Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

EeeeenHeeee!

Ahsante kwa taarifa, na hasa hiyo picha.

Lakini si mwanafunzi hutokea akamzidi mwalimu wake? Ni nadra sana kumpata mwanafunzi akawa 'replica' wa mwalimu aliyemfundisha.

amzidi kwa kipi? mana kila wanachokihubiri kiliasisiwa na Maalim Seif, Utofauti mkubwa utatokana na wakati wanaoufanyia siasa, Maalim Seif alianza siasa katika kipindi kigumu sana.
 
amzidi kwa kipi? mana kila wanachokihubiri kiliasisiwa na Maalim Seif, Utofauti mkubwa utatokana na wakati wanaoufanyia siasa, Maalim Seif alianza siasa katika kipindi kigumu sana.
Kwahiyo wewe hutaki kabisa muungano?

#MaendeleoHayanaChama
 
Anatumia udhaifu wa CCM kujibaraguza hivi.

Huu muungano ulipoanzishwa, ile ilikuwa ni hatua ya mwanzo tu. Lengo lilikuwa ni kuendelea kuuimarisha kadri watu wa pande mbili walivyoweza kushirikiana na kuelewana.
Badala ya kufanya juhudi kuuimarisha muungano, CCM wakazembea, na kundi lililokuwa halitaki muungano huko visiwani likapamba moto na kuanza kulegeza/kudhoofisha badala ya kuimarisha muungano.

CCM wakadhani njia bora ya kuwatuliza hawa ni kuwakubalia mambo waliyodai. Kila walipowapa jambo moja, wanaanza kudai la pili. Sasa wamefikia hatua ya kudai uhuru kamili, yaani kuvunja muungano.

Sioni kiongozi mwenye uwezo wa kuwakabili hawa kwa wakati huu, na kelele zitakuwa kubwa sana, hasa wakati huu wa Samia.
Ccm wamefeli mno na wanazidi kuonyesha udhaifu kwa namna wanavyoshughulikia suala la muungano.
zitto junior Tindo Pascal Mayalla Nguruvi3 JokaKuu
 
Kwahiyo wewe hutaki kabisa muungano?

#MaendeleoHayanaChama

Muungano ni uhuni tu uliotengnezwa na wahuni kwa ajili ya maslahi yao. Ili tuwe na Amani na utulivu kila mtu awe na nchi yake. hapo ndipo tunapoweza kuishi kama majirani wema kuliko kulazimisha udugu ambao haupo. Hizi ishu za muungano zisiposhughulikiwa huko mbeleni zinaweza kuja kutuletea matatizo makubwa sana.
 
Ni sawa na kufuga Simba halafu siku akikubadilikia ushangae.

Othman Masoud ilikuwa wazi ipo siku ataleta vurugu serikalini.
 
wazanzibari wanahitaji maendeleo sio malumbano ambayo hayana tija.

tulieni muijenge zanzibari acheni kurudisha nyuma nia njema ya Mhe. Rais Hussein kwa wazanzibari.
 
Wewe huoni faida ya umoja amani na undugu..kingine bahari na vilivyomo.

Muungano unafaida nyingi..mpungufu yaliyopo yalekebishwe tuwe na serikali moja ama tatu.

#MaendeleoHayanaChama
Sioni faida yoyote bali unyonyaji na yoyote anaendana na utofauti wa kimawazo na huu muungano haramu ni adui wa nchi.

Umoja na mshikamano kila nchi inakuwa na Umoja huo na nchi nyengine kuhusu bahar na mengine isiwe hoja yakutokuwepo na Umoja.

Tatizo lá watanganyika waznz wakitoa mawazo yao juu ya muungano inakuwa shida kubwa ni ati wamejenga bara.

Hata watanganyika wapo walionje ya tanganyika wamejenga kila kitu na kuekeza huko.
 
Mkuu unajua kuna watanganyika wangapi walioko Zanzibar?
Hili jibu lako inaonyesha hujui uhalisia ngoja nikuache.
Nionyeshe Mtanganyika mwenye ekari 5 za eneo Zanzibar nikuonyeshe Mpemba mwenye ekari 50 Tanganyika.
 
