Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hasira ya nini badala ya kumfundisha? Hata mimi sijawahi kukutwa na uchawi wowote wala kuuona unadhani nitaamini?
Nitabisha tu maana sijawahi kuona kitu chochote cha kichawi kwenye maisha yangu.
Mtoa mada badala ya kuuliza aelezwe, ameanza kuwaita 'wajinga' wale wanaojua..
👇👇

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi​

Ulimwengu una elimu pana mno isiyofundishwa mashuleni ambayo hakuna mtu mmoja anayeweza kuifahamu yote.
Tatizo ni pale mtu anapojidai anajua jambo ambalo hajui
 
Nafikiri watu wanaangamia kwa kukosa maarifa hayo unayosema mazingaombwe so uchawi?? Na kama sio uchawi hebu fanya na wewe hayo mazingaombwe ili tuproove kwamba so uchawii... Kuna mazingaombwe ya kichawi niliwahi kuyaona mwaka 2012 nikikuhadithia hapa hutoamini kwa kuwa umejengeka kutoamini uchawi.. Wachungaji wenyewe makanisani wanakiri kwamba uchawi upo na wengine hadi wanataja vijiji ulipokithiri
Yaani unasikiliza wachungaji ambao uwepo wa uchawi ni mtaji kwao?
 
Kwa hio unapinga kitu ambacho haukijui,

Shirk ni neno la kiarabu lenye maana jumuishi ya uchawi au ushirikina ila uchawi na ushirikina vinatofautiana

Magick & Magic ni kitu kimoja, huu ni uchawi ambao hutumia nguvu za asili (super natural powers) zinazokuzunguka kuleta mrejesho

Witch craft ni ushirikina ambao hauwezi kufanyika bila kuambana na uchawi (magic) ila hufanyika kwa lengo la kuwadhulu watu au kumdhulu mtu fulani kwa sababu fulani

Ushaelewa hapo au bado umekaza ubongo yaan bado ubongo wako umekakamaa huelewielewi
Unatupotosha kwa maneno mengi lakini contents hamna. Wale magician wanafanya mgic tricks za kutoa shilingi sikioni na njiwa kwa kofia hawana usupernatural wowote. wanasomea tu zile tricks.
 
Na mimi zamani nilikuwa mjinga kama wewe. Lakini polepole nikaanza kuona mwanga. Vitu vingi nilivyodhani uchawi nikaona vina explanation nzuri tu. Jielimishe utatoka huko. Kuamini uchawi ni ujinga mkubwa, kwa nini? Hizo imani za kichawi zipo kwenye uchumi, afya, elimu, mambo ya kijamii, siasa, ujenzi nk nk. So ukiwa nazo unakuwa mjinga mjinga kwenye nyanja karibu zote za maisha. Ni hatari sana.
Uchawi una "fungu lake" na mimi siyo mjinga wa kuamini kuwa kuumwa magonjwa ni kurogwa!

Ninachotaka hapa katika hoja hii, uungame na utudhihirishie kuwa uchawi haupo period

Hayo mengine unayobwabwaja hakuna jipya hapo ni siasa tu unapiga na kila mtu anayajua unayoyaongea wewe.

Kila siku wanasema anayesema kitu kipo ndiye anayetakiwa kuleta ushahidi kuwa kipo, siye anayesema hakipo. Weww ndiye utudhihirishie kuwa imani juu ya uchawi ina msingi wenye mantiki. Lakini sishangai kwa mchawi kutofahamu hilo.
 
Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza. Nimekuja kugundua kuwa mambo mengi yanayoaminika kutokana na uchawi, yanaaminika hivyo sababu ya watu kuwa wajinga. Nitoe mifano.

1. Kuna mtu alikuwa anapata kinyesi cheusi. sasa sababu ya ujinga akawa anaamini amerogwa. Lakini kumbe kile kinyesi cheusi ni dalili ya vidonda vya tumbo, na ule weusi ni madini chuma kutoka kwenye damu inayomvuja tumboni.

2. Mtu mwingine akasema wazungu nao wachawi sana. kuna kijiji watu walikuwa wanakufa kwa radi. Mzungu akaja akasimamisha kamnara tu radi ikaacha kuua watu.

3. Wengi wanaamini vichaa wanaotembea barabarani wamerogwa. Lakini vichaa karibu vyote vinatokana na vichocheo kuyumba au kujeruhiwa kwa ubongo.

4. Watu wanaamini bundi wanatumiwa na wachawi sababu wanatembea usiku. Lakini tunajua uwezo wa bundi kuona usiku ndiyo unamuwezesha kufanya mawindo yake usiku.

5. Watu kwa ujinga wa kushindwa kupiga hesabu za mapato na matumizi, na kuweza kutunza pesa wanasingizia chuma ulete.

6. Magonjwa mengi hapo zamani yalidhaniwa kuwa yanatokana na kurogwa. Lakini sababu zake hasa zimekuja kufahamika. ujinga ndiyo ulifanya watu waamini kuna kurogwa. Kuna mchezaji amefariki juzi mguu unaoza yeye anasema ametupiwa jini.

