Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Hali si shwari kati ya Hussein Mwinyi na Othman Masoud. Hawaelewani kuhusu suala la Muungano

Kweli yule anapenda sana kupotosha. Nimemshangaa anavyojaribu kupotosha hata issue ya electoral votes za Marekani. State ndogo ni ndogo tu, hata kama electoral college system ikitumika. State yenye 3 electoral votes, kwa mfano, inakuwa na sauti kubwa pale tu candidates wanapokuwa wanachuana vikali kiasi kwamba atakayeshinda hiyo state ndiye atakuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais. Otherwise, candidate anaweza kushindwa uchaguzi small states kibao, yet akashinda uchaguzi kama amezivuna electoral votes za majority ya zile states kubwa zaidi.
Kupotosha imekuwa ada ya OMO na anafanya hivyo kutokana na chuki iliyomjaa dhidi ya Watanganyika

Naendelea kumweka wazi kwa kutumia maneno yake, tafadhali rejea clip hii

Clip: OMO anasema mambo ya muungano ni ya pamoja, upande mmoja umeyachukua na Zanzibar haishirikishwi katika kutunga sera ''policy'' yeye akiita sheria

Hoja: Miswada ya serikali inapitia baraza la Mawaziri la JMT.
VP ni mjumbe wa Baraza na Rais wa Zanzibar ni mjumbe tena kwa kuapishwa na Jaji mkuu wa Tanzania.
Mfano, SSH alikuwa VP na Shein Rais wa Zanzibar

Pili, Zanzibar ina Wabunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa ambao ni kutoa CCM na ACT
Wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na watu 2,500 kama yule wa ACT Wazalendo kutoka jimbo la ''Donge''

Wakiwa Dodoma wanakura sawa na Mbunge yoyote wa Bunge. Vipi OMO anasema Zanzibar haina uwakilishi?

Tatu, kuna Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi wanaoingia Bunge la JMT, wanalipwa na kodi za Watanganyika kuiwakilisha Zanzibar

Nne, Wabunge wa Zanzibar wanaochaguliwa na watu 2,500 hadi 6,000 wana kura za mambo ya Tanganyika. Wabunge hao wapo katika kamati za Bunge za mambo yasiyo ya muungano . Kwanini OMO haoni ukweli huu? Nani anadhulumika hapo!

Tano, kama sheria zinatungwa JMT na kubambikiziwa Zanzibar, OMO asome kifungu hiki cha katiba ya Zanzibar ya 2010 na aeleza ni kwavipi sheria na sera za JMT zinaweza kutumika Zanzibar bila idhini hii hapa chini

132.(1) Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.

Rejea Clip Dakika 7.29
OMO anasema Zanzibar haiendelei kiuchumia kwasababu haina nyenzo za kuisaidia akizitaja kama
1. Kodi
2. Fedha
3. Mambo ya nje

Hoja: OMO ni makamu wa Rais na kiongozi wa ACT na aliwahi kuwa AG . Katiba ya Zanzibar 2010 inasema ;

133.(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria iliyotugwa na Baraza la Wawakilishi au kwa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu na Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

(2) Masharti yaliyomo katika kijifungu cha (1) cha kifungu hiki hayatalizuia Bunge kutumia mamlaka yake ya kutoza kodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya Muungano kwa mujibu wa madaraka ya Bunge hilo kwa kujua kwamba mashauriano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano yamefanywa na kukubalika sehemu zote mbili kabla kupitishwa Sheria.

Suala la kodi llimejibika, tuangalie mengine

Hoja: Suala la fedha halieleweki OMO analizungumzia kwa maana ipi, kwamba, Zanzibar haina pesa au kwamba Zanzibar haina fedha yake! hili ni tata hata hivyo tutafafanua kwa kadri

Bajeti ya Zanzibar 2022/23 inaonyesha mamlaka ya mapato Zbar (ZRB) itakusanya Takribani bilioni 500 na TRA Takribani milioni 400. Pesa hizo zinabaki Zanzibar .

