Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Propaganda uchwara, Alshabaab wapo hapo jirani tu Kenya na Islamic State wapo hapo tu Msumbiji tena Gabo Delgado.

Haya mambo muwe mnaandika au kuambiana mkikutana mazezeta.
Kwahiyo unataka tuwaache ili waikaloe zenji..muungano unamapungufu yake sana..ila kuipa uhuru kamili zenji ni kuhatarisha maisha ya watanganyika.

Tunazijua itikadi hizo zikikita mizizi..

#MaendeleoHayanaChama
 
Pamoja na bandiko lako reeefu,hv nn kinachofanya kung'ang'ana na huu muungano?????
 
Halafu eti Nyerere alitaka tuungane na Burundi sijui saa hizi hali ingekuwaje, tungekuwa na makundi ya waasi wenye silaha kila kona.
Acha kupotosha nchi ya wachaga tumeungana nayo tuko poa tu
 
Huyu OMO mnamuonea sana! Katika nchi yote bara na visiwani hakuna kiongozi mkweli asiye na chembe ya unafiki kama OMO. Nilifuatilia mazungumzo haya alikuwa very balanced! Kwenye credit alitoa credit penye marekebisho aliyagusia bila unafiki!
Muacheni!!
 
Nyerere alituingiza kwenye jinamizi la muungano unaotupa shida mpaka leo.

Tanganyika tukatae hili zigo la Zanzibari. Wana nini cha mno cha kutubebesha zigo?
Hawa watu bora watoke tu kwenye huu Muungano. Maana kila siku ni kulalamika tu.

Cha kushangaza, mchango wao kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa Tanganyika ni mdogo sana ukilinganisa na ule wa Tanganyika, kwa nchi yao.
 
Pamoja na bandiko lako reeefu,hv nn kinachofanya kung'ang'ana na huu muungano?????
Tatizo wanzanzibar mnajikaanga wenyewe kwa wenyewe. Bara kazi yao ni kuwaletea kuni na kuwaacha nyie mkoke moto, muinjike sufuria, muweke mafuta na kujikaanga wenyewe. Sasa hivi rais ni kutoka Zanzibar, kwa nini asikubali mabadiliko ya katiba yatakayozingatia maslahi ya wazanzibar wanayodai? Bungeni Dodoma mnaenda kufanya nini kama mnaona muungano haufai? Nachelea kusema malalamiko yenu ni visingizio baada ya uongozi wenu kushindwa kuwaletea wananchi wake maendeleo. Punguzeni kula urojo na viongozi wenu waache kutumikia serikali ya muungano na mjiongoze wenyewe kama mnadhani mambo ni rahisi sana.
 
Likijengwa daraja tu kutuunganisha hakuna atakayepinga muungano. Ni wanasiasa tu kupenda vyeo, wazanzibar wote walitoka bara.
 
Ni kujisumbua tu. Hakuna mtu atathubutu kuuvunja huu Muungano. Marekani leo wanaadhimisha zaidi ya miaka 200 ya Uhuru ikiwa ni dola kubwa leo watu wafikirie Utanganyika na Uzanzibari. Muungano siyo suala la sera za vyama. Ukijaribu kuvunja Muungano hata uwe upinzani wewe ni mhaini. Utakabiliwa kama mhaini. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Hakuna muungano, kuna uvamizi. Nyerere alivamia Zanzibar kama Putin alivyovamia Ukraine. Kupinga uvamizi siyo uhaini. Ni haki ya kila mtu.
 
Katiba mpya tu na serikali 3, ili sote tuchangie equally kwenye hilo li Union. Tutakuwa tumemaliza utata. Yaani mini ngekuwa mzanzibar ningetaka serikali kamili
 
Kwahiyo unataka tuwaache ili waikaloe zenji..muungano unamapungufu yake sana..ila kuipa uhuru kamili zenji ni kuhatarisha maisha ya watanganyika.

Tunazijua itikadi hizo zikikita mizizi..

#MaendeleoHayanaChama
Maisha ya watanganyika yataathirika vipi kama Muungano utavunjika? Kabla ya Aprili 1964 waliishi vipi?

Amandla....
 
Hizi kero kila siku watu full kulalamika si uvunjwe tu tubaki na Tanganyika yetu,tuwaachie nchi yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…