Hali ilivyo nchini Somalia

Hali ilivyo nchini Somalia

Mwezi March nilienda nchini Somalia kikazi chini ya shirika la umoja wa mataifa liitwalo Internation Organization for Migration.

Ili kufupisha maada.Nilichokishuhudia huko nchini somalia kilinishangaza sana nikilinganisha na hali ya nyumbani tanzania.Yaani somalia ukiondoa ile hofu ya alshabaab vitu vingine vyote ni rahisi kuliko nchini kwetu tanzania.

Mfano, niliuliza gunia la mchele la kilo 100 na bei ilikuwa hela za kitanzania 60000 kwa mjini mogadishu na miji ya pembezoni bei ilikuwa ya chini zaidi mafuta (petroli ilikuwa Tsh 2500), diesel ni tshiling 2000.na mafuta ya taa ni 1500.Bei hizi ni za kuanzia mwezi wa 8.2022.

Miundombinu kama barabara, hosipitali na umeme zinajengwa kwa kasi sana nchini somalia tofauti na tanzania ambapo ni mwendo wa konokono, pesa ya Somalia ina thamani kubwa dhidi ya pesa ya tz.

Watanzania wenzangu kwa nini tunazidiwa na somalia kimaendeleo? Yaani nchi inavita toka 1990 hadi leo lakini ina maendeleo zaidi kuliko tanzania.Sababu ni nini inayotufanya watz maisha yawe magumu kuliko somalia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Elimu bado inahitajika Nani anakwambia ufananishe Bei ya bidhaa za nchi ya watu kwa currency yako ??

Mfano Michelle sijui elf 60
Je wajua kupata pesa baada ya kubadili iwe elf 60tzs Kuna urahisi na ugumu kulingana na sehemu

US tzs 60k unaeza pata kwa masaa pungufu ya matano. Somalia sijui ila inaweza kuwa ngumu zaidi..tz ndo kabisa week kibarua ndo unaeza pata hio hela
 
Elimu bado inahitajika Nani anakwambia ufananishe Bei ya bidhaa za nchi ya watu kwa currency yako ??

Mfano Michelle sijui elf 60
Je wajua kupata pesa baada ya kubadili iwe elf 60tzs Kuna urahisi na ugumu kulingana na sehemu

US tzs 60k unaeza pata kwa masaa pungufu ya matano. Somalia sijui ila inaweza kuwa ngumu zaidi..tz ndo kabisa week kibarua ndo unaeza pata hio hela
Wewe ndiyo unahitaji elimu ili ujue kuwa somalia imeendelea kuliko tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuendelea ni majengo? Ni sawa na Kenya ..30% ya vijana Nairobi no robbers

Fool you
Somalia kila kitu rahisi.watoto wanatibiwa bure lakini tanzania kwa sasa ni pesa.wajawazito wanajifungua bure lakini tanzania ni pesa.tanzania tulichoizidi somalia ni kutokuwepo kwa alshabaab tu.Huduma zote zingine upatikanaji wake ni rahisi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasomali wana uthubutu na hilo hadi kwenye nchi za watu. Mfano mzee Kinana.
 
Kule lazima wanyooke maana hakuna kuleteana ubabe
Mkinyukana mwishowe mtaishi kwa adabu

Ova
 
Mimi ni Tomaso sijaamini chochote ulichoandika bila picha!!

Ungetuwekea picha za jiji la Mogadishu ukaweka na price tag za magunia ya vyakula sokon na petrol station ungepiga picha sehemu ya bei tuone tulinganishe otherwise itakuwa unatumia vibaya kishikwambi cha sensa wakati wenzako wako bize juu ya miti wanasaka network we uko JF.

FAO wametangaza Somalia wanakufa njaa mvua hamna kwa miaka 4 mfululizo inakuwaje bei ya vyakula iwe chini kuliko wanapoagiza? yaani hata mtoto wangu hapa humpati!

kwa uandishi huu usioweka mambo muhimu nafikiri wewe ni Kolo FC oya oya au?
 
Mwezi March nilienda nchini Somalia kikazi chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa liitwalo Internation Organization for Migration.

Ili kufupisha mada Nilichokishuhudia huko nchini Somalia kilinishangaza sana nikilinganisha na hali ya nyumbani Tanzania. Yaani Somalia ukiondoa ile hofu ya Al-Shabaab vitu vingine vyote ni rahisi kuliko nchini kwetu Tanzania.

Mfano, niliuliza gunia la mchele la kilo 100 na bei ilikuwa hela za kitanzania 60,000 kwa mjini mogadishu na miji ya pembezoni bei ilikuwa ya chini zaidi mafuta (petroli ilikuwa Tsh 2500), diesel ni tshiling 2000.na mafuta ya taa ni 1,500.Bei hizi ni za kuanzia mwezi wa 8.2022.

Miundombinu kama barabara, hosipitali na umeme zinajengwa kwa kasi sana nchini somalia tofauti na tanzania ambapo ni mwendo wa konokono, pesa ya Somalia ina thamani kubwa dhidi ya pesa ya Tanzania.

Watanzania wenzangu kwa nini tunazidiwa na Somalia kimaendeleo? Yaani nchi ina vita toka 1990 hadi leo lakini ina maendeleo zaidi kuliko Tanzania. Sababu ni nini inayotufanya Watanzania maisha yawe magumu kuliko Somalia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana wanatwambia twende Burundi huwezi kusikia wakisema Twende Somalia.
 
Back
Top Bottom