Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

One spark is capable of starting an uncontrollable fire!
 
Wouldn’t that question apply to you also, and all other contributors who are separatist.
Mi sijifichi, nataka uvunjwe na tutauvunja!

Yamevunjika madola yaliyotawala dunia, sembuse ki Muungano cha ku forge na kuficha makaratasi.

Kuna mambo hapa Tanzania ni settled matters. Hayajawahi kuwa mjadala. Hata mateja Mirembe hawasemi tuwahamishe Wakristo waende Zambia, nchi ya Kikristo, au Waislamu waende Libya kwa Waislamu wenzao. Wamakonde hawatarudishwa Msumbiji. Haya yasiyo na mjadala yanaitwa settled matters.

Muungano IS NOT a settled matter. Lolote linaweza kutokea. Bado tunabishana, wote hatuutakia isipokuwa Wazenji wenye vyeo Bara na Wabara wanaodhani Nyerere alikuwa Yohana Mtakatifu na Karume ni swahiba wa Mtume.

Zanzibar haina manufaa kwa Tanganyika, ni mzigo. Tunataka tuuvunje Muungano!
 
Kama hamtaki Muungano jifanyeni mnajikuna muondoke huku bara kuelekea kwenu Zanzibar. Ili muanze moja kuja kama wawekezaji.
 
One spark is capable of starting an uncontrollable fire!

..ndio nimekwambia hiyo mioto unayoiogopa ilianzishwa na vyama tawala / dola vilivyofilisika.

..Ccm ina kila dalili za chama tawala kilichofilisika, na kimefanya mauaji ktk nyakati mbalimbali, hivyo, kinao uwezo wa kufanya jambo baya zaidi hapa nchini.
 
Kama watawala/dola pekee ndio wangekuwa na uwezo wa kusababisha lawlessness, basi hii dunia isingekuwa inahangaika na terrorism kila uchao!
 
Kama watawala/dola pekee ndio wangekuwa na uwezo wa kusababisha lawlessness, basi hii dunia isingekuwa inahangaika na terrorism kila uchao!

..hata hao terrorist huwa ni watu wanaopambana na watawala wakatili, wakandamizaji.

..Ni kweli magaidi ni watu wabaya, na njia wanazotumia hazikubaliki.

..Lakini mara nyingi huwa wana magomvi na watawala wahuni na makatili.
 
Hoja hii wengi hawaielewi na ahsante kuieleza tena

Hakuna anayemshambulia Othman Masoud Othman(OMO) kwa kuzungumzia muungano
Hakuna anayemtuhumu kwa kutoa hoja zake kama kiongozi wa ACT au mtu binafsi

Tunahoji hoja zake anazojenga juu ya uongo, uzushi na unafiki!

Nitaweka clip mbili akizungumzia BoT halafu wasomaji mtaelewa kwanini OMO ni mnafiki au hajui anaongea nini
 
Katika clip hapa juu msikilize OMO akisema haya kuhusu East Africa Currency Board na BoT

Dakika 9.44
OMO
anasema '' Zanzibar ilikuwa mwanachama wa East Afrika Currency Board na Baada ya muungano share zake katika BoT ilikuwa 11%. Kulikuwa na mgogoro hadi mwaka 1996 ambapo WB ilikuja kusuluhisha na kuamua kuwa Zanzibar ipewe 4.5% hadi suala litakapomalizwa na kuanzia hapo halijashughulikiwa tena''

Hoja:
East African Currency board iliamuliwa kuvunjwa mwaka 1965 na kusimamisha shughuli mwaka 1966
Hoja ya kwamba baada ya ''muungano'' share za Zanzibar ziliingizwa BoT ni uzushi na uongo, mwaka 1964 BoT haikuwepo

Sasa msikilize OMO yule yule hapa chini

Dakika 45.56
OMO anasema '' Baada ya East Currency Board luvunjwa Karume alikataa shea za Zanzibar zisiingizwa BoT bali ilundwa People Bank of Zanzibar (PBC), kwamba, Jumbe , Abdul Wakili hadi Salimini waliona tatizo. Katika kipindi chote Zanzibar haijawahi kutumia Bank Kuu.''

