Hali ni mbaya hii nchi kila kundi linateseka isipokuwa viongozi

Hali ni mbaya hii nchi kila kundi linateseka isipokuwa viongozi

Kila Kona tunaona mabango ya sifa na mapambio kwa mkuu "anaupiga mwingi anaupiga mwingi" lakini hali halisi ya mtaani ni tofauti sana kwa sasa upatikanaji wa pesa mtaani umekuwa ni mgumu mno gharama za maisha nazo zipo juu wananchi tunateswa sana hakuna kundi la watanzania lenye unafuu isipokuwa Viongozi wetu pekee ndio wanaofaidi keki ya taifa ata wewe mkuu ulikiri wazi kuwa wateule wako wanakula sana watanzania wengi wamebakia kubangaiza

Vijana na ukosefu wa ajira
Wastaafu na kikokotoo
Watumishi na udogo wa mishahara
Machinga na migambo
Wafanyabiashara na utitiri wa Kodi
Wakulima na ukosefu wa masoko
Siku tukijitambua hayo mateso yatakwisha, tunakazi ya uchawa tu Nchi inatafunwa na wachache.
 
Wewe chawa unajielewa kweli…

Kwani huwez kupita bila kuchafua uzi wa watu?

Wao wamachinga, watumishi wenye madaraja y chini, mama ntilie na waadhirika wengine wa kimfumo sio wapiga kazi?

Sikia acha kupoteza muda na kujitia pamba masikioni.

Ata ujumbe wa nyumba kumi hutopata
tuliza mihemko basi kamanda 🐒

mvivu ni mvivu tu kumjua ni rahisi sana....

hakuna upotoshaji utakatiza mbele ya mchapakazi hodari, makini, mnyonge nisiestahili na kiongozi wa wanainchi nikaacha kuukanusha na kuusahihisha kwa maslahi mapana ya wanaJF wasiyostahili kupotoshwa 🐒

kuhusu ujumbe wa nyumba 10 umenifurahisha sana dah 🤣

wakati nasoma chuo kikuu, eneo nilikokua nimepanga nilikua mjumbe wa shina bana, huwez pata barua ya serikali ya mtaa bila kwanza kupitia kwangu, dah aise ilikua raha sana 🤣
 
Na bado, huu Mwaka mpaka tuseme..

Kuna mambo wawili tuu hapa, uwe chawa labda unaweza ambulia chenga chega za keki y taifa.

Au kusimama kwenyekile unachokiamini kwan ni bora kuulinda utuwako dhidi y tamaa ya muda kuliko kujivua nguo kwa kusifia anguko la taifa lako
 
Back
Top Bottom