Zanzibar inapata 4.5% ya pato la Tanganyika , kiasi hicho ni kikubwa kuliko makusanyo ya kodi za ZRB na TRA. Kuna mikopo na Misaada na wakati huo huo Bajeti haionyeshi
Matumizi ya wizara ya ulinzi na Usalama
Mambo ya nje
Mambo ya ndani
Taasisi zote za muungano JMT
OMO anapolalamika Zanzibar haina pesa yeye angetaka ipate nini zaidi?
Kama OMO anataka Zanzibar iwe na sarafu yake basi aseme wazi '' vunja muungano''

Hoja: Wizara ya mambo ya nje ni ya muungano. Hatuwezi kuwa na muungano tukiwa na uwakilishi mara mbili.
Laiti ingalikuwa hivyo tungalikuwa na viti viwili katika UN. Ni wapi Zanzibar inanyimwa fursa?

Kuhusu kukopa, OMO afahamu Tanzania kuwa mdhamini wa Zanzibar ni baraka si ugonjwa kama anavyotusi

China wanajua akiwa AG, OMO aliongoza Zanzibar kukataa kulipa deni la Tanesco la Bilioni 50+ takribani dola milioni 16. Wachina wanajua Dollar milioni 200 ambazo ni takribani na bilioni 700-800 kwa leo ni karibu 1/3 ya Bajeti ya Trilioni 2.5, wanachelea kutoa mkopo bila udhamini wa JMT au Tanganyika
OMO aelewe wakopeshaji hawatoi zawadi wanaangalia pesa zao pia .

Nadhani Zitto na ACT wamshauri, kama ni kuongea awe na ''facts'' si leo anaongele moja la BoT kesho jingine.

Pia wamshauri aache chuki dhidi ya Watanganyika bali aelekeze malalamiko yake kwa Wazanzibar Wabunge JMT, wale kutoka BLW wanaokuja Dodoma na Wawakilishi katika baraza la mawaziri ambao leo wapo na CCM
 
Huyu jamaa ni mtu wa ovyo sana. Kama yeye ni miongoni mwa viongozi bora wa ACT huko Zanzibar, basi kiongozi wao mbovu sijui atakuwa mtu wa aina gani.
 
Sio kupora. Tutatumia kwa sababu Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
 
Kwa maoni yangu, huyu mtu anatakiwa awekwe pembeni, apate muda wa kutosha ajishughulishe na siasa, kwasababu ACT ndani ya GNU wanatakiwa kutekeleza Ilani na sera za CCM!.

Ushauri kama huu kumhusu mtu huyu huyu niliwahi kuutoa kule nyuma na ukatekelezwa, Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

P
Unamuweka vipi pembeni? Unadhani Kenyatta amependa kukaa na Rutto mpaka leo wanamaliza wote muhura?

Hivi ule uanasheria wako na kutetea katiba na haki za wengine huwa unaishia tu kwa Halima Mdee na wenzake?
 
..Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.

..Hussein Mwinyi anamuona Othman Masoud kama mchochezi asiyetaka Wazanzibar wawe kitu kimoja.

Msikilize Othman Masoud hapa chini.
View attachment 2280710

Hussein Mwinyi amejibu hapa.

View attachment 2280711
Pasco kaupiga mwingi sana hapa.
 
Tatizo ambalo Watanganyika hawataki kulisema au kujifanya hawalioni ni Rais wa Zanzibar kuteuliwa Dodoma na Watanganyika, tungewaachia Wazanzibar wafanye wenyewe mchakato wa kuteuwa wagombea wao Urais.

Mfano hai ni sasa, Zanzibar inatawaliwa na Mtanganyika Hussein Mwinyi hii ni fact, na Hussein Mwinyi haijui Zanzibar kama huyo OMO, hawezi kufanya debate popote na OMO kuhusu Zanzibar, anachokijuwa Hussein ni uchumi wa blue tu, labda advantage ya Hussein ni mtu muungwana siyo katili kama Magufuli, hii ndio sababu pekee pamoja na joto la OMO lakini Hussein atawavusha salama Wazanzibar.

Ila nawasihi Watanganyika wenzangu tuache unafki, kwenye muungano huuntumewafanyia sana dhulma Wazanzibar kama mtu uko serious kweli unasimama katika haki.

