Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Demi anaefanya hivyo huyo sio mchawi huyo ni mshirikina

Emu jua kuwatofautisha hawa watu wawili wewe unajichanganya sana, kuna mchawi na pia kuna mshirikina, sasa huyo unaemzungumzia hapo sio mchawi huyo ni mshirikina, kuna tofauti kubwa kati ya uchawi na ushirikina

Kuelewa itakua ni ngumu sana km hauwezi kutofautisha kipi ni kipi na kipi ni kipi
Uchawi na ushirikina hakuna tofauti yoyote, uchawi ni neno la kibantu na ushirikina limetoholewa kutoka katika lugha ya kiarabu (shirk). yote yanajaribu kuelezea possibility ya kufanya vitu kwa njia isiyo ya kawaida
 
Hasa kama akisema Anamwamini Mungu lakini haamini katika uwepo wa uchawi
Nje ya mada nina swali. Kuna uhusiano wowote usiku nikamuota adui wangu. Halafu siku hiohio nikafikwa na baya( hapa naongelea nishaota zaidi ya mara 7 na mara hizi zote huishia siku yangu kuharibikiwa kazini kwangu).
 
Jina lako linaonyesha umesoma Biology miongoni kwa masomo nlokuwa nayeweza ila nlipuuza (sijajuaga kwa nini)
Sema endelea kupambana safari bado ipo ndefu utakuja unalia lia hapa JF,
Matumizi mabaya ya pesa siezi laumu uchawi ila
......what the force behind?
 
Nje ya mada nina swali. Kuna uhusiano wowote usiku nikamuota adui wangu. Halafu siku hiohio nikafikwa na baya( hapa naongelea nishaota zaidi ya mara 7 na mara hizi zote huishia siku yangu kuharibikiwa kazini kwangu).
Kwa ninavyoelewa kuhsu ndoto.
Ndoto ni matokeo ya ubongo kujikarabati. Kwenye ubongo Kuna mawimbi yanahusika na kumbukumbu ambayo Yapo slow sana.
hivyo ukitumia muda mwingi kufikiria, ndivyo hayo mawimbi Yana take too long time kuchakata fikra zako.
Kwahiyo ukienda kulala hayo mawimbi yanaendelea kufanya kazi na ndiyo sababu ya kupata ndoto.
Kwamfano kwa situation uliyokuwa nayo jaribu kufanya experiment ya kuangalia mpira na kufatilia habari za michezo kuanzia asubuhi Hadi jion, au jaribu kuangalia video za ngono (just experiment) kwa karibu siku nzima, then chunguza aina ya ndoto utakazoota, utakuta zinashadadia sana na kitu ulichotumia muda mrefu kukiwaza
 
Hiyo namba 4 ya Bundi fanya upya utafiti huna taarifa sahihi.
Na log OFF.
Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza. Nimekuja kugundua kuwa mambo mengi yanayoaminika kutokana na uchawi, yanaaminika hivyo sababu ya watu kuwa wajinga. Nitoe mifano.

1. Kuna mtu alikuwa anapata kinyesi cheusi. sasa sababu ya ujinga akawa anaamini amerogwa. Lakini kumbe kile kinyesi cheusi ni dalili ya vidonda vya tumbo, na ule weusi ni madini chuma kutoka kwenye damu inayomvuja tumboni.

2. Mtu mwingine akasema wazungu nao wachawi sana. kuna kijiji watu walikuwa wanakufa kwa radi. Mzungu akaja akasimamisha kamnara tu radi ikaacha kuua watu.

3. Wengi wanaamini vichaa wanaotembea barabarani wamerogwa. Lakini vichaa karibu vyote vinatokana na vichocheo kuyumba au kujeruhiwa kwa ubongo.

4. Watu wanaamini bundi wanatumiwa na wachawi sababu wanatembea usiku. Lakini tunajua uwezo wa bundi kuona usiku ndiyo unamuwezesha kufanya mawindo yake usiku.

5. Watu kwa ujinga wa kushindwa kupiga hesabu za mapato na matumizi, na kuweza kutunza pesa wanasingizia chuma ulete.

6. Magonjwa mengi hapo zamani yalidhaniwa kuwa yanatokana na kurogwa. Lakini sababu zake hasa zimekuja kufahamika. ujinga ndiyo ulifanya watu waamini kuna kurogwa. Kuna mchezaji amefariki juzi mguu unaoza yeye anasema ametupiwa jini.

7. Kanuni za kilimo zinajulikana lakini unakuta kuna watu wanaamini mtu anaweza kuroga apate mazao mengi, au akakuroga usipate mazao ya kutosha.

8.Madini yanapopatikana na jinsi ya kuyachimba huwa inafahamika, l;akini watu huwa wanaamini yanapatikana kwa uchawi.

