Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

Hali ninayokutana nayo katika Biashara inatisha nimefunga biashara 3 nimebakiza moja inayopumulia mipira, Msaada wa kiroho unahitajika

Kuota uko shule unafanya mtihani mara nyingi hii ndoto inahusiana na stress na msongo wa mawazo. Unawaza sana kuhusu kufirisika . Unaweza maliza waganga na usipate suluhu. Unatakiwa kujipanga upya
 
Njoo pM nikutumie namba za waganga wawili nawakubali sana.

Mmoja namuita Digala mwingine namuita masta mtoto.

Tanga
PM umeipiga LOCK tutakujaje sasa mkuu?

mimi Juzi hapa nilipigwa nyungu ya mawe ilikuwa kidogo nikimbie uchi😂😂😂

yani huo mtungi ulichemka kabisa halafu nikafukizwa, jiwe la moto likadumbukizwa humo aisee ilikua bahati tu kuendelea kuwemo kwenye hio shuka😅😅😅😅
IMG_20240907_120739_462.jpg
 
PM umeipiga LOCK tutakujaje sasa mkuu?

mimi Juzi hapa nilipigwa nyungu ya mawe ilikuwa kidogo nikimbie uchi😂😂😂

yani huo mtungi ulichemka kabisa halafu nikafukizwa, jiwe la moto likadumbukizwa humo aisee ilikua bahati tu kuendelea kuwemo kwenye hio shuka😅😅😅😅View attachment 3092991
Ulikuwa unasumbuliwa na malazi ya Kichwa.
 
Habari Wakuu, Maelezo mengi yatawachosha.

Nilianza Biashara 2019, ya umachinga nikawa nachukua bidhaa mjini napeleka vijijini, Biashara ilikubali nilikuwa napiga profit nzuri sana kwa siku, Biashara yangu haikuwa na ushindani wala haikuwa ya kufikilisha kama kuna faida napata, Ila nilikuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya Laki moja hadi 3 kwa siku,

Nikaendelea na Biashara hii kwa mda wa Mwaka mmoja nikaamua kununua kiwanja na kujenga nyumba yangu wa kwanza ya kuanzia maisha, nikahamia, Nikaendelea kukomaa nikajenga nyumba ya pili ya ndoto zangu...

Kwa bahati nzuri location niliyojenga kwa mbele kuna barabara nikaona sio mbaya nikajiongeze nikajenga Viflemu vya biashara nikapata na wapangaji nikaanza kupokea vikodi. Kiukweli nilianza kuona natimiza ndoto kimasihara sana.

Mwaka juzi nikapambana nikapata kigari nikanunua,, na baadae nikawaza biashara ya Umachinga sio Biashara ya kudumu, Hivyo nikaona nijiwekeze nikaona ni bora nifungue vitega uchumi vingine ili nitanue biashara..

Nikaamua kufungua Duka la kwanza katika moja ya flem zangu, Mwanzoni biashara ilienda vzuri hadi nikawa najiuliza nilikuwa nachelewa nini.

Baadae nikaona shemej yenu nae anafaa apate biashara yake ili asinitegemee na Yy nikatafta location nikamfungulia Cafe ya kuuza misosi napo biashara ikatiki nikaongeza kipato zaid nikazidi kuinjoy..

Nikaona niongeze ofisi ya tatu, Nikafungua Duka la spea za pikipiki eneo baada ya kuona location inafaa, Biashara zikazidi kupamba moto.

Cha ajabu na cha kushangaza ni ndani ya Mda mfupi biashara zote zimesimama hakuna mteja anakuja dukani kwangu watu wanapita tu na kwenda kununua bidhaa kwingine, cha kusikitisha ni kwamba upepo umenata ofisi zote, Pale kwa wife vyakula vinapikwa vinatupwa, Dukani panya wanashambulia vitu bila huruma, na hakuna mteja, Duka la spea hakuna wateja na mafundi wamehama sina fundi wala bidhaa haziuziki.

Nimeamua kufunga biashara zote maaa naona ni hasara tupu, Kwanza nilianza na Mgahawa wa wife, likafuata Duka na hivi juzi nimemalizia kufunga Duka la spea

Nimeamua kurudia biashara yangu ya awali ya Umachinga ambayo ndio ilinipa msingi.. cha ajabu nayo saizi wateja wangu wanataka kunikopa tu hamna la maana. Natoka nazunguka narudi nyumbani na pesa ya kula tu hamna cha maana.

Cha ajabu hata usiku nikilala naota ndoto za kutisha kama nipo kwetu kijijini, tena saa zingine naota nipo shule ya msingi nasoma na mara zingine naota nimepakazwa kinyesi mwili mzima. Jaman wakuu tusaidiane hapa najinasua vipi.

