Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hasira ya nini badala ya kumfundisha? Hata mimi sijawahi kukutwa na uchawi wowote wala kuuona unadhani nitaamini?
Nitabisha tu maana sijawahi kuona kitu chochote cha kichawi kwenye maisha yangu.
Mtoa mada badala ya kuuliza aelezwe, ameanza kuwaita 'wajinga' wale wanaojua..
👇👇

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi​

Ulimwengu una elimu pana mno isiyofundishwa mashuleni ambayo hakuna mtu mmoja anayeweza kuifahamu yote.
Tatizo ni pale mtu anapojidai anajua jambo ambalo hajui
 
Yaani unasikiliza wachungaji ambao uwepo wa uchawi ni mtaji kwao?
 
Unatupotosha kwa maneno mengi lakini contents hamna. Wale magician wanafanya mgic tricks za kutoa shilingi sikioni na njiwa kwa kofia hawana usupernatural wowote. wanasomea tu zile tricks.
 
Uchawi una "fungu lake" na mimi siyo mjinga wa kuamini kuwa kuumwa magonjwa ni kurogwa!

Ninachotaka hapa katika hoja hii, uungame na utudhihirishie kuwa uchawi haupo period

Hayo mengine unayobwabwaja hakuna jipya hapo ni siasa tu unapiga na kila mtu anayajua unayoyaongea wewe.
 
Kila siku wanasema anayesema kitu kipo ndiye anayetakiwa kuleta ushahidi kuwa kipo, siye anayesema hakipo. Weww ndiye utudhihirishie kuwa imani juu ya uchawi ina msingi wenye mantiki. Lakini sishangai kwa mchawi kutofahamu hilo.
 

Kwa kweli watu wanaoamini uchawi akili zao ni za hovyo kila akipata hata homa anajua kalogwa, Hapa jirani kuna mama anaumwa Homa ya Ini na Hospital wameambiwa lakini kila siku kwa waganga wao wanachoamini kalogwa tu yaani ukimuona magonjwa utamhurumia kila siku madawa ya kienyeji hosptali hawaendi tena!
 
Kwa nini chuma ulete hawaibi pesa za benki??
 
Hakuna uchawi hapo, labda ulipatwa na deja vu
 
Mbona Wazungu walikuloga ukaacha mila zako ukafuata zao mf. ( Dini zao). Mtu kugundua uchawi ni elimu ya hali ya juu. Unamkuta kijana hajasoma ila kitendo cha kugundua tu Kuna uchawi akawa na hali nzuri kiuchumi kuzidi yule msomi ambae haamini katika uchawi. Nikusaidie kidogo, " kila penye mambo mazuri hasa kiuchumi, uchawi unashamiri". Hakika nakuambia, hata wanaohubiri neno la Mungu uchawi upo. Biblia yangu kwenye ubongo inasema "enyi wana wa Dunia mnaangamia kwa kukosa maarifa" wake up! Life is a game, play it well.
 
Inasikitisha sana. Na kama ni magonjwa ya kuambukiza kama TB unakuta familia nzima inateketea, na hapo ndiyo wanazidi kuamini kuwa wanaandamwa na wachawi.
 
Ujinga wa wanaoamini uchawi ni wa kusikitikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…