9. Mara kuna uchawi wa kuleta mvua na hali habari ya ujio wa mvua na kutokuja zinajulikana.

10. Wengine wanaamini uchawi unaweza kukusaidia kwenye uvuvi.

11. wengine wanasema kuna wachawi huwa wanaingilia watu kingono!!1!

Kiufupi, wajinga wakishindwa kuelewa kitu wanasingizia uchawi. Hakuna kitu kinafunua ujinga wa mtu kama imani yake juu ya habari za kichawi. Jinsi ilivyo kali ndivyo ujinga wake ulivyo mkali zaidi.
 
Uchawi na ushirikina hakuna tofauti yoyote, uchawi ni neno la kibantu na ushirikina limetoholewa kutoka katika lugha ya kiarabu (shirk). yote yanajaribu kuelezea possibility ya kufanya vitu kwa njia isiyo ya kawaida
Hilo ni darasa pana, wewe uliezoea kukuza ubongo huwezi kujua tofauti ilipo alafu soma vizuri nilichokiandika usisome kwa kukurupuka,

Nmesema uchawi sio ushirikina ila ili ushirikina uwepo uchawi lazima uhusike, sasa uchawi ni nini na ushirikina ni nini hayo ni maelezo mengi

Nipe tofauti kati ya hivi vitatu magic, magick and witch craft

Naona jinsi ubongo wako ulivyokakamaa jambo hilo huwezi kulielewa katu kamwe yaan ubongo wako umeshakakamaa hautaki kuelewa kabisa,
 
Hilo ni darasa pana, wewe uliezoea kukuza ubongo huwezi kujua tofauti ilipo alafu soma vizuri nilichokiandika usisome kwa kukurupuka,

Nmesema uchawi sio ushirikina ila ili ushirikina uwepo uchawi lazima uhusike, sasa uchawi ni nini na ushirikina ni nini hayo ni maelezo mengi

Nipe tofauti kati ya hivi vitatu magic, magick and witch craft

Naona jinsi ubongo wako ulivyokakamaa jambo hilo huwezi kulielewa katu kamwe yaan ubongo wako umeshakakamaa hautaki kuelewa kabisa,
Toa definition ya uchawi na ushirikina
 
Mimi nakazia ni wajinga ndio.

Na kusingizia kwamba uchawi wetu huu tunaofundishana humu eti umezungumzwa mpaka kwenye vitabu vitakaatifu ni ujinga mara mbili yake.

Neno uchawi na mchawi linalozungumziwa kwenye kitabu takatifu cha biblia, halina maana ya huu uchawi tunaoaminisha humu wa sijui kupaa na ungo usiku, sijui kuingia ndani bila kuonekana au kinyumenyume au kugeuzana misukule na kwenda kulima mashamba, neno uchawi ndani ya biblia halina maana hiyo. Kwa lugha asili za biblia naweza kusema wachawi wanaozungumzwa kwenye biblia ni wanamazingaombwe na sio hawa wetu wa sijui kurogana, kupaa na ungo nk
Nafikiri watu wanaangamia kwa kukosa maarifa hayo unayosema mazingaombwe so uchawi?? Na kama sio uchawi hebu fanya na wewe hayo mazingaombwe ili tuproove kwamba so uchawii... Kuna mazingaombwe ya kichawi niliwahi kuyaona mwaka 2012 nikikuhadithia hapa hutoamini kwa kuwa umejengeka kutoamini uchawi.. Wachungaji wenyewe makanisani wanakiri kwamba uchawi upo na wengine hadi wanataja vijiji ulipokithiri
 
Kwa hio unapinga kitu ambacho haukijui,

Shirk ni neno la kiarabu lenye maana jumuishi ya uchawi au ushirikina ila uchawi na ushirikina vinatofautiana

Magick & Magic ni kitu kimoja, huu ni uchawi ambao hutumia nguvu za asili (super natural powers) zinazokuzunguka kuleta mrejesho

Witch craft ni ushirikina ambao hauwezi kufanyika bila kuambana na uchawi (magic) ila hufanyika kwa lengo la kuwadhulu watu au kumdhulu mtu fulani kwa sababu fulani

Ushaelewa hapo au bado umekaza ubongo yaan bado ubongo wako umekakamaa huelewielewi
 
Sasa kama bank wanajenga kwa uchawi na kafara kwanini wanaweka ulinzi na ma camera? Kwanini wasitumie uchawi kulinda mali zao?
Hapa mkuu unachanganya vitu viwili vitu vya kiroho na vya kawaida nikiwa na maana hiii ulinzi wa camera na walinzi unakuwepo kwa ajili ya wezi na majambazi
 
Back
Top Bottom