Hali si shwari Bodi ya Mikopo (HESLB)

Hongera sana

ubarikiwe pia kuwapigania wengine, kifupi hali ni mbaya sana bila tamko lolote vijana wengi watakosa fursa ya kusoma mwaka huu
 
Noted mkuu, mamlaka zipo humu ni imani yangu watafanyia kazi
 
ukipita kwenye kurasa za kijamii za bodi ,comments za vijana zinaonesha wamekata tamaa kabisa na hii bodi ya mikopo.

RAIS, TISS, TAKUKURU Imulikeni bodi
 
Pole kwao!

Nadhani muda umefika sasa vijana wakimbilie vyuo vya kati ili wapate skills na kujiajiri!

Nadhani pia serikali imesaidia kupatikana kwa mikopo kwa diploma ambapo ada zao ni nafuu kuliko shahada,waliopata asilimia chache za mkopo wakasome diploma yenye tija kuliko kung'ang'ania shahada ambayo ni ngumu kupata ajira huko mbeleni!!
 
Sasa wanaleta message hii: Applicant's profile is not seen.

Ina maana gani hii, watu wa ajabu sana
 
Noted champ,wapo humu watalifanyia kazi
 
Tunapowaambia hiyo Bodi ya Mikopo ni 🚮 muwe mnatuelewa. Hiyo Bodi inaendeshwa kihuni sana. Na nfiyo maana sishangai kuona mnufaika aliyemaliza mkopo wake mwaka 2017, akianza kukatwa makato upya na kwa sababu zisizoeleweka.

NB: kwa wale wazazi/walezi wenye uwezo, ni bora kuwalipia watoto wao ada, ili tu kuwaepusha na dhuluma kutoka kwenye hii Bodi inayoendeshwa kienyeji.
 
Chief hali ni mbaya sana kwa vijana, mchakato umegubikwa na kukosa uwazi kabisa

bila tamko la mamlaka za umma ,wengi watashindwa kusoma mwaka huu
 
Pesa iliyotolewa na serikali ifanyiwe stiff monitoring je imetumika ipasavyo?

sipa za wachache waliopata ada imekua kichekesho kabisa.kundi kubwa halijapata mkopo !!

Hii nchi ni yetu sote, wapeni mikopo vijana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…