Zanzibar nje ya Muungano ingekuwa tayari ni Dubai ndogo, nakumbuka enzi ya mwinyi nguo nzuri za dukani tulikuwa tukienda kununuwa Zanzibar.
 
Uchumi upi huo wa Zanzibar uliporwa na Tanganyika ?...acheni kujenga hoja za uongo na uzushi.
Pascal Mayalla

Uchumi si ndiyo huo uliojenga hizo forex reserves zilizotajwa?

He now fears that Nyerereʼs government is trying to gain control over Zanzibarʼs relatively hefty foreign exchange reserves. The two leaders will probably continueto make compromises in order to keep the union going, partly because their prestige would suffer if it were dissolved. Thus the union is likely to muddle along as long as Nyerere and Karume are in power, but few other Tanzanians would mourn its passing.
 
Hussein Mwinyi amejibu hapa.

View attachment 2280711

..Othman Masoud anamuona Hussein Mwinyi kama mateka asiyeweza kuitetea Zanzibar, hadhi, maslahi, na haki zake.

..Hussein Mwinyi anamuona Othman Masoud kama mchochezi asiyetaka Wazanzibar wawe kitu kimoja.

Msikilize Othman Masoud hapa chini.
View attachment 2280710

Hussein Mwinyi amejibu hapa.

View attachment 2280711
Mkuu

Mkuu JokaKuu, kwa ruhusa yako, naomba kulitumia bandiko lako hili kama mbegu ya kuoteshea bandiko langu fulani.
P
 
Mkuu JokaKuu
Ingalikuwa vema ukiweka clip nzima ya Othman Masoud kwasababu kuna mengi

Sishangai mtifuano kwasababu, OMO kama wanavyomwita ni mpotoshaji hasa linapokuja suala la muungano.
Angalia interview ya Clouds 360 ina mengi ya kapotosha kwa makusudi au kutojua

Watangazaji watatu wa Clouds hawakuweza kuuliza, kusahihisha au kutaka ufafanuzi kutoka kwa Othman alipoongea . Walimwacha ahutubie badala ya mahojiano. Watangazaji walisikitisha katika viwango! shame

clip ni kwa hisani ya Clouds media

Dakika 48
Masoud Othman anasema ''Tanganyika na Zanzibar ziliungana zikiwa sovereign states, baada ya muungano ikawa shared sovereignity. Moja ya matakwa ya shared sovereignty ni kuwa na Policy na kwamba sheria zinatungwa na upande mmoja na baraza la mawaziri la JPM ,Zanzibar haikuwakilishwa''

Hoja: Hoja ya VP Masoud si ya kweli.
Katika shared sovereignty Tanganyika impoteza Zanzibar imebaki nayo kupitia SMZ inayoamua mambo yao.

Kuhusu sera kutungwa kwa upande mmoja nalo si kweli.
Zanzibar ina Wabunge na Wabunge kutoka BLW wanaoiwakilisha katika Bunge la JMT.

Kwamba maamuzi yanafanywa kwa kura ni kweli kwasababu Wazanzibar ndani ya JMT wanaamua hata mambo yasiyo ya muungano kwa kura ile ile anayoikataa Masoud Othman, mbona halisemi hilo?

Kamtumhumu JPM kwamba baraza lake la Mawaziri halikuwa na uwakilishi kutoka Zanzibar.
VP Othman alikuwa AG anafahamu Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa Cabinet kwa kuapishwa
Kwamba VP SSH alikuwa mjumbe wa Cabinet. Hivi hawa si viongozi wa juu wa Zanzibar, VP Othman alitaka uwakilishi gani?Lakini pia alikuwepo Waziri Mbarawa akisimamia wizara isiyo ya muungano, hilo anasemaje?

Dakika 53
VP OMO anasema ''resource za muungano zitawanywe ili Zanzibar ipate biashara na ajira.
Akatoa mfano Elimu ya juu ambako Zanzibar hakuna chuo kikuu''

Hoja: Haiwezekani resource za Tanganyika ziwekwe Zanzibar kwasababu mambo makuu ya muungano ni machache sana.

