic and witchcraft really existed people would have weaponized them long time ago, We would have magic missiles, Enchanted bullets, invisible Rockets and arcane nukes.
 
Hapana.

Nitakupa mfano,

Ukishajua mwanzilishi wa JF ni Maxence Melo, Huihitaji tena imani kwamba Jamii forums ilianzishwa na Maxence Melo.

Maana tayari unajua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kwamba mwanzilishi wa JF ni Maxence Melo.

Kitu ambacho hukijui ndio unakua na imani nacho maana huna uhakika wala uthibitisho wa kitu hicho.

Hivyo imani si kujua.

Imani ni kutokuwa na uhakika, ushahidi wala uthibitisho.
Imani sio kutokuwa na uhakika hahahaha
Imani Ni kuwa na uhakika Mia asilimia mbona huelewi? Kama huna uhakika hiyo sio imani Ni upagani. Lkn ukizungumzia uthibitisho ndipo tunapata kupitia shuhuda Sasa.
 
Huo Ni mfano tu.
Mama anadai wakati wanahama alipoteza daftari la maelekezo ya dawa tiba za asili hivyo alikuwa amekariri hiyo tu.
Sasa chukulia hiyo ambayo kwa udogo wake lkn pesa zilikuwa zinamkuta amekaa tu nyumbani. Je Kama angekuwa nazo zote unafikiri ingekuwaje? Alafu ujue Mimi mwenyewe najua namna yakutibu coz alivyokuwa anatibu mama hata Mimi nikiamua naweza Tena naweza ifanya kimjini nikapata pesa nyingi sana. Lkn siwezi mimi nimeshaokoka now.
Sasa ukitibu watu wakakupa pesa au ukawa na wateja wengi unawapa tiba asilia ukitajirika ndio utasema uchawi umekupa utajiri?

Mama ako alikuwa anatoa huduma ya kitabibu kupitia miti shamba wewe unamuita mchawi najua dini ndio imekukaririsha hivyo
 
Naona kauzi ka mwamba kanazidi kupepea tu.
Mpaka dakika hii, Hakuna aliyeweza kueleza na kuthibitisha ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi au ushirikina.

Au ni nchi gani duniani, Raia wake walifanikiwa kwa nguvu za kichawi, kishetani na kishirikina?

Wanaleta stori stori tu zisizo na uthibitisho wowote ule.
 
Imani sio kutokuwa na uhakika hahahaha
Imani Ni kuwa na uhakika Mia asilimia mbona huelewi? Kama huna uhakika hiyo sio imani Ni upagani. Lkn ukizungumzia uthibitisho ndipo tunapata kupitia shuhuda Sasa.
Thibitisha kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho ni tajiri gani mkubwa duniani alifanikiwa kwa uchawi au ushirikina?
 
Wengi wenu mnakariri tu mkiona fulani katupiwa jini au kachukuliwa msukule kwakuwa mnaamini na kuaminishwa na dini zenu pia mnaamini pesa inavutwa kupitia sijui majini na misukule bila uthibitisho wowote

Wazee pesa hailogeki wala haivutwi kwa misukule kama mnaweza kavuteni za BOT tuone

Watu wanahaso from scratch miaka na miaka wakitusua mnakaa kwenye vijiwe vyenu kusema wameloga sijui freemason na mavitu mengine ya hovyo
 
Uchawi wa kiafrika ungekuwa na nguvu kweli wange waloga wazungu kipindi kile cha utumwa na ukoloni.

Uchawi wa kiafrika ndio uleule wa kina Kinjeketile Ngwale kwenye vita vya majimaji alivyo wadanganya wenzake wakisema "maji! maji! maji!" Risasi zitabadilika kuwa maji kweli. Matokeo yake walifyatuliwa kama njiwa wakafa.

Sasa ndio habari zilezile za uchawi huohuo usio na nguvu yeyote,Bado waafrika maskini wanabaki wakiuamini. Kumbe hauna lolote.

If magic and witchcraft really existed people would have weaponized them long time ago, We would have magic missiles, Enchanted bullets, invisible Rockets and arcane nukes.
Sasa mkuu...
Ujawahi kutana na kesi mtu kalogwa au hiyo ni nini..

Hata uchawi nao una limit yake unaposema kurusha missile hizo sijui kuwaloga wazungu, ukute hyo stage ni kubwa sana ya hali ya juu..

Ila huku mtaani mtaani mbona watu wanalogwa kaka
 
Wengi wenu mnakariri tu mkiona fulani katupiwa jini au kachukuliwa msukule kwakuwa mnaamini na kuaminishwa na dini zenu pia mnaamini pesa inavutwa kupitia sijui majini na misukule bila uthibitisho wowote

Wazee pesa hailogeki wala haivutwi kwa misukule kama mnaweza kavuteni za BOT tuone

Watu wanahaso from scratch miaka na miaka wakitusua mnakaa kwenye vijiwe vyenu kusema wameloga sijui freemason na mavitu mengine ya hovyo
Ety mkuu ..
Naskia baressa alianza kushona viatu..?
Nauliza tuu japo nje ya mada 🙌😀😀
 
Back
Top Bottom