Jidanganye! Unaijua baraza la usalama la Marekani? Wajumbe ni wakuu wa vyombo vyote( CIA,NSA,JESHI,FBI NA WASHAURI WA USALAMA WA NJE NA NDANI) Hawa wakikaa ndo wanafanya maamzi ya hatima ya Marekani kivita au kwenye operation yoyote yenye risk scenario. Rais anakuwa pale kwenye kikao kujilizisha tu nakupokea ufafanuzi na kuuliza maswali na kuidhinisha... ! Mission ikifanikiwa atanufaika kisiasa mission iki fail wanajeshi wa Marekani wakapoteza maisha kwenye nchi ya kigeni huo mzigo anabebeshwa mabegani kwake for the rest of his life. NAMALIZIA KWA KUSEMA HALI YA SASA YA AFYA YA BIDEN HAIIZUII MAREKANI KUFANYA CHOCHOTE POPOTE
Acha ujinga na mawazo ya kizamani. Kwa zamani tulikuwa hatuwalaumu watu wenye akili kama yako, maana mitandao ya kijamii na teknolojia ya kuweza kukufanya mtu ufuatilie jambo na kuujua ukweli ilikuwa hamna.
Vilaza wengi walipata source kwa njia za movie za kina Rambo, Anord, Chuck Norris nk. Hivyo kuamini kuwa Marekani ni nchi ambayo inaweza kupata ushindi popote na kwenye nchi yoyote kama walivyoona katika movie za kina Rambo 😂😂😂
Lakini sasa dunia imeweza kujua mengi zaidi kupitia mitandao hii ya kijamii na kugundua kuwa yale waliyokuwa wanayawaza katika akili yao kuhusu Marekani kushinda vita popote hayakuwa kweli bali ni movie tu ndo ziliwadanganya.
Japo siujui umri wako lakini nina imani ukitafuta watu wenye uelewa mkubwa wa kujua mambo zaidi yako watakwambia vizuri ni nini kilichowapata Wamarekani kule Vietnam hadi kupelekea kulazimisha kila mfanyakazi, mwanafunzi na raia wa kawaida kujiunga na jeshi la nchi hiyo kwa lazima ili wapelekwe vitani Vietnam. Tukiachana na hiyo vita ya Vietnam, turudi hapa hapa jirani yetu Somalia. Marekani alipeleka jeshi lake, ndege zake za kivita, manoary, vifaru nk. Lakini walitwangwa sawa sawa mpaka wakakimbia na kuacha baadhi ya silaha zao ambazo ndio zilikuja kutumiwa baadae na alshabab. Hizo vita ninazokwambia hapo juu nahisi zilitokea ukiwa haujazaliwa hivyo kuelewa kwako kutakuwa kwa shida sasa.
Sasa ngoja nikupe mfano wa vita ambavyo pia Marekani kashindwa huku wewe ukiwa umeshazaliwa. Vita vyenyewe ni hivi vya Afghanistan.Nafikiri umeona jinsi Marekani tena akiwa na washirika wake Uingereza, Ufaransa, Ujeruman nk walivyoshindwa na kuamua kukimbia bila ya kufikia lengo lao. Hapo Syria mpaka leo wameshindwa kumn'goa Asad ambae walipanga kumtoa kipindi kile vita ilipoanza katika nchi yake.
Hizo nchi zote ninazokwambia kuwa zimemshinda Marekani kuanzia Vietnam, Somalia, Afghanistan na Syria ni za hovyo tu hazina Teknolojia, hazitengenezi silaha, hazina jeshi lenye nguvu wala chochote cha maana. Sasa ndo unafikiri Marekani ataweza kuthubutu kutia pua Iran kwenye nchi ambayo inateknolojia ya hali ya juu. Leo hii ukisikia Hezbulla kapiga kambi ujue ni teknolojia ya Iran ndo imeona ilipo kambi hiyo na kuwapa direction vijana ya wapi pa kupiga. Iran inaunda ndege ambazo hazionekani hata kwenye rada za Marekani na Israel, moja ni ile ya juzi iliyotumwa na vijana wa houth. Iliingia na kupiga na kuua. Sasa unaweza kujiuliza kwa ulinzi wa anga na ardhini wa Israel akishirikiana na Marekani yake, ndege ile iliweza kupitaje na kwenda kutekeleza mission yao iliyopangwa. Hapo bado sijakwambia zile ndege zisizo na ruban ambazo Iran alimpa mrusi na kubadilisha muundo wa vita kule Ukraine hadi nchi za Magharibi kuilaumu Iran na kuomba iwekewe vikwazo zaidi na UN kwa sababu ya kuipa Urusi ndege zenye maangamizi makubwa huko Ukraen. Kwahivyo hilo swala sijui la baraza la usalama kukaa na raisi Marekani wala lisikupe presha. Kila operation ya vita inapopangwa hilo baraza la usalama hukaa na raisi na bado hupoteza pambano kama nilivyokwambia katika hizo nchi hapo juu.
Marekani mwenyewe anafahamu kuwa kuingia kwenye vita na nchi kama Iran sio sawa na kuingia vitani na Somalia au Afghanistan. Iran ana kila kitu ambacho hizo nchi zilizomfanya Marekani ashindwe hazina.
Hao Iran sio waarab, wayahudi, wahindi, wachina wala wazungu. Hao ni waajemi ambao walishatawala sehemu kubwa ya dunia toka Yesu na Mtume Muhamadi hawajazaliwa, nenda kasome hata vitabu vya dini au google itakwambia. Jamaa wako vizuri kivita kabla hata dini hazijaundwa wala mitume hawajazaliwa alafu unakuja na habari za baraza la kina rambo kukutana 😂😂😂