Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Kwa mifumo yetu huyu OMO nadhani siku zake zinahesabika kwenye hicho kiti. Lakini kingine usikute OMO wametofautiana na Mwinyi kwenye cake ya Zanzibar, usikute OMO kalazimisha jambo mwenzake kagoma basi kaamua atoke kivyake. Lingine ukimuangalia OMO shavu limejaa mno halafu anatafuta umaarufu ili watu waje wafe, sijui atafaidika nini.
 
Kwa sasa lipo wazi chunguza ata mada zingine za maswala ya muungano JF contributors wengi msimamo wao awauelewi tena huu muungano.

Ni watu wachache sana wenye nguvu ya kuutetea muungano bara kutoka moyoni.

Kikubwa kinachowachosha wa bara ni hizi tabia zao za choyo ‘chetu chao; na chao ni chao’.

Hao ACT wazalendo upande wa bara ata aileweki agenda yao nini tena, baada ya kuwakabidhi CUF ya Maalim Seif chama na wenyewe wanaenda na mdundo wao tu.
Tatizo ukitaka Zanzibar itoke Muungani nakuhakikisha looser ni wazazibar walioko bara na wataganyika walioko Zanzibar. Wa huku bara watafukuzwa kama walioko visiwani. Yaani hilo valangati litakuwa balaa. Hili jambo mi naona si jambo la kujadili kabisa ni ujinga. Na kizanzibar chenyewe kwa mabadiliko ya tabia nchi unaweza kukuta miaka ijayo itamezwa na maji
 
Ngoja tushuhudie mtanange. Ila hadi sasa Othman 3-0 Mwinyi
 
Tatizo ukitaka Zanzibar itoke Muungani nakuhakikisha looser ni wazazibar walioko bara na wataganyika walioko Zanzibar. Wa huku bara watafukuzwa kama walioko visiwani. Yaani hilo valangati litakuwa balaa. Hili jambo mi naona si jambo la kujadili kabisa ni ujinga. Na kizanzibar chenyewe kwa mabadiliko ya tabia nchi unaweza kukuta miaka ijayo itamezwa na maji
Muungano unapovunjika settlers wanachagua uraia au kuendelea kuishi kwa kanuni mpya za wageni; sidhani kama kuna kufukuzana.

Ila wazanzibari wanaweza wafukuza wabara kwa jinsi walivyo; we waache tu nimecheka hapo kwenye mabadiliko ya tabia za nchi kisiwa chenyewe kinaweza zama baharini miaka ijayo.
 
Huwaga nashangaa sana, Mtu Makini na asiyepinda kama Othman Masoud Kufanya kazi na Mtu kama Ayatollah, Yuda Kabwe Mwami
Mkuu Bramo, usifikiri hapo kuna kazi inafanyika kati ya hao wawili. It's marriage of convinience, huyo Ayatola akiwa hana lake, na wala hana la kusema au kufanya lolote juu ya hali iliyopo.
 
Tafuta bidhaa za trade Zanzibar miaka hiyo uone hizo resources walikuwa wanatoa wapi.

Bila ya muungano kitu kikubwa kilichobaki ni karafuu tu.

Ardhi ya uwekezaji sasa hivi wanaangalia visiwa vidogo vya pembeni mainland Zanzibar hakuna tena mahala pa kujengwa mahotel makubwa.

Na utalii wenyewe umekuzwa na bara wanakuja mbugani kisha wanamalizia Zanzibar.

Waisraeli wamewezaje kujenga uchumi wao wakati wana ardhi ndogo na hawana rasilimali nyingi? Ukishapata jibu utajua dunia ya leo unaweza kuinua uchumi bila ya kuwa na ardhi kubwa yenye rasilimali nyingi. Na unaweza kuwa na ardhi kubwa na rasilimali nyingi na bado ukawa maskini kama unavyoiona Congo au Tanzania.
 
Muungano unapovunjika settlers wanachagua uraia au kuendelea kuishi kwa kanuni mpya za wageni; sidhani kama kuna kufukuzana.

