Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pole sana mkuu.
Ni swali tu ambalo nahitaji uelewa, hivi kwenye usaili hasa serikalini, swala la ulemavu ni kigezo au ni kipaumbele katika kupata ajira? Naomba kujuzwa.
Kwa sababu kwa hali iliyopo sasa sidhani kama issue ni walemavu vs wasiokuwa walemavu, unless otherwise uwe competent na bado ufanyiwe figisu kutokana na hali yako. Ninachofahamu Issue ya ajira ni janga la kitaifa.
I stand to be corrected.
Hizo ni mambo kutoka nje , tunapokopa ndiyo wanataka hivyo ...Kwa sasa hawa madogo wa TRA wajiangalie sana wanawake watachukuliwa kinoma .Afadhari hii mada umeweka hapa.
Hii nchi ina mambo ya Ajabu sijawahi ona, yaan mtu ana ajiriwa hadi kwa kuangaliwa Sexual Orientation yake, huu si upumbavu kabisa.
Kazi haiihitaji sexual affairs, inahusu mambo mengine kabisa, lakini hapo utaangalizwa hadi nani una date nae, km si ulofa n nn?
Li nchi ndo maana haliendelei, kutwaa ubaguzi wa kipumbavu usio na tija, una muacha mtu mwenye vigezo na sifa stahiki kwa kazi husika, kisa mapungufu yake, na una mchukua mwingine hata hajui lolote kisa ana ukamilifu fulani, jamani inaumiza hatariii.
Tupaze sauti, kuondoa sintofahamu hii.
Dah nmejisikia vibaya sana kwa kweli mungu awatangulie lakn unaposikia fursa kama bajaj za mikopo kwa walemavu please changamkia fursa siku ukipata ajira unaendelea na Career yako usikae tu kusubiria ajiraNiende kwenye mada moja kwa moja!!.
Nimekuwa moja ya wahanga wa hili Tatizo kwa muda mrefu sana
Kati ya watu wanaosoma kwa mateso makubwa sana ni watu wenye ulemavu, kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hii inatokana na miundo mbinu mingi kuwa tofauti na Hali zetu watu wenye ulemavu.
Wakati mtu mwenye ulemavu anapambna akiamini kuwa yeye hawez kulima, kutembeza mitumba, Wala kufanya kazi ngumu za ujenzi akitegemea akili yake tu ya darasani angalau impe mwanga wa maisha.
Baada ya ajira huyu mtu mwenye ulemavu anaanza kuzunguka na baiskeli yake au magongo yake kweny interview mbalimbali, wakati mwingine hufanyika mikoani, au kwenye majengo yasiyo na lift.
Wengi wanaishia kukata tamaa sana.
Kuna sehemu niliwahi kataliwa kabisa kisa mimi ni mlemavu kwamba siwezi kufanya hio kazi kwasababu nitakuwa naenda sana hospitali, yaani trip kazini trip hospitali. Wanahisi labda sisi ni wagonjwa fulani hivi,
Inaumiza sana sana, naongea kwa niaba Yao sana.
Wengi walioajiriwa ni sababu za kisiasa, ili ionekane hawabaguliwi hasa kwenye sekta zinazohusiana na walemavu ndio huko wamejazwa!
Nina watu nawajua ni walemavu, wanapitia kipindi kigumu sana lakini wakiwa na elimu Yao kichwani! Yaani huu unyanyapaa huwezi ona kwa jicho la kawaida! Ni dhamira za watu.
Kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!! We feel pain sana sana
Natimiza mwaka wa saba(7) tangu nimalize digrii yangu ya usimamizi wa fedha..
Serikali haitujali tena, zaidi ya kutulazimisha tukope pesa tuu.
Wadau wapo kimaslahi na kisiasa zaidi wapate attention wakati wanatoa misaada.
Hata vyama vya walemavu sasa hawana la kusema baada ya kulamba sukari
Sisi tukimbilie wapi zaidi yenu wadau wa hapa JF, tusaidieni kupaza sauti sisi walemavu tuliopambana kusoma kwa bidii, tunatamani kubeba tofali angalau tupate mkate wa kila siku lakini Hali zetu hazituruhusu.
