Katika clip hapa juu msikilize OMO akisema haya kuhusu East Africa Currency Board na BoT
Dakika 9.44
OMO anasema '' Zanzibar ilikuwa mwanachama wa East Afrika Currency Board na Baada ya muungano share zake katika BoT ilikuwa 11%. Kulikuwa na mgogoro hadi mwaka 1996 ambapo WB ilikuja kusuluhisha na kuamua kuwa Zanzibar ipewe 4.5% hadi suala litakapomalizwa na kuanzia hapo halijashughulikiwa tena''
Hoja:
East African Currency board iliamuliwa kuvunjwa mwaka 1965 na kusimamisha shughuli mwaka 1966
Hoja ya kwamba baada ya ''muungano'' share za Zanzibar ziliingizwa BoT ni uzushi na uongo, mwaka 1964 BoT haikuwepo
Sasa msikilize OMO yule yule hapa chini
Dakika 45.56
OMO anasema '' Baada ya East Currency Board luvunjwa Karume alikataa shea za Zanzibar zisiingizwa BoT bali ilundwa People Bank of Zanzibar (PBC), kwamba, Jumbe , Abdul Wakili hadi Salimini waliona tatizo. Katika kipindi chote Zanzibar haijawahi kutumia Bank Kuu.''
Hoja :
Clip ya kwanza OMO anasema kwamba baada ya muungano 1964 Pesa za Zanzibar ziliingizwa BoT.
Muungano ulikuwa 1964 , BoT ilianzishwa 1966 lakini pia anaaminisha umma kuwa shea zilihamishwa mara moja.
Clip ya pili anasema Karume (aliyekuwa mwasisi wa muungano) hakuhamisha shea bali alitengeneza PBZ hadi wakati wa Salimini na kwamba Zanzibar haikuwahi kutumia BoT
Hivi tushike lipi kati ya clip hizo mbili? Inakuwaje mtu mmoja ana position mbili tofauti katika suala moja?
Huu kama si uongo na uzushi ni kitu gani!
JokaKuu