Ila wazanzibari wanaweza wafukuza wabara kwa jinsi walivyo; we waache tu nimecheka hapo kwenye mabadiliko ya tabia za nchi kisiwa chenyewe kinaweza zama baharini miaka ijayo.
Hicho kisiwa nina uhakika kitakuja kuzama miaka ijayo maana kipo tambalale mno. Sasa kuhusu kufukuzana upande wa Zanzibar inawezekana ikaleta shida maana wa Zanzibar wengi wanawachukia watu wa bara na kuwaona ni wakoloni. Mi nadhani bora tuungane kabisa tuwe nchi moja rais mmoja kule apelekwe mkuu wa mkoa tu
 
Waisraeli wamewezaje kujenga uchumi wao wakati wana ardhi ndogo na hawana rasilimali nyingi? Ukishapata jibu utajua dunia ya leo unaweza kuinua uchumi bila ya kuwa na ardhi kubwa yenye rasilimali nyingi. Na unaweza kuwa na ardhi kubwa na rasilimali nyingi na bado ukawa maskini kama unavyoiona Congo au Tanzania.
How much military aid does US give to Israel? - BBC News

Hiyo ni misaada ya US pekee, Jews are rich watu kama hakina Abromovich kila investment opportunity wanapeleka Israel its not short of FDI, wana export wine and spirit, tourism ni biashara both religious pilgrimages and tourism (mpaka wana regulate idadi ya visitors, wanasambaza nishati Palestine, wana-uza bidhaa Palestine, collect taxes in Palestine, wana-mafuta yao; to name a few.

Yaani unataka kuifananisha Zanzibar na Israel; walau ungesema Seychelles.
 
Akishinda kwa watu kukubali hoja zake, basi na iwe hivyo. Akishindwa, atokomee mbali.
Othman Masoud hawezi kutokomea mbali, kwa sababu madai ya kuvunja au kurekebisha Muungano sio hoja za Othman, na yeye si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho kulaani Muungano. Haya ni madai ya kudumu ya mamilioni ya Watanganyika na Wazanzibari.

Muungano ni tatizo. Tutaendelea kudai uvunjwe!
 
Othman hawezi kutokomea mbali kwa sababu madai ya kuvunja au kurekebisha Muungano sio hoja za Othman na Othman si wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho kulaani Muungano. Haya ni madai ya kudumu ya mamilioni ya Watanganyika na Wazanzibari.

Muungano ni tatizo. Tutaendelea kudai uvunjwe!
Ni mamilioni mangapi ya waTanganyika wanaounga mkono anayosimamia Othman? Huko Zanzibar kuna mamilioni mangapi?
Unataka kumpa ukuu asiostahili kuwa nao.

Na ninaomba unielewe hapo uliponi'quote', sehemu ya kwanza nimeeleza kama atakuwa na ushawishi, kama unavyouona wewe kwa waTanzania na wakakubaliana naye, basi iwe kama hivyo watakavyoamua waTanzania wenyewe.
Wewe umeamua kwenda kwenye hicho kipande cha pili, wakati ambapo waTanzania wanakataa hoja zake, sasa hapo atakuwa anampambania nani tena, hadi wewe uone kwamba "haendi popote"?
Ndiyo, anaweza asiende popote, lakini atakuwa anabaki kubweka tu kama kichaa mitaani akisikilizwa na hao wachache unaowaona wewe kuwa mamilioni.
 
Mkuu JokaKuu
Ingalikuwa vema ukiweka clip nzima ya Othman Masoud kwasababu kuna mengi

Sishangai mtifuano kwasababu, OMO kama wanavyomwita ni mpotoshaji hasa linapokuja suala la muungano.
Angalia interview ya Clouds 360 ina mengi ya kapotosha kwa makusudi au kutojua

Watangazaji watatu wa Clouds hawakuweza kuuliza, kusahihisha au kutaka ufafanuzi kutoka kwa Othman alipoongea . Walimwacha ahutubie badala ya mahojiano. Watangazaji walisikitisha katika viwango! shame

clip ni kwa hisani ya Clouds media

Dakika 48
Masoud Othman anasema ''Tanganyika na Zanzibar ziliungana zikiwa sovereign states, baada ya muungano ikawa shared sovereignity. Moja ya matakwa ya shared sovereignty ni kuwa na Policy na kwamba sheria zinatungwa na upande mmoja na baraza la mawaziri la JPM ,Zanzibar haikuwakilishwa''

Hoja: Hoja ya VP Masoud si ya kweli.
Katika shared sovereignty Tanganyika impoteza Zanzibar imebaki nayo kupitia SMZ inayoamua mambo yao.

Kuhusu sera kutungwa kwa upande mmoja nalo si kweli.
Zanzibar ina Wabunge na Wabunge kutoka BLW wanaoiwakilisha katika Bunge la JMT.

Kwamba maamuzi yanafanywa kwa kura ni kweli kwasababu Wazanzibar ndani ya JMT wanaamua hata mambo yasiyo ya muungano kwa kura ile ile anayoikataa Masoud Othman, mbona halisemi hilo?

Kamtumhumu JPM kwamba baraza lake la Mawaziri halikuwa na uwakilishi kutoka Zanzibar.
VP Othman alikuwa AG anafahamu Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa Cabinet kwa kuapishwa
Kwamba VP SSH alikuwa mjumbe wa Cabinet. Hivi hawa si viongozi wa juu wa Zanzibar, VP Othman alitaka uwakilishi gani?Lakini pia alikuwepo Waziri Mbarawa akisimamia wizara isiyo ya muungano, hilo anasemaje?

