Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Kwema Wakuu!

Nimeshawahi kuishi Mafinga mara kadhaa lakini sijawahi kuona baridi kama ya Juzi jumatatu tarehe 19. Dadeki baridi mpaka ukungu weñye barafu nyepesi ilikuwa inadondoka.

Nimefika Saa nane Usiku nikitokea Dsm. Nilitamani nirudi kwèñye Basi, Aiseeh! Pale Stendi nikaona makundi mawili ya Vijana yakiwa yamezunguka Moto wakiwa wanaota.
Nikavaa sweta Mbili, koti Moja lakini Wapi, nikaona sina namna Hapa Acha Nani nikaote Moto.

Wenyeji wakawa wananishangaa huku wakijaribu kutaka kunijua kama ninahitaji msaada gàni au nahitaji Usafiri WA bodaboda kwani wôte pale niligundua nu bodaboda, Mimi sikujali Wala nini, sikutaka kusalimu kwa sauti kûbwa, nikamsalimia aliyekaribu yàngu Kwa sauti ya chini. Nao wakanipuuza wakaendelea na Stori zào.

Nami nikaanza kutafakari nitaanzaje harakati zangu Siku ya Kesho Asûbuhi hasa kile kilichonipeleka. Saa yàngu mkononi ikinionyesha NI Saa Nane narobo.

Najua Baadhi ya Lodge nzuri zilizopo Hapa Mafinga, hivyo nikawa natafakari niende Ipi iliyokaribu,
Mara ñàona bodaboda mmoja anakoswakoswa na Lori pale Barabarani. Vijana wanapiga Milunzi huku wakishangilia, Wengine wakipiga kelele la shangwe.
Taikon nashusha pumzi kutuliza kihoro kilichokuwa kimenianza kutokana na kuona tukio lile.

Yule bodaboda Manusura akaja pale nikawa namsahili, Hofu yake ilikuwa dhahiri usoni licha ya kuwa alikuwa anaongea na wenzake waliokuwa wanamtania Tania.

Anasema Mikono ilikuwa imeshika ganzi kutokana na baridi Kali kiasi kwamba alishindwa kukata Kona Hali iliyosababishwa akoswekoswe na lile Lori.

Basi Stori ikawa baridi jinsi inavyowapa changamoto. Kîla mmoja akieleza baridi ilivyosababisha hatari ya waô kupata ajali kama mjuavyo Vijana.

Wàpo wateja pale ambao walikuwa wanaenda maeneo ya chini Kabisa àmbapo wanadai Huko kûna baridi la kufa Mtu hivyo waliwakataa kuwabeba.

Kuangalia saa inaniambia Saa tisa. Mpaka asûbuhi yalibaki masaa matatu tuu. Nikaona sina haja ya kuchukua Lodge. Nikaamua kukesha na wale Vijana kupata uzoefu mpya.

Aiseeh! Maisha haya, ukiona unapata chàkula na unaishi Vizuri Mshukuru Sana Mungu. Kûna Watu wanahangaika na wanafanya Kazi katika mazîngira Magumu hasa ikiwemo hawa bodaboda wa Mafinga.

Niligundua pia Vijana wa bodaboda wa Mafinga wanajitambua na kuelewa mambo ya kitaifa kama mambo ya Katiba, mambo ya Haki za kiraia na mambo ya Kisiasa ya Chadema na ccm.
Ingawaje wamekata TAMAA na Maisha, wanafanya mambo ilimradi.

Zaidi, niliwapenda Kwa Sababu licha ya Hali ngumu ya Kazi Yao lakini haikuwaondolea Ûtu na ukarimu Kwa Wageni àmbao tulifika pale Stendi.
Tofauti na maeneo mengine ya nchi niliyowahu kufika Kama Kahama Mjini, Mwanza mjini, Arusha Mjini, Mbeya Mjini, Moshi Mjini, Morogoro Mjini, na Dsm. Àmbapo Miji hiyo ukifika utakutana na usumbufu wa bodaboda au wapiga debe wakikung'ang'ania kama Mpira wa Kona.

Mafinga majira ya usiku ukishuka bodaboda watakuja lakini hawatakusumbua.

Pia suala la utapeli WA nauli Mahali unapoenda nimegundua Hawana TAMAA ndogondogo,
Nakumbuka Wakati fulani nilifika Arusha Saa saba Kasoro Usiku, kuuliza bajaji Ilipo hoteli àmbayo najua Kabisa Ipo upande WA Nyuma Kwa umbali usiozidi kilomita Moja, lakini Baadhi ya madereva wengi wa Arusha wanatamaa, hizô nauli walizokuwa wanataja utabaki kuwaonea huruma, na wewe hata kama unapajua jifanye upajui ili upime uaminifu wao.