VP OMO hakusema gharama za resource hizo anazotaka ziwekezwe Zanzibar zinalipwaje na Zanzibar.
Kwasasa Zanzibar haina mchango wowote kwanini resource za muungano zipelekwe huko.

Pili, Masoud Othman aelewe suala la elimu ya juu si la muungano. Ni suala lililoongezwa na akina Marehemu Sitta katika kusiadia Zanzibar hivyo kutojengwa chuo huko ni sawa kikijengwa ni fadhila.
Zanzibar wana wizara ya elimu ya juu sasa anataka ya muungano ifanye nini ? Zanzibar inachangia nini?

Dakika 51 anasema Rais wa JMT anachaguliwa na Tanganyika kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura Zanzibar. Makamu wa Rais Othman akatolea mfano Marekani ambako California ina watu milioni 40 na Maine milioni 1.6 na Wyoming milioni 1 akisema mfumo huo unahkikisha hata state ndogo zinapata kauli kwa kutumia kile alichokiita ''Collegiate''

Hoja: Hakuna kitu kinachoitwa ''collegiate'' katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani bali electoral college.

States zimepewa idadi ya Wajumbe watakaochaguliwa kwenda kumchagua Rais.
Rais anaweza kuchaguliwa kwa electoral college votes (270) za state chache

Hivyo kuna majimbo yenye wajumbe wanaoweza kufikisha 270.
Mfano California 55, New York 29, Texas 38, Florida 29, Pen state 20, Michigan 16, Georgia 16, N.Carolina 15, Maryland 10, Tenn 11, Illnoi 20, virginia 13, S.Carolina 9. State 12 zinaweza kumchagua Rais wa Marekani kwa kura 270 zinazohitajika.

Mfumo huo unawafanya wagombea wasipoteze muda na pesa za kampeni huko Montana wajumbe 3, Wyoming 3, au Vermont 3. kwa mantiki hiyo VP alipotosha au hakujua mfumo unafanyaje kazi

Hata Tanzania bado kuna suala la mikoa. Mfano mikoa ya kanda ya ziwa inaweza kumchagua Rais
Tukifuata mfumo wa Marekani bado Zanzibar itakuwa na viti vichache kwasababu katika constituents za Tanzania Zanzibar ni ndogo sana Wabunge wake wakichaguliwa na watu 2,500 lakini wanakura sawa pale Dodoma. Hivi Makamu wa Rais halioni hili kweli.!!!

Wamarekani sasa hivi wanataka popular vote kwa kujua mfumo wa electoral college si mzuri. Hillary Clinton alishinda popular vote kwa kura milioni 3 lakini Trump alimshinda kwa electoral college na kuwa Rais

Pengine alichokusudia kusema ni kwamba states zimepewa Maseneta 2 bila kujali ukubwa ili maamuzi yazingatie hata zile ndogo. Kinyume cha hivyo OMO alipotosha sana

Bank kuu:
VP Othman anasema Karume aliona tatizo hakukubali kuingia BoT hadi Salimini. Kwamba Zanzibar ilikuwa na PBZ baada ya kuvunjika EAC currency board

Hoja: Hapa VP anatueleza kwamba yale madai ya Zanzibar kuingiza pesa BoT yanayowapa 4.5% ya pato la Tanganyika ni uongo na kwamba pesa hizo hawakupaswa kupewa bali ni hisani.
Lakini pia VP othman hakueleza nini kilimfanya Salimin akaingiza nchi BoT? Hakueleza je ZPB ambayo ipo hadi leo inamilikiwa na nani?

Dakika 23
OMO anasema Zanzibar ingesaidia muungano kutokana na historia yake na kwamba kuna KM 200 za bahari zenye mafuta na gesi katika vitalu 9, 10.

Hoja Historia ya Zanzibar ni ya biashara ya pembe za ndovu na utumwa, haina manufaa kwa Tanzania leo hii.