7. Kanuni za kilimo zinajulikana lakini unakuta kuna watu wanaamini mtu anaweza kuroga apate mazao mengi, au akakuroga usipate mazao ya kutosha.

8.Madini yanapopatikana na jinsi ya kuyachimba huwa inafahamika, l;akini watu huwa wanaamini yanapatikana kwa uchawi.

9. Mara kuna uchawi wa kuleta mvua na hali habari ya ujio wa mvua na kutokuja zinajulikana.

10. Wengine wanaamini uchawi unaweza kukusaidia kwenye uvuvi.

11. wengine wanasema kuna wachawi huwa wanaingilia watu kingono!!1!

Kiufupi, wajinga wakishindwa kuelewa kitu wanasingizia uchawi. Hakuna kitu kinafunua ujinga wa mtu kama imani yake juu ya habari za kichawi. Jinsi ilivyo kali ndivyo ujinga wake ulivyo mkali zaidi.

Kwa kweli watu wanaoamini uchawi akili zao ni za hovyo kila akipata hata homa anajua kalogwa, Hapa jirani kuna mama anaumwa Homa ya Ini na Hospital wameambiwa lakini kila siku kwa waganga wao wanachoamini kalogwa tu yaani ukimuona magonjwa utamhurumia kila siku madawa ya kienyeji hosptali hawaendi tena!
 
Kwa nini chuma ulete hawaibi pesa za benki??
Lycaon pictus mzee wangu uchawi upo wala usinidanganye mzee kujifanya kila kitu kutoamini ,japo kuna watu wanazidisha hata kitu cha ujinga wake anasingizia kurogwa,

Hiyo namba nane unapigwa ndumba kweupe kabisa ,unalima ww wanakuja kuvuna wenyeji kichawi na ww unapata kiduchu,usiombe yakukute.

Chuma ulete ndio usiseme kabisa yan kaa pembeni mzeeee,ni chuma ulete kweli na ipo advanced sasa hivi mtu anaweza pita tu njia akakuchukulia hela bila kuja dukani na kukupa buku ww ukaona kakupa ellfu 10.

Yangu ni hayo tu.
 
Hakuna uchawi hapo, labda ulipatwa na deja vu
Siku moja vijana wangu wa kazi walinipigia simu saa saba usiku. Wakaniambia Kuna watu wanafanya vurugu eneo langu la biashara.
Niliamka na kuelekea huko.
Kufika pale segerea oilcom Kuna Kona Kali kuelekea stand. Mm nilinyoosha kuelekea kwa CDF mstafu. Ile naachha Barabara kuu, nikasikia mlio wa break Kisha kishindo kikubwa. Nilipochungulia nikaona gari kwenye mtaro imepinduka tairi ziko juu.
Nikashuka kwenye gari ili nikatoe msaada. Nilipofika sehemu ya tukio nikakuta Ile gari haipo. Tukio hili tulishuhudia mm na mlinzi wa petrol station.
JE, HUU SI UCHAWI?
 
Mbona Wazungu walikuloga ukaacha mila zako ukafuata zao mf. ( Dini zao). Mtu kugundua uchawi ni elimu ya hali ya juu. Unamkuta kijana hajasoma ila kitendo cha kugundua tu Kuna uchawi akawa na hali nzuri kiuchumi kuzidi yule msomi ambae haamini katika uchawi. Nikusaidie kidogo, " kila penye mambo mazuri hasa kiuchumi, uchawi unashamiri". Hakika nakuambia, hata wanaohubiri neno la Mungu uchawi upo. Biblia yangu kwenye ubongo inasema "enyi wana wa Dunia mnaangamia kwa kukosa maarifa" wake up! Life is a game, play it well.
 
Kwa kweli watu wanaoamini uchawi akili zao ni za hovyo kila akipata hata homa anajua kalogwa, Hapa jirani kuna mama anaumwa Homa ya Ini na Hospital wameambiwa lakini kila siku kwa waganga wao wanachoamini kalogwa tu yaani ukimuona magonjwa utamhurumia kila siku madawa ya kienyeji hosptali hawaendi tena!
Inasikitisha sana. Na kama ni magonjwa ya kuambukiza kama TB unakuta familia nzima inateketea, na hapo ndiyo wanazidi kuamini kuwa wanaandamwa na wachawi.
 
Mbona Wazungu walikuloga ukaacha mila zako ukafuata zao mf. ( Dini zao). Mtu kugundua uchawi ni elimu ya hali ya juu. Unamkuta kijana hajasoma ila kitendo cha kugundua tu Kuna uchawi akawa na hali nzuri kiuchumi kuzidi yule msomi ambae haamini katika uchawi. Nikusaidie kidogo, " kila penye mambo mazuri hasa kiuchumi, uchawi unashamiri". Hakika nakuambia, hata wanaohubiri neno la Mungu uchawi upo. Biblia yangu kwenye ubongo inasema "enyi wana wa Dunia mnaangamia kwa kukosa maarifa" wake up! Life is a game, play it well.
Ujinga wa wanaoamini uchawi ni wa kusikitikiwa.
 
Back
Top Bottom