DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hapo kuna unafiki mkubwa sana ndugu yangu, mlemavu lazima apewe kipaumble kwa vile ni special group isipokuwa kutokana na ulemavu wake kuna kazi ni uwongo hawezi kufanya kabisa ...Kwa kazi za serikali 90% walemavu wanaweza kufanya inategemea na ulemavu gani ...Nawafahamu wakuu wa vitengo kama wawili ni walemavu , wako nondo balaa kichwani kuzuri hata matokeo yao ya chuo ni mazuri .

Kuwatenga walemavu ni unafiki kwa vile bado kuna 50/50(wanawake kupewa kipaumbele) , kuna asilimia ya raia wa zanzibar ..Vile vile nchi inapokea pesa kutoka kweny mashirika ya kimataifa ili kukuza usawa wa kijinsia na kusaidia walemavu .

Ukisoma mwongozo kwa taasisi za serikali walemavu wanakula bata kama wanaweza kufanya kazi , wana dis-abled allowance...Wana mda mzuri tu wa kwenda kuangalia ishu zao za afya .

Mtoa mada amasema kwamba wanaonekana watasumbua kwenye kuondoka kila mara kazini ili kufuatilia matibabu , hii ni uongo maana ninajua hata hao wasiokuwa walemavu wana excuses kila mara ni yale yale tu ..Hivi ushawahi kuona usumbufu wa mwanamke mwenye mimba ni kama kazini hayupo , bado akizaa atakaa pending kwa mda .​
 
Hizo ni mambo kutoka nje , tunapokopa ndiyo wanataka hivyo ...Kwa sasa hawa madogo wa TRA wajiangalie sana wanawake watachukuliwa kinoma .
 
Dah nmejisikia vibaya sana kwa kweli mungu awatangulie lakn unaposikia fursa kama bajaj za mikopo kwa walemavu please changamkia fursa siku ukipata ajira unaendelea na Career yako usikae tu kusubiria ajira
 
Mtu am-tag mama Doroth anaweza akalifikisha hili mbali.
 
Dah nmejisikia vibaya sana kwa kweli mungu awatangulie lakn unaposikia fursa kama bajaj za mikopo kwa walemavu please changamkia fursa siku ukipata ajira unaendelea na Career yako usikae tu kusubiria ajira
Bajaji za mkopo kiukweli zinasaidia sana!! C wote ambao wanauwezo wa kuendesha bajaji, Kuna ndug wengi hawana uwezo wa kusikia, wengine wanauono hafifu.. ni serikali ukae chini iunde namna ya kuwa recruit tu wanapotoka vyuo vikuu
 
Asant kiongozi umenena vyema sana!! Lakn hoja yangu kuu. Ni Walemavu kupata fursa za ajira hapo ndo lilipo ombi langu!! Maisha baada ya kuwa amepata ajira nafikiri inategemea na mtu..

Ombi langu serikali isikie kilio chetu, Kuna marafiki nawafaham Wana miaka mpka kumi wapo tu nyumban!!
 
Jitahidini muwe chawa wa mama😆
 
Sasahiv ukienda kweny maofis mengi utakuta wadada wazuri wenye mashepu Yao ndo wamejaa!! Lakn wenye kigezo Cha ueledi wachache!! Mtanisamehe naongea nilichokishuhudia
Ni kweli kabisa mkuu, nashuhudia ki taasisi fulani madem wapo na ni empty set kinyama.

wanacho jua ni kuvaa nguo za hovyo tu, Kisha kukutana migahawani.
 
Walimwengu hawana huruma wakishashiba wao inatosha hawaangalii wengine
 
Ni kweli kabisa mkuu, nashuhudia ki taasisi fulani madem wapo na ni empty set kinyama.

wanacho jua ni kuvaa nguo za hovyo tu, Kisha kukutana migahawani.
Mkuu wengi Tulisoma sana kwasababu hatupendi kudharaulika! Lakn tunakutana na Changamoto nyingine ya kutafuta ajira, kwenda huku na huko! Kiukweli ni mateso...
 
Tunaelewa bt kuna muda nako huwezi laumu sana. Hata miundombinu mingi ya ofisi zetu si rafiki kwa wenzetu.

Hata katika ujenzi miundombinu ya wenzetu inaongeza gharama sana.

Jiulize tu hata nyumba zetu tunazojenga ni rafiki kwa wenye ulemavu?
 
Tunaelewa bt kuna muda nako huwezi laumu sana. Hata miundombinu mingi ya ofisi zetu si rafiki kwa wenzetu.

Hata katika ujenzi miundombinu ya wenzetu inaongeza gharama sana.

Jiulize tu hata nyumba zetu tunazojenga ni rafiki kwa wenye ulemavu?
ungekuwa mlemavu, ambaye ulisumbuka kusoma kwa bidii, ili angalau ujikwamue;! Halafu mtu akupe sababu Kama hizo

Kwamba hata kuajiri kwasababu hajajenga barabara kwa ajili yako!! Inauma

Sijui Kama unaujua uchungu wa kushinda njaa Hali ukiwa na vyeti kabatin
 
Watu wamekuwa wabinafsi ila nafasi zenu kisheria zipo kabisa...Hii hata bungeni ilitakiwa kuwe na asilimia kwa watu special .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…