Pili, mafuta na gesi yameondolewa na Zanzibar katika mambo ya muungano kupitia katiba ya 2010.
Ingawa Zanzibar inafadika na mapato ya gesi na madini yenyewe haitaki kuwa mshiriki.
Makamu wa Rais anapotosha sana

Dakika 24
OMO anasema Singapore ilikuwa katika muungano na Malaysia nailipojitoa uchumi wake ni mkubwa kuliko wa Tanzania na inaweza kufadhali bajeti

Hoja: VP Masoud anawaambia Wazanzibar wakitoka nje ya muungano watakuwa matajiri kama Singapore.

Hakuna tatizo ni mtazamo wake, anatakiwa achochoea kuni muungano uvunjike Zanzibar iwe Singapore

Katika video hii anazungumzia Zanzibar kunyimwa fursa ya kukopa akitolea mfano wa milioni 200 kutoka China
Anasema Tanganyika ipo hoi na Zanzibar ikitaka kupita Tanganyika inaweka vikwazo

Hoja: Mataifa yanakopesha kwa kuangalia uwezo wa nchi kulipa.
China walisita wakijua mdhamini lazima awe chumi kubwa Tanganyika.

Makamu wa Rais aelewe Zanzibar iliruhusiwa kukopa, jambo jema kwani litapunguza mzigo kwa Tanganyika.

Anachotakiwa ni kuendelea kusisitiza tu waende kukopa bila kutumia jina la JMT, walipe wenyewe na watafute wadhamini wenyewe! Tanganyika haina sababu za kuzuia Zbar wasikope ! haina bali kauli tu za kuzua na kuifanya Tanganyika ionekane ni waovu sana ! Chuki yake dhidi ya Tanganyika imefuruta

Muungano wa ccm acha waparuane.
 
Hata Machogo wanamsakama sana na kubwa ni Mzenji na mafanikio anayoipatia Tanzania hayajawahi kupatikana au hata kufikiriwa tokea Tanganyika ipate uhulu.
Leo hii Tanzania wanatembea vifua mbele tena wanajiona fahari kujijulisha kuwa ni Mtanzania ,sio miaka ya iliyopita tukiitwa vibaka.
Nasema uongo ndugu zanngu ?
 
..Mwinyi angekuwa wise asingekubali chama chake na vyombo vyake kuuwa Waznz na kuharibu uchaguzi ili yeye apate madaraka.

..Othman Masoud anajiamini kwasababu ana rekodi ya kusimamia maslahi ya Waznz. Pia mambo anayoyazungumza yanaungwa mkono na Waznz.
Kwa kweli OMO hakuna jipya analoleta, yeye anakazia yale yale. Tukumbuke Maalim aliwahi kusema alichotaka ni serikali ya mkataba lakini serikali 3 ndio cuf na ukawa walipigania. Kwenye rasimu ya warioba zanzibari walitaka 3 na wakubwa serikalini pia walitaka 3. Walimgeuka OMO dakika za mwisho yeye akasimamia hoja akafukuzwa. CCM ndio walisabotage rasimu ya warioba wakafuta 3 wakarudi 2.
Ukisoma michango yetu humu utaona wengi wanamkosoa OMO kwa argument zake hasa kuhusu facts. Je kuna popote aliposema hataki muungano? Kama ni muungano basi twende 3 mbili zimepitwa na wakati vinginevyo tuagane tuwe jirani wema tushirikiane hivyo hakuna haja ya kulazimishana.
 
Tatizo ambalo Watanganyika hawataki kulisema au kujifanya hawalioni ni Rais wa Zanzibar kuteuliwa Dodoma na Watanganyika, tungewaachia Wazanzibar wafanye wenyewe mchakato wa kuteuwa wagombea wao Urais.
Nadhani hili si tatizo la Watanganyika ni tatizo la CCM na hasa CCM Zanzibar.

Hakuna Mtanganyika anayesema Rais wa Zanzibar ateuliwe Dodoma, ni Wazanzibar wanaokuja wenyewe.

CCM wana kamati maalum Zanzibar kwanini isikatae?
Kwanini Wazanzibar kwa umoja wao wasigomee mgombea anayetoka Bara?