Dakika 53
VP OMO anasema ''resource za muungano zitawanywe ili Zanzibar ipate biashara na ajira.
Akatoa mfano Elimu ya juu ambako Zanzibar hakuna chuo kikuu''

Hoja: Haiwezekani resource za Tanganyika ziwekwe Zanzibar kwasababu mambo makuu ya muungano ni machache sana.

VP OMO hakusema gharama za resource hizo anazotaka ziwekezwe Zanzibar zinalipwaje na Zanzibar.
Kwasasa Zanzibar haina mchango wowote kwanini resource za muungano zipelekwe huko.

Pili, Masoud Othman aelewe suala la elimu ya juu si la muungano. Ni suala lililoongezwa na akina Marehemu Sitta katika kusiadia Zanzibar hivyo kutojengwa chuo huko ni sawa kikijengwa ni fadhila.
Zanzibar wana wizara ya elimu ya juu sasa anataka ya muungano ifanye nini ? Zanzibar inachangia nini?

Dakika 51 anasema Rais wa JMT anachaguliwa na Tanganyika kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura Zanzibar. Makamu wa Rais Othman akatolea mfano Marekani ambako California ina watu milioni 40 na Maine milioni 1.6 na Wyoming milioni 1 akisema mfumo huo unahkikisha hata state ndogo zinapata kauli kwa kutumia kile alichokiita ''Collegiate''

Hoja: Hakuna kitu kinachoitwa ''collegiate'' katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani bali electoral college.

States zimepewa idadi ya Wajumbe watakaochaguliwa kwenda kumchagua Rais.
Rais anaweza kuchaguliwa kwa electoral college votes (270) za state chache

Hivyo kuna majimbo yenye wajumbe wanaoweza kufikisha 270.
Mfano California 55, New York 29, Texas 38, Florida 29, Pen state 20, Michigan 16, Georgia 16, N.Carolina 15, Maryland 10, Tenn 11, Illnoi 20, virginia 13, S.Carolina 9. State 12 zinaweza kumchagua Rais wa Marekani kwa kura 270 zinazohitajika.

Mfumo huo unawafanya wagombea wasipoteze muda na pesa za kampeni huko Montana wajumbe 3, Wyoming 3, au Vermont 3. kwa mantiki hiyo VP alipotosha au hakujua mfumo unafanyaje kazi

Hata Tanzania bado kuna suala la mikoa. Mfano mikoa ya kanda ya ziwa inaweza kumchagua Rais
Tukifuata mfumo wa Marekani bado Zanzibar itakuwa na viti vichache kwasababu katika constituents za Tanzania Zanzibar ni ndogo sana Wabunge wake wakichaguliwa na watu 2,500 lakini wanakura sawa pale Dodoma. Hivi Makamu wa Rais halioni hili kweli.!!!

Wamarekani sasa hivi wanataka popular vote kwa kujua mfumo wa electoral college si mzuri. Hillary Clinton alishinda popular vote kwa kura milioni 3 lakini Trump alimshinda kwa electoral college na kuwa Rais

Pengine alichokusudia kusema ni kwamba states zimepewa Maseneta 2 bila kujali ukubwa ili maamuzi yazingatie hata zile ndogo. Kinyume cha hivyo OMO alipotosha sana

Bank kuu:
VP Othman anasema Karume aliona tatizo hakukubali kuingia BoT hadi Salimini. Kwamba Zanzibar ilikuwa na PBZ baada ya kuvunjika EAC currency board

Hoja: Hapa VP anatueleza kwamba yale madai ya Zanzibar kuingiza pesa BoT yanayowapa 4.5% ya pato la Tanganyika ni uongo na kwamba pesa hizo hawakupaswa kupewa bali ni hisani.
Lakini pia VP othman hakueleza nini kilimfanya Salimin akaingiza nchi BoT? Hakueleza je ZPB ambayo ipo hadi leo inamilikiwa na nani?

Dakika 23
OMO anasema Zanzibar ingesaidia muungano kutokana na historia yake na kwamba kuna KM 200 za bahari zenye mafuta na gesi katika vitalu 9, 10.

Hoja Historia ya Zanzibar ni ya biashara ya pembe za ndovu na utumwa, haina manufaa kwa Tanzania leo hii.