Tuliamini katika elimu nayo imetusaliti, nchi imetutenga, tuna hari mbaya sana
Bajaji za mkopo kiukweli zinasaidia sana!! C wote ambao wanauwezo wa kuendesha bajaji, Kuna ndug wengi hawana uwezo wa kusikia, wengine wanauono hafifu.. ni serikali ukae chini iunde namna ya kuwa recruit tu wanapotoka vyuo vikuuDah nmejisikia vibaya sana kwa kweli mungu awatangulie lakn unaposikia fursa kama bajaj za mikopo kwa walemavu please changamkia fursa siku ukipata ajira unaendelea na Career yako usikae tu kusubiria ajira
Hicho ndiyo kiwango ulichofikia cha kutumia akili yako!Pole sana..
Lakini je hata ungekuwa wewe ,ungeweza kumuacha mtu ambaye si mlemavu ukaajiri mlemavu?
Asant kiongozi umenena vyema sana!! Lakn hoja yangu kuu. Ni Walemavu kupata fursa za ajira hapo ndo lilipo ombi langu!! Maisha baada ya kuwa amepata ajira nafikiri inategemea na mtu..Hapo kuna unafiki mkubwa sana ndugu yangu, mlemavu lazima apewe kipaumble kwa vile ni special group isipokuwa kutokana na ulemavu wake kuna kazi ni uwongo hawezi kufanya kabisa ...Kwa kazi za serikali 90% walemavu wanaweza kufanya inategemea na ulemavu gani ...Nawafahamu wakuu wa vitengo kama wawili ni walemavu , wako nondo balaa kichwani kuzuri hata matokeo yao ya chuo ni mazuri .
Kuwatenga walemavu ni unafiki kwa vile bado kuna 50/50(wanawake kupewa kipaumbele) , kuna asilimia ya raia wa zanzibar ..Vile vile nchi inapokea pesa kutoka kweny mashirika ya kimataifa ili kukuza usawa wa kijinsia na kusaidia walemavu .
Ukisoma mwongozo kwa taasisi za serikali walemavu wanakula bata kama wanaweza kufanya kazi , wana dis-abled allowance...Wana mda mzuri tu wa kwenda kuangalia ishu zao za afya .
Mtoa mada amasema kwamba wanaonekana watasumbua kwenye kuondoka kila mara kazini ili kufuatilia matibabu , hii ni uongo maana ninajua hata hao wasiokuwa walemavu wana excuses kila mara ni yale yale tu ..Hivi ushawahi kuona usumbufu wa mwanamke mwenye mimba ni kama kazini hayupo , bado akizaa atakaa pending kwa mda .
Jitahidini muwe chawa wa mama😆Niende kwenye mada moja kwa moja!!.
Nimekuwa moja ya wahanga wa hili Tatizo kwa muda mrefu sana
Kati ya watu wanaosoma kwa mateso makubwa sana ni watu wenye ulemavu, kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hii inatokana na miundo mbinu mingi kuwa tofauti na Hali zetu watu wenye ulemavu.
Wakati mtu mwenye ulemavu anapambna akiamini kuwa yeye hawez kulima, kutembeza mitumba, Wala kufanya kazi ngumu za ujenzi akitegemea akili yake tu ya darasani angalau impe mwanga wa maisha.
Baada ya ajira huyu mtu mwenye ulemavu anaanza kuzunguka na baiskeli yake au magongo yake kweny interview mbalimbali, wakati mwingine hufanyika mikoani, au kwenye majengo yasiyo na lift.
Wengi wanaishia kukata tamaa sana.
Kuna sehemu niliwahi kataliwa kabisa kisa mimi ni mlemavu kwamba siwezi kufanya hio kazi kwasababu nitakuwa naenda sana hospitali, yaani trip kazini trip hospitali. Wanahisi labda sisi ni wagonjwa fulani hivi,
Inaumiza sana sana, naongea kwa niaba Yao sana.
Wengi walioajiriwa ni sababu za kisiasa, ili ionekane hawabaguliwi hasa kwenye sekta zinazohusiana na walemavu ndio huko wamejazwa!
Nina watu nawajua ni walemavu, wanapitia kipindi kigumu sana lakini wakiwa na elimu Yao kichwani! Yaani huu unyanyapaa huwezi ona kwa jicho la kawaida! Ni dhamira za watu.
Kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!! We feel pain sana sana
Natimiza mwaka wa saba(7) tangu nimalize digrii yangu ya usimamizi wa fedha..