Uchaguzi wa 2020 Kamati ya CCM ilimchagua yule Waziri kiongozi wa zamani, ilipofika Dodoma akapigwa chini.

Wajumbe wa kamati kuu na Halmashauri kuu wapo CCM kutoka Zanzibar, wakampitisha Mwinyi

Si Watanganyika, ni CCM na utaratibu wao na Wazanzibar wa CCM wanakubali utaratibu

Yule Waziri kiongozi wa zama amepewa bakuli hivi karibuni, analamba asali mjengoni
Mfano hai ni sasa, Zanzibar inatawaliwa na Mtanganyika Hussein Mwinyi hii ni fact, na Hussein Mwinyi haijui Zanzibar kama huyo OMO, hawezi kufanya debate popote na OMO kuhusu Zanzibar, anachokijuwa Hussein ni uchumi wa blue tu, labda advantage ya Hussein ni mtu muungwana siyo katili kama Magufuli, hii ndio sababu pekee pamoja na joto la OMO lakini Hussein atawavusha salama Wazanzibar.
Mfano ule wa Waziri kiongozi wa zamani aliyechaguliwa Zanzibar akapigwa chini Dodoma siyo Watanganyika

Unakumbuka katiba ya Warioba?
Wazanzibar walikuja na agenda moja, mwisho wa siku akina P. Kificho wakahitilifiana na kuwakana akina OMO.

Ila nawasihi Watanganyika wenzangu tuache unafki, kwenye muungano huuntumewafanyia sana dhulma Wazanzibar kama mtu uko serious kweli unasimama katika haki.
Tuonyeshe dhulma kwa uhalisia ili nasi tufunguke macho na tuache kutetea dhulma
Zanzibar nje ya Muungano ingekuwa tayari ni Dubai ndogo, nakumbuka enzi ya mwinyi nguo nzuri za dukani tulikuwa tukienda kununuwa Zanzibar.
Kinachowashinda ni kitu gani?

Unasahau soko la Zanzibar lipo Tanganyika, na kwamba siku hizi hakuna ujamaa tena Watanzania wanasafiri wanafanya biashara. Bandari ya Bagamoyo inapanda nani atashusha kontena 30 Zanzibar!

Hilo ndilo limewasukuma Zanzibar wakalalamika kuhusu mizigo yao kutozwa kodi inapoingia Tanganyika.

Ni kero ambayo sasa hivi ''Mwenzao' kwa kumtumia Bw Mpango wamerhusu bidhaa za Zanzibar ziingie bara bila kutozwa kodi. Hili ni kwa gharama za Tanganyika ndiyo maana hata OMO hakutaka kuliongelea

Wafanyabiashara wa Zanzibar watakwepa kodi na kupitisha bidhaa buree kama ilivyokuwa huko nyuma
Tanganyika tutaumia kwasababu kodi na tozo zitaongezeka kwa gharama za kuwafurahisha Wazanzibar

Umewahi kuwasikia hawataki muungano! kila siku wanataka serikali 3 au mkataba. Tuliwauliza mkataba ufaidishe nini Tanganyika, wakachomoa sasa hivi wanasema 3 ili wajibanze

Na usisahau Tanganyika imebeba nusu ya Wazanzibar!
 
