Kazanazo
JF-Expert Member
- Aug 16, 2023
- 2,582
- 4,554
Ni siku nyingine tena, nawasalimu
Hapa simaanishi hali ya kiuchumi bali hali ya kimaadili mitaa imechafuka sana ila tunaowaita viongozi wapo kimya sijui maana ya uongozi ni nini?
Wanawake wanadhalilika sana wengine kwa kupenda wengine kwa kutokupenda. Wanawake ndio kioo cha maadili, hali ya kupuuza na kuacha wajiuze, watembee uchi kama bidhaa, watukanwe matusi ya nguoni kama wafanyavyo wasanii na watu wengine mtaani na udhalilishaji mwingine ni kukididimiza kizazi na jamii kwa ujumla
Uongozi ni kuonesha dira njema katika taifa katika nyanja zote kiuchumi na kijamii, kitendo cha viongozi kukalia kimya suala hili la udhalilishaji wa wanawake ni kukwepa uwajibikaji nashauri mamlaka ziangalie suala hili kwa undani na wachukue hatua stahiki
Wanawake ni mama zetu, dada zetu na ndugu zetu kumdhalilisha mwanamke yeyote ni sawa na kumdhalilisha mama yako au dada yako jamii ilitazame hili
Ahsanteni