Hakuna Watu wanapata shida kama bodaboda wa Mafinga nyakati za Usiku

Kwema Wakuu!

Nimeshawahi kuishi Mafinga mara kadhaa lakini sijawahi kuona baridi kama ya Juzi jumatatu tarehe 19. Dadeki baridi mpaka ukungu weñye barafu nyepesi ilikuwa inadondoka...
Mwakaleli huko baridi ni balaa!kipindi tunasoma huko kwa mababu zetu kipindi Cha baridi tunaingia darasani saa tatu,hata mwalimu hawezi kuandika ubaoni!
 
Mjifunze hata kujua miezi ya baridi hapa Tanzania ili ubebe hata makoto
. Kuanzi June-August hunipeleki Makambako Njombe,Makete Lushoto na sehemu yoyote inayosifika kwa baridi hapa Tz.
Kama Umeoa huko mna magonjwa au umefiwa!
 
Naelewa hali iliyokukumba.

2018 Nishawahi kukosea step nikajikuta sheli ya CF Mafinga pale Kinyanambo C saa 10 alfajiri. Nilidhani ile restaurant pale ni 24/7 kumbe inafungwa usiku.

Sikuwa na usafiri, hapakuwa na boda, palikuwa na mlinzi tu kwenye vile vibanda wanavyokulaga abiria wa mabasi. Tazama picha

Isitoshe, sikuwa na sweta wala koti. Nilivaa mashati yote niliyokuwa nayo kwenye begi, moja juu ya jingine. Palikuwa na ukungu usio wa kawaida, huoni zaidi ya mita 100 mbele. Naweka picha japo sidhani kama itatenda haki

Kibanda kilikuwa na umeme. Nilichomeka laptop, nikawasha, nikaandika kaprogram ka kuifanya CPU iwe busy sana, hivyo kuzalisha joto jingi ambalo likawa linapulizwa na feni ya laptop.

Nikaitega laptop kwenye yale matundu ya hewa iwe karibu na pua yangu, ili niweze kupumua hewa ya joto inayotoka kwenye laptop, nisipate baridi ndani ya mwili. Masaa yakapita, asubuhi ikafika, nikaingia kazini.
 
Ndio maana ile kanda inaongoza kwa kale kaugonjwa kakongwe kakuitwa "Juliana" na katakuwepo sana maana hali ya hewa sio rafiki.
 

Basi wewe ndio ungetakiwa uanzishe huu Uzi maana Moto uliokupata ni zaidi. Unaelewa hali hii zaidi na zaidi.

Yaani bila moto Kila kitu ulichovaa kinafreeze na baridi inaukuta mwili,mateso yanaanza kama Kawa.

Yaani usiombe ukajichanganya ukafika Maeneo ya Mafinga au njombe kama huna miundombinu ya kujikinga na baridi na umgeni unaweza ukafa
 
jitahidi sehemu za baridi mbali na sweta usikose kipisi cha bhang na pakiti ya fegi. HILI SITAKUSHAURI TENA
 
Asûbuhi imefika, napanda boda dadeki, mishipa ya kichwa inauma Kwa kupulizwa na Upepo, Lips za midomo inauma na ukisema uachie mdomo meno yanagongana na unaweza kujing'ata.
Huku siô poa
Leo utakunywa chai ukirudi home mdomo utakuwa umeungua, utasimulia maana hapo bado hujasema!
 
Nenda Njombe ukashuhudie baridi..mafinga cha mtoto mbona..
Bahati mzuri nazijuwa sehemu zote mbili.

Mafinga kuna season yake jua linawaka na baridi inapiga.

Sasa ukienda Njomba nyumba nyingi kuna fire place kama nyumba za ulaya kwa ajili ya kuchoma kuni za kuleta joto ndani.

My last experience Njombe nilikaa wiki moja hotelini na kuna maji moto lakini nilioga siku mbili tu, siku tano nilikuwa naoga kizulu narowesha kitaulo kwenye maji moto na kujifuta ukishavaa nguo unapiga pafyumu yako imeisha hiyo.

Kwa kifupi Mafinga na Njombe ni kama National na Panasonic hata Makambako ni walewale tu hakuna Pub za nje ni Pub za ndani.
 
Makambako baridi kavu emu nenda uje ufungue uzi
MAkambako baridi la kawaida Sana ngoja tukuelekeze tunao jua maeneo ambayo ni hatari kwa baridi 1 makete kitulo 2 mbeya isyonje 3 njombe town 4 mafinga haya maeneo ni hatari ukipita lazima mwili usisimuke ikifika Saa Tisa inashuka kama mvua na huwa inachoma hadi parachichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…