Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Tatizo wanzanzibar mnajikaanga wenyewe kwa wenyewe. Bara kazi yao ni kuwaletea kuni na kuwaacha nyie mkoke moto, muinjike sufuria, muweke mafuta na kujikaanga wenyewe. Sasa hivi rais ni kutoka Zanzibar, kwa nini asikubali mabadiliko ya katiba yatakayozingatia maslahi ya wazanzibar wanayodai? Bungeni Dodoma mnaenda kufanya nini kama mnaona muungano haufai? Nachelea kusema malalamiko yenu ni visingizio baada ya uongozi wenu kushindwa kuwaletea wananchi wake maendeleo. Punguzeni kula urojo na viongozi wenu waache kutumikia serikali ya muungano na mjiongoze wenyewe kama mnadhani mambo ni rahisi sana.
Hela ya kuendesha serikali watolee wapi..labda wakaombe kwa wajomba zao umani..ili waje watawaliwe tena na sultani..mana hakuna cha bure.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakuna muungano, kuna uvamizi. Nyerere alivamia Zanzibar kama Putin alivyovamia Ukraine. Kupinga uvamizi siyo uhaini. Ni haki ya kila mtu.
Alivamia wapi mbona karume alishiriki kikamilifu hadi kuwa makamu wa kwanza wa zenji.

Nyie ndio wanasiasa njaa mnapigania maslahi yenu wala sio ya zenji.

Muungano mapungufu yapo ila hauvunjwi tunayalekebisha kuelekea kuwa na serikali moja tu..

Hizi mbili ndio zinatuletea shida.

#MaendeleoHayanaChama
 
Maisha ya watanganyika yataathirika vipi kama Muungano utavunjika? Kabla ya Aprili 1964 waliishi vipi?

Amandla....
Zamani kulikua na tishio la vita baridi sasahivi kuna tishio la ugaidi..nadhani unaelewa zenji kulitokea nini hadi mashehe wale wakawekwa ndani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hizi kero kila siku watu full kulalamika si uvunjwe tu tubaki na Tanganyika yetu,tuwaachie nchi yao!
Kuvunja muungano haipaswi ila tunauweka sawa kwa kuondoa shida zote na kuwa na serikali moja tu.

Ili hizi kelele za wanasiasa njaa ziishe.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapana, huyu ni 'hardliner' maradufu zaidi ya Maalim.

Seif alipokuwa akipewa ulaji alinyamaza kidogo, huyu ni kama unamchochea zaidi unapomteua kwenye nafasi yoyote!
Pamoja na hayo, sidhani kuwa huyu anayo haiba na hadhi aliyokuwa nayo Maalim Seif kwa wafuasi wake. Sijui kama Masoud alishawahi kugombea nafasi yoyote ya uchaguzi na wananchi wakampa kura kama alizokuwa akipata Maalim.
Kwa hiyo mtu anayepewa ulaji na kutulia kumbe ndio mzuri kuliko asiyenyamazishwa na ulaji?
 
Huyu akili Hana ana ajenda ya Siri, ana dai Tanzania haiendelei kwa sababu ni kubwa na Zanzibar ni ndogo ikiachwa iende peke yake, itaendelea haraka! Maendeleo ya nchi hayafati ukubwa!! Rawnda na Burundi ni nchi ndogo na hazijaendelea, China na USA ni ma nchi makubwa na yameendelea
Mbona unamlisha maneno hajasema hivyo, au umeshindwa kuelewa hiyo analogy aliyotumia
 
Alivamia wapi mbona karume alishiriki kikamilifu hadi kuwa makamu wa kwanza wa zenji.

Nyie ndio wanasiasa njaa mnapigania maslahi yenu wala sio ya zenji.

Muungano mapungufu yapo ila hauvunjwi tunayalekebisha kuelekea kuwa na serikali moja tu..

Hizi mbili ndio zinatuletea shida.

#MaendeleoHayanaChama

Aliyofanya Karume hayatuhusu maana hakuna aliyempigia kura. Karume ni Mnyasa aliyewekwa madarakani na Okello Mganda. Kwanza umeshawahi kusikia muungano upande mmoja unapeleka majeshi kukalia upande mwingine? Huo ni uvamizi siyo muungano.
 
Walikubaliana ndio mana kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Moja ya mambo ya muungano ni ulinzi na usalama.

Wewe hizbu acha kuwapotosha wa zenji kwa maslahi yenu.. inyi mlifukuzwa mtoke zenji..mnaingangania ya nini tena..si mrudi umani kwenu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tungeungana na Burundi tungetajirika maana tungewadhibiti Rwanda kijeshi na kufaidi biashara na Congo DR. Tena labda hata Rais wa Rwanda tungemsimika kibaraka wetu. Hilo litakuja one day
Mbona mentality za kipuuzi sana hizi, Tanzania ina ardhi, maziwa, madini, bandari, mito na misitu kibao imeshindwa kuendeleza hizi potential ipate maendeleo ikafanye uharamia nchi za watu,?
 
..Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.

..Hussein Mwinyi anamuona Othman Masoud kama mchochezi asiyetaka Wazanzibar wawe kitu kimoja.

Msikilize Othman Masoud hapa chini.

Hussein Mwinyi amejibu hapa.

Mmmm
 
Walikubaliana ndio mana kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.

Moja ya mambo ya muungano ni ulinzi na usalama.

Wewe hizbu acha kuwapotosha wa zenji kwa maslahi yenu.. inyi mlifukuzwa mtoke zenji..mnaingangania ya nini tena..si mrudi umani kwenu.

#MaendeleoHayanaChama

Makubaliano ya Karume na Nyerere hayatuhusu. Hakuna aliyempigia kura Karume. Aliwekwa madarakani na Okello na baadaye majeshi ya Nyerere yaliletwa kumlinda. Huo ni uvamizi siyo muungano.
 
Wazanbari wanalalamika, Watanganyika wanalalamika, wengi wanasema muungano wana uunga mkono. Rasimu ya warioba imesema wananchi wamependekeza serikali 3. Hizi 3 zingejibu malalamiko karibu yote. Tatizo liko wapi? CCM ndio wameshikilia serikali 2 na kupindua maoni ya wananchi. Walitumia kila mbinu kupenyeza rasimu yao na kumfurusha warioba na tume yake wasiwe na mchango bungeni. Dawa ni serikali 3.
 
Hapana, huyu ni 'hardliner' maradufu zaidi ya Maalim.

Seif alipokuwa akipewa ulaji alinyamaza kidogo, huyu ni kama unamchochea zaidi unapomteua kwenye nafasi yoyote!
Pamoja na hayo, sidhani kuwa huyu anayo haiba na hadhi aliyokuwa nayo Maalim Seif kwa wafuasi wake. Sijui kama Masoud alishawahi kugombea nafasi yoyote ya uchaguzi na wananchi wakampa kura kama alizokuwa akipata Maalim.

Huyu ni katika wanafunzi wa Siasa Maalim Seif kama ulikua hulifahamu. Hapo akiwa na Ismail Jussa wakiwa wadogo sana.
8ffda-jussa-na-maalim-alipotoka-gerezani.jpg
 
Zamani kulikua na tishio la vita baridi sasahivi kuna tishio la ugaidi..nadhani unaelewa zenji kulitokea nini hadi mashehe wale wakawekwa ndani.

#MaendeleoHayanaChama
Unaamini kuwa Zanzibar nje ya Muungano itakaribisha magaidi?

Amandla...
 
Back
Top Bottom