Hali si shwari Bodi ya Mikopo (HESLB)

Hali si shwari Bodi ya Mikopo (HESLB)

Ndugu wa kiafrika hawachang kama hawana uhakika wa kula pesa waliyochanga ama umekufa
🥹Balaa yaani mtoto ishu ya kusoma haswa mjini angalau vijijini wana moyo japo hawana pesa ...Kuna vijiji mtoto akienda kusoma basi atapewa chochote kile kila nyumba .
 
mimi nakumbuka media zilitufuata kutuhoji pale ofisi za bodi mwenge mpakani. kina Abdul nondo wakaja wakapaza sauti sana later on president magufuli akasema hela yake aliyo itenga kwa wanafunzi haijaisha aiseeh bodi ya mikopo wakatoa batch fasta tena yenye hela nyingi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] watapata wawe wapoleee.
 
Wakuu poleni na mapambano. sitaki niwapotezee wakati niende moja kwa moja kwenye mada.

Kilio changu ni upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2023/2024 kumegubikwa na utata mkubwa kutokana na sababu zifuatazo

1.Account za waliokosa hazina notifications zozote kuwa kakosa mkopo awamu hii ama nyingine. ili upate taarifa lazima uje mitandaoni washkaji waweke screenshot ndio utajua kuna wale ambao wako allocated

2. Kilio cha ufinyu wa ada , wanufaika waliopangiwa kinasikitisha sana imagine ada ya programe ni 1.5 M lakini bodi wanatoa ada 200k kwelii!

3. Hawatoi list ya majina ya watu waliopata kiasi kwamba hili zoezi linaendeshwa pasipo uwazi wowote wakuu. tofauti na mwanzo miaka ya 2015s walikua wanatoa list na ku updates kwenye account

4. Status kwenye account ya mnufaika imekua ikibadilika mara kwa mara mfano unaweza pata status ya "congratulations your application is verified complete wait for allocation process" later on wanakuambia application is not complete rekebisha sehemu fulani !!

Note: Ndugu zangu mimi ni miongoni mwa wale ambao walipata mkopo kwa mbinde sana ,Kama sio MUNGU kumtumia Abdul Nondo sidhani kama ningetoboa kwani Rais magufuli alitoka hadharani nakusema pesa yake aliyotenga kwa ajili ya wanafunzi haijaisha aiseeh wakaja kutoa Batch nyingine tukapata mikopo asilimia 100 wotee,MAMA SAMIA WASAIDIE HAWA VIJANA WAPATE HAKI YAO, TUNAIMANI NAWEWE
Lucas mwashambwa uje pande hii utuambie kulikoni unatudanganga kuhusu mafanikio ya Hangaya......
 
Tulionufaika na mikopo mwisho ni 2019-2020. Baada ya hapo wanufaika wakaaanza kupigwa mchinjo, yaani hela kiduchu kuliko uhitqji. Sasa unajikazq hivohivo miaka 3 unamaliza kwa shida unakuja tena kusota mtaani.
 
Tulionufaika na mikopo mwisho ni 2019-2020. Baada ya hapo wanufaika wakaaanza kupigwa mchinjo, yaani hela kiduchu kuliko uhitqji. Sasa unajikazq hivohivo miaka 3 unamaliza kwa shida unakuja tena kusota mtaani.
so sad man ,vijana hawana nuru tena tuwasemee vijana nao wapate fursa ya kusoma
 
Back
Top Bottom