Hili jibu lako inaonyesha hujui uhalisia ngoja nikuache.
Nionyeshe Mtanganyika mwenye ekari 5 za eneo Zanzibar nikuonyeshe Mpemba mwenye ekari 50 Tanganyika.

Watu wapo kwenye kupignania utaifa wao unaleta hoja za ekari 50? Hata waarabu kutoka UAE wanajichukulia tu maeneo Bara bila ya hata kuwa na Muungano.
 
Sioni faida yoyote bali unyonyaji na yoyote anaendana na utofauti wa kimawazo na huu muungano haramu ni adui wa nchi.

Umoja na mshikamano kila nchi inakuwa na Umoja huo na nchi nyengine kuhusu bahar na mengine isiwe hoja yakutokuwepo na Umoja.

Tatizo lá watanganyika waznz wakitoa mawazo yao juu ya muungano inakuwa shida kubwa ni ati wamejenga bara.

Hata watanganyika wapo walionje ya tanganyika wamejenga kila kitu na kuekeza huko.

Kutoa mawazo kuhusu muungano au kuzungumzia muungano si kosa hata kidogo na halitakuwa kosa

Tunachosema hapa ni kuwa katika maongezi au mazungumzo uwepo ukweli

VP Othman Masoud sehemu kubwa ya hoja zake ni upotoshaji akiongozwa na chuki dhidi ya Tanganyika

Makamu wa Rais wa Zanzibar hapaswi kusema Tanganyika ni Wagonjwa na hawafai kukopa kwa niaba ya Zanzibar
Makamu wa Rais hafai kuweka madai yasiyo na ukweli kwamba Tanganyika inaziba njia za Zanzibar

VP hapaswi kuzungumza kwa kificho akichochea mambo, anapaswa kusema wazi .
Mfano aseme Zanzibar wakiondoka kwenye muungano watakuwa kama Singapore.
Kwamba wanatakiwa kuomba kura ya maoni kama Scotland. Na kwamba matatizo ya Zanzibar yanasababishwa na Tanganyika ! aseme wazi asijifiche fiche kwa unafiki hata kama ni utamaduni wa kizanzibar

Makamu wa Rais wa Zanzibar anaaminisha dunia kwamba Tanganyika haitaki Zanzibar ikope! anatoa mfano wa China. Huyu haelewi kuwa bajeti ya Zanzibar ina subsidy ya Tanganyika, na kwamba Tanganyika inalipa 4.5% ya pato lake kwa Zanzibar bure kwa mujibu wake!

Hoja ni kwamba OMO aache kujificha ficha na kuzungumzia vichoroni, atoke wazi na kusema hataki muungano kama A. Salehe na yule wa London Rajab. Uhuru huo anao lakini hana uhuru wa kutoa madai ya uongo, kudanganya umma. OMO anaweza kudanganya Wazanzibar, hapa tuanamwambia nope! aache uzushi, uongo na unafiki

Hivi kwanini Wazanzibar wanaona Tanganyika ni tatizo na CCM pale Kisonge na Kisiwa ndui!
 
..ameleta vurugu gani?

..kuna watu walioleta vurugu na dhuluma Znz kuliko viongozi wa Ccm na Smz?
Othman Masoud ni mtu asieutaka Muungano ata Zanzibar ipewe nini atakuja na dai jipya.

Sasa kwa yeyote mwenye kuelewa misimamo yake si ajabu kuona uzushi, uongo na sumu anayosambaza leo.

Binafsi ukipekua mada ya kutafuta mrithi wa Maalim Seif, kabla ya ACT kupeleka jina lolote nilisema watamteua huyo jamaa (kumbuka hakuwa na senior position ndani ya chama muda huo) bali itakuwa kwa sababu la kuanzisha vugu-vugu la kuuvunja muungano tu.

Maalim Seif alikuwa moderate kwenye kudai nyongeza ya autonomy ya Zanzibar and wise kuepuka vurugu. Huyu Othman Masoud ni radical na ajali sana lolote zaidi ya independence again ukisoma hizo mada za kutafuta replacement nilisema ACT wakimteua huyo jamaa serikali imkatae kwa sababu mbeleni wanamtengenezea jukwaa la kugawa wazanzibari (na ndio kinachoanza kutokea sasa).

