Hali halisi ilivyo Ajira portal: Hii ndiyo serikali ya CCM inayojinasibu kumwaga ajira kwa maelfu ya wahitimu

Hali halisi ilivyo Ajira portal: Hii ndiyo serikali ya CCM inayojinasibu kumwaga ajira kwa maelfu ya wahitimu

Hapo

Tatizo tunapenda kulalamika bila kuleta suluhisho.
Hapo kosa la serikali ni lipi?
Waajiri wakati hawana nafasi kwasababu tu wewe umesoma?
Waajiri wakati hawajaandaa cha kukulipa?
Na wewe kizibo vilevile huna akili
 
Kazi iendelee broo na dada zangu trust me jiajirin hii serikal haina mpango na nyie anza na kidogo hicho hicho trust me....
Bora wewe umesema neno Serikali haina mpango na Vijana wasio na kadi ya chama cha Vegetables
 
Naishauri hivi serikali;
Iongeze kima cha chini cha mshahara mpaka milioni 1
Umri wa kustaafu kwa hiari upunguzwe mpaka miaka 45 na wa lazima uwe 50
 
Naishauri hivi serikali;
Iongeze kima cha chini cha mshahara mpaka milioni 1
Umri wa kustaafu kwa hiari upunguzwe mpaka miaka 45 na wa lazima uwe 50
chrome_screenshot_3 Feb 2025 02_28_22 GMT+03_00.png
 
Kwa kipindi cha kuanzia July 2023 hadi December 2024 serikali imetoa ajira nyingi sana, Tatizo lililopo wahitimu ni wengi sana na sio rahisi serikali iwaajiri wote.
 
Duniani kote serikali siyo mwajiri mkuu. Kazi ya serikali inayojitambua ni kuwapa vijana elimu nzuri inayowawezesha kujiajiri pamoja na kuandaa mazingira mazuri katika sekta binafsi ili vijana wake waweze kuajiriwa huko. Serikali inayoshindwa kuwapa vijana wake elimu bora (ikiwemo ya vitendo) na kuimarisha sekta binafsi ambayo ndiye mwajiri mkuu basi serikali hiyo inastahili lawama kwa kuwatelekeza vijana wake.
Upo sahihi
 
Kwa kipindi cha kuanzia July 2023 hadi December 2024 serikali imetoa ajira nyingi sana, Tatizo lililopo wahitimu ni wengi sana na sio rahisi serikali iwaajiri wote.
Ajira nyingi with respect to what? Unasema umetoa ajira 11,000 wakati mahitaji halisi ni 400,000 ma unajisifia kwamba umetoa ajira nyingi?
 
Hakuna la maana zaidi ya utapeli tapeli tupu, sahivi kuna interview ya walimu zaidi ya siku 40 itafanyika ni namna ya kupiga pesa, kumbe zoezi lingeweza kufanyika hata ndani ya siku 2 au 3
Huna hoja ww unajua interview wanafanya wangapi? Nyie tu uchaguzi wa baraza la vjana mlikesha nao siku 3 ndo uwe na audacity ya kudisi interview!!! Tafuta hoja ww ulichoandika hapo ni trash
 
Ni dhahiri shairi kuna tatizo la ajira kwa vijana kwa bara zima na ni tatizo sugu na linalofedhehesha na kuumiza haswa vijana na wazazi wenyewe kiujumla. Nipo hapa kuwakumbusha fursa zilizotolewa na serikali kwa vijana kwenda kusoma VETA bure ambapo dirisha limefunguliwa tarehe 30jan had 12feb fika kweny chuo cha veta upate form au tembelea tovuti ya wizara ya kazi na ajira kwa maelezo zaidi. Huko kuna koz mbalimbali kama umeme wa magar, umeme wa viwandan na majumban na nyinginezo nyingi.
 
Mkuu nimekimbilia hiyo ya security hata yenyewe haipo tena 😭😭
 
Katika maelfu na maelfu ya wahitimu walipo mitaani, Serikali haina nafasi hata moja ya kumuajiri mhitimu wa Accounting?

Pamoja na wingi wa wahitimu hususan vijana, serikali imeamua kuwafungia vioo vijana Gen Z! ina maana Serikali nzima, pamoja na thinktank zake imefeli kabisa kuokoa taifa la vijana waliosoma kwa taabu na kuishia kupoteza matumaini huku wengine wakijikita kwenye betting, michezo ya kubahatisha, kazi zisizo rasmi, nk.

Huku wakikata tamaa kabisa na kuamua kutupa vyeti vyao na ujuzi walio nao, huku serikali ikiwa imekosa kabisa namna ya kuwasaidia.

INASIKITISHA SANA!

View attachment 3221534
View attachment 3221544
Inasikitisha Kwa kweli
 
Mkuu endelea kubaki CHADEMA na wajinga wenzako
 
Back
Top Bottom