Hoja :
Clip ya kwanza OMO anasema kwamba baada ya muungano 1964 Pesa za Zanzibar ziliingizwa BoT.
Muungano ulikuwa 1964 , BoT ilianzishwa 1966 lakini pia anaaminisha umma kuwa shea zilihamishwa mara moja.

Clip ya pili anasema Karume (aliyekuwa mwasisi wa muungano) hakuhamisha shea bali alitengeneza PBZ hadi wakati wa Salimini na kwamba Zanzibar haikuwahi kutumia BoT

Hivi tushike lipi kati ya clip hizo mbili? Inakuwaje mtu mmoja ana position mbili tofauti katika suala moja?
Huu kama si uongo na uzushi ni kitu gani!

JokaKuu
 
..hata hao terrorist huwa ni watu wanaopambana na watawala wakatili, wakandamizaji.

..Ni kweli magaidi ni watu wabaya, na njia wanazotumia hazikubaliki.

..Lakini mara nyingi huwa wana magomvi na watawala wahuni na makatili.

Wewe unadhani terrorists wanahamasishwa na ndimi zinazotumika vizuri?
 
Mali gani za Zanzibar zimewahi kuporwa na Watanganyika? Huyo Bakhressa unayemtolea mfano kuwa ni Mzanzibari, angelowea bara kama Watanganyika wangekuwa waporaji?

Naongelea uchumi wa Zanzibar siyo mali za watu binafsi. Uchumi ukijengwa mnakuja kupora mkiwa mnavaa koti la muungano.

Kweli yule anapenda sana kupotosha. Nimemshangaa anavyojaribu kupotosha hata issue ya electoral votes za Marekani. State ndogo ni ndogo tu, hata kama electoral college system ikitumika. State yenye 3 electoral votes, kwa mfano, inakuwa na sauti kubwa pale tu candidates wanapokuwa wanachuana vikali kiasi kwamba atakayeshinda hiyo state ndiye atakuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais. Otherwise, candidate anaweza kushindwa uchaguzi kwenye small states kibao, yet akashinda uchaguzi kama amezivuna electoral votes za majority ya zile states kubwa zaidi.
 
Mzigo gani? Nyie machogo si mnasubiri mafuta ya Zanzibar yachimbwe mpore hela za Wazanzibari mkiwa mmevaa koti la muungano?
 
Mzigo gani? Nyie machogo si mnasubiri mafuta ya Zanzibar yachimbwe mpore hela za Wazanzibari mkiwa mmevaa koti la muungano?

Hii dunia haiwezi kuishiwa watu wa ajabu ajabu. Tunavijua vituko vyenu. Natural Gas, Gold, Giamond, Tanzanite na raslimali zingine za mainland ni mali zetu Watanzania wote (wa Bara na visiwani), lakini raslimali za Zanzibar ni za Wazanzibari.
 
Wewe si ndiye uliandika haya maneno? Mbona unarukwa na akili tena?

Tueleze juu ya uporaji unaohofia! Kuna Wapemba kibao huku bara. Kwanini wanakaa na kufanya shughuli zao za maendeleo kwa waporaji?

Mbona nimeshakufafanulia hapo juu kwamba naongelea uchumi siyo mali binafsi? Unaanza kujitoa fahamu mapema?
 
Wewe unadhani terrorists wanahamasishwa na ndimi zinazotumika vizuri?

..terrorist kwako anaweza kuwa shujaa kwa mwingine.

..kwa mfano, wewe unaona Ccm ni mashujaa, lakini wako Waznz wanawaona ni magaidi / madhalimu terrorists.
 
..terrorist kwako anaweza kuwa shujaa kwa mwingine.

..kwa mfano, wewe unaona Ccm ni mashujaa, lakini wako Waznz wanawaona ni magaidi / madhalimu terrorists.

Labda kama hujui maana ya terrorist na maana ya shujaa. Aliyekuambia mimi nawaona CCM ni mashujaa ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…