Mgawanyiko ya Hizbu na asili Zanzibar auna tofauti na Loyalists na Unionist (North Ireland) bila ya serikali ya uingereza apakaliki kule; ndio kama visiwani bila ya bara.

Asifananishe na Scotland kutumia vita za kifalme kama sababu; huo ni utaratibu mwingine wa mediaeval chiefdoms ambapo walikuwa wanaona wenyewe kwa wenyewe wafalme Europe na kupelekeana vita wakati mwingine kwa madai ya fulani yeye ndio mrithi. King George wa uingereza alikuwa mjerumani mbona hizi sio nchi moja leo. Sasa asichanganye historia za kifalme na siasa nation unions ni vitu viwili tofauti.

Anyway mimi sio pro muungano anymore tuwaache tu wafanye yao; ila kwa serikali huyo jamaa ni tatizo.

Ana siasa za ki demagoguery za kutunga uongo na kuhamasisha makundi kusambaza uongo wake plus ana malalamiko ya kitoto sana ata EAC community kuna baadhi ya sheria zinatungwa kwenye bunge community na nchi wanachama wote wana implement that is how Union works mkishakubaliana maswala ya Union na mkaliwekea bunge la kutunga sheria.

Yeye anapotosha jinsi sheria zinavyotungwa anaongopa ya kuwa serikali ya Tanzania ndio guarantor wa mikopo yao waki default bara inatakiwa kulipa ndio maana wakopeshaji wanataka ridhaa ya serikali kuu kwanza. Wao madeni ya ndani kulipa shida tu; wana madeni ya TANESCO in billions tsh awataki kurejesha god know madeni yao mengine yenye guarantee ya serikali kama ata wanachangia kulipa.

Huyo jamaa ni muongo na nakubaliana kabisa na wanaosema interview zake anazofanya huwa akutani na watu wenye uelewa mpana ndio maana anaropoka ovyo uongo.

Kama nilivyosema awali huyo jamaa ni tatizo la serikali kwa upande namuunga mkono for one simple reason it’s time ya kuuvunja huu muungano. My reasons are kwa umoja wao viongozi wa Zanzibar ni ungrateful people and selfish wanataka vya bara tu vyao nehi.
 
Video mbona zina sturter sanaa!??
 
Unaamini Wazanzibar wote (ikiwemo Ccm Zanzibar ) wanakubaliana na msimamo wa OMO mpaka uhitimishe hivi ?
Kalamu Nguruvi3 Pascal Mayalla zitto junior Tindo
Kilatha
Kichuguu
Yes nakubaliana na JokaKuu kwamba tukutane huko EAC au SADC

Nakubaliana naye pia kwamba hata CCM Zanzibar wanakubaliana na OMO, tatizo ni unafiki walio nao

Ndiyo maana tunasema, OMO kalianzisha sasa CCM Zanzibar wamuunge mkono kuhusu kura ya maoni ya muungano
Huku bara tutawaunga mkono pia na wakishinda hewala waondoke kwa amani kabisa !
 
Yes nakubaliana na JokaKuu kwamba tukutane huko EAC au SADC

Nakubaliana naye pia kwamba hata CCM Zanzibar wanakubaliana na OMO, tatizo ni unafiki walio nao

Ndiyo maana tunasema, OMO kalianzisha sasa CCM Zanzibar wamuunge mkono kuhusu kura ya maoni ya muungano
Huku bara tutawaunga mkono pia na wakishinda hewala waondoke kwa amani kabisa !
Ila chama chake cha sasa (Act) hasa upande wa bara huenda wakawa na mtizamo tofauti na yeye.
 
..Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.

..Hussein Mwinyi anamuona Othman Masoud kama mchochezi asiyetaka Wazanzibar wawe kitu kimoja.

Msikilize Othman Masoud hapa chini.
View attachment 2280710


Hussein Mwinyi amejibu hapa.

View attachment 2280711
Paschal Mayala ndiye anachochea huu ugomvi sijui anafaidika nini
 
Back
Top Bottom