Kwa upande wangu napendelea kujinasua katika hiki kifungo kupitia wataalam wa jadi ndipo imani yangu inanituma japo sijui ni wapi nitaanzia wala ni wapi nitaishia,
siwiwi na walokole kuponya tatzo langu, kama yupo ambae alishawahi kukutwa na janga kama hili na akachomoka na kurudi katika hali yake ya kawaida anisaidie Pm Iko wazi jamani. Ndugu tusaidianane, Napitia fedheha kubwa sana, Nimejaribu kushirikisha akili yangu ila imefika ukomo,

Napewa namba za wataalamu wengi ila ukimpigia katika maongezi pyschologically nawastukia ni wapigaji wengi wao wanajisifia ila ukipima maongezi yake unaona kama hayana uhalisia.. Na mwisho wanataka kutumiwa pesa ili wanisaidie.
Ndoto zako zinashaaria umevikwa roho YA aibu,nuksi,mikosi Na fedheha,gundu Nyota imeibiwa Kibali kimeibiwa ,pia roho YA kukurudisha nyuma kimaendeleo usipochukua hatua utakuja kuuza Gari mpaka nyumba ufilisike kabisa ndo lengo la maadui zako.......ushaurii Wangu Archana Na mambo ya jadiii hayo ndo yatazidi kukumaliza mwishowe uchanganyikiwe.....unasema hutaki uende Kwa walokole akili yako inakutuma uende Kwa watu Wa jadii,hizo Sio akili zako zinakuambia Bali Ni izo roho zilizoko ndani yako zinakukataza usiende Kwa walokole sababu zinajua ukienda Kwa walokole zitaangamia mambo yako yatafufuka upya
 
Yani izo ndoto za kurudi kijijini na mashuleni zote zinaashiria umetupiwa roho ya kurudishwa nyuma ndo mana hamna jambo linaloenda mbele
Na kutoka kwenye Ivo vifungo ni kupitia maombi coz uko kwa waganga unaenda kupotea mazima.
Kuna Uzi umu ndani umezungumzia vizuri maswala ya kiroho ukiufatilia itakusaidia sana.
Surely ndomana hapigi hatua Bali anarudi nyuma kiuchumi
 
Sijawahi kuishi kwa mashart mkuu, lakini kwa hii fedheha ninayopitia saiz hata kama kuna masharti nitakuwa tayari kuyapokea kwa mikono miwili, usiombe uone unafirisika mkuu hiko kiskie kwa jirani yako ila kisiwe kwako. Unaweza kuwa unaongea peke yako njian
Biashara zilivokua zinapamba moto ulikua unatumia jadi au
 
Fata huu ushauri uliopewa nenda kwenye maombi kama upo dar nenda kkkt kimara korogwe au kkkt Kariakoo uponyaji bure dakika mbili tu umeoshwa kwa damu y’a Mwanakondo ( Yesu) stori kwisha nyota hiyo inarudi hayo mavi umechafuliwa ulimwengu wa roho wateja wanakuona unanuka hakuna atakaye sogea ndoto shule maana umerudishwa nyuma kijiji huo uchawi unatoka uko kwenu usipo angalia utarudi kijijini upo mjini kopo tu vitu vinaaanza roho then mwilini kwa waganga utapoteza ufalme kwa ufalme haufitiniki cha msingi atakuwekea jini lakutuliza kingine kuwa msiri asa kwenye maendeleo Bila nguvu y’a Mungu utoboi tumepita uko kwenye hizo ndoto za shule kuona unajisaidia choo kichafu ila niliposurrender mikono juu kwa Yesu kristo damu yake iliniosha nikawa mpya natembea kifua mbele atakayeroga kwa vida mu vya kuku sijui ng’Ombe anakutana na nguvu y’a damu
Hi ndoto YA kujisaidia Choo kichafu Hua inamaanisha nn
 
Wewe hujalogwa wala nini. Tatizo lako ni kama la watanzania wengine la kushangilia ushindi kabla mechi hajaisha. Mwaka 2019 hadi leo ni miaka 5. Kosa lako ni kufanya mambo mengi bila kuacha biashara iwe imara kwanza. Kujenga nyumba kadhaa, frems na kununua gari kisha kugawanyisha mtaji na kufungua biashara tatu ni kosa baya. Mbaya zaidi ukaiacha biashara iliyokuletea mafanikio. Wewe umejivuruga mwenyewe. ACHA KUKURUPUKA PIA PUNGUZA TAMAA. Tatizo lako halihitaji mganga wala mchungaji. Tuliza akili anza upya.
 
Tatizo hauna appreciation, huwezi sema nikajenga vifremu, nikapokea vikodi,

Je, unataka Mungu akupe wakati wewe huwezi kupokea?

Ngoja wapewe wengine watakaomshukuru Mungu.

Omba toba, toa sadaka, Mungu atakukumbuka tena.
 
PM umeipiga LOCK tutakujaje sasa mkuu?

mimi Juzi hapa nilipigwa nyungu ya mawe ilikuwa kidogo nikimbie uchi😂😂😂

yani huo mtungi ulichemka kabisa halafu nikafukizwa, jiwe la moto likadumbukizwa humo aisee ilikua bahati tu kuendelea kuwemo kwenye hio shuka😅😅😅😅View attachment 3092991
Ilikuwa wapi hii kiongozi 😄🔥
 
Back
Top Bottom