Kwa kweli OMO hakuna jipya analoleta, yeye anakazia yale yale. Tukumbuke Maalim aliwahi kusema alichotaka ni serikali ya mkataba lakini serikali 3 ndio cuf na ukawa walipigania.
Maalimu alitaka serikali ya mkataba akaulizwa ndio kitu gani? Hakuwa na jibu. Ile ilikuwa njia rahisi ya kusema hataki muungano lakini kulitokea tatizo. Wahafidhina wa CCM wakiongozwa na Idd S walisema ASP itarudi na hapo Maalimu hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali 3. Wazo la serikali ya mkataba lilikuwa la kipuuzi sana. Hivi Tanganyika inahitaji mkataba na Zanzibar ili inufaike na nini. Hawa akina OMO walikuwa nyuma ya hoja hiyo na ya kuvunja muungano
Kwenye rasimu ya warioba zanzibari walitaka 3 na wakubwa serikalini pia walitaka 3. Walimgeuka OMO dakika za mwisho yeye akasimamia hoja akafukuzwa. CCM ndio walisabotage rasimu ya warioba wakafuta 3 wakarudi 2.
Tena walioua ule mchakato ni CCM Zanzibar akina Pandu. Kilichotokea ni kutoaminiana na Unguja wakijawa na hofu kwasababu hoja za serikali ya mkataba zilionyesha jambo nyuma yake
Ukisoma michango yetu humu utaona wengi wanamkosoa OMO kwa argument zake hasa kuhusu facts.
Hana facts bali uongo na uzushi tu, tumeonyesha bila kificho. OMO hashambuliwi kwa haki yake ya maoni bali kauli zake za kuzua zisizo na ithbati za kujaza watu ghadhabu na kuwadanganya Wazanzibar masikini akijua kabisa anawadanganya. Ni mzushi tu soma hoja zake utuonyeshe ''fact' moja tu
Je kuna popote aliposema hataki muungano?
Hilo hazungumzi wazi anajificha ficha kwa vi hadithi kama kile cha Scotland na Singapore na kwamba Zanzibar inaonewa inanyimwa haki wakati anajua ni wakati akiwa AG hata bili ya umeme hawakuweza kulipa halafu anataka bilioni 800 kutoka china! Hao Wachina wana habari zote!
Kama ni muungano basi twende 3 mbili zimepitwa na wakati vinginevyo tuagane tuwe jirani wema tushirikiane hivyo hakuna haja ya kulazimishana.
Hizo 3 wakiridhika, kama hawataki hewala njia nyeupe !
 
Mzigo gani? Nyie machogo si mnasubiri mafuta ya Zanzibar yachimbwe mpore hela za Wazanzibari mkiwa mmevaa koti la muungano?
Hizi kelele zote zinatengenezwa na wahizbu..nyie jamaa ni watu wa hovyo sana.

Kwa staili hiyo mnayoenda nayo nadhani mmeimis 2001

#MaendeleoHayanaChama
 
Tatizo ambalo Watanganyika hawataki kulisema au kujifanya hawalioni ni Rais wa Zanzibar kuteuliwa Dodoma na Watanganyika, tungewaachia Wazanzibar wafanye wenyewe mchakato wa kuteuwa wagombea wao Urais.

Mfano hai ni sasa, Zanzibar inatawaliwa na Mtanganyika Hussein Mwinyi hii ni fact, na Hussein Mwinyi haijui Zanzibar kama huyo OMO, hawezi kufanya debate popote na OMO kuhusu Zanzibar, anachokijuwa Hussein ni uchumi wa blue tu, labda advantage ya Hussein ni mtu muungwana siyo katili kama Magufuli, hii ndio sababu pekee pamoja na joto la OMO lakini Hussein atawavusha salama Wazanzibar.

Ila nawasihi Watanganyika wenzangu tuache unafki, kwenye muungano huuntumewafanyia sana dhulma Wazanzibar kama mtu uko serious kweli unasimama katika haki.

Zanzibar nje ya Muungano ingekuwa tayari ni Dubai ndogo, nakumbuka enzi ya mwinyi nguo nzuri za dukani tulikuwa tukienda kununuwa Zanzibar.
Ili mtuletee mahizbu na washenzi kama omo mvunje muungano..mkitaka tuvunje muungano leteni ule mchanga uliochanganywa kisha tuchambue wa zenji pembeni wa Tanganyika pembeni...hapo ndio tutavunja muungano.

Tunaelekea kuwa na serikali moja JMT...hizi mbili zimetuchosha.

Hakuna cha uhuru kamili wa zenji hilo sahauni maisha mkilete chokochoko nadhani historia huwa mnaifahamu vyema na kumbukumbu mnazo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hawa akina OMO walikuwa nyuma ya hoja hiyo na ya kuvunja muungano
Kwani kutaka kuvunja muungano ni kosa ?

Kwa nini mnatulazimishia Muungano?

Wewe Mtanganyika unafaidika nini na kakisiwa landless kale ka Zanzibar ??????
 
Back
Top Bottom