Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Hakuna watu wajinga kama watu wanaoamini habari za kichawi

Haiwezi kua bure pia si kila mtu anaweza kumudu hizo gharama hata uwe billionare na ndio maana hua hawaendi kuiba pesa bank
Nawaza hizo gharama ni kiasi gani hadi washindwe. Watu wanaua ili kupata utajiri na kweli anaupata kama mnavyoamini...ashindwe vipi kuua aende marekani.
 
Bado umekaza ubongo Demi
Nimesema kwamba wachawi utajiri wao sio pesa tunazotumia mimi na wewe, kwetu sisi mimi na wewe pesa ndio nguvu, ila utajiri wa wachawi upo katika nguvu za Imani yao sio haya makaratasi (fedha/pesa) kwao haya makaratasi sio chochote sio lolote ndio maana hauwakuti wameenda kukwapua bank na uchawi wa hivyo haupo maana Imani yao haiwaambii kua utajiri wao ni haya makaratasi,

Na pia umesema kwamba kuna watu wana utajiri wa kichawi narudia utajiri wa kichawi sio pesa unazozishika, yes wapo nakubariana nawe lakini sio wa kuiba bank ni wa kujishughulisha na kufanya kazi km binadamu wengine sio kufanya kazi kichawi,

Akihitaji kua na maendeleo lazima atajishughulisha ili apate pesa ila sio kwenda kuiba pesa bank kichawi

Na sio kwamba akiwa na pesa basi huo ndio utajiri wake hapana utajiri kwake km kweli yeye ni mchawi utajiri wake sio haya makaratasi
Mmmh haya
 
Kumbe unajua kueleza vizuri sasa ukaleta mambo ya technology ukachanganya mambo.

Unasemaje utajiri wa kichawi ni pesa ndogo elf 10, 20 wakati tunaonyeshwa matajiri ambao mnasema wanatumia uchawi?
Watu wanapata utajiri kichawi. Iweje useme utajiri wa kichawi ni wa pesa ndogo.
Kila kitu katika dunia ya kichawi kinaenda kwa kanuni na utaratibu maalumu,baadhi ya watu wanaamini science katika dunia ya nyama ni matokeo ya science mama yaani uchawi mfano ili upate maji unatakiwa kuwa na Hydrogen +Oxygen kwa uchawi ili kumroga mtu unatakiwa kuwa na nguo yake,jina,unyayo n.k ndio uchanganye na vitu maalumu hizo ni kanuni(formula )ukikosea kanuni hupati jibu sahihi.
 
Nawaza hizo gharama ni kiasi gani hadi washindwe. Watu wanaua ili kupata utajiri na kweli anaupata kama mnavyoamini...ashindwe vipi kuua aende marekani.
Demi anaefanya hivyo huyo sio mchawi huyo ni mshirikina

Emu jua kuwatofautisha hawa watu wawili wewe unajichanganya sana, kuna mchawi na pia kuna mshirikina, sasa huyo unaemzungumzia hapo sio mchawi huyo ni mshirikina, kuna tofauti kubwa kati ya uchawi na ushirikina

Kuelewa itakua ni ngumu sana km hauwezi kutofautisha kipi ni kipi na kipi ni kipi
 
Juzi kati nilikuwa nasoma habari za wahindi wekundu walivyokuwa wanapigana na wazungu huko Marekani. Sasa wahindi wale walikuwa wanategemea nyati kama chakula chao, hivyo walikuwa wakiwawinda kwa akili ili wasiishe. Wazungu wao wakawa wanawawinda kupata ngozi, hivyo waliwaua hovyo na kuacha mizoga porini. wahindi wakajianda kwenda kupigana na waharibifu hao. sasa wakaenda kwa mganga wao. mganga akawatengenezea dawa kuwa wakipigwa risasi, risasi zitayeyuka(Kama Kinjeketile tu). walipoenda vitani walipigwa vibaya na wengi wakafa. waliporudi walimghadhabikia sana yule mganga.

Cha ajabu hadi leo kuna watu wanaenda kwa waganga wawape dawa za kuzuia risasi. Haya ni maswala ya watu wajinga.
Hii ipo chief, kuna dozi unapewa hakuna siraha inaweza penya mwili wako
Tembea uone.

Sent from my Phantom6-Plus using JamiiForums mobile app
 
Demi anaefanya hivyo huyo sio mchawi huyo ni mshirikina

Emu jua kuwatofautisha hawa watu wawili wewe unajichanganya sana, kuna mchawi na pia kuna mshirikina, sasa huyo unaemzungumzia hapo sio mchawi huyo ni mshirikina, kuna tofauti kubwa kati ya uchawi na ushirikina

Kuelewa itakua ni ngumu sana km hauwezi kutofautisha kipi ni kipi na kipi ni kipi
Nilishakuelewa kaka yangu.
Lakini mshirikina si anapewa ujuzi na mchawi. Au na hili sijaelewa?

Basi hii bangi niliyovuta leo feki...si kwa kuyumbisha akili yangu kiasi hiki.
 
Nilishakuelewa kaka yangu.
Lakini mshirikina si anapewa ujuzi na mchawi. Au na hili sijaelewa?

Basi hii bangi niliyovuta leo feki...si kwa kuyumbisha akili yangu kiasi hiki.
Demi kwa kweli hio bangi ulivyovuta imekubangua kweli na utakua haujazimua na nyota

Sasa ipo hivi, mshirikina sio mchawi ila anautumia uchawi kufanya ushirikina, nataka twende taratibu naona wewe nikikupeleka haraka haraka unatoka kapa yaan hauelewi

Niambie kwanza hapo umeelewa au bado ubongo umekakamaa?
 
Nawaza hizo gharama ni kiasi gani hadi washindwe. Watu wanaua ili kupata utajiri na kweli anaupata kama mnavyoamini...ashindwe vipi kuua aende marekani.
Wanaoweza hayo wameenda tulio shindwa tunaenda kila siku kwa kutumia uchawi useful internet
 
Demi kwa kweli hio bangi ulivyovuta imekubangua kweli na utakua haujazimua na nyota

Sasa ipo hivi, mshirikina sio mchawi ila anautumia uchawi kufanya ushirikina, nataka twende taratibu naona wewe nikikupeleka haraka haraka unatoka kapa yaan hauelewi

Niambie kwanza hapo umeelewa au bado ubongo umekakamaa?
I like it slow.. thanks 😅😅.
Nimeelewa haya tuendelee. Lazima kieleweke leo
 
Back
Top Bottom