Hali ilivyokuwa katika Jiji la Dar wakati vijana CHADEMA wakimchukulia fomu Mbowe

Kwani mbowe kugombea tena anavunja kipengele gani cha katiba ya chama? Demokrasia ipo ktk sanduku la kura, usituyeyushe.
...ni kweli hajavunja katiba ya chama je wewe unaamini ndani ya chadema hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuwa mwenyekiti zaidi ya mbowe? Kama hayupo basi mbowe afai kuendelea kuwa mwenyekiti kwasababu kashindwa kuwaandaa vijana wengine kuongoza chama kwa miaka 15 akiwa na nia mbaya...kama wapo vijana wengine kwanini wasipewe nafasi waongoze? Chama ni taasisi kwanini chama kitegemee mtu mmoja?
 
Vijana wa Chadema wamemchangia Mwenyekiti wa chama chao mh Mbowe kiasi cha sh 5,600,000 ili zimsaidie kuchukua fomu na kufanya kampeni kwa ajili ya kutetea nafasi yake.

Vijana hao waliokusanyika mtaa wa Ufipa yalipo makao makuu ya Chadema wakiwa wamevalia sare za chama chao wamesema kwa sasa hakuna mtu yoyote aliyejitolea kwa hali na mali kuitumikia Chadema zaidi ya Mbowe.

Wamesema Mbowe ni mwamba anayeweza kuwavusha katika safari yao ya kuelekea Ikulu mwakani yaani 2020

Source TBC habari!
TBC hii ya magufuli? Basi mbowe atakua km sio pandikzi la ccm basi atakua amefika(amenunuliwa) km lipumba ili aiue chadema vipande2. Kwa tulipofika mbowe akae pembeni awe mshauri mkuu aachie damu changa ziendeshe cha kwa mashlahi ya taifa.
 
TBC ni luninga ya taifa bwashee!
 
TBC hii ya magufuli? Basi mbowe atakua km sio pandikzi la ccm basi atakua amefika(amenunuliwa) km lipumba ili aiue chadema vipande2. Kwa tulipofika mbowe akae pembeni awe mshauri mkuu aachie damu changa ziendeshe cha kwa mashlahi ya taifa.

Mbowe na jiwe nani damu changa?
 
Hakuna kijana hata mmoja aliyechanga pesa izi ni propaganda kuwazuia watu wenye ushawishi ndani ya chadema wakate tamaa kuchukua form.
 
Mbona katumia mbinu za kizamani? Hii ni sinema km zile sinema za bongo muvi za kina mlela na ebitoke....

Halaf ukiangalia hyo picha ati Chadema makao makuu miaka yote mnakaa kwenye banda la bata si bora mchange mjenge ofis ya kisasa ... kweli?
 
Mh.Mbowe kuchaguliwa tens kuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo atakuwa ameungana moja kwa moja na Mh.Rais JMP kuwa wanachokilhitaji Watanzania sio Demokrasia bali ni Maendeleo.
Maendeleo hayana vyama....
 
si muumini wa vyama..ila nadhan kuzidi mshikilia mbowe kama mwenyekiti ni kupoteza karata ya kulaumu Magufuri kuibaka demokrasia..najaribu fikiri tu nje ya box
Hhahhaha, kwa utawala huu ni bora Mbowe akaendelea kuwa mwenyekiti
 
TBC ndiyo mdudu gani?
Vijana wa Chadema wamemchangia Mwenyekiti wa chama chao mh Mbowe kiasi cha sh 5,600,000 ili zimsaidie kuchukua fomu na kufanya kampeni kwa ajili ya kutetea nafasi yake.

Vijana hao waliokusanyika mtaa wa Ufipa yalipo makao makuu ya Chadema wakiwa wamevalia sare za chama chao wamesema kwa sasa hakuna mtu yoyote aliyejitolea kwa hali na mali kuitumikia Chadema zaidi ya Mbowe.

Wamesema Mbowe ni mwamba anayeweza kuwavusha katika safari yao ya kuelekea Ikulu mwakani yaani 2020

Source TBC habari!
Screenshot_20191125-162412.jpeg
 
Back
Top Bottom