Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Kwa mifumo yetu huyu OMO nadhani siku zake zinahesabika kwenye hicho kiti. Lakini kingine usikute OMO wametofautiana na Mwinyi kwenye cake ya Zanzibar, usikute OMO kalazimisha jambo mwenzake kagoma basi kaamua atoke kivyake. Lingine ukimuangalia OMO shavu limejaa mno halafu anatafuta umaarufu ili watu waje wafe, sijui atafaidika nini.
 
Tatizo ukitaka Zanzibar itoke Muungani nakuhakikisha looser ni wazazibar walioko bara na wataganyika walioko Zanzibar. Wa huku bara watafukuzwa kama walioko visiwani. Yaani hilo valangati litakuwa balaa. Hili jambo mi naona si jambo la kujadili kabisa ni ujinga. Na kizanzibar chenyewe kwa mabadiliko ya tabia nchi unaweza kukuta miaka ijayo itamezwa na maji
 
Ngoja tushuhudie mtanange. Ila hadi sasa Othman 3-0 Mwinyi
 
Muungano unapovunjika settlers wanachagua uraia au kuendelea kuishi kwa kanuni mpya za wageni; sidhani kama kuna kufukuzana.

Ila wazanzibari wanaweza wafukuza wabara kwa jinsi walivyo; we waache tu nimecheka hapo kwenye mabadiliko ya tabia za nchi kisiwa chenyewe kinaweza zama baharini miaka ijayo.
 
Huwaga nashangaa sana, Mtu Makini na asiyepinda kama Othman Masoud Kufanya kazi na Mtu kama Ayatollah, Yuda Kabwe Mwami
Mkuu Bramo, usifikiri hapo kuna kazi inafanyika kati ya hao wawili. It's marriage of convinience, huyo Ayatola akiwa hana lake, na wala hana la kusema au kufanya lolote juu ya hali iliyopo.
 

Waisraeli wamewezaje kujenga uchumi wao wakati wana ardhi ndogo na hawana rasilimali nyingi? Ukishapata jibu utajua dunia ya leo unaweza kuinua uchumi bila ya kuwa na ardhi kubwa yenye rasilimali nyingi. Na unaweza kuwa na ardhi kubwa na rasilimali nyingi na bado ukawa maskini kama unavyoiona Congo au Tanzania.
 
Hicho kisiwa nina uhakika kitakuja kuzama miaka ijayo maana kipo tambalale mno. Sasa kuhusu kufukuzana upande wa Zanzibar inawezekana ikaleta shida maana wa Zanzibar wengi wanawachukia watu wa bara na kuwaona ni wakoloni. Mi nadhani bora tuungane kabisa tuwe nchi moja rais mmoja kule apelekwe mkuu wa mkoa tu
 
How much military aid does US give to Israel? - BBC News

Hiyo ni misaada ya US pekee, Jews are rich watu kama hakina Abromovich kila investment opportunity wanapeleka Israel its not short of FDI, wana export wine and spirit, tourism ni biashara both religious pilgrimages and tourism (mpaka wana regulate idadi ya visitors, wanasambaza nishati Palestine, wana-uza bidhaa Palestine, collect taxes in Palestine, wana-mafuta yao; to name a few.

Yaani unataka kuifananisha Zanzibar na Israel; walau ungesema Seychelles.
 
Akishinda kwa watu kukubali hoja zake, basi na iwe hivyo. Akishindwa, atokomee mbali.
Othman Masoud hawezi kutokomea mbali, kwa sababu madai ya kuvunja au kurekebisha Muungano sio hoja za Othman, na yeye si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho kulaani Muungano. Haya ni madai ya kudumu ya mamilioni ya Watanganyika na Wazanzibari.

Muungano ni tatizo. Tutaendelea kudai uvunjwe!
 
Ni mamilioni mangapi ya waTanganyika wanaounga mkono anayosimamia Othman? Huko Zanzibar kuna mamilioni mangapi?
Unataka kumpa ukuu asiostahili kuwa nao.

Na ninaomba unielewe hapo uliponi'quote', sehemu ya kwanza nimeeleza kama atakuwa na ushawishi, kama unavyouona wewe kwa waTanzania na wakakubaliana naye, basi iwe kama hivyo watakavyoamua waTanzania wenyewe.
Wewe umeamua kwenda kwenye hicho kipande cha pili, wakati ambapo waTanzania wanakataa hoja zake, sasa hapo atakuwa anampambania nani tena, hadi wewe uone kwamba "haendi popote"?
Ndiyo, anaweza asiende popote, lakini atakuwa anabaki kubweka tu kama kichaa mitaani akisikilizwa na hao wachache unaowaona wewe kuwa mamilioni.
 
Kwa kweli imevuka mipaka. Na anatumia ruzuku ya ACT inayotokana kwa sehemu kubwa na walipa kodi wa Tanganyika.
Hata wakikopa, watalipa kwa hela zipi?
 

Kwa hiyo unafikiri US military aid ndiyo imeinua uchumi wa Israel? Unajua tofauti ya military aid vs economic aid? Halafu hayo mafuta yanachimbwa wapi? Au unazungumzia gesi ambayo wameanza kuchimba siku za karibuni tuu? Na kabla hawajaanza kuchimba hiyo gesi uchumi wao ulikuwa mkubwa tayari.

Siri ya maendeleo yao ni Wayahudi wa diaspora (diaspora jews). Wako diaspora matajiri hao akina Abromovich, wako wenye uchumi wa kati (madaktari, ma engineers, mawakili, n.k), wako maskini lakini asilimia yao kubwa wanaisapoti Israel. Zanzibar ina diaspora kubwa sana, kuna matajiri, kuna wenye uchumi wa kati, kuna wenye uchumi wa chini na wote Zanzibar ikipata mamlaka kamili, diaspora wataisaidia kiuchumi. Kwa sababu wote ni Zanzibar nation. Nyie machogo mtabaki kuyaonea wivu maendeleo ya Zanzibar na kuleta uhasama. Uhasama na wivu kama ule alioujenga Nyerere dhidi ya Kenya baada ya Kenyatta kuukata Muungano wa Kenya na Tanzania na kuiona Kenya inaendelea kiuchumi wakati Tanzania inakwama.
 
Kwani sasa hivi hao wazanzibar matajiri wanazuiwa na nani kuisaidia Zanzibar?
 
Othman Masoud ni mtu asieutaka Muungano ata Zanzibar ipewe nini atakuja na dai jipya.

Anyway mimi sio pro muungano anymore tuwaache tu wafanye yao;
Kama Othman Masoud hataki Muungano, na wewe pia huujali Muungano, why are you hyperventilating in attacking and disparaging him?

Othman hataki Muungano, na mimi siutaki Muungano, na ma milioni ya Wazanzibari na Watanganyika HATUTAKI MUUNGANO, kwa nn mtulazimisheeee?
 
Kwani sasa hivi hao wazanzibar matajiri wanazuiwa na nani kuisaidia Zanzibar?

Unataka wajenge uchumi wa Zanzibar ili machogo mje kupora mali zao na kuifilisi tena? Si mlishafanya zamani au unafikiri tumesahau? Unafikiri nyie mtakubali Zanzibar ipate maendeleo wakati nyie mnakwama huko bara bila ya kuja kufanya fujo huku? Kuwa realistic kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…