Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Well said!
 
Wazenji wengi hawana fahamu kuwa Muungano huu ni "iron-clad" yaani hauvunjiki sababu waliouanzisha ni marehemu kwasasa.

Wapiga kelele kama hao kina Othman ni kuwatumia "watu wasiojulikana" tu wapelekwe chocho na kutulizwa!
 
Binafsi sioni umuhimu wa muungano hoja za kutetea muungano ni hoja za enzi ya Soviet error... kuanzia sababu za kiusalama na kiulinzi hata kijamiii Tanganyika tumepoteza sana na bado tunaendelea kupoteza sana kwa huu muungano wa mchongo .
 
Huyu akili hana ana ajenda ya Siri, ana dai Tanzania haiendelei kwa sababu ni kubwa na Zanzibar ni ndogo ikiachwa iende peke yake, itaendelea haraka! Maendeleo ya nchi hayafati ukubwa!! Rawnda na Burundi ni nchi ndogo na hazijaendelea, China na USA ni ma nchi makubwa na yameendelea
 
Huyu jamaa nimemfuatulia vizuri sana muda mrefu tangu akiwa CCM tena kwa cheo cha mwanasheria mkuu wa SMZ.

Kama kwenye bunge la katiba aliamua kusimama na Wazanzibar na kukubali kupoteza nafasi ya AG wa SMZ ni lazima mjue huyu ni zaidi ya Maalim Seif, Maalim Seif anamzidi huyu jamaa umri tu, historia na kuwa ndio icon ya upinzani Zanzibar, sikushangaa hata kidogo baada ya kifo cha Maalim Seif ni yeye ndio akateuliwa kuziba nafasi ya Maalim ya VP.

Na kwakuwa Rais wa JMT ni Mzanzibar huyu jamaa hakuna wa kumnyamazisha, awamu ya sita ndio ya kuclear dhuluma zote walizofanyiwa Wazanzibar.
 
Zenji itafuga magaidi...ikipewa nchi yake.

Bora tuendelee kuwabeba tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.
Msikilize Othman Masoud hapa chini.
Kwa maoni yangu, huyu mtu anatakiwa awekwe pembeni, apate muda wa kutosha ajishughulishe na siasa, kwasababu ACT ndani ya GNU wanatakiwa kutekeleza Ilani na sera za CCM!.

Ushauri kama huu kumhusu mtu huyu huyu niliwahi kuutoa kule nyuma na ukatekelezwa, Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

P
 
Ahsante kwa sahihisho nilimaanisha Singapore. Kwamba Zanzibar ijitoe ili iwe Singapore

Watangazaji hawakuwa na ufahamu hata pale walipotakiwa kumhoji. Mathalan hawawezi kumuuliza kama msimamo wake ni serikali 3 ikiwa hawajamuuliza iwapo anataka muungano hasa baada ya kuonyesha wazi hautaki

Pili, VP OMO kama walivyo Wazanzibar wanaongelea fursa tu humsikii akizungumzia mchango wa Zanzibar
Eti anataka taasisi za muungano zipelekwe Zanzibar wakati ambapo taasisi hizo zina mbadala kule
Mfano kuna sababu gani za kupeleka Tanzania Bureau of standard wakati kuna Zanzibar Bureau of standard

Anasema eti uhamiaji ni suala la muungano lijadiliwe na pande zote, well, Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa Cabinet kwanini halijadili. Kuna Wabunge wa Zanzibar wakiwemo wa ACT kwanini hawazungumzi pale Dodoma

Halafu anataka usawa kwasababu nchi ina shared sovereignty wakati usawa huo haupo katika ''shared cost''

Sina tatizo akichochoea kuni wavunje muungano nina tatizo anapowafanya watu wote mazuzu kama wale anaohutubia

Wadai kura ya maoni si kulalama na kujenga hoja nyepesi zisizo na ithbati.
 
Kwani kero za muungano hazikupatiwa ufumbuzi wa kudumu ?...Maana hazikusikika kabisa mwanzoni mwa awamu hii .
Nguruvi3
 
dhulma ni zipi mkuu? zitaje chache.

but what I know ni kuwa if someone outsmart you, unajipanga! ( Nyerere outsmarted Karume and all Zanzibaris and this will remain forever kwakuwa jeshi lina kambi ukizingua sana unaliwa kichwa)
 
Huyu si hardliner ni kwamba hautaki muungano. Ukisikia kauli zake utashangaa sana

Rejea clip ya pili ya bandiko#6 anatukana na kusema Tanganyika ni wagonjwa wameziba njia za Zanzibar
OMO hajui gharama za ving'ora anavyozunguka navyo, usalama wa nchi wa mipaka na ndani n.k.

Wachina hawataki kuipa Zanzibar kwa kuchelea kuwa haidhaminiki kwa uchumi wake.
Yeye anasema Tanganyika inawazibia, akili za jabu sana, kwamba izibe Zanzibar isikope kwa faida gani.
Kauli zote hizo ni kuchochoea kwamba Zanzibar inapunjwa ingawa haelezi kwa lipi bali lalama tu

Kuna watu waliojificha lakini hawataki muungano. VP OMO, Ali Salehe na yule wa London Rajabu
Jitokezeni mpige chapuo kura ya maoni. OMO katoa mfano wa Scotland katika jitihada za kuwaambia Wazaznibar wadai kura ya maoni. Tatizo lake hasemi wazi anatumia code na kuzua uongo dhidi ya Tanganyika

OMO waambie ACT wasidai tume ya uchaguzi au katiba mpya, Wazanzibar wadai kura ya moni tutawaunga mkono 100%
 
Halafu eti Nyerere alitaka tuungane na Burundi sijui saa hizi hali ingekuwaje, tungekuwa na makundi ya waasi wenye silaha kila kona.
Tungeungana na Burundi tungetajirika maana tungewadhibiti Rwanda kijeshi na kufaidi biashara na Congo DR. Tena labda hata Rais wa Rwanda tungemsimika kibaraka wetu. Hilo litakuja one day
 
Hii ni janja janja ya ccm kumtengeneza mpinzani wao huko Zanzibar baada ya Seif kufariki
 
Kama vipi wapasuane tu hakuna noma
 
Sijawahi ona mtu asiyefaa kuwa kiongozi km Othman, hafai na hatafika mbali mi mwongo mchochezi. Badala aunganishe wananchi anawagawa. Nia hasa ni nini? Tumkatae tumwone mpuuzi tu
 
Kama vipi wapasuane tu hakuna noma
yaani una maana waandae "usiku wa vitasa"? au unataka Mwinyi azipange na Othman wazipige kavu kavu kitaa?


Au kama litakuwa pambano la ubingwa kugombea mkanda wa kuwa mtemi wa Mji Mkongwe archipelago basi sasa uhakikishe ukumbini kuna "mapembe" ya kutosha na urojo, tena machogo wanaokaa mchambawima, mfereji wa wima, Nungwi na Bubu bu wasiruhusiwe kuingia ukumbini ati!

Marungu ya kutosha yawepo ukumbini kuwatoa machogo wote maana sie wazenji tunshaghadhibika yakhe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…