Vijana uaminifu ni Jambo kûbwa Sana.
Eleweni Siku hizi Mtu hawezi kwenda sehemu pasipo kuwa na ABC za muhimu za Eneo àmbalo anaenda.
Lazima Mtu aulize nauli ya Eneo analoenda Kabla hajafika Hapo Stendi, ajue bei ya hoteli au lodge atakayoenda Kulala, na umbali WA lodge au hoteli hiyo kutokea Stendi.

Hongereni bodaboda wa Mafinga Kwa kuwakilisha Vijana wenzenu WA Hapo Mafinga. Nimewapa marks 70%.
Hii inaonyesha kama utapata kijana wa huku kûna uwezekano akawa mwaminifu ingawaje haimaanishi Hakuna àmbao siô waaminifu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa, Mafinga
Polt Taikon, kule jotoridi ni chini ya nyuzi 9, ni hatari kwa uhai..!!
 
Niliusomaga nikasema kûna Mtu kapugwa na kitu kizito.

Kule hakunaga mlala nje
Ilikuwa safari ya misukosuko destination ilikuwa Songea Sasa nikapata mdau naye ni bodaboda akanilaza sebuleni kwake kwenye sofa akanipa mashuka tu ya kawaida aisee ni miongoni mwa usiku uliokuwa mgumu.

Mimi mwili wangu ni kama reptilian unasense baridi kwa haraka maana hata hapa mjini nikienda kuogolea siwezi kuzidisha nusu saa kwenye maji nitatoka natetemeka.

Wacha watu waje kutafuta maisha Dar maana unaweza kulala nje comfortable ila sio nyanda za juu kusini
 
Ilikuwa safari ya misukosuko destination ilikuwa Songea Sasa nikapata mdau naye ni bodaboda akanilaza sebuleni kwake kwenye sofa akanipa mashuka tu ya kawaida aisee ni miongoni mwa usiku uliokuwa mgumu.

Mimi mwili wangu ni kama reptilian unasense baridi kwa haraka maana hata hapa mjini nikienda kuogolea siwezi kuzidisha nusu saa kwenye maji nitatoka natetemeka.

Wacha watu waje kutafuta maisha Dar maana unaweza kulala nje comfortable ila sio nyanda za juu kusini

Pole Sana Mkûu.
Niliusoma nikasema kijana amekutana nacho katika mapambano
 
Niliwah kukaa hapo nikiwa shule Kwa miaka 4, nikaja kupita last year, baridi imepungua sn compare na those days 2000 - 2005, nakumbuka mvua za barafu zilikuwa zinanyesha Mpaka teacher anasimamisha kipindi but now namiss sn kuishi maeneo hayo Mishe Tu zinatubana huku Dar, ( Kawawa JKT)
 
Nilishawahi kufika Mafinga tena ilikuwa ni July aisee nilioga siku ya kwanza tu siku zingine 5 sikuoga nilifikia pale Lutheran VTC baridi mnoo kwanza niliposhuka tu kwenye gari nikaitupa ile juice niliyoinunua nikanunua gloves na mzura lakini wapiii mpaka naondoka pale nikaenda kuoga Mbeya mjini, na kuna sehemu kule Mbeya kama unaenda Tunduma panaitwa kwa Mpemba napo ni 🥶
 
Niliwah kukaa hapo nikiwa shule Kwa miaka 4, nikaja kupita last year, baridi imepungua sn compare na those days 2000 - 2005, nakumbuka mvua za barafu zilikuwa zinanyesha Mpaka teacher anasimamisha kipindi but now namiss sn kuishi maeneo hayo Mishe Tu zinatubana huku Dar, ( Kawawa JKT)
 
Kijana. Hatujafika Mafinga ila tushakutana na baridi kali sana sehemu nyingine duniani.
Ni sahihi ila kwa Tanzania Mafinga, Makete, Kilolo na Njombe hali ni mbaya sana.

Kwa wenzetu wanaweza kujilinda na hiyo baridi ila nilienda Makete kwa jamaa yangu Sanga, ile hatari mkuu na ndio maana kupindi cha baridi watu hufa kwani huwasha mkaa ndani kujiditiri baridi mwisho wa siku huleta mauti.
 
Back
Top Bottom