Pili, mafuta na gesi yameondolewa na Zanzibar katika mambo ya muungano kupitia katiba ya 2010.
Ingawa Zanzibar inafadika na mapato ya gesi na madini yenyewe haitaki kuwa mshiriki.
Makamu wa Rais anapotosha sana

Dakika 24
OMO anasema Singapore ilikuwa katika muungano na Malaysia nailipojitoa uchumi wake ni mkubwa kuliko wa Tanzania na inaweza kufadhali bajeti

Hoja: VP Masoud anawaambia Wazanzibar wakitoka nje ya muungano watakuwa matajiri kama Singapore.

Hakuna tatizo ni mtazamo wake, anatakiwa achochoea kuni muungano uvunjike Zanzibar iwe Singapore

Katika video hii anazungumzia Zanzibar kunyimwa fursa ya kukopa akitolea mfano wa milioni 200 kutoka China
Anasema Tanganyika ipo hoi na Zanzibar ikitaka kupita Tanganyika inaweka vikwazo

Hoja: Mataifa yanakopesha kwa kuangalia uwezo wa nchi kulipa.
China walisita wakijua mdhamini lazima awe chumi kubwa Tanganyika.

Makamu wa Rais aelewe Zanzibar iliruhusiwa kukopa, jambo jema kwani litapunguza mzigo kwa Tanganyika.

Anachotakiwa ni kuendelea kusisitiza tu waende kukopa bila kutumia jina la JMT, walipe wenyewe na watafute wadhamini wenyewe! Tanganyika haina sababu za kuzuia Zbar wasikope ! haina bali kauli tu za kuzua na kuifanya Tanganyika ionekane ni waovu sana ! Chuki yake dhidi ya Tanganyika imefuruta

Kwa kweli imevuka mipaka. Na anatumia ruzuku ya ACT inayotokana kwa sehemu kubwa na walipa kodi wa Tanganyika.
Hata wakikopa, watalipa kwa hela zipi?
 
How much military aid does US give to Israel? - BBC News

Hiyo ni misaada ya US pekee, Jews are rich watu kama hakina Abromovich kila investment opportunity wanapeleka Israel its not short of FDI, wana export wine and spirit, tourism ni biashara both religious pilgrimages and tourism (mpaka wana regulate idadi ya visitors, wanasambaza nishati Palestine, wana-uza bidhaa Palestine, collect taxes in Palestine, wana-mafuta yao; to name a few.

Yaani unataka kuifananisha Zanzibar na Israel; walau ungesema Seychelles.

Kwa hiyo unafikiri US military aid ndiyo imeinua uchumi wa Israel? Unajua tofauti ya military aid vs economic aid? Halafu hayo mafuta yanachimbwa wapi? Au unazungumzia gesi ambayo wameanza kuchimba siku za karibuni tuu? Na kabla hawajaanza kuchimba hiyo gesi uchumi wao ulikuwa mkubwa tayari.

Siri ya maendeleo yao ni Wayahudi wa diaspora (diaspora jews). Wako diaspora matajiri hao akina Abromovich, wako wenye uchumi wa kati (madaktari, ma engineers, mawakili, n.k), wako maskini lakini asilimia yao kubwa wanaisapoti Israel. Zanzibar ina diaspora kubwa sana, kuna matajiri, kuna wenye uchumi wa kati, kuna wenye uchumi wa chini na wote Zanzibar ikipata mamlaka kamili, diaspora wataisaidia kiuchumi. Kwa sababu wote ni Zanzibar nation. Nyie machogo mtabaki kuyaonea wivu maendeleo ya Zanzibar na kuleta uhasama. Uhasama na wivu kama ule alioujenga Nyerere dhidi ya Kenya baada ya Kenyatta kuukata Muungano wa Kenya na Tanzania na kuiona Kenya inaendelea kiuchumi wakati Tanzania inakwama.
 
Kwani sasa hivi hao wazanzibar matajiri wanazuiwa na nani kuisaidia Zanzibar?
 
Othman Masoud ni mtu asieutaka Muungano ata Zanzibar ipewe nini atakuja na dai jipya.

Anyway mimi sio pro muungano anymore tuwaache tu wafanye yao;
Kama Othman Masoud hataki Muungano, na wewe pia huujali Muungano, why are you hyperventilating in attacking and disparaging him?

Othman hataki Muungano, na mimi siutaki Muungano, na ma milioni ya Wazanzibari na Watanganyika HATUTAKI MUUNGANO, kwa nn mtulazimisheeee?
 
Kwani sasa hivi hao wazanzibar matajiri wanazuiwa na nani kuisaidia Zanzibar?

Unataka wajenge uchumi wa Zanzibar ili machogo mje kupora mali zao na kuifilisi tena? Si mlishafanya zamani au unafikiri tumesahau? Unafikiri nyie mtakubali Zanzibar ipate maendeleo wakati nyie mnakwama huko bara bila ya kuja kufanya fujo huku? Kuwa realistic kidogo.
 
Back
Top Bottom