Chadema sasa inapita ktk mazingira magumu kisiasa kuliko kawaida, taarifa kutoka ndani ya chama icho inaeleza kuwa chama icho iko ktk mgawanyiko kutokana na aina ya siasa wanazofanya. Ukitazama chama hicho kwa jicho la nje unaweza kudhani kuko shwari lkn kihulisia chadema ina ombwe la uongozi sasa. Ombwe ilo linatokana na cdm kukosa msemaji halali wa chama na msuguano wa chini kwa chini ndani ya uongozi na nje ya uongozi.
Kawaida taasisi yoyote lazima kuwa na msemaji mkuu wa chama anayeongea kwa niaba ya taasisi lkn kwa chadema jambo sasa halipo kila kundi linamekuwa na msemaji wake, mfano mh Edward Lowassa akitoa tamko linakuwa na chama, mh Freeman Mbowe akitoa tamko linakuwa tamko la chama, Dr Vicent akitoa tamko linakuwa la chama, Mh Tundu Lissu akitoa tamko linakuwa la chama, Mh Godbles Lema akitoa tamko linakuwa la chama na Tumaini Makene wkt mwingine unajiuliza hiki chama hakina utaratibu kila mtu msemaji hakuna tofauti kati ya wasemaji rasmi wa chama na matamko binafsi ya viongozi.
Kutokana na hili ilibidi nipitie watu wangu ndani Ufipa na Alpha kujua kulikoni ndipo nilipopewa taarifa kuwa ndani ya chama hicho sasa kila kundi linapambana na kundi lingine kujiuza kwa wanachama na wananchi ili 2020 kila kundi ijijengee umaarufu. Chama hicho sasa ina makundi mawili makubwa Cdm Mafisadi inayoungwa mkono na Lowassa na wahamiaji wake, Mbowe, Mashinji na Salum Mwalimu na kundi lingine ambalo sasa limepewa jina la siri kuwa Cdm watukutu linaongozwa na Tundu Lissu, Peter Msigwa, John Mnyika, Fredrick Sumaye na wafuasi wengi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Cdm Dr Silaa.
Tutaendelea next