Noja niwasaidie kidogo wavivu wa kufikiri na wabwatukaji, uchawi upo tena sana.
Uchawi ni swala la ulimwengu wa kiroho ambao binadamu hauwezi kuona kwa macho ya kawaida, nguvu za kiroho zinaonekana kwa jicho la tatu “third eye”
Swala la kusema mbona mchawi hawezi kuiba bank ni ufinyu wa kufikiri wa hali ya chini, na nikuambie tu hata leo mchawi akiingia ndani kwako hawezi kuiba hata mia yako
Kuna nguvu zimewekwa na wamiliki wa hizo pesa duniani kote, ndio maana unaona ni za moto hazishikiki na mchawi yoyote, Mungu hakushusha mapipa ya pesa duniani wala hakutengeneza bali tumezikuta, hivyo tambua pesa ina wamiliki wake wa hapa hapa duniani, hawashikiki na ndo watu wanaoongoza hii dunia, mwenye upeo mkubwa amenielewa.
Swala la mbona mchawi hawezi kuzamia nchi za nje pia ni umbumbumbu wa hali ya juu, kila eneo duniani lina watawala wake mangi ndio maana ww leo hii hauwezi kwenda kenya,south,canada,america bila kuwa na vibali, lasiivyo utaumia
Kila anga lina watu wake/wamiliki wachawi hawaruki ovyo ovyo.
Maswala ya kuiba pesa yapo ila ni chuma ulete, mazingaumbwe
Kama ww unaamini katika uwepo wa Mungu basi amini katika uwepo wa uchawi/shetani Maana zote ni nguvu za kiroho ila zina tenda tofauti, moja ina matendo ingine matendo machafu
Ila kama hauamini katika uwepo wa Mungu basi ntaheshimu mawazo yako kwamba uchawi haupo.