Serikali haitujali tena, zaidi ya kutulazimisha tukope pesa tuu.
Wadau wapo kimaslahi na kisiasa zaidi wapate attention wakati wanatoa misaada.
Hata vyama vya walemavu sasa hawana la kusema baada ya kulamba sukari
Sisi tukimbilie wapi zaidi yenu wadau wa hapa JF, tusaidieni kupaza sauti sisi walemavu tuliopambana kusoma kwa bidii, tunatamani kubeba tofali angalau tupate mkate wa kila siku lakini Hali zetu hazituruhusu.
Tuliamini katika elimu nayo imetusaliti, nchi imetutenga, tuna hari mbaya sana
Kama wamesha jiita vyura viziwi au kauli ya kula kwa urefu wako.Poleni sana sana
Lazima kelele zipigwe ziwafikie wahusika
Ni kweli kabisa mkuu, nashuhudia ki taasisi fulani madem wapo na ni empty set kinyama.Sasahiv ukienda kweny maofis mengi utakuta wadada wazuri wenye mashepu Yao ndo wamejaa!! Lakn wenye kigezo Cha ueledi wachache!! Mtanisamehe naongea nilichokishuhudia
Kama hawataliangalia na hili basi ni laana kwa TaifaKama wamesha jiita vyura viziwi au kauli ya kula kwa urefu wako.
Una dhani haya malalamiko wata yaona?, waki yaona wata yafanyia kazi??.
waki yafanyia kazi, je Kuna utekelezaji?
Mkuu uchawa nao ni kipaji kileeeJitahidini muwe chawa wa mama😆
Hali ni mbayaKama wamesha jiita vyura viziwi au kauli ya kula kwa urefu wako.
Una dhani haya malalamiko wata yaona?, waki yaona wata yafanyia kazi??.
waki yafanyia kazi, je Kuna utekelezaji?
Mkuu wengi Tulisoma sana kwasababu hatupendi kudharaulika! Lakn tunakutana na Changamoto nyingine ya kutafuta ajira, kwenda huku na huko! Kiukweli ni mateso...Ni kweli kabisa mkuu, nashuhudia ki taasisi fulani madem wapo na ni empty set kinyama.
wanacho jua ni kuvaa nguo za hovyo tu, Kisha kukutana migahawani.
Na kweny ajira hizi za serikali wengi huwa tuna indicate kabisa kwamba sisi ni Walemavu!! Lakin ndo inakuwa Kama huja indicate kituKama hawataliangalia na hili basi ni laana kwa Taifa
Tunaelewa bt kuna muda nako huwezi laumu sana. Hata miundombinu mingi ya ofisi zetu si rafiki kwa wenzetu.Pole sana Kwa hiyo changamoto Mkuu
Nafikiri watu wanaajiriwa Kwa kuzingatia weledi na tija ambayo unaweza kuongeza kwenye Taasisi husika.
Unaweza kuajiriwa ukiwa ni mlemavu wa ngozi/viungo ama chochote na ukawa na tija kwenye eneo husika.
Tuishi tukijua Kila mtu ni mlemavu mtarajiwa
Unaweza kuwa mzima sasa, lakini Bodaboda utakayopanda kesho ikakupa ulemavu keshokutwa
ungekuwa mlemavu, ambaye ulisumbuka kusoma kwa bidii, ili angalau ujikwamue;! Halafu mtu akupe sababu Kama hizoTunaelewa bt kuna muda nako huwezi laumu sana. Hata miundombinu mingi ya ofisi zetu si rafiki kwa wenzetu.
Hata katika ujenzi miundombinu ya wenzetu inaongeza gharama sana.
Jiulize tu hata nyumba zetu tunazojenga ni rafiki kwa wenye ulemavu?
Watu wamekuwa wabinafsi ila nafasi zenu kisheria zipo kabisa...Hii hata bungeni ilitakiwa kuwe na asilimia kwa watu special .Asant kiongozi umenena vyema sana!! Lakn hoja yangu kuu. Ni Walemavu kupata fursa za ajira hapo ndo lilipo ombi langu!! Maisha baada ya kuwa amepata ajira nafikiri inategemea na mtu..
Ombi langu serikali isikie kilio chetu, Kuna marafiki nawafaham Wana miaka mpka kumi wapo tu nyumban!!