Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Polt Taikon, kule jotoridi ni chini ya nyuzi 9, ni hatari kwa uhai..!!
 
Niliusomaga nikasema kûna Mtu kapugwa na kitu kizito.

Kule hakunaga mlala nje
Ilikuwa safari ya misukosuko destination ilikuwa Songea Sasa nikapata mdau naye ni bodaboda akanilaza sebuleni kwake kwenye sofa akanipa mashuka tu ya kawaida aisee ni miongoni mwa usiku uliokuwa mgumu.

Mimi mwili wangu ni kama reptilian unasense baridi kwa haraka maana hata hapa mjini nikienda kuogolea siwezi kuzidisha nusu saa kwenye maji nitatoka natetemeka.

Wacha watu waje kutafuta maisha Dar maana unaweza kulala nje comfortable ila sio nyanda za juu kusini
 

Pole Sana Mkûu.
Niliusoma nikasema kijana amekutana nacho katika mapambano
 
Niliwah kukaa hapo nikiwa shule Kwa miaka 4, nikaja kupita last year, baridi imepungua sn compare na those days 2000 - 2005, nakumbuka mvua za barafu zilikuwa zinanyesha Mpaka teacher anasimamisha kipindi but now namiss sn kuishi maeneo hayo Mishe Tu zinatubana huku Dar, ( Kawawa JKT)
 
Nilishawahi kufika Mafinga tena ilikuwa ni July aisee nilioga siku ya kwanza tu siku zingine 5 sikuoga nilifikia pale Lutheran VTC baridi mnoo kwanza niliposhuka tu kwenye gari nikaitupa ile juice niliyoinunua nikanunua gloves na mzura lakini wapiii mpaka naondoka pale nikaenda kuoga Mbeya mjini, na kuna sehemu kule Mbeya kama unaenda Tunduma panaitwa kwa Mpemba napo ni 🥶
 
Niliwah kukaa hapo nikiwa shule Kwa miaka 4, nikaja kupita last year, baridi imepungua sn compare na those days 2000 - 2005, nakumbuka mvua za barafu zilikuwa zinanyesha Mpaka teacher anasimamisha kipindi but now namiss sn kuishi maeneo hayo Mishe Tu zinatubana huku Dar, ( Kawawa JKT)
 
Kijana. Hatujafika Mafinga ila tushakutana na baridi kali sana sehemu nyingine duniani.
Ni sahihi ila kwa Tanzania Mafinga, Makete, Kilolo na Njombe hali ni mbaya sana.

Kwa wenzetu wanaweza kujilinda na hiyo baridi ila nilienda Makete kwa jamaa yangu Sanga, ile hatari mkuu na ndio maana kupindi cha baridi watu hufa kwani huwasha mkaa ndani kujiditiri baridi mwisho wa siku huleta mauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…