Hali halisi ilivyo Ajira portal: Hii ndiyo serikali ya CCM inayojinasibu kumwaga ajira kwa maelfu ya wahitimu

Hali halisi ilivyo Ajira portal: Hii ndiyo serikali ya CCM inayojinasibu kumwaga ajira kwa maelfu ya wahitimu

Duniani kote serikali siyo mwajiri mkuu. Kazi ya serikali inayojitambua ni kuwapa vijana elimu nzuri inayowawezesha kujiajiri pamoja na kuandaa mazingira mazuri katika sekta binafsi ili vijana wake waweze kuajiriwa huko. Serikali inayoshindwa kuwapa vijana wake elimu bora (ikiwemo ya vitendo) na kuimarisha sekta binafsi ambayo ndiye mwajiri mkuu basi serikali hiyo inastahili lawama kwa kuwatelekeza vijana wake.
Serikali ya mama imetekeleza hilo kwa weledi mkubwa kupitia taasisi yake maridhawa ya Chawa wa Mama😂,,,

huko ndiko zilikozaliwa wizara mbali mbali kama Masumbwi ya Mama, Marathon ya Mama, Goli la Mama n.k ni kuwa mbunifu tu, unaweza ukaja hata na "Kikoba cha Mama" ukapata support ya serikali.
 
Katika maelfu na maelfu ya wahitimu walipo mitaani, Serikali haina nafasi hata moja ya kumuajiri mhitimu wa Accounting?

Pamoja na wingi wa wahitimu hususan vijana, serikali imeamua kuwafungia vioo vijana Gen Z! ina maana Serikali nzima, pamoja na thinktank zake imefeli kabisa kuokoa taifa la vijana waliosoma kwa taabu na kuishia kupoteza matumaini huku wengine wakijikita kwenye betting, michezo ya kubahatisha, kazi zisizo rasmi, nk.

Huku wakikata tamaa kabisa na kuamua kutupa vyeti vyao na ujuzi walio nao, huku serikali ikiwa imekosa kabisa namna ya kuwasaidia.

INASIKITISHA SANA!

View attachment 3221534
View attachment 3221544
Nani aliyekwambia kijana akiishasoma LAZIMA aajiriwe na Serikali? Kama ni lazima, unatumia mfano wa nchi gani?
 
Serikali ya mama imetekeleza hilo kwa weledi mkubwa kupitia taasisi yake maridhawa ya Chawa wa Mama😂,,,

huko ndiko zilikozaliwa wizara mbali mbali kama Masumbwi ya Mama, Marathon ya Mama, Goli la Mama n.k ni kuwa mbunifu tu, unaweza ukaja hata na "Kikoba cha Mama" ukapata support ya serikali.
Haki ya nani nakuja na Sukuma Gang wa mama halafu nipige hela wakati huu wa uchaguzi.

Screenshot_20250202_222751_WhatsApp.jpg
IMG-20250131-WA0085.jpg
 
Back
Top Bottom